CHADEMA mtafukuza Wabunge na Madiwani wengi kwa kusifia utendaji wa Serikali ya awamu ya Tano

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya Madiwani wa CHADEMA kata za Kimandolu na Terrat, Mkoa wa Arusha kulimwa Barua eti kutokana na kuisifia Serikali kwa kuwaletea maendeleo katika Kata zao. Huu ni msiba mkubwa hasa kwa chama kinachojinasibu kuwa ni cha kidemokrasia na kinahamasisha mshikamano badala ya utengano

Kwanza niwaambie CHADEMA kuwa walichofanya Madiwani hao ni kueleza hisia zao hasa wakiangalia jinsi Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli inavyopeleka maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa. Hao walioisifia Serikali ni Madiwani wa CHADEMA ambao kwa dhati ya nyoyo zao wanakiri kuwa CCM imeboresha mambo mengi katika maeneo yao.

Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa wawakilishi wa Wananchi wa CHADEMA kuisifia Serikali ya Rais Magufuli. Joshua Nassari alishatangulia ijapokuwa hakulimwa Barua.

Kwa mwendo huu, kuna dalili kwa CHADEMA kufukuza wengi kwani kadri tutakavyoelekea 2020, Wabunge na Madiwani watashindwa kuficha hisia zao na hivyo kujikuta wanaisifia Serikali.
 
Mbona husemi ya Humphrey Polepole kutaka Nape atimuliwe ccm kwa kusema amekitoa chama shimoni..?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nape atajifukuza mwenyewe kama alivyofanya fisadi Lowasa
Tafadhali naomba usitumie neon fisadi maana mmeshindwa kuthibitisha na hata mmeombwa mmpeleke mahakamani mmeogopa. Mafisadi wapo hukohuko ccm.
 
Sophia Simba vipi? Ungefaa sana kuchukua nafasi yake kuanzia kule UWT na hata Ubunge .......
 
Back
Top Bottom