Ziara yangu East, Central & Great lake zone of Africa

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
KINACHOENDELEA KONGO DRC NI KILE KINACHOJULIKANA KAMA MKAKATI "MUGHARABU".

Makala yangu no 03. Juu ya ziara yangu East, Central & Great lake zone of Africa.
Na Comred Mbwana Allyamtu.

Tarehe 23/7/2016 nilivuka mipaka ya Rwanda na Kongo katika boda ya Gisenyi (Rubavu) na kaanza ziara yangu katika nchi ya kongo-DRC katika jiji la Goma ambalo ndio makao makuu ya jimbo la North Kivu(Nord Kivu). Ziara hiyo nchini Kongo ilinichukua mpaka katika miji ya Beni, Bunia, Ituri, Butembo, na baadae jiji la tatu kwa ukubwa kongo-DRC la Kisangani amabalo ndio makao makuu ya jimbo la Orientale. Kabla ya kuvuka kwenda Jamuhuri ya Afrika ya kati, kwa safari ya barabara yenye urefu wa zaidi kilomita 2700 KM ambazo zilinichukua zaidi ya siku tisa(9) kutokana na ubovu wa barabara ambazo zimekuwa hazipitiki kutokana na uchakavu. Pamoja na "adventure tour" hiyo nimepata kujifunza mambo mengi ambayo twapasa kujifunza na kutambua kwa kile kinacho endelea nchini Kongo-DRC.

Katika makala hii ya leo ya "KINACHOENDELEA KONGO DRC NI KILE KINACHOJULIKANA KAMA MKAKATI "MUGHARABU"." ni makala nilioamua kuandika kwa kile kinacho endelea DRC na kupelekea kuwepo kwa machafuko ya mauaji ya kutisha kwa raia, ubakaji na kujitanua kwa vikundi vya uasi hasa hasa katika Kongo mashaliki katika majimbo ya Kivu kusini, Orientale na Kivu kaskazini pamoja na hali ya kuchafuka kwa hali ya siasa huko Kinshasa kwa kile kinacho tafsiliwa kama "Mpango wa kutaka Kujiongezea muhura wa uongozi Joseph kabila kabange".

Kwa hiki kinachoendelea Kongo kinanifanya niikumbuke ile kauli ya Rais wa tatu (3) wa marekani Thomas Jeffason aliewahi kusema "The purpose of government is to enable the people of a nation to live in safety and happiness. Government exists for the interests of the governed, not for the governors." -(Thomas Jefferson 1803) kwa tafsili ya kiswahili isiyo rasmi ni "Lengo la uwepo wa serikali ni kuwafanya watu wa taifa hilo kuishi kwa usalama na furaha. Na serikali inakuwepo kwa masilahi ya watawaliwa na wala si watawala". Kwa kongo hali ni tofauti taifa hili linaendeshwa kwa masirahi ya watawala kwa kile kinachoitwa "mkakati Mugharabu" kwa viongozi wa kongo na nje ya Kongo kwa maslahi ya watawala. Ndio maana nikaona ni vyema tuujue "usahihi" wa hiki kinacho endelea nchini Kongo-DRC kwamaana Baba wa taifa la India Mahatma Ghandi aliwa nena kamba "usahihi ni muhimu mno kuliko ukweri na usahihi ndio uhai wa uhalisia" (Mahatma Ghandi-1947). Mantiki ya makala hii ni kuitazama Kongo katika upembuzi sanifu juu ya kile kinachoendelea Kongo-DRC hivi sasa katika nyanja kuu mbili (2) yani...
1- Mgogoro wa mashaliki ya kongo na kile kinachoitwa "Mkataba wa Lemela".
2-Mvutano wa kisiasa kongo-DRC kwa Joseph kabila kutaka kusalia Madalakani.

Kimsingi hata hivyo mantiki hizo mbili ndio mijadala mikubwa duniani juu ya Kongo-DRC kwani pande zote za dunia hujadili mustakabali wa kongo-DRC kwa kutazama nyanja hizo mbili nilizo zitaja hapo juu, hivyo basi leo nami nitafanya uyakinifu katika upembuzi juu ya muktadha huo kutokana na kile nilicho jionea na kujifumza nilipo kuwa nchini kongo-DRC. Kabla ya kubobea katika uchambuzi mujarabu si vibaya tukaifahamu kongo-DRC kijeografia, kiutamaduni, kihistoria na kiutawala

Kijeografia,
kongo-DRC ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika yenye ukubwa wa karibu 2.24 milioni na eneo ambalo ndio msitu mkubwa barani Africa unapatikana msitu wa Kongo, pia mto Kongo mto wa pili kwa ukubwa Afrika ukipatikana idadi ya wakazi wake ni milioni 72 kwa sensa ya 2013. Mji mkuu wake ni kinshasa.

Kiutawala,
Rais Joseph kabila ndie mkuu wa nchi serikali na mkuu wa majeshi. Na ni Rais wa nne (4) na kiongozi mkuu wa tano (5) toka nchi hiyo kupata uhuru tarehe 30/6/1960. Kiutawala nchi hiyo imegawanyika katika majimbo 11 ambayo ni Jimbo la Katanga, Jimbo la Bandundu, Jimbo la Orientale, Jimbo la West Kasai, Jimbo la East kasai, Jimbo la North Kivu, Jimbo la South Kivu, Jimbo la Bakongo, Jimbo la Equator, Jimbo la kinshasa na Jimbo la Maniema.

Kiutamaduni,
Kongo Kuna makabila makubwa 4 na mdogo madogo zaidi ya 500. Kati ya makabili hayo makubwa ni kabila la Luba, wakogomani, wakasai, na washinwa wanazungumza Lingala.

Kihistoria,
Kongo-DRC ni nimiongoni mwa nchi zenye historia kubwa sana barani afrika toka mwaka 500 BC lakin huwezi kuzungumza historia ya jamii ya Wabantu kuanzia migawanyiko ya makabila ya Wabantu toka mwaka 100 BC. Ukaacha kuitaja Kongo.

HISTORIA YA KONGO-DRC

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa walikuwa ni wawindaji wa jamii ya Wasani na Wabilikimo walio ishi kongo katika Katika karne ya 4BC badae walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi katika karne ya 2 BC. Jina la Kongo lahusiana na mto Kongo unaopitia nchi yote na pia Ufalme wa Kongo uliopatikana zamani katika sehemu za magharibi za Angola na Kongo ya leo. Upande wa kusini, kuanzia karne ya 17, kulikuwa na ufalme ulioitwa Dola la Kazembe, Ambalo lilikuwa Koloni binafsi.

Na baada ya mkutano wa Berin mwaka 1884-1885 Kongo ilianza kutawaliwa na Uberigiji ambayo iliwekeza kiuchumi Kongo na kuanzisha Makampuni makubwa ya migodi kama vile "Société Générale" na "Union Minière du Haut Katanga" yalichimba madini hasa katika jimbo la Katanga. Makampuni haya yalikuwa na athira kubwa. Jimboni Katanga ilikuwa maarufu kwa shaba iliyochimbwa huko. halafu pia kwa uranium iliyotumiwa kwa mabomu ya kwanza ya kinyuklia ya Marekani mwaka 1945. Kutokana na ukoloni na unyonyaji kukithili uliofanya na wakoloni wa uberigiji kwa mdaa ndipo vuguvugu la ukombozi lilipoanza. Kuanzia miaka ya 1920 Wakongo wengi walionyesha upinzani huo katika mahudhurio katika makanisa ya wazungu na kuanza kujiunga na madhehebu mapya ya wafuasi wa dini ya kiafrika ya Simon Kimbangu yaliyopigwa marufuku na Wabelgiji kuanzia mwaka 1926. Tangu mwaka 1950 upinzani uliongezeka na kuonyesha pia uso wa kisiasa.

VUGUVUGU LA UKOMBOZI NA HARAKATI ZA UHURU KONGO-DRC

Wabelgiji ambao hawakujiandaa kwa madai hayo mapya ya kutaka kujitawala kwa kongo ikawabidi wapaswe kukubali uchaguzi wa halmashauri za vijiji na miji mwaka 1957. Mwaka 1958 vyama vya kisiasa vilikubaliwa. Harakati mbili muhimu kati ya hivi zilikuwa Abako (Alliance de Bakongo) chini ya Joseph Kasavubu na MNC (Mouvement National Congolais) chini ya Patrice Lumumba. Mwaka 1959 mkutano wa wanasiasa Wakongo ulidai uhuru wa nchi Wabelgiji walijaribu kuchelewesha harakati hizo lakini baada ya kutambua matatizo serikali ya Ubelgiji ilitangaza mnamo Januari 1960 kuwa uchaguzi utaendeshwa haraka na baada ya miezi sita Wabelgiji watakabidhi nchi kwa wenyeji. Chama cha Patrice Lumumba MNC kilishinda kwa kura nyingi naye akawa kiongozi wa kwanza wa nchi huru kama waziri mkuu tarehe 30 Juni 1960.

