CHADEMA mnayo nafasi ya kusimama tena kabla ya 2025, ila zingatieni haya...

Kasanzu The Great

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
309
222
Kwa hali Kisiasa ilivyo, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kinatakiwa kifanye Mambo yafuatayo ili kiweze KUSIMAMA na kurejesha ushawishi wake Kama ilivyokuwa kabla 2015.

1. Achaneni na Magufuli

Ukifuatilia hotuba zako nyingi nikama Magufuli Yuko Madarakani. Agenda za mikutano yao imebeba "dhihaka" na kejeli dhidi ya Magufuli. Wanatakiwa wajue kwamba ni vigumh sana kupambana na mtu aliyekufa halafu ukashinda.

Inaonekana nikama walishajua kwamba kumtukana Magufuli kutaifurqhisha dola na kuwaacha wafanye mikutano yao bila "bughudha" lakini wanafanya harakati zao ziwe ziwe ngumu kueleweka.

2. Wamkabili Samia
Ukweli nikwamba CHADEMA hawataki kumuudhi Samia kwasasa ndio maana wanazunguka na kumung'unya Maneno. Ukifuatilia hotuba zao pamoja na mitandao ya kijamii Kila mtu atakubaliana namimi kwamba wanamuogopa Samia kumsema waziwazi. Yawezekana pengine wanahisi mikutano yao itazuiwa, wanavizia kuitwa Ikulu, au wanaona watazua upinzani wa kidola au ni mbinu ya kumfanya abweteke ili baadaye wake kumuattack akiwa na makosa mengi. Kitendo Cha kuendelea kuwa kuwa washangiliaji wa Samia watajikuta wanashindwa kuwarejesha wafuasi wao.

3. Waweke Mikakati yao Kanda ya Ziwa
Sio Siri kwamba baada ya Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa iliwapa sapoti kubwa. Kwasasa wawekeze nguvu huko bila shaka wataitikisa nchi. Kanda ya Ziwa kwasasa wanahisi Kama vile wameporwa mtu wao, Wanamsiba, wanamashaka Kama watatimiziwa matarajio yao. Ukipita kwenye mitaa ya Bukoba, Mwanza, Bariadi, Nzega, Tabora, Bunda, Musoma au Shinyanga utakubaliana namimi kwamba wananchi wanawasiwasi mkubwa. CHADEMA waondoe zile dhana za ukabila wawaone watu wa Kanda ya Ziwa Kama ndugu zao. Kwasasa Kuna dhana Kichwani mwa watu wa CHADEMA Kama vile watu wa Kanda ya Ziwa ni adui zao ndio maana Kila Jambo linalohusu maendeleo ya Kanda hii wanapinga nk.

4. Watambue kuwa Samia hana watu
Samia hana eneo analokubalika zaidi ya turufu ya CCM hata huko Zanzibar mizania ya kisiasa ikiwekwa sawa anaweza kupata Kura chache. Hii kwao ni fursa wakiamua kutimia akili. CCM haiko kitu kimoja Kama ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita. Uwezekano wa Kura za wanaccm kugawanyika ni mkubwa sana.

5. Wawasamehe wale wabunge 19
Ile time ya wabunge 19 inao uzoefu mkubwa kwenye harakati hizi ngumu. Ikiachiwa ikarudi kwenye chama itaongeza nguvu, itatumia mtaji wake kuandaa majimbo ambako 2025 majimbo mengi yatakuwa tayari yako CHADEMA. MFANO

Nusrat Hanje anaweza kuandaliwa kwenda Kigamboni

Ester Matiko - Tarime
Ester Bulaya - Bunda
Halima Mdee - Kawe nk.

Itasaidia kukusanya nguvu kutokea Bungeni na kuchagiza Harakati hizi.

Mwisho, ni Bora kusahau yaliyotokea na kuukabili ukweli wa Sasa. Kuna upepo mzuri wa kupita nao lakini tunaukataa na kutaka kupambana na Jana. Tuchukue hatua.

Kamanda Maganga
 
Chadema isingekuwa na ushawishi usingetumia muda wako kupandisha uzi hapa.

