CHADEMA muacheni Lowassa apumzike, uchokonozi utawaponza

ungewapa ccm kipindi kile walilikata jina la lowassa tungekuona una busara sana mmemtukana vya kutosha mzee wa watu tunajua mnavyomsumbua Mungu atamsaidia na atakuja kuwaambia Watanzania ni muda tu unasuburiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusiandikie matendo, mwambie aanze kuwachafua, cdm sio chama cha kigaidi useme atakuwa na jipya ambalo cdm hawajawahi kutakanwa nalo. Akitukanwa na wanaccm tena mpaka kuambiwa kajinyea jukwaani mbele ya Magufuli, alifanya nini na hao vijana wake? Acha kuabudu sanamu.
Leo kawa sanamu
IMG_20190303_170520.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri Mzuri Mkuu, ingawa hukuwahi kuwapa CCM wakati wanamkejeli..
Makonda, Polepole, Msukuma..nk Walivuka mipaka Walitukana kabisa..
Jiwe angepata heshima kubwa sana kama angetupilia mbali Maombi ya EL kurejea CCM ..
Chadema haijaathiriwa kuondoka kwa EL ila CCM ndiyo wanaaminisha hivyo..
Kuondoka kwa Dr. Slaa Kuliathiri CDM lakini si EL..
2020
Kwel .....?
IMG_20190303_170520.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na aseme tu, kwani yeye atakwepea wapi katika baya atakalo lisema kuwa hakulifanya wakati na yeye alikuwa CHADEMA.
 
Hakuna mtu anaweza kutoa siri za baraza la mawaziri hata kama ni Mbowe. Ukishakuwa waziri mkuu unabanwa na kiapo hadi kifo. Hiyo ni tofauti na Chadema, anaweza kusema lolote na si lazima aseme yeye!

Mtatafutana, hamjui kwenye siasa partners hufanya nini! Umeshaona Mbowe na Dr Slaa wakishambuliana? Mashabiki tusiojua lolote ndio wanaumizana kwa matusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kuhangaika, majibu uliyokwisha kupewa ulipaswa uendelee na mambo mengine. Hakuna mwenye habari tena na Lowassa ni sawa na mtu kuutuwa mzigo wa gunia la sukari ambalo pamoja na utwamu wake ni zito kubeba,
Huyo ni forgotten person tayari
 
Hakuna mtu anaweza kutoa siri za baraza la mawaziri hata kama ni Mbowe. Ukishakuwa waziri mkuu unabanwa na kiapo hadi kifo. Hiyo ni tofauti na Chadema, anaweza kusema lolote na si lazima aseme yeye!

Mtatafutana, hamjui kwenye siasa partners hufanya nini! Umeshaona Mbowe na Dr Slaa wakishambuliana? Mashabiki tusiojua lolote ndio wanaumizana kwa matusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
With due respect. Nina uhakika hana jipya la kushtusha. Sana sana itakuwa ni propaganda za uwengo kama hizi za kusema dereva wa marehemu Chacha Wagwe au dereva wa Lisu. Ila nakubaliana na wewe kuwa hata Chadema hawawezi ''kumchafua'' zaidi ya walivyokuwa wamemchafua kabla hajajiunga nao. Sana sana wataonekana ni wababaishaji tu. Badala ya kumsema vibaya wangeeleza ukweli i.e. 1. Kwanini hasa waliamua kucheza kamari ya kumpokea na kumfanya mgomea wao 2. Faida na hasara waliyoipata 3. Ni nini kifanyike way foward.
 
Wakuu,

Chadema kati ya mambo yanayosikitisha ni kutojifunza kupitia makosa wanayofanya. Wanapokosea zinatumika nguvu nyingi kuhalalisha makosa yao na kugeuza wakosoaji wao wenye nia njema maadui.

Mlipoingia kwenye mgogoro na Dr Slaa mwezi july 2015 mlianza kumchokonoa kwa kila namna kila mahali wakati Dr Slaa kwa heshima aliamua kukaa kimya. Baada ya miezi miwili ya propaganda ikalazimika Dr Slaa afunge mjadala kwa pigo la karne pale Serena.

Sasa mnaanza kufanya yale yale kwa Lowasa. Tunaona wanachama wenu maarufu na wabunge wanachofanya mitandaoni. Mnasahau mnadeal na mtu ambaye anakijua chama chenu kabla hata wengine hamjajua siasa ni mdudu gani.

Chadema narudia tena kuwaasa, wekeni utaratibu wa chama kutoa matamko na misimamo. Katibu mkuu Mashinji ameshaongea na kutoa msimamo tena kwa weledi mkubwa. Lakini akina Lema na wengine wameshaanza kuropoka na kukejeli kwa mtu ambaye hamjui anajua nini!