Mara baada ya mwaka mmoja baada ya uhuru hali ya siasa kongo-DRC ilichafuka kitu kilichopelekea mivutano ya kisiasa baina ya lumumba na kasavubu kitu kilicho pelekea vuguvugu la CONAKRY (Congo national du katanga resolution) liliokuwa linaongozwa na Moise Tchombe aliekuwa pandikizi wa wabeligiji kwenye mgogoro ulioitwa "paralazed of gorvement" au 'kujitenga kwa katanga' na kupelekea kupamba moto kwa hajizi za kisiasa mjini kinshasa baina ya fahari wawili kati ya utawala halali wa umma chini ya Patrice lumumba na Kikalagosi wa wazungu Joseph Kasavubu kitu kilichopeekea kuuwawa kwa lumumba 1961. Na nchi kushikwa na dikiteta Joseph Mubutu mwaka 1964 mala baada ya kuyanyakua madalaka kwa jopo la wanafunzi (12) waliokuwa wanendesha nchi kipindi cha mpito 1961-1964.

UTAWALA WA MUBUTU

Joseph-Désiré Mobutu aliyejiita baadaye Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga alikuwa rais na dikteta wa Zaire (Kongo-Kinshasa) kati ya miaka 1965 na 1997. Miaka ya 1970/1971 Mobutu alitangaza kile alichokiita "kampeni ya utamaduni wa Kiafrika". Alibadilisha jina la Kongo kuwa Zaire na raia wote waliagizwa kuacha majina yao ya Kikristo yenye asili ya Ulaya na kutumia majina ya asili ya Kiafrika. Suti za Kizungu zilipigwa marufuku na rais mwenyewe alianza kuvaa suti zilizoiga mfano wa Mao Tse Tung. Mobutu alianza kujiita "Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga" yaani "Shujaa mwenye enzi asiyeshindikana".

Kiuchumi alitaifisha makampuni ya kimataifa mara nyingi kwa kuzikabidhi kwa ndugu na wenzake. Lakini hadi mwaka 1977 hali ya uchumi ulizorota kiasi cha kumlazimisha kuwaomba wageni warudi tena. Chini ya Mobutu nchi kubwa ya Kongo-Zaire ilirudi nyuma. Mobutu alijitajirisha kupita kiasi wakati nchi yake ilioza. Mwaka 1984 mali yake binafsi nje ya Kongo ilikadiriwa kuwa dolar za Marekani bilioni 4. Nchi kubwa za Magharibi, kama vile Marekani na Ufaransa, walimvumulia na kumsaidia kwa sababu alionekana kama mwanasiasa anayepambana na Ukomunisti na harakati za ukombozi, kwa mfano Angola. Wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti nchi za magharibi hawakuona haja tena kumsaidia Mobutu.

Tangu mwaka 1990 alianza kukubali kukubali vyama vya upinzani hata akijaribu kuendeleza udikteta wake. Katika miaka 1996 na 1997 waasi walioongozwa na Laurent Kabila walienea katika mashariki ya Zaire kwa msaada wa nchi jirani Uganda na Rwanda. Kutokana na msukumo na kile kilicho kuwa kikielezwa kama kuyumba kwa serikali yake ndipo Mobutu alianza kumkubali mpinzani wake Etienne Tshisekedi na kumjumuisha katika serekali yake kama waziri mkuu lakini jeshi la Kabila likaendelea kusonga mbele.

Tarehe 16 Mei 1997 wapinzani wa kikundi cha waasi wa AFDL walisonga mbele na tayali walikuwa wamesha utwaa uwanja wa ndege wa Lubumbashi na Mobutu ambaye alikuwa amesha zidiwa na jeshi la waasi wa AFDL chini ya Laulent Kabila ndipo Mubutu alikimbia nchi.

Alikufa nje ya nchi, huko Moroko tarehe 7 Septemba 1997. Kabila alikuwa ameshaingia tayari Kinshasa tangu tarehe 20 Mei 1997 na kuchukua utawala. Pamoja na Laulent kabila kuikamata kongo-DRC bado Kongo-DRC aijatengamaa kabisa mpaka leo kitu kinacho pelekea kuendelea kuwepo kwa machafuko na kuzuka kwa waasi kutoka Uganda na Rwanda kila kukicha.

Mwaka 1964, Baba wa Taifa la China, mwanamapinduzi mkomunisti Mao Tse Tung alijisemea, "Tukiichukukua Congo tumeichukua Africa yote". Lakini pia katika kitabu cha Hearts of Darkness cha mwaka 1889, cha Joseph Conrad anaandika, ''Congo inapaswa kuwa moja kati ya mataifa tajiri duniani''. Hata leo Congo ni nchi tajiri kuliko hata watu mashuhuri wa zamani walivyo dhani. Ni vyema tukautazama utajili wa kongo-DRC ili tuone kitu kinachoifanya taifa hilo kuandamwa na mataifa lukuki duniani.

UTAJIRI WA CONGO.
1.Asilimia 80 ya ardhi ya Congo inafaa kwa kilimo, ni nchi yenye eneo kubwa sawa na Ulaya Magharibi. (England, France, Germany, Italy, Netherland, Spain, Portugal, Belgium, Austria, nk.)
2. Congo ina hazina ya asilimia 10 ya shaba ya dunia nzima. Asilimia 30 ya cobalt ya dunia nzima, dhahabu, Almasi, Platinum, Bauxite, Lead (risasi), madini ya fedha, Zink, na inazalisha asilimia 80 ya madini ya Coltan yanayotumika kutengeneza Simu, Sumaku, iPods, na injini za 'Jet'. Congo pia ni tajiri wa Uranium. Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia, Marekani waliipiga miji miwili ya Japan kwa mabomu ya atomic, Hiroshima na Nagasaki. Mabomu yale yalitengenezwa kwa madini ya Uranium iliyoibwa Congo.
3. Mto Congo ni mto wa pili kwa Ukubwa duniani, una maporomoko (Inga water falls) yanayoweza kuzalisha umeme na kusambazwa Africa na Ulaya kwa Pamoja.
4. Kuna aina 1100 za madini katika nchi yote ya Congo, Utajiri wa madini peke yake unakaribia dola trilioni 24, sawa na uchumi wa marekani na Ulaya kwa Pamoja.
5. Mafuta ambayo bado kuchimbwa, Misitu, wanyama, vivutio vya utalii vilivyopo Ituri na milima ya Virunga pamoja na mito na mabonde yenye unyevu na rutuba, maziwa, bahari, nk.
6. Miaka ya 1890s, wakati wa ugunduzi wa Rubber iliyotumika kutengeneza mifuko, matairi ya baiskeli, pikipiki na magari, Congo ilikuwa mzalishaji mkuu katika dunia. Leo haipo kwenye orodha.

Hata hivyo Leo hii, ni Miaka 126 baada ya mwandishi Joseph Conrad kuitabiria Congo kuwa moja kati ya mataifa tajiri duniani, bado ni moja kati ya mataifa madogo na masikini wa kutupwa duniani. Ikiwa na idadi ya Raia milioni 75, asilimia 80 ya Raia wake, sawa na raia 60 milioni wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku. Wageni kutoka nje na ndani ya Africa wameivamia Congo, kusababisha machafuko, kuvuruga utaratibu wa kiuchumi na kuiba mali za Congo, kuiacha hohehahe. Baada ya upembuzi sanifu juu ya kongo-DRC kiundani sasa ni vyema tujielekeze kwenye mjadala wetu mahususi juu ya kile tunacho kwenda kukijadili kama nilivyo kibainisha kwenye maelezo yangu hapo juu kama ifuatavyo..........
1- Mgogoro wa mashaliki ya kongo na kile kinachoitwa "Mkataba wa Lemela".
2-Mvutano wa kisiasa kongo-DRC kwa Joseph kabila kutaka kusalia Madalakani.

MKATABA WA LEMELA.

