CHADEMA msiige Tembo

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Napenda kutoa onyo kwa Chadema ,msijaribu kabisa kuiga mambu ya CUF ,na ikiwa mnataka kufanya wayafanyayo CUF basi tafuteni ushauri kutoka kwao ,CUF walipoamua kufanya mambu hayo ilikuwa hakuna hawaitambui serikali na pia wawakilishi wao walikuwa hawaendi kwenye vikao na kubwa zaidi hawamtambui hata Raisi .

Huku nyinyi mnaitambua serikali kwa hivyo ni lazima mufuate vile serikali inavyowataka ,sasa ikiwa mnataka kufanya mambo yenu bila ya kuifuata serikali basi ikataeni serikali na pia mumkatae raisi kama ndie mshindi halali na Raisi wa Tanzania,timizeni hayo kwanza hapo mtakuwa na nguvu kuandaa kila kitu.

Chadema wacheni mara moja kuwasukumiza wananchi katika vyombo vya dola wakati na vigogo na wabunge wenu wanaitambua serikali kuwa ipo kisheria.
 
upupu mtupu. Cuf ni tembo au wale wale. Chadema nguvu ya umma we wa wapi?
 
Inategemea na mtazamo wako kama watu au viatu,hayo ni wewe na akili yako inavyokutuma.
Kwa nionavyo Chadema bado wapo nyuma sana katika kufanya siasa zenye msimamo ukilinganisha na wenzao CUF ,ambao naweza kusema ni wazee wa upinzani ,wazoefu ,wenye kupanga yakapangika,CUF wakisema wanafanya maandamano basi wanafanya na mkutano unafanywa kwa ufupi lengo linafikiwa. Sasa nini lengo la Chadema katika vurugu za Arusha ,Je lengo lilifikiwa ?

Kwa uzoefu wangu wa siasa za mapambano Chadema wamefanikiwa katika kuipaka matope serikali ya Kikwete ,ila sidhani kama hilo ndio lengo lao ,Chadema wanapigania umeya ,nchi ina mikoa mingapi ,mnaenda kuulisha watu kwa sababu za kiti cha umeya ,sijui mmepaona hapo penye uzezeta wa Chadema ?
 
Inategemea na mtazamo wako kama watu au viatu,hayo ni wewe na akili yako inavyokutuma.
Kwa nionavyo Chadema bado wapo nyuma sana katika kufanya siasa zenye msimamo ukilinganisha na wenzao CUF ,ambao naweza kusema ni wazee wa upinzani ,wazoefu ,wenye kupanga yakapangika,CUF wakisema wanafanya maandamano basi wanafanya na mkutano unafanywa kwa ufupi lengo linafikiwa. Sasa nini lengo la Chadema katika vurugu za Arusha ,Je lengo lilifikiwa ?

Kwa uzoefu wangu wa siasa za mapambano Chadema wamefanikiwa katika kuipaka matope serikali ya Kikwete ,ila sidhani kama hilo ndio lengo lao ,Chadema wanapigania umeya ,nchi ina mikoa mingapi ,mnaenda kuulisha watu kwa sababu za kiti cha umeya ,sijui mmepaona hapo penye uzezeta wa Chadema ?

cuf ndo nyie nyie ccm b kwa hiyo unaunga mkono ccm kuchakachua umeya?
 
Mwiba naona wewe ni mwanasiasa tu !. CCM ni lazima ielewe huwezi kuzuia uhuru wa kuandamana bila kuwa na sababu ya msingi!. Vilevile ni lazima CCM waelewe nchi imebadilika na hairudi nyuma na badala ya kutafuta njia za kuizua Chadema ni bora mtumie huo muda kuleta maendeleo. Upinzania uliopo si wa Chadema bali ni wa watu hivyo kama unataka kulaumu basi laumu Watanzania wote?. Watu wamechoka umasikini na unyanyasaji hivyo huwezi kuzuia hivi vitu kwa maticho tena!. Zamani ilikuwa inawezekama ku control vyombo vya habari na sasa haiwezekani tena kwasababu kila kitu kina muda. Hivyo ni lazima muelewe muda wa kunyanyasa watu na kutishia watu umepitwa na dawa ya utawala ni maendeleo na si kupigana na Chadema. Chadema mnazidi kuwapa umashuhuri tu bila kujua.
 
Kwenye patashika za Arusha nawalaumu viongozi wa ngazi za juu wa Chadema kwa kushiriki katika vurugu za Arusha.
Vurugu ambazo ni za kuwania kiti cha Umeya ni aibu kubwa sana kuoneka viongozi wa juu kabisa wa Chadema kushiriki katika kugombea kiti cha Umeya tena ni aibu ,hili halina mbadala.