Chadema hakijawahi kushuka ushawshi tangu kisajiliwe. Wenye chama wanajua na hata Ndugai anajua fika.
 
Hiyo namba 5, ni upuuzi kwa mtu anayejifanya anaipenda CHADEMA kuiandika.

CHADEMA imekuwa ikizalisha viongozi makini toka kuundwa kwake.

Kila mtu ndani ya CHADEMA ni mzoefu na anaweza kugombea ubunge akashinda popote pale.
 
Namba 4 umeenda chaka, Samia anaungwa mkono na wanawake wengi(kama sio wote)pamoja na waislam wengi (nafikiri unawajua hawa jamaa walivyo wabaguzi libapokuja swala la mtu wa dini yao), kundi lingine ni wale wapenzi wa CCM kindakindaki, wao huwaambii kitu linapokuja suala la chama chao.
 
Nimekuelewa baadhi ya maeneo mengine nimekuelewa nusu, ila kwenye kusamehe wabunge 19 bila wao kuomba msamaha public ndio umekosea kabisa, hao vikaragosi 19 hawana lolote kama wanajiamini wako vizuri waende TLP au Chaumma wakaimarishe hivyo vyama.

- Chadema kuweka mkakati kanda ya Ziwa walishaweka siku nyingi operation Sangara ni mfano, kinachotakiwa sasa ni kuihuisha tu, ndio maana sasa mwenyekiti anazunguka mikoa hiyo kuwaamsha.

- Kuhusu kumkabili mama ameshaanza kukabiliwa muda tu, issue ya Katiba Mpya ilikuwa ni mwanzo wa kuonesha Chadema wako serious na ndio maana wamesema hawatashiriki uchaguzi wowote chini ya hii Tume iliyopo, unaposema waanze kumkabili mama nakuona wewe ndio uko nje ya muda.

- Kuachana na Magufuli hiyo nimegundua haiwezi kuondoka kwa dakika moja, mengi aliyofanya Magufuli muendelezo wake bado upo mpaka sasa.

Mfano. Uminywaji wa demokrasia (mkutano wa Mbowe Shinyanga kuzuiwa na polisi), hii ni tabia iliyorithiwa toka kwa Magufuli, haki za binadamu kuminywa (mf. utekaji uliotokea juzi maafisa wawili waliokuwa wakipigania Katiba Mpya).

Hapo utaona Magufuli ameacha cancer ya aina fulani ambayo itachukua muda kuondoka kwenye taifa letu, haitakuwa issue ya muda fupi, hivyo kuendelea kusemwa Magufuli kutaondoka taratibu pale hizo tabia zake zitapoisha.
 
Ndo Maana akitokea "Mwendawazimu" yeyote atakaye iidanganya "kuiua" Chadema ni dhahiri yeye ndo ataondoka kwani, kwasasa CDM ndo tumaini pekee kwa Watanzania wengi.
 
Naona huyu ni wale kambi ya Mwendazake, maji ya shingo. Ushauri wako wapelekee CCM. Ambao nao hawataki ubaguzi wa mwendazake watajirekebisha na kuleta umoja wa kitaifa na kuachana na ukabila na ukanda ulioletwa na mwendazake.
 
Chadema iko vizuri na itaendelea kuwa vizuri sana jinsi siku zinavyosonga.
 
Kumkabili Samia kwa nguvu nisingeshauri manake anaweza kugeuka MAGUFULI wa siku hizi.
 
Kwa sasa dai kuu la nchi yetu ni Katiba Mpya & Tume huru ya Uchaguzi - hayo mengine ya kuchaguana kwa kutumia tume ya uchaguzi ya CCM fanyeni nyie wana Lumumba na magenge yenu...!!

Na yeyote atakayejaribu kukwamisha upatikanaji wa katiba yetu mpya iwe kwa makusudi ama kwa kutojua basi adhabu ya Mungu utakuwa juu yake.

Mifano hai ipo ya watu waliojifanya wao wako juu ya mawazo na mipango ya Mungu, mnajua yaliyowapata !! Mungu yupo kazini kwenye hili.
 
Back
Top Bottom