Kuna dhana kuwa kile kinachoitwa "Mkataba wa Lemela" ni ajizi ya Mataifa ya Magharibi ndio yanahusishwa kwa kiasi kikubwa kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe, kufadhili vikosi vya waasi kwa idadi isiyohesabika, kukwapua madini na kuzinufaisha nchi hizo. Haitoshi, matatizo hayo hayaripotiwi kwenye vyombo vya habari vya magharibi isipokuwa tu pale maslahi yao yanapokuwa hatarini. Lakin pia kumekuwepo na dhana nyingine inayo zihusudu Rwanda na Uganda juu ya hiki kinachoitwa "mkataba wa lemela" Kwa mfano, inadaiwa kuwa Kikosi cha waasi wa M23 kinafanya kazi kwa maelekezo ya serikali ya Rwanda na kimefanikiwa kwa kiasi kuinua uchumi wa Rwanda kwa kudhibiti maeneo kadhaa ya machimbo ya madini, hofu ya mataifa makubwa juu ya M23 kutishia maslahi yao ndio iliyopelekea kuwatumia marais wa Africa kusini, Jacob Zuma na Tanzania, Jakaya Kikwete kutumiwa kwa mgongo wa AU, kupeleka majeshi yao Congo kupambana na M23 tu wakati kuna vikosi lukuki vinavyofadhiliwa na kupewa silaha kutoka magharibi. Hapa, dhana hii ikiwa ni kweli, basi viongozi hao wa Tanzania na Africa Kusini wanaingia katika historia chafu ya kusaidia upande mmoja unaoibia Congo kwa kisingizio cha kutunza Amani. Yawezekana pia walikuwa na maslahi yao binafsi badala ya maslahi ya Congo na mataifa yao.

Mkataba wa Lemela ni Nini? Kwa mujibu wa upembuzi wa Yericko nyerere kutoka kitabu chake cha "Ujasusi wa Madola" kaeleza kuwa Mkataba huu ni makubaliano yaliofanywa na viongozi wa Rwanda, Uganda, Sudani kusini na Ethiopia pamoja na kiongozi wa AFDL Laulent kabila juu ya kile Kinachoitwa vita vya sasa nchini Kongo ni utekelezaji wa “Makubaliano ya Lemera” ya mwaka 1996 yenye shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa Makubaliano yalifanywa kati ya Laurent Desire Kabila, akiwa kiongozi wa chama cha “kuikomboa Kongo” kutaka kuondosha utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko, kwa upande mmoja; na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda na Mashariki mwa Kongo. Makubaliano ambayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini na kujulikana kwa jina hilo, la "mkataba wa lemela" yalitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi. Taarifa zinaonyesha makubaliano yaliandaliwa mapema mjini Kigali na pale Lemera yalikuwa yanazinduliwa tu. Ilikubaliwa wakati huo kwamba hiyo ndiyo ingekuwa “asante” kwa Rwanda “kwa ukombozi wa Kongo.”

Laurent Desire Kabila alikuwa tayari amechoka Kwa takriban miaka 20 alikuwa akipambana na utawala wa Mobutu Sese Seko Mwaka 1996, mjini Kigali, Rwanda kilikuwa kimeundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita “wapinzani wa dikiteta Mobutu.” Hawa walikuwa Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda na wengine waliokuwa wakiishi mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Kongo. Katika kundi hilo alikuwemo Mkongomani, Jenerali Andre Kisasi Ngando; askari mtaalam wa kusomea. Anadaiwa kupata mafunzo nchini Cuba, Ujerumani na Bulgaria. Alikuwa akiongoza Wakongomani wapatao 600 katika kikundi hicho. Wakati kikundi hicho kinataka kuanza vita, kilitaka kuwa na msemaji. Kikundi hicho kilikwenda Tanzania, kiliomba ushauri wa Mwalimu Julius Nyerere “ambaye nae kwa ushauri wa TISS aliwapa Laurent Desire Kabila kuwa msemaji wa wapiganaji.”

Mwanzoni mwa vita ya kumg’oa Mobutu kikundi hiki kilijulikana kama cha Wanyamulenge. Dunia nzima ikaambiwa na kuaminishwa kuwa hayo yalikuwa “maasi ya Wanyamulenge.” Wanyamulenge ni watu wanaodaiwa kutoka kwenye vilima vya Mulenge vilivyoko wilaya ya Uvira katika jimbo la Kivu Kusini. Makabila ya asili ya hapo ni Wavira na Wafuliro pamoja na wabwale Wanaojiita Wanyamulenge ni Wanyarwanda.Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo; inawanyanyasa na inawanyima uraia. Haya yalikuwa madai makubwa sana yaliyovuta hisia kali na huruma kwa wapiganaji. Wapinzani, chini ya Jenerali Andre Kisasi Ngando, na msemaji mkuu wao Laurent Kabila waliteka, kama mchezo, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma. Wakavuka Ziwa Kivu na kuingia Kivu Kusini.Ilikuwa baada ya kukamata mji wa Bukavu, makao makuu ya Kivu Kusini na sehemu nyingi za jimbo hilo, wapiganaji wa Kinyarwanda waliingiza pendekezo la rais ajaye wa Kongo, kutoa Kivu Kaskazini na Kusini kwa Rwanda. Lakini kabla suala hilo nyeti kupewa uzito unaostahili, wapiganaji wa Kinyarwanda, baada ya kuteka Bukavu, wanadaiwa kuanza kupora mali, magari, vifaa vya nyumbani, dawa katika maduka, hatua ambayo ilielezwa kuwa uhamishaji wa mali za wakazi wa Bukavu na maeneo mengine.

Alikuwa Jenerali Ngando anayeripotiwa kupinga uporaji usiomithilika, jambo ambalo lilimletea uhasama kwa baadhi ya wapiganaji. Kuona hivyo, Laurent Kabila akamsaliti Jenerali Ngando. Ngando anasemekana kuuawa siku chache baada ya kutofautiana na wapiganaji juu ya uporaji Inaelezwa kuwa alimiminiwa risasi na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto katika mbuga ya wanyama ya Virunga. Kabila aliulizwa mara nyingi juu ya Ngando. Alikuwa na majibu tofauti Akiwa bado msituni alisema Jenerali Ngando amekamatwa na majeshi ya serikali na mara ametekwa na wanamgambo wa Mai Mai.Baadaye Kabila alisema Ngando alijeruhiwa na kupelekwa Ujerumani kwa matibabu Na wakati akiwa rais, aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa Ngando alikuwa askari kama askari wengine na kwamba alikufa kwenye mapambano.

Ilikuwa baada ya kifo cha Jenerali Ngando ndipo Kabila aliingizwa kwenye makubaliano ya kumega Kongo. Kwanza, kikundi cha wapiganaji kiligeuzwa kuwa chama cha AFDL (Alliance de front Democratique pour la Liberation du Congo). Kabila akapanda cheo na kuwa kiongozi wa chama cha ukombozi wa Kongo kutoka kuwa msemaji tu wa wapiganaji. Baada ya kuundwa kwa AFDL, jina la Wanyamulenge likatoweka kabisa Wapiganaji wakaitwa waasi wa Kongo. Taarifa zinasema kabla wapiganaji kutoka Bukavu na kuanza safari iliyomfikisha Kabila madarakani, waliingia katika mkataba ambao ndio umekuja kuitwa “Makubaliano ya Lemera.” Viongozi wakuu wa wakati huo wa baadhi ya nchi walipata nakala ya makubaliano hayo ya kumega Kongo-DRC. Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania, Namibia, Uganda, Burundi, Zambia, Ethiopia, Eritrea, Zimbabwe, Angola, Namibia, Sudan na baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani. Makubaliano ni pamoja na kufanya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini kutawaliwa na Wanyarwanda wa Kitutsi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Uganda; na kwamba utawala huo ambao ungefanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Kabila, ungetekelezwa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 1998.

Chini ya mpango huo, raia wa Kongo, wakazi wa Kivu Kaskazini wangehamishiwa Kivu Kusini, “taratibu na kwa utulivu huku makazi yao yakichukuliwa” na wavamizi. Hatua ya kwanza isingekuwa ngumu kwani Rwanda ingedai kuwa inapambana na wanamgambo wa Kihutu walioitwa Interhamwe ambao itaelezwa kuwa wanatishia amani nchini Rwanda Hivyo ndivyo imekuwa ikifanya hadi sasa. Makubaliano yalieleza kuwa kuchukuliwa kwa miji ya Goma na Butembo mkoani Kivu Kaskazini, sharti iwe hatua ya kwanza kwa kuwa hayo ndiyo maeneo yenye upinzani mkubwa. Kufanikiwa kwa awamu ya pili, kungetegemea mafanikio ya awamu ya kwanza, makubaliano yanadaiwa kueleza.Wafuatiliaji wa mahusiano ya Rwanda na Kongo wanasema ingawa mpango huo ulishindikana kutekelezwa kuanzia mwaka 1998, kuingia kwa majeshi ya Rwanda nchini humo hivi sasa, ni utekelezaji wa hatua ya kwanza ya Makubaliano ya Lemera; na tayari miji ya Goma na Butembo iko chini ya kile kinachoitwa “majeshi ya ushirikiano” ya Rwanda na Kongo. Kwa mujibu wa kitabu cha "Ujasusi wa Madola" cha ndugu Yericko Nyerere kina simulia juu ya makubaliano hayo, awamu ya pili ingekuwa kujaza wakazi wa Kaskazini katika Kivu Kusini na kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wazawa wangeenguliwa, kukosa uongozi na hivyo kunyimwa sauti.

