CHADEMA mlimuita Jakaya Kikwete dhaifu, kulikoni tena leo mnamuhitaji?

Kiswahili alipata F huyo. Busara na DHAIFU ni maneno mawili ambayo hayana uhusiano wowote ule. Na Sugu si msemaji wa Chadema.
Unaekewa tofauti ya udhaifu na busara?
Ukiambiwa mwiliwako hauna nguvu, iliuonyeshe kuwa unanguvu unaanza kupiga watu? Kumbe madakitari walikuwa na maana ya nguvu za kuhimili dawa fulani kwenye figo zako. Na hapo ndo utajionyesha kuwa zwazwa.
 

Upiga nyundo sehemu yenyewe haswaa.
 
Hawajawahi kujua wanasimamia misingi ipi

from the list of shame to worshiping Lowassa all the way from disrespecting jakaya to worship him

they demonized Magu and started worshipping Samia, and now they don’t know anything anymore
 
Nakumbuka John Mnyika, wakati wa utawala wa JK aliitisha mkutano na waandishi wa habari anawambia kuwa Tanzania imepata Rais dhaifu kuliko wakati wowote ule, walishindwa kuweka akiba ya maneno.
Kuwa dhaifu aimanishi hana busara ya kusuruhusa matatizo ya nyumbani kwake
 
Kwanini watu wengine mnashikilia sana hilo neno?

Kwani neno dhaifu lina tatizo gani?

Binadamu wote ni dhaifu hata Maandiko Matakatifu yanathibitisha hayo.

Kwani kuna binadamu mkamilifu asiye na udhaifu au upungufu kwa namna moja ama nyingine?

Angeongea kiingereza ungemuelewa vizuri au ?!

Jifunze kuwa na mtazamo chanya epuka mtazamo hasi!
 
Mkuu Petro, hata wewe tumia akili usifananishe embe na yai, hao akina polepole na Gwajima ni watu waliokiuka msimao wa chama na wameamu kuwa tofauti na chama. Na Mbilinyi sidhani kama ameasi chama chake na ni mtu muhimu, na alichokizungumzia ni jambo la busara sana. Hata Mbowe kama kiongozi wa kitanzania, anaweza kuleta suluhi na amani kwenye vyama vingine na hata jamii yoyote ya kitanzinia, hio ni uzalendo. Sio lazima tukurupuke tuonapo kila mtu akijibu kito mitandaoni tukamjibu
 

Soma huo ujumbe uuelewe, hajasifiwa wala kuhitajika, bali ametupiwa kitanzi ili huo unafiki wake uwe hadharani vizuri.
 
JK atusamehe tu tulimkosea sana,ni kama alitudekeza vile.
Naona umenasa kwenye hii propaganda mfu. JK hakuwa mwema kabisa, bali Magufuli alikuwa muovu mno, kiasi kwamba JK akaonekana ana afadhali. Lakini kwa taarifa yako JK ni mnafiki wa kiwango cha juu, na yeye ni sehemu ya huu utawala wa kihuni hapa nchini.
 
Mzee Kikwete alituachia uwanja wa wazi wa kufanya Siasa,na kimtazamo naweza kusema aliruhusu Demokrasia.

Katika kipindi cha Kikwete tulijizolea viti vingi na kuwa na matumaini kuwa tutaitwaa Dola huku tukimdharau kwa kumuita Gaidi na Dhaifu

Sidhani kama atakuja mtawala wa CCM ambae atatuvumilia kama Mzee Jakaya Kikwete

Mnyonge mnyongeni...
 

Haikuwa hisani bali ni kwa mujibu wa sheria. Viongozi wanavunja sheria mpaka inapotokea anayezitekeleza unahisi ni hisani. Huyo JK watu walitekwa, waliumizwa, nk. Hatuhitaji kuvumiliwa na viongozi wa ccm, bali tunahitaji sheria kufuatwa. Kama ni kuvumiliana basi iwe ni kwa wote na sio hisani ya kiongozi yoyote. Vile viti tulivyopata haikuwa hisani ya JK bali ushawishi wetu kwa umma, kama ni hisani basi ilibidi kila chama cha upinzani kipewe kama hisani.

Leo hii ccm wana viti vyote vya bunge, sio kwasababu wana uhalali wa umma, bali ni kiburi cha madaraka. Usitekwe na matumizi mabaya madaraka, mpaka uone aliyejitahidi ilikuwa ni hisani. Tupambane tupate haki yetu, na sio kutaka hisani. Hata kama watatuumiza hiyo ni kawaida sana kwenye maisha unapodai haki.
 
AMEN
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…