CHADEMA mnampuuza Mbowe!

CHADEMA mnampuuza Mbowe!

Mhe. Mbowe akiwa Mbeya alikiri wazi kuwa CHADEMA kwa miaka yote tangu kuanzishwa kwake kimekuwa ni chama cha HARAKATI... Lakini nilifurahi kusikia akiwaomba wenzake kuwa sasa ni wakati wa kukibadili Chama chao kutoka chama cha harakati na kuwa sasa chama cha SIASA.

Sasa ni karibu miezi mitano tangu atangaze na kuwasilisha ombi hili kwa wenzake lakini kwa masikitiko makubwa wenzake mmempuuza mwenyekiti wenu, badala ya kukibadilisha chama sasa mnakifanya cha harakati zaidi mpaka sasa mnapanga na kutekeleza kudhuru watu hasa wasiowaunga mkono.

Kumpuuza Mbowe kwenye wito wake huo ni kifo chenu na hivyo kuathirika kwa demokrasia nchini. Uwepo wenu umeleta joto zuri kwenye siasa na demokrasia nchini ukiachilia mbali vibweka vya baadhi ya viongozi wenu. Lakini nadhani sio tatizo la chama bali la viongozi wachache waliofanya CHADEMA kichaka cha kufichia rangi zao halisi.

MTAKAO CHANGIA PUNGUZENI MAPOVU NA MATUSI MJENGE HOJA.

nashukuru mungu wewe mwenyewe ndo umeanza na mapovu! Chama kipi cha kigaidi? CDM au CCM hivi ule mchezo wenu wa kuteka wagombea muda wa kurejesha fomu mmeuacha? kwa leo nijibu hilo tu then wenzangu watakuja na technic zenu nyingine za ugaidi mnaofanyia Watanzania
 
Mhe. Mbowe akiwa Mbeya alikiri wazi kuwa CHADEMA kwa miaka yote tangu kuanzishwa kwake kimekuwa ni chama cha HARAKATI... Lakini nilifurahi kusikia akiwaomba wenzake kuwa sasa ni wakati wa kukibadili Chama chao kutoka chama cha harakati na kuwa sasa chama cha SIASA.

Sasa ni karibu miezi mitano tangu atangaze na kuwasilisha ombi hili kwa wenzake lakini kwa masikitiko makubwa wenzake mmempuuza mwenyekiti wenu, badala ya kukibadilisha chama sasa mnakifanya cha harakati zaidi mpaka sasa mnapanga na kutekeleza kudhuru watu hasa wasiowaunga mkono.

Kumpuuza Mbowe kwenye wito wake huo ni kifo chenu na hivyo kuathirika kwa demokrasia nchini. Uwepo wenu umeleta joto zuri kwenye siasa na demokrasia nchini ukiachilia mbali vibweka vya baadhi ya viongozi wenu. Lakini nadhani sio tatizo la chama bali la viongozi wachache waliofanya CHADEMA kichaka cha kufichia rangi zao halisi.

MTAKAO CHANGIA PUNGUZENI MAPOVU NA MATUSI MJENGE HOJA.

Nashauri Mbowe kesha puuza tujadili

Ujangili wa Katibu Mkuu wa CCMK ama

Hatua zilizochukuliwa wa waliotumia rushwa kwenye chaguzi za CCM
 
-una audacity ipi ya kutoa ushauri kwa chadema wewe?

-kama chadema kitaathirika kwa namna yoyote kwa mujibu wa mtazamo ulioueleza si ndiyo utafurahi zaidi?next time ukiandika hapa uwe unafanya hivyo kama msomi.

-political state ya chadema kama chama cha siasa unaweza vipi kuitofautisha na political activism?unaweza vipi kui-distinguish kwa kutumia itikadi ya chama hiki?

-next time usiwe unatutia aibu vijana wenzako kwa kuandika andika tu ilimradi uonekane active.

-hizo siasa za kudhuru watu ni zipi.ni jambo la ajabu kabisa badala ya kunadi itikadi na sera za chama chako wewe unanadi udaku na majungu.ndiyo siasa mpya zilizoletwa na vijana huko kwenye chama chako?usiharibu taswira ya vijana wa taifa hili kwa uzembe na udhaifu unaouonyesha katika kuitumikia dhamana uliyopewa na chama chako

-umeachana na mradi wa kuzunguka kumtukana yule waziri mkuu aliyejiuzulu sasa unajaribu kutafuta umaarufu wa bei rahisi kupitia chadema.najua mfumo wa majimbo ni kitanzi kwenu,mna kazi ngumu sana sana.get prepared!

ben you are a thorn to nape, very good keep it up
 
-Una audacity ipi ya kutoa ushauri kwa CHADEMA wewe?

-Kama CHADEMA kitaathirika kwa namna yoyote kwa mujibu wa mtazamo ulioueleza si ndiyo utafurahi zaidi?Next time ukiandika hapa uwe unafanya hivyo kama msomi.