Msipojidhibiti mkaendelea na hizo kejeli mnataka kujikuta mnaingia kwenye vita na vijana wake ambao mnajua kazi yao kwenye propaganda. Mtajikuta badala ya kujenga chama kuelekea uchaguzi mkuu mnawekwa kwenye kona ya kujibu tuhuma muda wote.

Hili la EL mliingia cha kike kubalini makosa msonge mbele na msianze kazi ya kumchafua mtu ambaye mlimchafua wenyewe na kisha mkamsafisha! Hamuwezi tena kumchafua zaidi ya nyie kuabika zaidi.

Muacheni Lowasa apumzike na nyie jipangeni namna ya kukihuisha upya chama chenu ambacho kwasasa kimejaa ukakasi mbele ya wananchi ambao nyie ndio mlikuwa tumaini lao pekee.

Mkishupaza shingo muda utaongea!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujumbe wenye busara makini sana,big up!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja waendelee kumchezea Lowassa halafu alipuke hasira za kimasai atoe flash yenye siri zote za chadema aduplicate flash nyingi aitishe press conference halafu amwage kwa waandishi wa Habari siri zote na awagawie Kila Mwandishi flash yake yenye siri zote za chadema ndipo vichwa vyao vitakaa sawa
SI amwage Sasa anangoja nini ...Sana Sana "amelawiti siasa" tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MTAZAMO mkuu unajitahidi sana kuonekana huna upande unaoegemea kati ya CCM NA CHADEMA lakini unashindwa, kusema hivyo sio kwamba kwa kukurupuka bali kwa kusoma machapisho yako mengi tu humu na,kwa kweli kabisa huwa unaegemea ccm japo huwa unajitanabaisha kuwa huna upande.
 
Ushauri Mzuri Mkuu, ingawa hukuwahi kuwapa CCM wakati wanamkejeli..
Makonda, Polepole, Msukuma..nk Walivuka mipaka Walitukana kabisa..
Jiwe angepata heshima kubwa sana kama angetupilia mbali Maombi ya EL kurejea CCM ..
Chadema haijaathiriwa kuondoka kwa EL ila CCM ndiyo wanaaminisha hivyo..
Kuondoka kwa Dr. Slaa Kuliathiri CDM lakini si EL..
2020
Wanasema siasa hazina adui wa kudumu, lakini sikutegemea kama CCM wangeupokea huu mzigo. Lowasa ni kati ya waliofanya CCM ichukiwe sana. Nakubaliana na wewe, Jiwe hakufanya uamuzi sahihi kuungana tena na hili zigo.
 
MTAZAMO mkuu unajitahidi sana kuonekana huna upande unaoegemea kati ya CCM NA CHADEMA lakini unashindwa, kusema hivyo sio kwamba kwa kukurupuka bali kwa kusoma machapisho yako mengi tu humu na,kwa kweli kabisa huwa unaegemea ccm japo huwa unajitanabaisha kuwa huna upande.

Tena ccm yenyewe anaiegemea kisa ana hasira na cdm kwa Slaa kutokupewa nafasi ya kugombea urais. Ni kweli Slaa ndio alipaswa kuwa chaguo sahihi la urais kwa tiketi ya cdm hiyo 2015, lakini huo ndio uchafu wa siasa kwani hata yeye alipokuwa katibu mkuu kuna walioenguliwa kwa hila.
 
Wanasema siasa hazina adui wa kudumu, lakini sikutegemea kama CCM wangeupokea huu mzigo. Lowasa ni kati ya waliofanya CCM ichukiwe sana. Nakubaliana na wewe, Jiwe hakufanya uamuzi sahihi kuungana tena na hili zigo.
Jiwe hana ujanja wa kuwakataa kina Lowassa kwani hao kina Lowassa walikuwa wanapata madaraka kwa wizi wa kura, na jiwe naye anatumia njia hiyo hiyo tena kwa ukatili wa wazi, sasa atawaambia nini hao kina Lowassa. Mtu msafi hujitenga na wachafu na sio kinyume chake.
 
Ngoja waendelee kumchezea Lowassa halafu alipuke hasira za kimasai atoe flash yenye siri zote za chadema aduplicate flash nyingi aitishe press conference halafu amwage kwa waandishi wa Habari siri zote na awagawie Kila Mwandishi flash yake yenye siri zote za chadema ndipo vichwa vyao vitakaa sawa
He anazo CD ngapi kuliko Slaa?? wewe kichwa chako kizito kutunza kumbukumbu zako mwenyewe. Tangu ahamie Chadema ulikuwa unatuaminisha hana lolote na krshazeeka na ni fisadi aliemkimbia Simba the Koroshow man, Leo karudi huko huko kwenu ghafla akawa na ujana na nguvu kiasi hicho?? Kweli sifa ya kwanza ya mashabiki mfano wako ni unafiki
unafiki
 
Back
Top Bottom