CHADEMA na FALSAFA ZA WAARABU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA na FALSAFA ZA WAARABU

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by charityboy, Feb 26, 2011.

 1. c

  charityboy Senior Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufanya maandamano katika vitongozi mbalimbali vya mji wa Mwanza na kisha leo kuhamia Musoma ili kupinga kuongezeka kwa gharama za maisha, malipo ya dowans nk ni kufuata philosophy isiyofahamika. Warabu ni watu makini sana, wao wamefanya maandamano kudai matango tu baada ya miaka mingi ya utawala na hali isiyombaya ya uchumi.
  Chadema wanachofanya sasa ni kuiga falsafa ambayo haiwezi kufanya kazi bongo. Tanzania ni nchi iliyojiwekea utaratibu wa kukabidhiana madaraka kila miaka 5.
  Nawashauri CDM wasubiri 2015 vinginevyo watapoteza MVUTO.
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Charity boy,
  Jiandae kupangua HOJA motomoto, wenyewe wanakuja punde...
   
 3. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Charityboy,,,think of your name......
  Siasa si uchaguzi tu,siasa ni maisha ya kila siku,ni uchumi,na chadema tunatambua hilo,ni wajibu wa chadema kufanya siasa bila na kupinga upandaji hovyo wa gharama za maisha,ushauri wako ni batili na kamwe chadema hawatakubali....
  Chadema hawakurupuki,na wanachofanya ni sahihi bila kujali wewe charityboy utasemaje
  ni swala la muda tu
  saa ya ukombozi ni sasa
   
 4. N

  Nangisye Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mapema mno kuchukua hatua kama hizo kwani waliwastadi waarabu kuwa walianza mipango lini kwani naona wamekurupuka kufanya hivyo badala yake polisi hawatawafyatulia risasi ila watabomoa majengo ya serikali na kuharibu mali za watu binafsi hilo linaonekana wazi!
   
 5. c

  charityboy Senior Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawasubiri mkuu, hiki kichwa halafu ni charitable
   
 6. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Bado nashindwa kuelewa naomba mnieleweshe waungwana
  Endapo serikali ya JK akaanguka ina maana Cdm ndio watakaotwaa madaraka?
   
 7. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Binafsi sijaelewa ulichokuwa unamaanisha!
  I mean, the sh*t you wrote is just......!
  dustbin.gif
   
 8. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Charitable? Bwabwa?
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hatuhutaji kufuata utaratibu wa Waarabu kwa Tanzania.

  Nyerere huko aliko, atafanya kazi yake na kuondoa uozo hapa Tanzania.

  [​IMG]

  Akiita hawa Wanafunzi wake hata wawili wamfuate, mambo yatabadilika.
   
 10. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  swala hapa ni gharama ya maisha imepanda sana huo ndio ukweli, inflation rate imepanda mara tatu tangu 2005, ila mishahara ipo pale pale, sasa mimi binafsi sioni kama kuna tatizo CDM wakiandamana na wananchi kupinga hali hiyo, bila kujali wanachofanya kinafanana na waarabu au lah!
  au ungeshauri gharama za maisha zinapopanda kwa kiasi hiki je CDM au wananchi wantakiwa kufanyaje?
   
 11. c

  charityboy Senior Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nyerere keshakufa hana msaada wowote kwa sasa. Au unaabudu MAKABURI?
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wasomi historia za nchi za kiarabu tangia enzi za manabii, ndio watakapo jiona Tanzania ni tofauti kabisa na nchi hizo, CHADEMA MMECHANGANYIKIWA VIBYA sana , Mungu awarehemu !
   
 13. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Pilipili usiyokula yakuwashia nini?Kwanini wewe usisubiri 2015 kufanya analysis yako ya kilevi badala ya kuwataka Chadema wasubiri hadi mwaka huo?

  Jibu la wazi ni kwamba mnakereka sana kuona Chadema imeendelea kuwa imara licha ya hujuma zote mnazofanya dhidi yake.Mnaumia zaidi kuona mbinu wanazotumia Chadema zitakifanya chama hicho kiwe,technically,mshindi hapo 2015 kabla hata ya uchaguzi mkuu.

