CHADEMA mnaikosea dhana ya Demokrasia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mnaikosea dhana ya Demokrasia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Nov 6, 2011.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kwanini Chadema na wafuasi wake wanataka kuwafanya wananchi waelewe kwamba suala la ‘coalition government' ni jipya na halipo katika duru za siasa ulimwenguni? Kwanini wanadanganya wananchi kwamba CUF sasa imejizika kama chama pinzani na vilivyobakia ni vingine kama Chadema, NCCR na kadhalika?

  Binafsi nilikubaliana kabisa na msimamo wa Chadema juu ya kukataa kuunda kambi ya upinzani pamoja na CUF, na sikutegemea katika watu wote, Zitto angegwaya uamuzi ule wa wenzake ‘to walk away' from the president. Lakini hili la kuendelea kuibeza CUF ionekane kama msaliti sio sawa. Ina maana ikitokea Chadema wakawa in the same position kama CUF leo hii na kupelekea CCM kuchukua uamuzi wa kuunda na serikali ya pamoja na Chadema, Chadema watakataa? Wakikataa kimsingi hii itakuwa ni usaliti kwa wapiga kura; itaonyesha jinsi gani viongozi wa chadema wana uelewa finyu juu ya demokrasia ya vyama vingi lakini vile vile uchochezi wa vurugu kwa wananchi wasioelewa.

  Ni matumaini yangu na pia ya wengine wengi pamoja na wale wenye mapenzi mema kabisa na Chadema kwamba iwapo ikitokea Chadema watafanikiwa kupata kura nyingi sana majimboni kiasi cha kuifanya CCM isiweze kuunda serikali yake yenyewe, Chadema haitasita kukubali kuunda serikali ya pamoja na CCM kama wenzao CUF walivyofanya huko Zanzibar kwani hii ni hatua kubwa sana kwa chama cha upinzani kokote kule duniani, na CUF wanastahili pongezi kwa hilo, sio kubezwa.

  Hata nchi kama Uingereza na nyingine nyingi tu zimeunda serikali ya pamoja kama ilivyo CUF. Mfano nchini uingereza serikali ya sasa inaitwa Con- Dem government; pia kuna nchi nyingi katika hali kama hiyo na bado haifanyi vyama husika kuwa wasaliti - mfano UK, Canada, Australia, Japan, Israel, Ireland, India, Finland, Belgium, Germany etc; ni muhimu kwa Chadema kurekebisha hili vinginevyo kwasababu mmeshamwaga maji – kwamba coalition government ni usaliti wa chama cha upinzani, basi itabidi muwe na uhakika wa kushinda by a big majority kwani isipotokea hivyo na kuishia kuunda serikali ya pamoja, hiyo ndio itakuwa kwaheri kwa Chadema na CUF wataonekana wa maana zaidi machoni kwa wananchi kuliko chadema.

  Kilichotokea Zanzibar is simply a coalition government because no party on its own managed to achieve a majority in the parliament na hivyo kupelekea kuundwa kwa a cabinet of a parliamentary government. Tusiwapotoshe wananchi kwani yakiwakuta haya mtakuja umbuka sana na itakuwa too late. Tupo wana CCM tunaokipenda na kuki admire Chadema especially kwa mafanikio yake na vilevile changamoto nzuri wanazotupa CCM ili tuwe na umakini zaidi katika utawala na uendeshaji uchumi.

  Tafadhali msilipoteze hilo kwani ukweli bayana ni kwamba bila Chadema Madhubuti CCM madhubuti haiwezekani.
   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Mfano wako uliotoa ni irrelevant nafikiri hujui tofauti ya uchaguzi wa Tanzania na UK, Kwa system ya UK (First-past-the-post) yaani wana viti 650 vya bunge ili chama kiunde serikali lazima kiwe na angalau viti 326, Conservative walikuwa forced kuungana na Liberal according to their system, tofauti na system yetu (simple majority) ambayo hata kama una 30% ya kura unaweza kuunda serikali.

  Muungano wa CCM na CUF ni wa hiari(kupenda) hawalazimishwi na katiba kama UK CCM-Zanzibar ingeweza kuunda serikali bila hata kuishirikisha CUF. Sielewi hiyo big majority unayoisema hadi Chadema washinde inatoka wapi au iko kwenye katiba ipi, kwa tanzania kuunda serikali hakutegemei chama kina viti vingapi vya bunge niushindi wa urais tu unao count halafu hata huo ushindi si lazima uvuke 50% labda tubadili katiba.
   
 3. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pia kwa Uk Labour walikuwa na wabunge wengi kuliko hao Liberal Democratic, sasa kwann Conservative hawakuungana na chama cha pili? Badala yake wameungana na chama cha tatu kwa viti bungeni ni kwa sababu fahari wawili hawakai zizi moja.