-Political state ya CHADEMA kama chama cha siasa unaweza vipi kuitofautisha na political activism?Unaweza vipi kui-distinguish kwa kutumia ITIKADI ya chama hiki?

-Next time usiwe unatutia aibu vijana wenzako kwa kuandika andika tu ilimradi uonekane active.

-Hizo siasa za kudhuru watu ni zipi.Ni jambo la ajabu kabisa badala ya kunadi itikadi na sera za chama chako wewe unanadi udaku na majungu.Ndiyo siasa mpya zilizoletwa na vijana huko kwenye chama chako?Usiharibu Taswira ya vijana wa taifa hili kwa uzembe na udhaifu unaouonyesha katika kuitumikia dhamana uliyopewa na chama chako

-Umeachana na mradi wa kuzunguka kumtukana yule waziri mkuu aliyejiuzulu sasa unajaribu kutafuta umaarufu wa bei rahisi kupitia CHADEMA.Najua mfumo wa majimbo ni kitanzi kwenu,mna kazi ngumu sana sana.Get prepared!
Ben mbona unatokwa povu kijana?

Relax usije ukadondosha sumu iliyoko mfukoni.

Ushauri sio lazima uufuate ila angalieni msije mkamuuzi tajiri yenu mtalala njaa
 
This is too low kwa katibu mwenezi wa chama kikubwa tena kilichopo madarakani.
Yani nimejiskia aibu utadhani mimi ndo nimeandika hii thread.
 
Ben mbona unatokwa povu kijana?

Relax usije ukadondosha sumu iliyoko mfukoni.

Ushauri sio lazima uufuate ila angalieni msije mkamuuzi tajiri yenu mtalala njaa
Desperate attention Seeker.Leo utakua overjubilant nimekupa attention na kujibu post yako.Grow up brother! Umri unasogea sana na hizi siasa unazofanya zimepitwa na wakati kwa kasi.Simply,Grow up!
 
We mwenyewe umejipuuza, ulikuwa na hoja ya ufisadi kwenye UWEKEZAJI majengo ya UVCCM, ukaongwa ukuu wa wilaya ukanyamaza-ukajipuuza, ukawa na hoja ya kujivua gamba ikakushinda-umejipuuza, wewe na Mwenyekiti wako mkasema uchaguzi wenu ndani ya chama ulikuwa wa rushwa Makamo Mwenyekiti wako Mangula akasema atawaondoa mpakaleo wanatamba-umejipuuza.
Sasa sijui unapata wapi uhalali wa kuona watu wanapuuza maneno ya Mbowe wakati wewe ni kinara wa kujipuuza.
Nakwambia CHADEMA wanaelewa vyema maneno ya Mwenyekiti wao na wanatekeleza, ndio maana wanazidi kuzindua kanda Nchi nzima, we kalaga bao!

After all, kwani aliekwambia Mbowe aliposema waache harakati wakae kiutawala, alimaanisha waacha kuteka watu inaonesha kwa akili yako unafikiri harakati ni kuteka watu, you have got a very useless brain.
 
Ben mbona unatokwa povu kijana?

Relax usije ukadondosha sumu iliyoko mfukoni.

Ushauri sio lazima uufuate ila angalieni msije mkamuuzi tajiri yenu mtalala njaa

makada wa ccm mnaotumia style hii kufanya arguments huwa mnatupa credit nyingi sana kwasababu wanachama wa ccm wenye akili timamu hawapendezwi na hukimbia ccm kwa aibu hii mnayoifanya@
 
Hasira zipi tena mimi mkongwe hapa JF kaka.

Hivi Kuna hoja gani iliyoletwa hapa zaidi ya kujaza server tu.Nasi hatuchoki kuwapa shule,tena wewe sikutegemea kukosoa kwa namna niliyofanya maana umenizidi umri.Ila siasa zako hizi ningekushauri tu brotherly,chukua likizo ujitafakari kama kweli una-fit huku JF au kwenye political landscape ya Tanzania
Najua una maana gani
Ningekuwa kamanda basi ungeniona nina busara sana .... au SIO?
 
ukiona mkuu wa ile timu ya Lumumba ameamua kuingia jamvini basi jua wazi vijana wake wameshindwa kufikia malengo.hii ni wazi kuwa malipo ya leo hayatatolewa!
Mbaya zaidi hata babalao amekuja na hoja nyepesi na inayopandisha chat ya chadema.

Hivi Nape Nnauye unaweza kukubaliana nami kuwa umeitaja chadema kuliko ulivyoitaja ccm katika kipindi cha mwezi mmoja na ushee?
 
Last edited by a moderator:
We Nape Nnauye,

Why do you give it a damn about CHADEMA NA MATAMKO YA MBOWE?

