CHADEMA MMefungua NJIA!

CHADEMA MMefungua NJIA!

Nakubaliana na wewe kuanzia 2020 kama wakiendelea na kasi waliyo nayo sasa hivi!

Kwani iliwachukua NARC ya kenya muda gani kushinda? Na TNA je? Inahitajika nia ya dhati na uelewa wa kutosha kwa watanzania. 2015 Something good might happen!
 
mtatumia mbinu nyingi sana kujaribu kuwaaminisha watu kwamba 2015 hamtoki madarakani lakini nakuhakikishia kwamba hamtaamini macho yenu maana kura zenu zitakua za aibu tumechoka na ccm na wala hatuna mda wa kuwaongezea hata dakika 1 ya ziada pale ikulu.

Chadema na Makamanda wote, naona/nahisi gap somewhere.
Tuwahamasishe wananchi wa vijijini kujiunga na Jf ili wapate elimu ya uraia na waweze kufunguliwa macho kwani nguvu ya ccm iko juu ya upofu wa uelewa na elimu ya uraia wa wananchi wa vijijini walio wengi.
 
Kwani iliwachukua NARC ya kenya muda gani kushinda? Na TNA je? Inahitajika nia ya dhati na uelewa wa kutosha kwa watanzania. 2015 Something good might happen!

Mambo ya Kenya nimeshayaelezea hapo juu, huo unaoitwa Upinzani ulifanikiwa Kenya kwa sababu watu wale wale waliokuwa KANU walijimega na kuingia Upinzani, na ndio maana Kenya wanasiasa ni wale wale tu hao akina Bw.Uhuru Kenyata walikuwa KANU, hao akina Bw.Ruto wote chini ya Bw.Moi, na ndio maana hakuna jipya la maana Kenya kwa maana hakuna wakumnyooshea kidole mwenzake, hakuna wa kumshitaki Bw.Moi kwa maana woote walikuwa Serikali moja!

Hivyo la Kenya linaweza tu kutokea hapa kwetu kama CCM ikimeguka na kundi kubwa kukimbilia Upinzani, na sasa hilo likitokea tutakuwa hatujafanya kitu kwani hao hao tunaowashutumu kwa Ufisadi ndio watakaosaidia CHADEMA kushinda, watu kama akina Bw. Chenge aua Bw. Lowasa wakihamia CHADEMA hapo unaweza kutabiri kuanguka kwa CCM kwani wataondoka na timu yao, lkn pia hilo likitokea usitegemee cha watu kuhukumiwa kwa kesi ya EPA au Richmond au kesi ya RADAR!

Huyu katumwa kuleta ugoro wake hapa,kawaambie 2015 watanzania wasomi,vijijini,wazee mpaka vijana wanaiingza CDM Ikulu.
 
Ingawa ni ukweli ulio wazi kwamba Chama cha CHADEMA hakiwezi kushinda Uchaguzi wa Uraisi na Ubunge 2015, lakini ni jambo lililo wazi pia CHADEMA wamefungua njia ya mabadilko nchini mwetu!

Serikali ijayo ya CCM, haiwezi kuwa ya kisanii ukiilinganisha na ya sasa hivi, na nathubutu kusema pia Serikali zilizopita, na sio kwa sababu haiwezekani, bali ni kwa sababu CCM hawana jinsi bali kubadilika kwani kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo watu wanvyozidi kuhoji Uhalali wao wa kuongoza, hivyo basi naweza kusema 2015 ndiyo karata ya mwisho kwa CCM, na kama wasipobadilika basi 2020 au 2025 CHADEMA kama wataendelea na kasi hii hii walionayo sasa hivi ni lazima watashinda Uchaguzi wa Uraisi na Ubunge!

Kadri siku zinavyozidi kusogea ndivyo cdm inavyodharauliwa na watz, wametoka kwenye malengo ya upinzani na kuwa Magaidi, wanang'oa watu kucha na kutengeza mbinu za udini na ukabila ili Serikali ionekane inahusika nayo, baada ya watu kugundua hayo,Sasa walio wengi wanaamini CDM itakufa mapema iwezekanavyo!
Ushauri wako ni bure ndugu yangu, umeshauri mfu mtarajiwa!
 
Jama kaleta mada kama haegemei upande wowote lakini kulinga na majadiliano na maoini ya wanajamvi amedhihilisha yeye yu upande gani. Asante.
 
Yangu macho maana kilichotokea kwa CUF kipindi kile kinaweza kutumika tena'
 
Huwezi chukua nchi wakati unabagua nusu ya wapiga kura! Lema nani alimtuma?
takwimu gani zinazo thibitisha ubaguzi wa nusu ya watu? Usijidanganye sense yenyewe ilikimbiwa na baadhi ya taarifa hazikuruhusiwa kuwekwa, record umetoa wapi?
 
