PreGE2025 CHADEMA Msimbazi yamtaka Patrick Asenga ajieleze kwa kupinga Agenda ya 'No Reforms, No Election' mtandaoni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tawi la Msimbazi (maarufu Msimbazi Mama) kimemtaka mqanachama wa Chama hicho, Patrick John Asenga kuwasilisha barua ya kujieleza kufuatia taarifa mbalimbali ambazo Mwanachama huyo amezitoa kwenye mitandao ya kijamii akionesha kwenda kinyume na msimamo na agenda ya chama hicho ya NO REFORMS NO ELECTION.

Soma: Waraka wa wagombea 2020 na watia nia wa ubunge 55 wa CHADEMA. Wapinga chama kususia uchaguzi mkuu

Waraka wa CHADEMA tawi la Msimbazi uliotolewa leo Aprili 5, 2025 kwenda kwa Mwanachama huyo mwenye kadi No. CDME11126 ya tarehe 22/06/2021 ambayo ni kadi mpya ya kidijitali umemtaka kujieleza kwa maandishi ndani ya siku 14 kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na kwenda kinyume na msimamo wa vikao vya chama ambavyo ni pamoja na Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.

IMG_3879.jpeg
 
Ukiona kitu cha Chadema , CCM wanakishabikia na kukibebea mabango ujue wanufaika ni CCM.

Tangu kauli ya Nchimbi kuhusu no reform no election ndio hili kundi sasa limeibuka kwa nguvu .

Haina tofauti kama CCM ilivyokuwa ikimpigia upatu Mbowe huku na Abdul nae akipenyeza rushwa kwa kina Wenje.
 
Msilaumu watu wenye mawazo tofauti na Lissu, jiulizeni mmekosea wapi, sio kila mtu ni pandikizi

Acha kumsingizia Lissu No Reforms ni ya CHADEMA baada ya kupitishwa na vikao vyote vya chama.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tawi la Msimbazi (maarufu Msimbazi Mama) kimemtaka mqanachama wa Chama hicho, Patrick John Asenga kuwasilisha barua ya kujieleza kufuatia taarifa mbalimbali ambazo Mwanachama huyo amezitoa kwenye mitandao ya kijamii akionesha kwenda kinyume na msimamo na agenda ya chama hicho ya NO REFORMS NO ELECTION.

Soma: Waraka wa wagombea 2020 na watia nia wa ubunge 55 wa CHADEMA. Wapinga chama kususia uchaguzi mkuu

Waraka wa CHADEMA tawi la Msimbazi uliotolewa leo Aprili 5, 2025 kwenda kwa Mwanachama huyo mwenye kadi No. CDME11126 ya tarehe 22/06/2021 ambayo ni kadi mpya ya kidijitali umemtaka kujieleza kwa maandishi ndani ya siku 14 kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na kwenda kinyume na msimamo wa vikao vya chama ambavyo ni pamoja na Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.

View attachment 3294345
Hawa kina Asenga,John Mrema na Wakili msomi John Mallya ndiyo wanafanya ionekane kumbe kweli Chadema kilikuwa chama cha Wachaga maana kuondoka kwa Mbowe kwenye uenyekiti imewauma sana,haiwezekani watu walioshiriki kupitisha Azimio la No Reforms No Election chini ya Mbowe leo waone halifai chini ya uongozi wa Lissu.
 
Msilaumu watu wenye mawazo tofauti na Lissu, jiulizeni mmekosea wapi, sio kila mtu ni pandikizi
Hivi waliomfukuza yule mchungaji Arusha kwa kuhoji uhalali wa uteuzi wa mgombea urais CCM pale Dodoma siku ya kikao walikuwa akina nani.

Je hujui orodha ya wana ccm waliofukuzwa kutokana na kwenda kinyume na misimamo au taratibu za chama? Au wewe siyo mwanasiasa.

Kwa sasa vijana wenye akili timamu wapo ingawa ni wachache na hawayumbishwi na akili za kushikiwa.
 
Spearhead ni Lissu mkuu! Hata leo Mwenyekiti wa chama(Lissu) ametengua uteuzi wa CPA Ruge.
Ni kawaida, hata Marekan ,kinachofanya chama Cha Republican , ni TRUMP ndio anafanya.

Nadhan ni jambo jema Kwa Jambo zuri linapofanyika, sifa uende Kwa Kiongozi anayesimamia.

Waweza jiuliza, kwann wanaopinga NORENE ni wafuasi wa Mbowe?? Kwann hawakupinga wakati wa Mbowe??.
 
Hivi waliomfukuza yule mchungaji Arusha kwa kuhoji uhalali wa uteuzi wa mgombea urais CCM pale Dodoma siku ya kikao walikuwa akina nani.

Je hujui orodha ya wana ccm waliofukuzwa kutokana na kwenda kinyume na misimamo au taratibu za chama? Au wewe siyo mwanasiasa.

Kwa sasa vijana wenye akili timamu wapo ingawa ni wachache na hawayumbishwi na akili za kushikiwa.
Two wrongs don't make it perfect
 
Back
Top Bottom