  SUK za wenzetu ni tofauti na za kiafrika ambazo nyingi kama sio zote zimeundwa kwasababu chama tawala kimeshindwa uchaguzi lakini kwakuwa nec za nchi hizo sio huru chama tawala kinajitangazia ushindi na hilo ndilo Chadema wanasema ni usaliti kuungana na chama ambacho hakikushinda na kura zake nyingi wamezipata isivyohalali. Ila ninauhakika kama tume itatangaza matokeo ya kura kama zilivyopigwa Chadema inaweza kuungana na chama chochote ili kuunda SUK.

  Usihamasishe kuungana hamasisha matokeo kutangazwa kama yalivyo then tufikirie kuungana kwa maslahi ya taifa sio kwa maslahi ya viongozi wa juu. SUK za mtindo huu wa kiafrika hazina tija taifa na walalahoi.
   
 4. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwanza mimi nasema dhana ya kuungana siungi mkono. Kama mgombea uraisi kashinda basi ndie atakaeapishwa kuwa raisi hakuna haja ya kuita yule aliyeshindwa na kumpa labda uwaziri mkuu ili wakale wote kuku pale ikulu.

  Mimi nionavyo wala wote wanaofanya hivyo wanakuwa wameshindwa kwa wanapora ushindi wa yule aliyeshinda kwa hiyo ili kumpoza asilete vurugu anamhonga mamlaka madogo. Hiyo si sawa hata kidogo........
   
 5. W

  Wamtaa huu Senior Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Feedback,Zanzibar ilifanya mabadiliko ya katiba kabla ya uchaguzi mkuu uliopita.Is it that hayo mabadiliko hayakusema kitu kuhusu mgawanyo wa madaraka baada ya uchaguzi?Nachelea kuamini kuwa SUK Zanzibar siyo ya kikatiba.Naomba kueleweshwa zaidi.Respect mkuu...!
   
 6. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Serikali nyingi za kitaifa katika mataifa ya Afrika hazipo kikatiba bali zinakuja ili kukabiliana na hali halisi iliyojitokeza mara nyingi ikiwa ni chama tawala kugoma kuachia madaraka.

  Kenya Kibaki alijitangazia uhindi wenye utata, watu walikufa baadae ikaonekana suluhisho ni SUK. Hili halipo kwenye katiba ya Kenya lakini kwa kuwa chama cha Kibaki hakipo tayari kuachia ngazi ikalazimika hali iliyojitokeza.

  Zanzibar kwa muongo mmoja CCM wanashinda baada ya viongozi kutoka bara kwenda kushinikiza matokeo yatangazwe kwa mtazamo wao. CCM walishaliona hili na walijua hawana dawa nalo japokuwa ipo kikatiba lakini ilikuwa ni lazima serikali hiyo iongozwe na CCM na si CUF. Bila kujia impact hiyo CUF imepoteza umaarufu mara dufu. Hata mimi nasema wazi ikiwa matokeo ya kura yatakuwa na kweli na haki basi SUK itakuwa ndiyo suluhisho lakini endapo kuna madhambi yoyote yale halafu kama mbadala SUK haina tija kabisa.

  Hivyo mtoa mada zingatia yaliyosemwa na wenzangu pamoja na mimi kwa ufafanuzi.
   
 7. K

  Kamura JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mchambuzi,

  Umeongea logic tupu, waambie wasitangulize ubinafsi na matusi kama vile CCM wamefunga ndoa na CUF
   
 8. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye red - umemaliza yote!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Unaitwa mchambuzi ? Tafuta jina jipya rudi kale kiapo jiite mwanafunzi maana elimu ya kata haitoshi kukufanya uwe mchambuzi .Kama unabisaha angalia majibu ya wenzako juu ya maandiko yako .Mimi sichangii maana wewe ni mtuou mchumia tumbo .Unataka ukaawambie wake kuona post yako ili ulipwe ? Rudi kajipange kaka
   
 10. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Jina lako "Mchmbuzi" lilinipa hamasa ya kusoma bandiko lako nikiamini litakuwa na uchmbuzi wa kina waulicholenga. Lakini nimeishia kukatishwa tamaa na hoja zako dhalili zilizojaa dharau bila heshima hata kidogo. Serikali ya umoja wa ccm na cuf zanzibar haina manufaa kwa wanachi wa kawaida zaidi ya kuwanufaisha viongozi wa juu wa cuf na ccm kimadaraka. Mbaya zaidi sera za cuf zimewekwa kapuni na kwahiyo hata ile "slogan" yao ya haki sawa kwa wote imetupiliwa mbali sasa imebaki haki sawa kwa Maalimu Sefu,Juma Duni, Hamad Rashidi na wengine malizia wewe. Kwa kawaida serikali ya mseto huundwa na vyama vyenye itikadi zinazofanana, je itikadi ya kifisadi ya CCM ndio hiyohiyo ya CUF?
   
