Kwanza kabisa umepotoka vibaya sana unaposema 'falsafa za Waarabu'. Hizi si za Waarabu, hazikuanzia kwao. Nchi za Ulaya Mashariki kama vile Romania Czechoslovakia, Hungary, Ujerumani ya Mashariki, Poland etc walichukuwa hatua kama hizo kujikomboa na wakashinda.
Halafu kulikuwa nchi kama Philippines (alipong'olewa dikteta Marcos) na Indonesia (alipotimuliwa Dikteta Suharto)wa maandamano tu. Zote hizi hazikuwa nchi za Kiarabu. sitaji Iran alipotimuliwa Sha kwa maandamano, kwani baadhi yenu mtasema Wairani ni Waarabu.
Kwa ujuma hujui chochote unachokisema, unabahatisha bahatisha tu. So sad!!!!! Sijui elimu yako imekaaje vile?