Tumesikia viongozi wa CHADEMA wakilalamika tangu kiongozi wa chama chao alipopigwa risasi hakuna mtu yeyote mpaka leo hii aliekamatwa na polisi kuhusiana na tukio hilo la shambulizi.
Hapa kidogo inatia ukakasi, polisi wanafanya kazi yao kwa weledi mkubwa hawawezi kujikamatia tu mtu yeyote, wangefanya hivyo CHADEMA mngekua wa kwanza kusema wanakamatwa watu wasio na hatia, wa pili ingekua ile taasisi ya kutetea haki za CHADEMA Tanzania inayoongozwa na mwanamke polisi waliona suala limegubikwa na siasa.
Polisi walitaka kwenda Nairobi mheshimiwa akapaza sauti polisi wa Tanzania hawana uwezo wa kwenda kumuhoji Nairobi Hospitali, leo hii ni ajabu unaposema dereva anasumbuliwa nae pia anatakiwa kuhojiwa inashangaza unapotaka wengine wakamatwe lakini dereva hutaki nae aah hapa kidogo mjitafakari na hii siasa mbaya.
Mheshimiwa unaposema Muhimbili kuna huduma mbovu na usimamizi mbovu hapa unaendelea kujaza siasa wakati tulimuona mwenyekiti wenu wa kanda ya Pwani alilazwa pale na akasifia masuala yako na bunge.
Wewe pambana nao kimya kimya kudai haki yako kwanza mlisema hamtaki kikao na viongozi wa bunge kikao kiliitishwa Karimjee na Mbatia akahudhuria kwakuwa mlikua bado mna hasira muafaka haukufikiwa leo hii nini sasa mnalia na serikali.!