CHADEMA msipuuzie ushauri hata kama ni kutoka kwa shetani, sometimes the devils does good deeds

Ushauri kwa Pasco
Nakushauri kijana uombe kazi ya uchungaji katika kanisa la Rwakatare pale Mikocheni B; au kanisa la mzee upako pale ubungo. Ungefiti sana huko, kuliko unachokifanya sasa.

Ukipuuza ushauri huu, utakuwa kenge tu.
 
Sidhani ni sahihi kuandika vitu jumla jumla na kuona kama umejenga hoja !

Hebu eleza specifically ushauri gani ulitolewa katika maeneo hayo uliyoyataja (nimeyawekea rangi nyekundu) na uonyeshe jinsi wewe unavyouona kwamba huo ushauri ni wa maana....Halafu na sisi wengine tuta-judge au tukujibu (kwa pale tutakapoweza) kwa nini huo ushauri haukuchukuliwa..

Sio kuongea tu...ooh mlishauriwa kuhusu Ruzuku, kufukuza watu na bla bla nyingine !. Be specific !. Ukisema mlishauriwa kutomfukuza Zitto na bado mkamfukuza utaambiwa sababu !. Ukiuliza kuhusu kumfukuza Shonza utaambiwa sababu na hivyo hivyo kwa watu wengine na issues nyingine ! Lakini ukiongea jumla jumla inaonekana kama vile umengea kitu cha maana kumbe hakuna lolote !

Haiwezekani eti m-mpu-mbavu (wa-pu-mbavu) fulani wakawa wanasema kila siku (mara nyingi kwa kurudia rudia)...ooh CDM acheni kufukuza watu......halafu eti mi-puuzi mingine ije iseme...CDM mnashauriwa lakini mnakataa !. Kila issue ya kufukuzwa mwanachama au kuchukuliwa hatua za kinidhamu ina sababu zake specifically, kwa hiyo ni upuuzi kuunganisha cases zote na kutoa ushauri wa jumla na kutegemea CDM isikilize/izingatie huo upuuzi !.

Sitashangaa siku za mbeleni ukija kusema mlishariwa kuhusu ulinzi wa chama lakini mkapuuza (na hapa utakuwa ukimaanisha pamoja na vitu vingine ushauri wa kipuuzi wa Ludovick). Na mtu mwingine (especially walio wa-pu-mbavu na ambao wanasahau upesi) anaweza akaona umeongea point kweli sababu unaongea jumla jumla, lakini ukibanwa specifically utaje issue utakuta huna hoja yeyote bali, umesoma haya haya maneno yasiyo na kichwa wala miguu wanayosema akina Ludovick na Pasco to the extent ukaona kwamba ni vitu vya msingi kiasi cha wewe kuviendeleza na kumbe ni upuuzi mtupu !.

uko sahihi kabisa mkuu

kila la heri
 
......

Even the devil, sometimes does good deeds, msipuuze tena ushauri wowote!.

Asante

Nadhani Makene ametumia tafsida...kwenye maelezo yake...kwa kifupi nadhani alimaanisha....tupuuze aliyoongea/andika mleta uzi lakini tusimpuuze yeye , ukizingatia mwenendo wa mleta uzi kujihusisha na masuala ya kuumiza. rejea kauli za Kibanda. Hivyo yawezekana ana' preempt ' tukio analoliandaa huyo mtoa tahadhari....!!!

"devil does 'good' deeds as a bait for devil haters" stay away from devel
 
Nashukuru kwa kunielewa pamoja na kwamba nimetumia lugha kali kidogo !

hapana wala sio lugha kali kabisa, ya kawaida sana,

unavyoona wewe ukitaka ujibiwe vizuri lugha rahisi ni kutumia lugha kali au pole?

katika maswali yako kwenye ile thread limejibiwa lipi?

na unahisi nilichokuelewa ni kipi mpaka umeshukuru?
 
CHADEMA kila mara wanasema walianza na Mungu na watamaliza na Mungu!