Viongozi hawa walikuwa waonekane katika valangati za kitaifa na pia wasiwe mstari wa mbele ,jamani mkuu wa majeshi haongozi vita au hili WaChadema hawalijui ? Inakuwaje Mbowe ,Slaa wawepo mbele tena kwenye vurugu za Umeya ,hili ni kosa kubwa sana na itabidi wapangaji mufikirie ,kasheshe za aina hii wanakwenda mgambu tu sio wakuu wa mapambano ,yaani kama Serikali ingekuwa na nia mbaya ingeweza kuwamaliza hapohapo akina Mbowe na Slaa ,nia ambayo ilikusudiwa kufanyiwa viongozi wa CUF kule Pemba na Unguja,ubaya mtupu lakini hapa inaonekana damu nzito .

Hivyo napendelea kusema kuwa uongozi umefanya kosa kubwa sana katika kujitokeza na kuwepo mstari wa mbele zaidi ukihusisha ugombezi wa Umeya.Kwani mapambano bado ndio yapo katika stage za mwanzo mwanzo kabisa ,mapambano sio kugombania kiti cha umeya mapambano ni kuing'oa CCM katika uongozi ,CUF wamefanikiwa kuiong'oa nusu na 2015 wanaiweka upande kabisa na kuitoa nje.
 
mimi naamini chadema ni wanasiasa zaidi ya cuf. lkn wasiwasi wangu kwamba watu tz bara kama wanaweza mapambano ya kudumu kama wapemba
WaTanganyika ni woga ile mbaya ,vita vya Uganda WaPemba ndio waliokuwa mstari wa mbele.Kama si WaZanzibari vita ile tungepoteza.
 
mimi naamini chadema ni wanasiasa zaidi ya cuf. lkn wasiwasi wangu kwamba watu tz bara kama wanaweza mapambano ya kudumu kama wapemba

Ninakuhakikishia zipo sehemu zinaweza kuliko Wapemba mara tano, ila si zote! Kwa mfano hutegemei mapambano yatokee Tanga! Lakini Arusha yawezekana, Mara yawezekana, Kilimanjaro shemu kadhaa yawezekana, Mwanza imeamka, Mbeya wanaamka, wanatoka, Iringa wanapiga mswaki na kunyoa ndevu, nk. Watu wasifanye mchezo. Nguvu ya umma siyo lelemama.
 
Ningependa kuuliza kwa wanaJF wakubwa kwa wadogo waume na wake vijana na watoto ,hivi inakuwaje kumezuka watu humu JF ambao inaonekana kuwa ni wapenzi wa Chama Cha Chadema.Watu hawa wanakuwa na majibu ya matusi au ni lazima waandike matusi ,je hivi ndivyo Chadema ilivyo na ndio wanachama wake wanakuwa na midomo iliyojaa matusi.

Ingawa ukitazama watu hawa utaona hawazidi hata mwaka tangu wajiunge hapa JF ,wamezuka kama uyoga ,wao akili zao zinawatuma kuitetea Chama chao cha chedema kwa matusi au sijui tuseme ndio urithi wamerithi kwa wazazi wao au ukoo wao mzima.Kwani mambo mengine huwa ni ya kurithi na ndugu zetu hawa inaoeneka wanafuata wazazi wao,ingawa mimi siwaoni tenaa watu wa ajabu zaidi ya kuona ni tabia walizolelewa nazo lakini kama binadamu inabidi tukumbushane kuwa hapa sio pahala pa kutoa matusi ,mtu na matuzi yake abaki nayo hukohuko kwa wazazi wake.
 
hebu nendeni mkakojoe nyinyi chadema sisi hatutaki umwagaji damu na uishie hukohuko kwenu!
 
Huyu mwiba siku za mwanzo naingia jf nlkuwa namheshimu sana, najilaumu sn kuweka imani yng juu ya mtu hopeless!
Kwanini mtu mkongwe ktk majamvi unakosa busara hata ile ya abc?...you sound a nursery school pup!
Umeambiwa na nan kuwa walikuja kugombea umeya we mwanazayuni? Unachokiona wewe kuwa kiko wrong hapa nchin ni umeya wa Arusha tu?...spoonfed you rascal!
 
Du kumbe hata historia huijui!!

Hitoria gani na huo ndio ukweli.nakumbuka kama leo nilikuwa kwenye redio ,nipo juu ya mti majeshi ya uganda yanapita chini baada ya kukatiza tu nikatoa data kwenye kikosi cha mizinga na hapo ndipo tulipoweza kusonga mbele na yapo mengi tu,ila wenzetu ni woga ile balaa !
 
nijuavyo hao cuf ndio waliochemka vibaya, tena vibaya sana. labda mwanakijiji atafafanua zaidi. miye kuchambua mambo ya siasa si mjuzi sana
 
CUF bara/zanzibar = CCMB.

Evidence based politics: Uchaguzi wa meya Mwanza juzijuzi, wadiwani wawili na pekee wa CUF Mwanza waliorewa na CCM na kuiongezea CCM kura mbili pamoja na kwamba kula hizo za ziada hazikufua madafu.
 
Back
Top Bottom