Kuna mambo mawili aidha haufahamu mfumo wa nchi yetu ulivyo au unafahamu na umeamua tu kutokuutambua ili ujifurahishe, ukweli ni kwamba kwa mfumo huu hakuna Chama kinachoweza kuishinda CCM 2015, kumbuka Raisi wa Tanzania ni Raisi mpaka pale Raisi mwingine anapoteuliwa, kwa maana hiyo hata wakati wa Uchaguzi bado yeye ni Raisi na ana full madaraka na anaweza pia kusitisha Uchaguzi muda wowote na hakuna wa kumuuuliza kitu, anaweza kuifuta CHADEMA kesho na hakuna kitu CHADEMA wanaweza kufanya, huo ndio ukweli!

Prezidaa Kikwete anaweza kuifuta Chadema na hakuna kitu kitafanyika???!!! It's so funny to hear that from you mdau! Nadhani huelewi kwamba ndani ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuna wana-Chadema! ndani na Serikali ya Jakaya kuna wana-Chadema hata kama wanaimba u-CCM! Prezidaa aifute Chadema uone moto wake!!! Tendwa alileta mikwala mbuzi eti Chadema inafanya fujo hivyo atakifuta, niambie ameishia wapi??? Alipowaita makamanda wa Chadema waende ofisini kwake kwani walienda? Aliwafanya nini pamoja na kwamba yeye ndio msajili wa vyama!
 
Ukinisoma vizuri sijasema kwamba Bw.Kikwete anataka kuifuta CHADEMA la hasha! bali nimesema kutokana na Mamlaka makubwa aliyokuwa nayo Raisi wa TZ ana uwezo wa hata kufuta Chama chochote cha Siasa kama akiamua kufanya hivyo, yaani Raisi wa Tanzania ana uwezo wa kuajiri na kufukuza kazi mtu yoyoyte yule Tanzania, ndicho nilichomaanisha!
Kitu ambacho hakipo kwenye nchi ambazo huwa kuna ubadilishwaji wa Serikali kwa njia ya Uchaguzi!

Mambo ya Kenya nimeshayaelezea hapo juu, huo unaoitwa Upinzani ulifanikiwa Kenya kwa sababu watu wale wale waliokuwa KANU walijimega na kuingia Upinzani, na ndio maana Kenya wanasiasa ni wale wale tu hao akina Bw.Uhuru Kenyata walikuwa KANU, hao akina Bw.Ruto wote chini ya Bw.Moi, na ndio maana hakuna jipya la maana Kenya kwa maana hakuna wakumnyooshea kidole mwenzake, hakuna wa kumshitaki Bw.Moi kwa maana woote walikuwa Serikali moja!

Hivyo la Kenya linaweza tu kutokea hapa kwetu kama CCM ikimeguka na kundi kubwa kukimbilia Upinzani, na sasa hilo likitokea tutakuwa hatujafanya kitu kwani hao hao tunaowashutumu kwa Ufisadi ndio watakaosaidia CHADEMA kushinda, watu kama akina Bw. Chenge aua Bw. Lowasa wakihamia CHADEMA hapo unaweza kutabiri kuanguka kwa CCM kwani wataondoka na timu yao, lkn pia hilo likitokea usitegemee cha watu kuhukumiwa kwa kesi ya EPA au Richmond au kesi ya RADAR!

Baod 2015 ni mbali kwa maana kwamba upinzani unaweza kujijenga zaidi na kujipatia nafasi zaidi. Hatuwezi kuwa conclusive mapema hivyo
 
Kadri siku zinavyozidi
kusogea ndivyo cdm inavyodharauliwa na watz, wametoka kwenye malengo ya
upinzani na kuwa Magaidi, wanang'oa watu kucha na kutengeza mbinu za
udini na ukabila ili Serikali ionekane inahusika nayo, baada ya watu
kugundua hayo,Sasa walio wengi wanaamini CDM itakufa mapema
iwezekanavyo!
Ushauri wako ni bure ndugu yangu, umeshauri mfu mtarajiwa!

Chadema ni mkono wa Mungu kuikomboa Tanzania. Chadema imetufumbua macho! Kwa mbali tunaona mwanga katika kiza kinene. Mungu ibariki Tanzania!
Mungu ibariki Chadema!!!
 
ingawa ni ukweli ulio wazi kwamba chama cha chadema hakiwezi kushinda uchaguzi wa uraisi na ubunge 2015, lakini ni jambo lililo wazi pia chadema wamefungua njia ya mabadilko nchini mwetu!

serikali ijayo ya ccm, haiwezi kuwa ya kisanii ukiilinganisha na ya sasa hivi, na nathubutu kusema pia serikali zilizopita, na sio kwa sababu haiwezekani, bali ni kwa sababu ccm hawana jinsi bali kubadilika kwani kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo watu wanvyozidi kuhoji uhalali wao wa kuongoza, hivyo basi naweza kusema 2015 ndiyo karata ya mwisho kwa ccm, na kama wasipobadilika basi 2020 au 2025 chadema kama wataendelea na kasi hii hii walionayo sasa hivi ni lazima watashinda uchaguzi wa uraisi na ubunge!

still 850 days t2015 cdm to magogoni
 
Chadema ni mkono wa Mungu kuikomboa Tanzania. Chadema imetufumbua macho! Kwa mbali tunaona mwanga katika kiza kinene. Mungu ibariki Tanzania!
Mungu ibariki Chadema!!!