Hatua nyingine ilikuwa kuanzisha benki ya kusaidia wavamizi katika Kivu mbili, kujenga nyumba zipatazo 600,000 na kujiimarisha katika nchi ya kigeni – Kongo. Inaaminika kuwa Kabila alikubaliana na masharti ya makubaliano kwa kuwa lengo lake lilikuwa moja tu: Kuingia ikulu ya Kinshasa kwa msaada wowote kutoka kwa yeyote; Mungu au shetani. Ilikuwa baada ya makubaliano hayo, Kabila alisonga mbele na hatimaye kushinda na kuingia ikulu ya Kinshasa akiwa na wapiganaji wa Rwanda, akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda, ambaye sasa ni wazili wa ulimzi wa Rwanda James Kabarebe. Baada ya kuingia ikulu, Kabila aliwasiliana na Mwalimu Julius K.Nyerere mjini Dar es Salaam chini ya uratibu wa TISS, chaguo la Tanzania lilikuwa nikuzuia uuzwaji huo wa ardhi ya Kongo, Mashauriano yaliyochukua sura dhahili ya nguvu ya Tanzania katika ujasusi yalimpa nguvu Kabila na alipowarejelea wabia wake aliwageuka dhahiri shahiri. Ilikuwa baada ya miaka miwili ya urais, alitangaza, tena kwa jeuri, kuwa wageni wote waondoke nchini. Aliongeza kwa kufafanua, kwamba Wanyarwanda warudi kwao na kusema anawashukuru kwa kazi waliyofanya.

Kabila alinukuliwa akisema kuwa hayo (Makubaliano ya Lemera) ni “makubaliano ya porini” na kwamba yeye hakuwa na madaraka ya kuuza nchi. Alisema hakatai kuwepo mkataba, lakini akataka hilo “lipelekwe kwa wananchi kupitia bungeni ili wananchi wenyewe waamue.” Kilichomshangaza zaidi Kabila, baada ya kutangaza kuwa Wanyarwanda warudi kwao, ni kwamba aliyekuwa wa kwanza kuondoka na kukimbilia Afrika Kusini, alikuwa waziri wake wa mambo ya nje aliyeitwa Bizima Karaha (Bizimana Karahamuheto). Katika mshangao na labda kejeli, Kabila alisema, “Kumbe nchi ilikuwa imevamiwa! Hata waziri wangu wa mambo ya nje alikuwa Mnyarwanda?” Hiyo ilifuatiwa na kufukuzwa kwa James Kabarebe aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Kongo na kurudi Rwanda nakuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda.


Kabila aliuawa kabla hajamaliza kunyukana na Rwanda. Aliuawa na mmoja wa “watoto” wake yaani vijana wadogo waliokuwa watu wa karibu sana na waliomlinda tangu akiwa msituni. Kuna maelezo tatanishi juu ya kifo chake. Kuna wanaodai aliyemuua alitumwa na waliokuwa wakitaka atekeleze makubaliano ya Lemera; lakini wengine wanadai ni karata za nchi za Magharibi. Kwa kuwa Jonas Savimbi aliuawa katika mwaka moja tu baada ya kifo cha Kabila, inadaiwa kulikuwa na mkono wa mataifa makubwa; hili likitaka kuingia Kongo na hivyo kuomba msaada wa kuondoshwa kwa Kabila huku likiwezesha kukamatwa na kuuawa kwa Savimbi. Siasa hizi hazijafafanuliwa.

Kuingia kwa Joseph Kabila, anayedaiwa kuwa mtoto wa kufikia wa Laurent Kabila, kunaonekana kuleta mgeuko mwingine kuelekea kule ambako “baba” yake alikataa. Kinachoitwa makubaliano kati ya serikali ya Rwanda na ile ya Kongo kinaonekana wazi kuwa utekelezaji wa mpango wa awali ambao Laurent Kabila alikataa Aidha, kukamatwa kwa Jenerali Laurent Nkundabatware na kuhifadhiwa nchini Rwanda kunaelezwa kuwa sura kamili ya “kuheshimu kazi ya maandalizi aliyokuwa akifanya nchini Kongo.” Kuna madai kuwa Nkundabatware, Mnyarwanda kutoka Rwanda, lakini Rwanda inasema ni Mkongomani, hakuwa na jeshi lolote nchini Kongo Aliongoza majeshi ya Rwanda hadi hapo ilipoonekana kuwa mazingira yamekuwa mazuri kwa Rwanda kuingilia kwa kisingizio cha “kufukuza Interhamwe na kuweka usalama mpakani.” “Hata akipelekwa Kongo leo hii, Kabila atamlinda Jenerali Nkundabatware, labda kama wakuu wa Kongo na Rwanda watakuwa wamegundua kuwa amewasaliti,” ananukuliwa Mutereba Rwakibela mpiganaji wa kundi la M23 mjini Goma.

Rwanda imeingia Kongo. Nani ataiondoa? Hali ya amani eneo la maziwa makuu imezorota, Baadhi ya nchi jirani zimekuwa watazamaji tu wakati nyingine zikiwa katika maandalizi ya kunufaika kutokana na mgogoro wa nchi hii. Moses Byaruhanga, aliyekuwa waziri katika ofisi ya rais (Siasa) nchini Uganda, alisema nchi yake inaunga mkono “shirikisho la Kivu na Kisangani” na kwamba wanasubiri kuona serikali ya Kinshasa inalionaje suala hilo. Katika medani za kijasusi, kumekuwa na taarifa za kukamilisha kumegwa kwa mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kutoka Jamhuri ya Kongo na kuzifanya muungano wa Jamhuri ya Kivu Kauli ya msemaji wa ikulu Uganda inaongeza uwezekano wa kuimega Kongo pale inapohusisha jimbo jingine la Orientale yenye makao makuu yake ya jimbo Kisangani ambako kwa nyakati tofauti majeshi ya Uganda yanadai kuwinda waasi wa Lord’s Resistance Army (LRA). Kiongozi wa LRA, Joseph Kony amekuwa akipambana na majeshi ya serikali ya Yoweri Museveni kwa zaidi ya miaka 20. Uganda sasa inadai kuwa Kongo inatumika kama kichaka cha waasi hao. Kauli ya Uganda haipishani na mipango inayodaiwa kufanywa na Rwanda ingawa Rwanda, kupitia balozi wake mjini Dar es Salaam iliwahi kukaririwa ikisema haina mpango wowote wa kuigawa Kongo. Jumuiya ya kimataifa imetekwa kwa propaganda za Interhamwe, Wanyamulenge, waasi wa LRA na kumbukumbu za mauaji ya kimbari.

Lakini ujasusi wa Rwanda unapita kwenye kipindi kigumu kwani Idara ya ujasusi nchini Rwanda (NISS) inatumia kila njia kudhibiti wanaoitwa wahaini, mathalani mauaji ya aliyekuwa mkuu wa ujasusi bwana Patrick Karegeya. Kutokana na kuonekana kuanza kuwasaliti kwa kutoboa siri ya "mkataba wa lemela" hadharani. Baada ya kuitazama kwa kina kabisa kipengele cha kwanza (1) sasa ni vyema tujielekeze kwenye hoja ya pili (2) "Mvutano wa kisiasa kongo-DRC kwa Joseph kabila kutaka kusalia Madalakani".

2-MVUTANO WA KISIASA KONGO-DRC KWA JOSEPH KABILA KISALIA MADALAKANI.