 11. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  CUF haizungumzii sheria zilizopo bali hali halisi. Hebu tuchukue mfano wako au sheria iliyopo kuwa una 25% ya kura zote unaunda serikali. Kwa maneno mengine unawaongoza 75% ambao hawakutaki, je wewe unajisikiaje katika hali kama hiyo?

  Pili sheria si Biblia au Msahafu ambao haiwezekani hata neno moja kubadilishwa, pale sheria isipofanya kazi ni muhimu kubadilishwa tena haraka sana.

  Kuwa realistic ndio tonaweza kutokana na umasikini.
   
 12. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  muoneeni huruma huyo mchambuzi. binafsi mwanzoni nilishtuka na kusema huyu mtambuzi hii ajali imemletea ugonjwa gani tena kichwani. Nkagundua kumbe ni Mchambuzi, nadhani wewe mchambuzi nenda tu mirembe inawezekana dozi yako hukuimaliza. Hivi kwa akili yako muungano unaotokana na 'ufedhuli' wa magamba una tija gani zaidi ya kuwaziba tu midomo CUF kule zenji? Pukutisha uchafu kunako ubongo akili inaweza kurudi, jitahidi
   
 13. S

  Sambega Member

  #13
  Nov 6, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  SUK ije kwa njia kama hiyo ya UK lakini sio chama tawala kishindwe uchaguzi au kihisi harufu ya kushindwa ndio kitangaze SUK. Hiyo hapana.

  Na kwa tz, ccm hawatakiwi kubaki madarakani kwa mgongo wa SUK. Wakishindwa uchaguzi waondoke mazima na kama wakishinda basi wabaki mazima.
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Katiba ya Zanzibar ilibadilishwa kuwezesha kuunda serikali ya umoja lakini si kulazimisha mshindi aungane, mimi huwa nayalinganisha na makubaliano tu kama ya MoU, maana muungano unategemea na grace ya aliyeshinda, mgawanyo wa madaraka unakuja tu endapo makubaliano yamefikiwa. System ya UK mfano Liberal wangekataa kuungana na Cons, Labour sidhani kama wangekubali uchaguzi ungerudiwa tofauti na katiba ya Zanzibar hata kama CUF wangekataa kuungana uchaguzi usingerudiwa.

  Mimi naona huu muungano wetu ni kiini macho tu hauna tofauti na kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja maana kunakuwa hakuna challenger serikali inajifanyia itakavyo kwa sababu inajua hakuna atakayehoji. Tunajionea leo Zanzibar Seif alivyonyamazishwa, tujiulize yale aliyokuwa anayapigia kelele just a year ago yametekelezwa? Kwa kuongeza tu mkataba wa Con na Lib ni wa miaka mitano baada ya hapo kila mtu na lwake.
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Mchambuzi,

  tafadhali nafikiri wewe ndiye unayewapotosha wananchi, GNU haikuundwa kwa sababu hiyo katiba yetu na ya Zanzibar haihitaji lazima uwe na 50%+1 ni simple majority system, najua ulikuwa na mawazo mazuri lakini yanakosa ground supports (simple basics) kwenye katiba.
   
 16. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Jibu lako ni rahisi sana nafikiri umeshajijibu KATIBA hiyo 25% unayoisema inakubalika kwa katiba tuliyonayo sasa.
   
 17. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  CUF iliingizwa mjini. Tuangalie mseto wa Cons.na Liberals kabla ya kuunda serikali walikaa na kukubaliana mambo ya msingi kuhusu sera ya serikali yao ya mseto. Lakini jiulize CUF Zanzibar kuna sera zao zozote zimeingizwa ktk serikali ya GNU? Maana tunaambiwa sera zinazotekelezwa ni za CCM. Kuna tatizo hapo. Na kwasababu CCM wanalijua hilo hawatakubali hata siku kuachia kiti cha rais wa Znz.
   
 18. j

  jigoku JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mtaongea yote na kuponda yote lakini msingi wa matatizo hapa ni CCM.na ni aibu kulinganisha mfumo wa uchaguzi wa TZ na UK,Japan nk kama ulicyotaja.hapa hakuna haki ya kweli ipo kwenye makaratasi tu.
  All in all CCM ndio kiini cha matatizo yote,na wala sio suala la kuwalaumu Chadema hawajui Demokrasia,je CCM ndo wanajua demokrasia?
  Posho hizo zinztuhangaisha
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Huo wala sio mtazamo wako bali umetumwa na humu jf is wrong turn
   
 20. B

  Bubona JF-Expert Member

  #20
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwenye red umedanganya!!. Katiba ya Zanzibar ilifanyiwa marekebisho kabla ya uchaguzi. Wakaweka bayana utaratibu wa serikali ya mseto (wanapenda iitwe serikali ya umoja wa kitaifa) kupitia mabadiliko haya. Unamaanisha nini?. Kwamba matokeo ya Parliamentary elections yalijulikana kabla ya Uchaguzi?. Unahitaji kuhurumiwa!!!
   
Loading...