Usilitaje jina lake bure.
Mungu hawezi kupanga mipango ya kuua wandishi wa habari.
We utakuwa mpagani,maana hujui unayemtaja ni nani.
 
Mleta mada ni gamba na mnachojidanganya hatuwezi kuwazuia ila hamtaamini 2015 tutakapokuwa maggoni na wezi wa mali za umma watakapokuwa wananyea ndoo!

Mimi hasa yule aliye mkunja twiga wetu hadi akalingana na piltoni akafanikiwa kupita naye kwenye mfuko wa shati pale KIA, yaani huyo nadhani anstahili yale yalo mpata Gadafi kabisaaa....!
 
Pamoja na kwamba kwa tafsiri sahihi ya Kiswahili sanifu , Kijakazi ni Mfanyakazi wa Mtu ( housegirl ) wa ndani , bado naamini sana uwezo wao na ndiyo maana huachiwa watoto wawatunze na kuwalisha , 2015 serikali mpya , chama kipya CHADEMA kama huamini nakutakia Maisha Marefu .
 
Mimi hasa yule aliye mkunja twiga wetu hadi akalingana na piltoni akafanikiwa kupita naye kwenye mfuko wa shati pale KIA, yaani huyo nadhani anstahili yale yalo mpata Gadafi kabisaaa....!

Utasubiri sana nani kakwambia Afrika kuna haki? Utashangaa sasa hao unaowaita Mafisadi kesho wanaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na CHADEMA, sijui utasemaje, kwani kuna mtu alikuwa anapiga kelele kama Bw. Maalim Seif? yuko wapi sasa hivi? kapewa gari Nyumba na king'ora kimya, kila siku anasafiri, amekaa India wiki 2 kwa gharama yetu (Serikali), yale yale aliyokuwa anayapigia kelele alipokuwa nje ndiyo anayafanya leo!

Kwa kifupi Afrika usiamini mwanasiasa hata siku moja, usishwawishike kirahisi hivyo, huyo Dr Bw. Slaa unamwona leo anawaponda akina Bw.Lowasa, utashanga kesho wameshikana mikono na kufanya kampeni pamoja sijui utasemaje?

Mimi niliyaona Kenya 2007, Bw. Raila kalalamika kuibiwa kura na Bw.Kibaki uadui wa kufa mtu, watu wakachinjana, siku mbili baadaye Bw. kibaki na Bw. Raila wakakuktana hoteli ya Kitalii wakicheza Gofu na kukubaliana kushirikiana na kuunda Serikali pamoja, vipi wale waliokufa? sikusikia hata neno moja, hata tu kutambua mchango wao!
Hata kama una matatizo ya kichumi na unaona mambo hayaendi AFRIKA usiamini mwanasiasa na usishawishike kiraisi!

Jiepushe na visasi kaka tatizo la Tanzania ni zaidi ya wizi wa mali za umma!! Lazima kuwa na checks and balances ambazo chanzo chake ni Katiba, nadhani umeona Kenya kwenye ruling ya rufaa ya RO/CORD the supreme court iliamua mchakato wa ununuzi wa vifaa vyote vya kupigia kura zile mashine za kisasa zote nk uchunguzwe, kama uesikia DPP kamwagiza Mwenyekiti wa Ethical and Anti corruption commission afanye uchunguzi, kuona kama kulikuwa na rushwa maana hakukuwa na transparency na kuna Mama mmoja Alisha jiuzuru kwa ajili ya interference toka kwenye Executive kwenye mchakato mzima wa manunuzi! Bila hayo kwa Katiba tarajiwa ambayo tayari ninaiangalia kwa "MIWANI YANGU YA MBAO" tayari CHAMA DOLA wamesha influence destiny ya Katiba hiyo sioni jinsi gani tutaweza kwenda mbele!!
Mwanzoni mwa thread yako nilishatuna ila hapo kwenye red bila kutafuna maneno katiba imeshabakwa na masisiem na kitakachokuja ni rangi ya jalada ndio itabadilika.....
 
Kuna mambo mawili aidha haufahamu mfumo wa nchi yetu ulivyo au unafahamu na umeamua tu kutokuutambua ili ujifurahishe, ukweli ni kwamba kwa mfumo huu hakuna Chama kinachoweza kuishinda CCM 2015, kumbuka Raisi wa Tanzania ni Raisi mpaka pale Raisi mwingine anapoteuliwa, kwa maana hiyo hata wakati wa Uchaguzi bado yeye ni Raisi na ana full madaraka na anaweza pia kusitisha Uchaguzi muda wowote na hakuna wa kumuuuliza kitu, anaweza kuifuta CHADEMA kesho na hakuna kitu CHADEMA wanaweza kufanya, huo ndio ukweli!

Chadema sio makaratasi na kwa taarifa yako tu ni kuwa Chadema ni wananchi wanyonge waliochoka kudhulumiwa miaka 51 sasa na kama ana mamlaka hiyo afanye anachoweza ila kitakachompata amuulize Mubaraka.....
Hii dunia sio ya masisiem lazima waishi kwa haki na usawa kama hawataki tutawalazimisha...
 
Back
Top Bottom