  Halafu mzembe wewe wa kufikiri hujihangaishi kufahamu kuwa kitakachofanyika 2015 ni hitimisho la jitihada za chama cha siasa kuomba kupewa ridhaa ya kuongoza.CCM itahukumiwa kwa matendo yake,and so will be Chadema na wengineo.Mfano mwepesi kwa ngumbaru wa tafakari ni kama huu:kwa mkulima kupata mavuno shurti apande mbegu shambani kitambo kabla hajavuna.Wanachofanya Chadema ni kilekile anachofanya mkulima shambani:kupanda mbegu ya ushindi ili hatimaye kuvuna zao liitwalo ushindi.Lakini pia,Chadema kama chama makini hakiwezi kulala huku Watanzania wakigeuzwa punching bag ya mafisadi.Hivi kwa mwenendo wa bunge la Makinda,mahakama iliyofurika wateule wa Kikwete serikali (executive branch of the state) iliyojaa mafisadi,na a virtually dormant civil society, kimbilio la watanzania ni wapi kama sio kwa opposition parties?

  Endelea kusubiri 2015,achana na sie "tunaopoteza muda kwa maandamano".Why should you care anyway?
   
 14. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nani akueleweshe?Kama mada huielewi si bora uhamie kwenye "nyepesi nyepesi"?
   
 15. c

  charityboy Senior Member

  #15
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Werevu hawawapati hata siku moja. CDM bado mnahitaji miaka mingi ya KUNYONYA kabla ya kupewa nchi. Hii nchi tuna uchungu nayo sana hatuwezi kuwapa kirahisi.
   
 16. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu Washawasha, ningependa RA na serikali yake waanguke tangu miaka kadhaa iliyopita lakini sijawaza nini kitatokea baada ya hapo. Hii nchi kwa sasa inamilikiwa na RA na watu wanadhani kuvumilia huu ushoga wa wanasiasa ndo kulinda amani. Hofu yangu ni kwamba si rahisi kumwondoa madarakani mfanyabiashara kama RA kwa kuwa yeye hakai Ikulu wala katika majengo yoyote ya Serikali. Maandamano ya CDM yakionesha kuimarika zaidi, yeye anasafiri na kuwaagiza wafanyakazi wake (ambao sisi tulidhani ndo tumewachagua kutuongoza) wayamalize haraka vinginevyo hatawapa fedha ya kampeni katika uchaguzi ujao au atawafukuza Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Chama Chake. Huwezi kuamini nguvu itakayotumika hapo.Kwa kujibu swali lako si CDM watakoingia moja kwa moja madarakani, isipokuwa (RA akiwaamuru kuweka silaha chini) itaundwa serikali ya Umoja wa kitaifa kwa muda ili kuelekea Uchaguzi huru na wa haki. Wakati wa kampeni, kwa kuwa wanasiasa wa nchi zetu wanapenda sana madaraka, baadhi yao watauza utu wao na wa wale waliowaunga mkono kwa RA au mfanyabiashara mwingine Fisadi ili waingie madarakani na mwisho wa siku tutarudi palepale japokuwa mtindo unaweza kuwa tofauti na huu kwa kiasi fulani.
   
 17. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbe unaimba taarabu mie nilidhani unachangia ! sorry kajiunge Jahazi wanakusubiria huko sio hapa JF
   
 18. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Sababu naona chama pekee cha upinzani ambacho kimeshikia bango hili suala ni CDM ndio nilikuwa nataka kujua ni katiba gani itawapatia madaraka kama JK akianguka?
   
 19. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwalimu Nyerere aliisha wahukumu wapinzani siku nyingi sana, mnazoona zote hizi vurugu za CDM ni laana ya huyu mzee
   
 20. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Je ?katiba ya Jamuhuri inatamka hayo maneno ya kwamba itaundwa na Serikali ya umoja wa kitaifa?
   
Loading...