Mvutano huu umetafsiliwa kama mgogoro wa kikatiba kwa kuwa muhura wa kabila kumalizika mwezi september mwaka huu wa 2016 kitendo hicho cha kabila kudai kuwa usalama na hali ya nchi aijakaa sawa kuruhusu uchaguzi kufanyika kitu kilicho pelekea kuwepo kwa mivutano ya kisiasa ya ndani. Wataalamu wa mambo wameeleza kuwa kukwamishwa kwa uchaguzi Kongo-DRC ni kutokana na sababu kubwa 3 ambazo ni
1- Kupunguwa kwa ushawishi wa Joseph kabila katika siasa za kongo-DRC juu ya kuwepo na vuguvugu la mabadiliko na mageuzi ya kiuchumi kutoka kwenye milengo ya kisiasa inayopinga vikali hali ya mambo yanayoendelea hivi sasa kongo-DRC kwa muda mulefu wakongo wamekuwa na hamu ya kuyatazama maendeleo kitu ambacho serikali ya Joseph kabila imeonekana kushindwa kutekeleza maendeleo kama alivyo haidi. Katka Kongo miundombinu ni mibovu na wala hakujakuwa na jitihada zozote zinazoonesha kuwepo kwa marekebisho ya nchi chini ya uongozi wak kabila kwa mda wote alipoudumu kama Rais.
2-Kusalia madalakani kwa Joseph kabila ili kumalizia utekelezaji wa mkataba wa Lemela ili kuhakikisha anafanya kile ambacho wakubwa walio muweka madalakani kinatekelezwa kwa hiki ndio kitu ambacho kabila amekuwa akionekana kuwa mratibu mzuri wa kuhakikisha anaiuza kongo-DRC mikononi mwa wanyaranda na waganda pamoja na mabeberu wa magharibi. Imekuwa ikitajwa mara kwa mara na kuaminika kuwa Joseph kabila si mkongomani. "Kabila hayuko mkongo hivyo hata uchungu na kongo hana na kuigawa nchi kwake ni kitu cha kawaida na unaona kajikusanyia mali ya nchi nzima na ndio tajili wa kwanza kongo-DRC" alisema Makebo Matata mkazi wa mji wa Goma. aliongeza kusema "Hiv hii hali unaiona ikiendekea huku mashariki mwa kongo-DRC ni kile kinachoitwa kumalizika kwa 'mkakati Mugharabu' wa kuiuza Kongo kwa mkataba wa msituni" alimaliza Matata kwa kusema hivyo.
1471618768594.jpg

3-Ushawishi wa siasa za Moise Katumbi Kongo. Katumbi ambaye huko nyuma alikuwa gavana wa jimbo la Katanga ameonekana kung'ara katika medani za siasa mala baada ya kutangaza nia yake ya kuwa atagombea urais ameanza kuwa tishio kwa serikali ya kabila kutokana na kuonekana kuwa na mvuto na ushawishi mkubwa kwa wakongomani kutokana kuonekana kuwa mtu wa maendeleo kitu kinachojionesha katika utawala wake kule katanga hali iliyopelekea kabila kuanza kumdhibiti kisiasa. Hivi karibuni mahakama moja mjini kinshasa imemuhukumu miaka mitatu kwenda gerezani katumbi kwa kosa la ubadhilifu wa kuuza Nyumba kinyume na sheria. Hata hivyo amekuwa akikabiliwa na tuhuma ya uhaini ya kuingiza wageni nchini kongo-DRC kwa kutaka kuihujumu serekali ya kabila. "Sisi tutamchagua Katumbi hatuto kubali hujuma zozote anazofanyiwa na kabila" alisema mama moja kwa shahuku.

Mwisho japo sio kwa umuhimu wake kuna umuhimu mkubwa sana Tanzania kuingilia hali ya mambo DRC ili kuinusuru na kile kinacho itwa "kuuzwa kwa nchi" je sisi Tanzania tuko na haja ya kuwa taifa msuluhishi juu ya hili?.
Katika kutamatisha makala hii Hadi leo hii, ardhi ya Congo bado imebarikiwa lakini Raia wake wamelaaniwa. Magonjwa, vita, umasikini na uhalifu ndio mkate wa kila siku wa wananchi wa CONGO, hali utajiri wao unajenga Ulaya na Marekani.
PAMOJA NA KUITAZAMA DRC SWALI LA KUJIULIZA KATIKA TAMATI YA MAKALA HII JE NI NANI WA KUIOKOA CONGO DRC?

"Kufatia mauaji ya mjini Beni wikii hii nitumie fursa hii kutoa salam za lambilabi kwa taifa la kongo-DRC "Mécoñdeleancè por le Congolé"."

"Mungu ibriki Afrika, Mungu ibariki kongo-DRC, Mungu wabaliki wakongomani."

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu

copy rights reseved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail. Com
1471618717181.jpg
 
Makala yangu no 03. Juu ya ziara yangu East, Central & Great lake zone of Africa.

Tarehe 23/7/2016 nilivuka mipaka ya Rwanda na Kongo katika boda ya Gisenyi (Rubavu) na kaanza ziara yangu katika nchi ya kongo-DRC katika jiji la Goma ambalo ndio makao makuu ya jimbo la North Kivu(Nord Kivu).

Ziara hiyo nchini Kongo ilinichukua mpaka katika miji ya Beni, Bunia, Ituri, Butembo, na baadae jiji la tatu kwa ukubwa kongo-DRC la Kisangani amabalo ndio makao makuu ya jimbo la Orientale.

Kabla ya kuvuka kwenda Jamuhuri ya Afrika ya kati, kwa safari ya barabara yenye urefu wa zaidi kilomita 2700 KM ambazo zilinichukua zaidi ya siku tisa(9) kutokana na ubovu wa barabara ambazo zimekuwa hazipitiki kutokana na uchakavu. Pamoja na "adventure tour" hiyo nimepata kujifunza mambo mengi ambayo twapasa kujifunza na kutambua kwa kile kinacho endelea nchini Kongo-DRC.

Katika makala hii ya leo ya "KINACHOENDELEA KONGO DRC NI KILE KINACHOJULIKANA KAMA MKAKATI "MUGHARABU"." ni makala nilioamua kuandika kwa kile kinacho endelea DRC na kupelekea kuwepo kwa machafuko ya mauaji ya kutisha kwa raia, ubakaji na kujitanua kwa vikundi vya uasi hasa hasa katika Kongo mashaliki katika majimbo ya Kivu kusini, Orientale na Kivu kaskazini pamoja na hali ya kuchafuka kwa hali ya siasa huko Kinshasa kwa kile kinacho tafsiliwa kama "Mpango wa kutaka Kujiongezea muhura wa uongozi Joseph kabila kabange".

Kwa hiki kinachoendelea Kongo kinanifanya niikumbuke ile kauli ya Rais wa tatu (3) wa marekani Thomas Jeffason aliewahi kusema "The purpose of government is to enable the people of a nation to live in safety and happiness. Government exists for the interests of the governed, not for the governors." -(Thomas Jefferson 1803) kwa tafsili ya kiswahili isiyo rasmi ni "Lengo la uwepo wa serikali ni kuwafanya watu wa taifa hilo kuishi kwa usalama na furaha.

Na serikali inakuwepo kwa masilahi ya watawaliwa na wala si watawala". Kwa kongo hali ni tofauti taifa hili linaendeshwa kwa masirahi ya watawala kwa kile kinachoitwa "mkakati Mugharabu" kwa viongozi wa kongo na nje ya Kongo kwa maslahi ya watawala. Ndio maana nikaona ni vyema tuujue "usahihi" wa hiki kinacho endelea nchini Kongo-DRC kwamaana Baba wa taifa la India Mahatma Ghandi aliwa nena kamba "usahihi ni muhimu mno kuliko ukweri na usahihi ndio uhai wa uhalisia" (Mahatma Ghandi-1947). Mantiki ya makala hii ni kuitazama Kongo katika upembuzi sanifu juu ya kile kinachoendelea Kongo-DRC hivi sasa katika nyanja kuu mbili (2) yani...

1- Mgogoro wa mashaliki ya kongo na kile kinachoitwa "Mkataba wa Lemela".
2-Mvutano wa kisiasa kongo-DRC kwa Joseph kabila kutaka kusalia Madalakani.

Kimsingi hata hivyo mantiki hizo mbili ndio mijadala mikubwa duniani juu ya Kongo-DRC kwani pande zote za dunia hujadili mustakabali wa kongo-DRC kwa kutazama nyanja hizo mbili nilizo zitaja hapo juu, hivyo basi leo nami nitafanya uyakinifu katika upembuzi juu ya muktadha huo kutokana na kile nilicho jionea na kujifumza nilipo kuwa nchini kongo-DRC. Kabla ya kubobea katika uchambuzi mujarabu si vibaya tukaifahamu kongo-DRC kijeografia, kiutamaduni, kihistoria na kiutawala

Kijeografia
Kongo-DRC ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika yenye ukubwa wa karibu 2.24 milioni na eneo ambalo ndio msitu mkubwa barani Africa unapatikana msitu wa Kongo, pia mto Kongo mto wa pili kwa ukubwa Afrika ukipatikana idadi ya wakazi wake ni milioni 72 kwa sensa ya 2013. Mji mkuu wake ni kinshasa.