Maneno hayo yananipeleka kwenye hoja yako katika sentensi uliyoandika ambayo inasomeka,

Hoja yangu hapa ni kuwa, kwa nini huyu mungu wa CHADEMA anapenda chama kiendelee kuwa ni chama cha upinzani miaka yote!.

Huyu mungu wa CHADEMA kama angekuwa ni Mungu tunayemfahamu na kumsujudu, mwenye uwezo wote basi CHADEMA kwa sasa ingekuwa madarakani. Katika miaka zaidi ya ishirini kwenye ulingo wa siasa, CHADEMA ina wabunge kama 48 kati ya wabunge 357. CHADEMA kina madiwani kama 326 kati ya 3,335.

Huyu mungu wa CHADEMA lazima atakuwa ni shetani wanayedhani ni Malaika.

Sisi wanaCCM tunaomba waendelee kuwa na huyu mungu wao wanayedhani ni Mungu huku wakidharau maneno ya Maraika wa Mwenyezi Mungu.

Kura zinaibiwa bhana, hli mbona huliongelei? Hata wewe unajua. Hata JK kuwa rais, kura zimeibiwa, na najua utabisha pia
 
Your Problems will Keep on worsening simply bcoz ya unafiq wako.
Take it from me.
How does that concern you?? hujajua unafiki ni sifa?? uko wapi wewe?

mimi ni bonge la mnafiki...juzi nilisema chadema wazuri leo ninasema ni vimeo......is that so??
 
How does that concern you?? hujajua unafiki ni sifa?? uko wapi wewe?

mimi ni bonge la mnafiki...juzi nilisema chadema wazuri leo ninasema ni vimeo......is that so??

The same concern you had regarding JF members joined prior to 2010, i had also but in a bit different way.
Mie nilidhan sie Ma Senior tulio join kabla ya 2010 hatunaga unafiq, sasa kusikia kuna mnao ji Proud kabisa na unafiq ina shangaza sana.
Ni Sheeeeeeedah kwa kweli
 
The same concern you had regarding JF members joined prior to 2010, i had also but in a bit different way.
Mie nilidhan sie Ma Senior tulio join kabla ya 2010 hatunaga unafiq, sasa kusikia kuna mnao ji Proud kabisa na unafiq ina shangaza sana.
Ni Sheeeeeeedah kwa kweli

wewe usijibizane na mnafiki bana, sio vizuri ushauri tu
 
hapana wala sio lugha kali kabisa, ya kawaida sana,

unavyoona wewe ukitaka ujibiwe vizuri lugha rahisi ni kutumia lugha kali au pole?

katika maswali yako kwenye ile thread limejibiwa lipi?

na unahisi nilichokuelewa ni kipi mpaka umeshukuru?

Hao unaojibishana nao siyo wa caliber yako, hawawezi kukuelewa.
 
Wanabodi,
Chadema kimekuwa kikishauriwa mambo mengi humu jukwaani, ila kimekuwa kichwa ngumu kupokea baadhi ya ushauri, kwa hoja kuwa unatoka kwa watu wasiokitakia mema, na wengine kufikia kiwango cha kuwaona kama ni shetani!.

Msemaji wa Chadema
Tumaini Makene akakiri wazi kuwa Chadema inapuuza kila ushuri kwa watu ambao sio inside Chadema. Kuna akina sisi tusio vyama pia tumeshauri sana, tumepuuzwa, tunaisubiria post-2015 tuje tukumbushane humu tulishauri nini, tukajibiwa nini na matokeo ni nini!.

Lengo la uzi huu ni kuwakumbusha tuu Chadema kuwa ushauri ni ushauri tuu, sio lazima waufuate ila kama chama makini, wanapaswa wausikilize!, wauzingatie! waupime! kama ni wa maana waufuate, kama ni hovyo ndipo waupuuzie!, hata kama ushauri huo unatoka kwa shetani!.

Thanks.

Pasco

@Pasco

I used to respect you like a matured big brother, though i started to doubt your capacity of thinking for being the LIKES "king giver", You give "likes" even on Injudicious which cannot ring a bell in the smart upstairs, no wonder you even spend time to think and like the work of your crony now by the name Angel without creaking your mind that this you call angle now cannot deserve that bonnet!