Ni kweli unataka kuona CHADEMA kikiwa Imara zaidi machoni pa watu (ndivyo mtazamo wako ulivyo kwamba kikiacha kuwa cha harakati tipo kitakuwa na kibali zaidi kwa watu)?

Never, hakuna mwanasiasa anaetaka kuona chama anachopingana nacho kinakuwa imara na kutilia umaanani ikiwa ni pamoja na kukishauri chama hicho kufanya mambo ambayo yatakuwa imara....OTHERWISE ATAKUWA NI MAMLUKI KWA KUPIGANIA UIMARA WA CHAMA ANACHOPINGANA NACHO na kwa lugha nyingine tutasema ATAKUWA KATIBU MWENEZI WA CHAMA ANACHOKIPINGA

Please give your damn time, efforts and resources kukijengea chama chako nguvu na uwezo wa kusimamia serikali katika utekelezaji wa sera na ahadi mlizoahidi kuliko kujidai kuwa katibu Mwenezi wa CHADEMA na maazimio au Matamshi ya Mwenyekiti...Au UMEKUWA KATIBU MUHTASI WA MBOWE KUKUMBUSHIA MATAMKO YAKE?

Kama mtanzania wa Kawaida nisiyependelea lichama lolote, KWA KUWA CHAMA CHAKO KIKO KINASHIKILIA DOLA, MKUMBUSHE KIKWETE NA TIMU YAKE KUTEKELEZA AHADI ALIZOTUAHIDI WATANZANIA KULIKO KUTUKUMBUSHA KAULI ZA MBOWE
 
Last edited by a moderator:
Najua una maana gani
Ningekuwa kamanda basi ungeniona nina busara sana .... au SIO?

Ukamanda ni philosophical term,kama kweli ungeweza ku-fit kifalsafa ni obvious lazima ungekua na busara.Since you're not and you'll never be as long as unaendelea kuwa na mentality hiyo hiyo kwa umri huu,then hilo ni mjadala mwingine wa kusikitisha.
 
Brother naona unatupia thread dhaifu ya upotoshaji na kupoteza muda wa watu wa kufikiri namna ya kujadili mambo ya msingi ya taifa hili

Mimi naomba nikushauri kitu kmoja, ya kwamba wewe ni kiongozi mkubwa sana katika CCM hivyo ni bora ukawa unakuja jambo ambalo watu wakichangia watakupa mawazo ya namna ya kwenda kuyatumia kuimarisha chama chako na utendaji wa serikali inayolalamikiwa sana na wananchi

Sifa yenu na kuendelea kuwepo kwenu CCM ni pale matakapoweza kutimiza ahadi zenu kwa watanzania.Kinyume chake ni kuwa umbea kama huu uliouleta hapa kwa sifa na hadhi yako ndo unaharibu kabisa

Matatizo ya nchi hii Mr Nape si CHADEMA, si Mbowe, si Dr W. P. Slaa na wala si wale wanawakosoa na kuwazomea wakati mwingine. Matatizo ya nchi yetu ni ninyi CCM na KAMWE HAMTAWEZA KUYATATUA KWA PROPAGANDA ZA KIPUUZI KAMA UNAVYOFANYA SASA......maana km kiongozi mkubwa wa ngazi ya juu wa chama km wewe unakuja na utumbo kama huu, wanachama na wafuasi wa kawaida watafanyaje sasa?...Ni wazi watatoa kucha na meno watu ambao wako kinyume nao!!!
 
Mhe. Mbowe akiwa Mbeya alikiri wazi kuwa CHADEMA kwa miaka yote tangu kuanzishwa kwake kimekuwa ni chama cha HARAKATI... Lakini nilifurahi kusikia akiwaomba wenzake kuwa sasa ni wakati wa kukibadili Chama chao kutoka chama cha harakati na kuwa sasa chama cha SIASA.

Sasa ni karibu miezi mitano tangu atangaze na kuwasilisha ombi hili kwa wenzake lakini kwa masikitiko makubwa wenzake mmempuuza mwenyekiti wenu, badala ya kukibadilisha chama sasa mnakifanya cha harakati zaidi mpaka sasa mnapanga na kutekeleza kudhuru watu hasa wasiowaunga mkono.

Kumpuuza Mbowe kwenye wito wake huo ni kifo chenu na hivyo kuathirika kwa demokrasia nchini. Uwepo wenu umeleta joto zuri kwenye siasa na demokrasia nchini ukiachilia mbali vibweka vya baadhi ya viongozi wenu. Lakini nadhani sio tatizo la chama bali la viongozi wachache waliofanya CHADEMA kichaka cha kufichia rangi zao halisi.

MTAKAO CHANGIA PUNGUZENI MAPOVU NA MATUSI MJENGE HOJA.

Samahani ndugu Nape,kwani we ni msemaji wa Mbowe?naomba jibu mkuu.
 
Back
Top Bottom