Kiutawala.
Rais Joseph kabila ndie mkuu wa nchi serikali na mkuu wa majeshi. Na ni Rais wa nne (4) na kiongozi mkuu wa tano (5) toka nchi hiyo kupata uhuru tarehe 30/6/1960. Kiutawala nchi hiyo imegawanyika katika majimbo 11 ambayo ni Jimbo la Katanga, Jimbo la Bandundu, Jimbo la Orientale, Jimbo la West Kasai, Jimbo la East kasai, Jimbo la North Kivu, Jimbo la South Kivu, Jimbo la Bakongo, Jimbo la Equator, Jimbo la kinshasa na Jimbo la Maniema.

Kiutamaduni
Kongo Kuna makabila makubwa 4 na mdogo madogo zaidi ya 500. Kati ya makabili hayo makubwa ni kabila la Luba, wakogomani, wakasai, na washinwa wanazungumza Lingala.

Kihistoria
Kongo-DRC ni nimiongoni mwa nchi zenye historia kubwa sana barani afrika toka mwaka 500 BC lakin huwezi kuzungumza historia ya jamii ya Wabantu kuanzia migawanyiko ya makabila ya Wabantu toka mwaka 100 BC. Ukaacha kuitaja Kongo.

HISTORIA YA KONGO-DRC

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa walikuwa ni wawindaji wa jamii ya Wasani na Wabilikimo walio ishi kongo katika Katika karne ya 4BC badae walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi katika karne ya 2 BC. Jina la Kongo lahusiana na mto Kongo unaopitia nchi yote na pia Ufalme wa Kongo uliopatikana zamani katika sehemu za magharibi za Angola na Kongo ya leo. Upande wa kusini, kuanzia karne ya 17, kulikuwa na ufalme ulioitwa Dola la Kazembe, Ambalo lilikuwa Koloni binafsi.

Na baada ya mkutano wa Berin mwaka 1884-1885 Kongo ilianza kutawaliwa na Uberigiji ambayo iliwekeza kiuchumi Kongo na kuanzisha Makampuni makubwa ya migodi kama vile "Société Générale" na "Union Minière du Haut Katanga" yalichimba madini hasa katika jimbo la Katanga. Makampuni haya yalikuwa na athira kubwa.

Jimboni Katanga ilikuwa maarufu kwa shaba iliyochimbwa huko. halafu pia kwa uranium iliyotumiwa kwa mabomu ya kwanza ya kinyuklia ya Marekani mwaka 1945. Kutokana na ukoloni na unyonyaji kukithili uliofanya na wakoloni wa uberigiji kwa mdaa ndipo vuguvugu la ukombozi lilipoanza.

Kuanzia miaka ya 1920 Wakongo wengi walionyesha upinzani huo katika mahudhurio katika makanisa ya wazungu na kuanza kujiunga na madhehebu mapya ya wafuasi wa dini ya kiafrika ya Simon Kimbangu yaliyopigwa marufuku na Wabelgiji kuanzia mwaka 1926. Tangu mwaka 1950 upinzani uliongezeka na kuonyesha pia uso wa kisiasa.

VUGUVUGU LA UKOMBOZI NA HARAKATI ZA UHURU KONGO-DRC

Wabelgiji ambao hawakujiandaa kwa madai hayo mapya ya kutaka kujitawala kwa kongo ikawabidi wapaswe kukubali uchaguzi wa halmashauri za vijiji na miji mwaka 1957. Mwaka 1958 vyama vya kisiasa vilikubaliwa. Harakati mbili muhimu kati ya hivi zilikuwa Abako (Alliance de Bakongo) chini ya Joseph Kasavubu na MNC (Mouvement National Congolais) chini ya Patrice Lumumba.

Mwaka 1959 mkutano wa wanasiasa Wakongo ulidai uhuru wa nchi Wabelgiji walijaribu kuchelewesha harakati hizo lakini baada ya kutambua matatizo serikali ya Ubelgiji ilitangaza mnamo Januari 1960 kuwa uchaguzi utaendeshwa haraka na baada ya miezi sita Wabelgiji watakabidhi nchi kwa wenyeji. Chama cha Patrice Lumumba MNC kilishinda kwa kura nyingi naye akawa kiongozi wa kwanza wa nchi huru kama waziri mkuu tarehe 30 Juni 1960.

1471619091725.jpg


Mara baada ya mwaka mmoja baada ya uhuru hali ya siasa kongo-DRC ilichafuka kitu kilichopelekea mivutano ya kisiasa baina ya lumumba na kasavubu kitu kilicho pelekea vuguvugu la CONAKRY (Congo national du katanga resolution) liliokuwa linaongozwa na Moise Tshombe aliyekuwa pandikizi wa Wabeligiji kwenye mgogoro ulioitwa "paralazed of government" au 'kujitenga kwa katanga' na kupelekea kupamba moto kwa hajizi za kisiasa mjini kinshasa baina ya fahari wawili kati ya utawala halali wa umma chini ya Patrice lumumba na Kikalagosi wa wazungu Joseph Kasavubu kitu kilichopeekea kuuwawa kwa lumumba 1961. Na nchi kushikwa na dikiteta Joseph Mubutu mwaka 1964 mala baada ya kuyanyakua madalaka kwa jopo la wanafunzi (12) waliokuwa wanendesha nchi kipindi cha mpito 1961-1964.

UTAWALA WA MOBUTU

Joseph-Désiré Mobutu aliyejiita baadaye Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga alikuwa rais na dikteta wa Zaire (Kongo-Kinshasa) kati ya miaka 1965 na 1997. Miaka ya 1970/1971 Mobutu alitangaza kile alichokiita "kampeni ya utamaduni wa Kiafrika".

Alibadilisha jina la Kongo kuwa Zaire na raia wote waliagizwa kuacha majina yao ya Kikristo yenye asili ya Ulaya na kutumia majina ya asili ya Kiafrika. Suti za Kizungu zilipigwa marufuku na rais mwenyewe alianza kuvaa suti zilizoiga mfano wa Mao Tse Tung. Mobutu alianza kujiita "Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga" yaani "Shujaa mwenye enzi asiyeshindikana".

1471619026055.jpg


Kiuchumi alitaifisha makampuni ya kimataifa mara nyingi kwa kuzikabidhi kwa ndugu na wenzake. Lakini hadi mwaka 1977 hali ya uchumi ulizorota kiasi cha kumlazimisha kuwaomba wageni warudi tena. Chini ya Mobutu nchi kubwa ya Kongo-Zaire ilirudi nyuma. Mobutu alijitajirisha kupita kiasi wakati nchi yake ilioza. Mwaka 1984 mali yake binafsi nje ya Kongo ilikadiriwa kuwa dolar za Marekani bilioni 4.

Nchi kubwa za Magharibi, kama vile Marekani na Ufaransa, walimvumulia na kumsaidia kwa sababu alionekana kama mwanasiasa anayepambana na Ukomunisti na harakati za ukombozi, kwa mfano Angola. Wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti nchi za magharibi hawakuona haja tena kumsaidia Mobutu.

1471618984708.jpg


Tangu mwaka 1990 alianza kukubali kukubali vyama vya upinzani hata akijaribu kuendeleza udikteta wake. Katika miaka 1996 na 1997 waasi walioongozwa na Laurent Kabila walienea katika mashariki ya Zaire kwa msaada wa nchi jirani Uganda na Rwanda.

Kutokana na msukumo na kile kilicho kuwa kikielezwa kama kuyumba kwa serikali yake ndipo Mobutu alianza kumkubali mpinzani wake Etienne Tshisekedi na kumjumuisha katika serekali yake kama waziri mkuu lakini jeshi la Kabila likaendelea kusonga mbele.

Tarehe 16 Mei 1997 wapinzani wa kikundi cha waasi wa AFDL walisonga mbele na tayali walikuwa wamesha utwaa uwanja wa ndege wa Lubumbashi na Mobutu ambaye alikuwa amesha zidiwa na jeshi la waasi wa AFDL chini ya Laulent Kabila ndipo Mubutu alikimbia nchi.

Alikufa nje ya nchi, huko Moroko tarehe 7 Septemba 1997. Kabila alikuwa ameshaingia tayari Kinshasa tangu tarehe 20 Mei 1997 na kuchukua utawala. Pamoja na Laulent kabila kuikamata kongo-DRC bado Kongo-DRC haijatengamaa kabisa mpaka leo kitu kinachopelekea kuendelea kuwepo kwa machafuko na kuzuka kwa waasi kutoka Uganda na Rwanda kila kukicha.