I know you have the right to collect and connect the dots, but sorry to say, this shit is too low for you to comprehend the logic you are trying to drive. Otherwise i will think you are birds of a feathers flocking together.

Should i expect white from charcoal?! Ghoosh..
- Kaka this is just out of the planet sio rahisi sana siku hizi kuona mawe mazito kama haya JF I dont care the message I like the words used, unatisha mkuu!!

Le Mutuz
Thank you Mohammed mtoi hapo umemaliza.. Pasco Ni gamba tu

Ni muendelezo tuu wa kumkumbuka Kamanda Mohamed Mtoi aliwahi kuniambia nini!.

RIP Kamanda Mohamedi Mtoi!.

Pasco
 
Wanabodi,
Chadema kimekuwa kikishauriwa mambo mengi humu jukwaani, ila kimekuwa kichwa ngumu kupokea baadhi ya ushauri, kwa hoja kuwa unatoka kwa watu wasiokitakia mema, na wengine kufikia kiwango cha kuwaona kama ni shetani!.

Msemaji wa Chadema Tumaini Makene akakiri wazi kuwa Chadema inapuuza kila ushuri kwa watu ambao sio inside Chadema. Kuna akina sisi tusio vyama pia tumeshauri sana, tumepuuzwa, tunaisubiria post-2015 tuje tukumbushane humu tulishauri nini, tukajibiwa nini na matokeo ni nini!.

Lengo la uzi huu ni kuwakumbusha tuu Chadema kuwa ushauri ni ushauri tuu, sio lazima waufuate ila kama chama makini, wanapaswa wausikilize!, wauzingatie! waupime! kama ni wa maana waufuate, kama ni hovyo ndipo waupuuzie!, hata kama ushauri huo unatoka kwa shetani!.
Ni katika kukumbushana tuu kuhusu kupokea ushauri.
Huu ni ushauri mwingine wa bure
Handling of Serious Security Issues: Kama Chadema Takes Things For ...
Paskali
 
Mkuu yanayoendelea kuna 'state of denial' kwamba hawaamini kuna tatizo.
Katika matibabu, mgonjwa akiwa katika state of denial ni ngumu kwa tiba na huishia pabaya

Laiti wangekuwa na mfumo imara wa uongozi uliojengwa katika mazingira halali, hii isingekuwa hoja na mahasimu wasingeweza kuwahujumu, wangekuwa na agenda ya kupambana na matatizo ya nje ya kujenga mazingira huru na sawa katika sanduku la kura

Kilichofanyika jana ni busara mbovu. Kwamba ni busara yenye ubovu kwasababu imefunika matatizo haikuondoa matatizo. Ili kuwa na busara njema, lazima waende katika mzizi wa tatizo

1. Wakubali kuna tatizo linalohitaji suluhu ya kudumu na si dawa ya kutuliza maumivu

2. Wasikilize hoja wasizotaka kuzisikia ili kuelewa, grievance, grudge, concern and reservations zinazosababisha tatizo kujirudia

3. Watengeneze mazingira ambayo mtu atakaposhindwa kuyafuata hakuna vikao vya masaa mengi bila kujali wanahitaji masaa mengi kuhangaika na mfumo unaowanyima haki

Ni lazima wawe na uongozi legit ukiwa na mandate na support ya kila mmoja
Mkuu Nguruvi3, asante kwa hii, kwanza ningekuomba upandishe uzi mahsus wa ushauri kwa Chadema, baada ya kilichotokea jana, uamuzi wa Kamati Kuu kuwasamehe ushauri huu ni ushauri mzuri kwa Chadema, nazidi kuwasisitizia Chadema wasikatae ushauri, na naamini kama Chadema wangekuwa makini kupokea ushauri unaotolewa humu jf, ambako ni nje ya box, saa hizi, wasingefikia hapa walipofika.

P
 
Back
Top Bottom