Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,755
Jamaa wanateseka sana...Sema hawakutegemea kama mzee angerudi ghafla..Wakuu,
Chadema kati ya mambo yanayosikitisha ni kutojifunza kupitia makosa wanayofanya. Wanapokosea zinatumika nguvu nyingi kuhalalisha makosa yao na kugeuza wakosoaji wao wenye nia njema maadui.
Mlipoingia kwenye mgogoro na Dr Slaa mwezi july 2015 mlianza kumchokonoa kwa kila namna kila mahali wakati Dr Slaa kwa heshima aliamua kukaa kimya. Baada ya miezi miwili ya propaganda ikalazimika Dr Slaa afunge mjadala kwa pigo la karne pale Serena.
Sasa mnaanza kufanya yale yale kwa Lowasa. Tunaona wanachama wenu maarufu na wabunge wanachofanya mitandaoni. Mnasahau mnadeal na mtu ambaye anakijua chama chenu kabla hata wengine hamjajua siasa ni mdudu gani.
Chadema narudia tena kuwaasa, wekeni utaratibu wa chama kutoa matamko na misimamo. Katibu mkuu Mashinji ameshaongea na kutoa msimamo tena kwa weledi mkubwa. Lakini akina Lema na wengine wameshaanza kuropoka na kukejeli kwa mtu ambaye hamjui anajua nini!
Msipojidhibiti mkaendelea na hizo kejeli mnataka kujikuta mnaingia kwenye vita na vijana wake ambao mnajua kazi yao kwenye propaganda. Mtajikuta badala ya kujenga chama kuelekea uchaguzi mkuu mnawekwa kwenye kona ya kujibu tuhuma muda wote.
Hili la EL mliingia cha kike kubalini makosa msonge mbele na msianze kazi ya kumchafua mtu ambaye mlimchafua wenyewe na kisha mkamsafisha! Hamuwezi tena kumchafua zaidi ya nyie kuabika zaidi.
Muacheni Lowasa apumzike na nyie jipangeni namna ya kukihuisha upya chama chenu ambacho kwasasa kimejaa ukakasi mbele ya wananchi ambao nyie ndio mlikuwa tumaini lao pekee.
Mkishupaza shingo muda utaongea!
Sent using Jamii Forums mobile app