Mwaka 1964, Baba wa Taifa la China, mwanamapinduzi mkomunisti Mao Tse Tung alijisemea, "Tukiichukukua Congo tumeichukua Africa yote". Lakini pia katika kitabu cha Hearts of Darkness cha mwaka 1889, cha Joseph Conrad anaandika, ''Congo inapaswa kuwa moja kati ya mataifa tajiri duniani''. Hata leo Congo ni nchi tajiri kuliko hata watu mashuhuri wa zamani walivyo dhani. Ni vyema tukautazama utajili wa kongo-DRC ili tuone kitu kinachoifanya taifa hilo kuandamwa na mataifa lukuki duniani.

UTAJIRI WA CONGO.
1.Asilimia 80 ya ardhi ya Congo inafaa kwa kilimo, ni nchi yenye eneo kubwa sawa na Ulaya Magharibi. (England, France, Germany, Italy, Netherland, Spain, Portugal, Belgium, Austria, nk.)

2. Congo ina hazina ya asilimia 10 ya shaba ya dunia nzima. Asilimia 30 ya cobalt ya dunia nzima, dhahabu, Almasi, Platinum, Bauxite, Lead (risasi), madini ya fedha, Zink, na inazalisha asilimia 80 ya madini ya Coltan yanayotumika kutengeneza Simu, Sumaku, iPods, na injini za 'Jet'. Congo pia ni tajiri wa Uranium. Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia, Marekani waliipiga miji miwili ya Japan kwa mabomu ya atomic, Hiroshima na Nagasaki. Mabomu yale yalitengenezwa kwa madini ya Uranium iliyoibwa Congo.

3. Mto Congo ni mto wa pili kwa Ukubwa duniani, una maporomoko (Inga water falls) yanayoweza kuzalisha umeme na kusambazwa Africa na Ulaya kwa Pamoja.

4. Kuna aina 1100 za madini katika nchi yote ya Congo, Utajiri wa madini peke yake unakaribia dola trilioni 24, sawa na uchumi wa marekani na Ulaya kwa Pamoja.

5. Mafuta ambayo bado kuchimbwa, Misitu, wanyama, vivutio vya utalii vilivyopo Ituri na milima ya Virunga pamoja na mito na mabonde yenye unyevu na rutuba, maziwa, bahari, nk.

6. Miaka ya 1890s, wakati wa ugunduzi wa Rubber iliyotumika kutengeneza mifuko, matairi ya baiskeli, pikipiki na magari, Congo ilikuwa mzalishaji mkuu katika dunia. Leo haipo kwenye orodha.

Hata hivyo Leo hii, ni Miaka 126 baada ya mwandishi Joseph Conrad kuitabiria Congo kuwa moja kati ya mataifa tajiri duniani, bado ni moja kati ya mataifa madogo na masikini wa kutupwa duniani. Ikiwa na idadi ya Raia milioni 75, asilimia 80 ya Raia wake, sawa na raia 60 milioni wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku.

Wageni kutoka nje na ndani ya Africa wameivamia Congo, kusababisha machafuko, kuvuruga utaratibu wa kiuchumi na kuiba mali za Congo, kuiacha hohehahe. Baada ya upembuzi sanifu juu ya kongo-DRC kiundani sasa ni vyema tujielekeze kwenye mjadala wetu mahususi juu ya kile tunacho kwenda kukijadili kama nilivyo kibainisha kwenye maelezo yangu hapo juu kama ifuatavyo..........

1- Mgogoro wa mashaliki ya kongo na kile kinachoitwa "Mkataba wa Lemela".
2-Mvutano wa kisiasa kongo-DRC kwa Joseph kabila kutaka kusalia Madalakani.

MKATABA WA LEMELA.

Kuna dhana kuwa kile kinachoitwa "Mkataba wa Lemela" ni ajizi ya Mataifa ya Magharibi ndio yanahusishwa kwa kiasi kikubwa kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe, kufadhili vikosi vya waasi kwa idadi isiyohesabika, kukwapua madini na kuzinufaisha nchi hizo. Haitoshi, matatizo hayo hayaripotiwi kwenye vyombo vya habari vya magharibi isipokuwa tu pale maslahi yao yanapokuwa hatarini. Lakin pia kumekuwepo na dhana nyingine inayo zihusudu Rwanda na Uganda juu ya hiki kinachoitwa "mkataba wa lemela"

Kwa mfano, inadaiwa kuwa Kikosi cha waasi wa M23 kinafanya kazi kwa maelekezo ya serikali ya Rwanda na kimefanikiwa kwa kiasi kuinua uchumi wa Rwanda kwa kudhibiti maeneo kadhaa ya machimbo ya madini, hofu ya mataifa makubwa juu ya M23 kutishia maslahi yao ndio iliyopelekea kuwatumia marais wa Africa kusini, Jacob Zuma na Tanzania, Jakaya Kikwete kutumiwa kwa mgongo wa AU, kupeleka majeshi yao Congo kupambana na M23 tu wakati kuna vikosi lukuki vinavyofadhiliwa na kupewa silaha kutoka magharibi.

Hapa, dhana hii ikiwa ni kweli, basi viongozi hao wa Tanzania na Africa Kusini wanaingia katika historia chafu ya kusaidia upande mmoja unaoibia Congo kwa kisingizio cha kutunza Amani. Yawezekana pia walikuwa na maslahi yao binafsi badala ya maslahi ya Congo na mataifa yao.

Mkataba wa Lemela ni Nini? Kwa mujibu wa upembuzi wa Yericko nyerere kutoka kitabu chake cha "Ujasusi wa Madola" kaeleza kuwa Mkataba huu ni makubaliano yaliofanywa na viongozi wa Rwanda, Uganda, Sudani kusini na Ethiopia pamoja na kiongozi wa AFDL Laulent kabila juu ya kile Kinachoitwa vita vya sasa nchini Kongo ni utekelezaji wa “Makubaliano ya Lemera” ya mwaka 1996 yenye shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa Makubaliano yalifanywa kati ya Laurent Desire Kabila, akiwa kiongozi wa chama cha “kuikomboa Kongo” kutaka kuondosha utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko, kwa upande mmoja; na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda na Mashariki mwa Kongo.

Makubaliano ambayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini na kujulikana kwa jina hilo, la "mkataba wa lemela" yalitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi. Taarifa zinaonyesha makubaliano yaliandaliwa mapema mjini Kigali na pale Lemera yalikuwa yanazinduliwa tu. Ilikubaliwa wakati huo kwamba hiyo ndiyo ingekuwa “asante” kwa Rwanda “kwa ukombozi wa Kongo.”

Laurent Desire Kabila alikuwa tayari amechoka Kwa takriban miaka 20 alikuwa akipambana na utawala wa Mobutu Sese Seko Mwaka 1996, mjini Kigali, Rwanda kilikuwa kimeundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita “wapinzani wa dikiteta Mobutu.”

Hawa walikuwa Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda na wengine waliokuwa wakiishi mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Kongo. Katika kundi hilo alikuwemo Mkongomani, Jenerali Andre Kisasi Ngando; askari mtaalam wa kusomea. Anadaiwa kupata mafunzo nchini Cuba, Ujerumani na Bulgaria. Alikuwa akiongoza Wakongomani wapatao 600 katika kikundi hicho. Wakati kikundi hicho kinataka kuanza vita, kilitaka kuwa na msemaji. Kikundi hicho kilikwenda Tanzania, kiliomba ushauri wa Mwalimu Julius Nyerere “ambaye nae kwa ushauri wa TISS aliwapa Laurent Desire Kabila kuwa msemaji wa wapiganaji.”

Mwanzoni mwa vita ya kumg’oa Mobutu kikundi hiki kilijulikana kama cha Wanyamulenge. Dunia nzima ikaambiwa na kuaminishwa kuwa hayo yalikuwa “maasi ya Wanyamulenge.” Wanyamulenge ni watu wanaodaiwa kutoka kwenye vilima vya Mulenge vilivyoko wilaya ya Uvira katika jimbo la Kivu Kusini. Makabila ya asili ya hapo ni Wavira na Wafuliro pamoja na wabwale Wanaojiita Wanyamulenge ni Wanyarwanda.

Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo; inawanyanyasa na inawanyima uraia. Haya yalikuwa madai makubwa sana yaliyovuta hisia kali na huruma kwa wapiganaji. Wapinzani, chini ya Jenerali Andre Kisasi Ngando, na msemaji mkuu wao Laurent Kabila waliteka, kama mchezo, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma. Wakavuka Ziwa Kivu na kuingia Kivu Kusini.

Ilikuwa baada ya kukamata mji wa Bukavu, makao makuu ya Kivu Kusini na sehemu nyingi za jimbo hilo, wapiganaji wa Kinyarwanda waliingiza pendekezo la rais ajaye wa Kongo, kutoa Kivu Kaskazini na Kusini kwa Rwanda. Lakini kabla suala hilo nyeti kupewa uzito unaostahili, wapiganaji wa Kinyarwanda, baada ya kuteka Bukavu, wanadaiwa kuanza kupora mali, magari, vifaa vya nyumbani, dawa katika maduka, hatua ambayo ilielezwa kuwa uhamishaji wa mali za wakazi wa Bukavu na maeneo mengine.

Alikuwa Jenerali Ngando anayeripotiwa kupinga uporaji usiomithilika, jambo ambalo lilimletea uhasama kwa baadhi ya wapiganaji. Kuona hivyo, Laurent Kabila akamsaliti Jenerali Ngando. Ngando anasemekana kuuawa siku chache baada ya kutofautiana na wapiganaji juu ya uporaji Inaelezwa kuwa alimiminiwa risasi na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto katika mbuga ya wanyama ya Virunga.

Kabila aliulizwa mara nyingi juu ya Ngando. Alikuwa na majibu tofauti Akiwa bado msituni alisema Jenerali Ngando amekamatwa na majeshi ya serikali na mara ametekwa na wanamgambo wa Mai Mai.Baadaye Kabila alisema Ngando alijeruhiwa na kupelekwa Ujerumani kwa matibabu Na wakati akiwa rais, aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa Ngando alikuwa askari kama askari wengine na kwamba alikufa kwenye mapambano.

1471618939646.jpg


Ilikuwa baada ya kifo cha Jenerali Ngando ndipo Kabila aliingizwa kwenye makubaliano ya kumega Kongo. Kwanza, kikundi cha wapiganaji kiligeuzwa kuwa chama cha AFDL (Alliance de front Democratique pour la Liberation du Congo). Kabila akapanda cheo na kuwa kiongozi wa chama cha ukombozi wa Kongo kutoka kuwa msemaji tu wa wapiganaji. Baada ya kuundwa kwa AFDL, jina la Wanyamulenge likatoweka kabisa Wapiganaji wakaitwa waasi wa Kongo.

Taarifa zinasema kabla wapiganaji kutoka Bukavu na kuanza safari iliyomfikisha Kabila madarakani, waliingia katika mkataba ambao ndio umekuja kuitwa “Makubaliano ya Lemera.” Viongozi wakuu wa wakati huo wa baadhi ya nchi walipata nakala ya makubaliano hayo ya kumega Kongo-DRC. Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania, Namibia, Uganda, Burundi, Zambia, Ethiopia, Eritrea, Zimbabwe, Angola, Namibia, Sudan na baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani.

Makubaliano ni pamoja na kufanya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini kutawaliwa na Wanyarwanda wa Kitutsi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Uganda; na kwamba utawala huo ambao ungefanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Kabila, ungetekelezwa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 1998.

Chini ya mpango huo, raia wa Kongo, wakazi wa Kivu Kaskazini wangehamishiwa Kivu Kusini, “taratibu na kwa utulivu huku makazi yao yakichukuliwa” na wavamizi. Hatua ya kwanza isingekuwa ngumu kwani Rwanda ingedai kuwa inapambana na wanamgambo wa Kihutu walioitwa Interhamwe ambao itaelezwa kuwa wanatishia amani nchini Rwanda Hivyo ndivyo imekuwa ikifanya hadi sasa.

Makubaliano yalieleza kuwa kuchukuliwa kwa miji ya Goma na Butembo mkoani Kivu Kaskazini, sharti iwe hatua ya kwanza kwa kuwa hayo ndiyo maeneo yenye upinzani mkubwa. Kufanikiwa kwa awamu ya pili, kungetegemea mafanikio ya awamu ya kwanza, makubaliano yanadaiwa kueleza.Wafuatiliaji wa mahusiano ya Rwanda na Kongo wanasema ingawa mpango huo ulishindikana kutekelezwa kuanzia mwaka 1998, kuingia kwa majeshi ya Rwanda nchini humo hivi sasa, ni utekelezaji wa hatua ya kwanza ya Makubaliano ya Lemera; na tayari miji ya Goma na Butembo iko chini ya kile kinachoitwa “majeshi ya ushirikiano” ya Rwanda na Kongo.

Kwa mujibu wa kitabu cha "Ujasusi wa Madola" cha ndugu Yericko Nyerere kina simulia juu ya makubaliano hayo, awamu ya pili ingekuwa kujaza wakazi wa Kaskazini katika Kivu Kusini na kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wazawa wangeenguliwa, kukosa uongozi na hivyo kunyimwa sauti.

Hatua nyingine ilikuwa kuanzisha benki ya kusaidia wavamizi katika Kivu mbili, kujenga nyumba zipatazo 600,000 na kujiimarisha katika nchi ya kigeni – Kongo. Inaaminika kuwa Kabila alikubaliana na masharti ya makubaliano kwa kuwa lengo lake lilikuwa moja tu: Kuingia ikulu ya Kinshasa kwa msaada wowote kutoka kwa yeyote; Mungu au shetani.

Ilikuwa baada ya makubaliano hayo, Kabila alisonga mbele na hatimaye kushinda na kuingia ikulu ya Kinshasa akiwa na wapiganaji wa Rwanda, akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda, ambaye sasa ni waziri wa ulimzi wa Rwanda James Kabarebe. Baada ya kuingia ikulu, Kabila aliwasiliana na Mwalimu Julius K.Nyerere mjini Dar es Salaam chini ya uratibu wa TISS, chaguo la Tanzania lilikuwa nikuzuia uuzwaji huo wa ardhi ya Kongo, Mashauriano yaliyochukua sura dhahili ya nguvu ya Tanzania katika ujasusi yalimpa nguvu Kabila na alipowarejelea wabia wake aliwageuka dhahiri shahiri.

Ilikuwa baada ya miaka miwili ya urais, alitangaza, tena kwa jeuri, kuwa wageni wote waondoke nchini. Aliongeza kwa kufafanua, kwamba Wanyarwanda warudi kwao na kusema anawashukuru kwa kazi waliyofanya.

Kabila alinukuliwa akisema kuwa hayo (Makubaliano ya Lemera) ni “makubaliano ya porini” na kwamba yeye hakuwa na madaraka ya kuuza nchi. Alisema hakatai kuwepo mkataba, lakini akataka hilo “lipelekwe kwa wananchi kupitia bungeni ili wananchi wenyewe waamue.”

Kilichomshangaza zaidi Kabila, baada ya kutangaza kuwa Wanyarwanda warudi kwao, ni kwamba aliyekuwa wa kwanza kuondoka na kukimbilia Afrika Kusini, alikuwa waziri wake wa mambo ya nje aliyeitwa Bizima Karaha (Bizimana Karahamuheto).

Katika mshangao na labda kejeli, Kabila alisema, “Kumbe nchi ilikuwa imevamiwa! Hata waziri wangu wa mambo ya nje alikuwa Mnyarwanda?” Hiyo ilifuatiwa na kufukuzwa kwa James Kabarebe aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Kongo na kurudi Rwanda nakuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda.

Kabila aliuawa kabla hajamaliza kunyukana na Rwanda. Aliuawa na mmoja wa “watoto” wake yaani vijana wadogo waliokuwa watu wa karibu sana na waliomlinda tangu akiwa msituni. Kuna maelezo tatanishi juu ya kifo chake. Kuna wanaodai aliyemuua alitumwa na waliokuwa wakitaka atekeleze makubaliano ya Lemera; lakini wengine wanadai ni karata za nchi za Magharibi.

Kwa kuwa Jonas Savimbi aliuawa katika mwaka moja tu baada ya kifo cha Kabila, inadaiwa kulikuwa na mkono wa mataifa makubwa; hili likitaka kuingia Kongo na hivyo kuomba msaada wa kuondoshwa kwa Kabila huku likiwezesha kukamatwa na kuuawa kwa Savimbi. Siasa hizi hazijafafanuliwa.

1471618907763.jpg


Kuingia kwa Joseph Kabila, anayedaiwa kuwa mtoto wa kufikia wa Laurent Kabila, kunaonekana kuleta mgeuko mwingine kuelekea kule ambako “baba” yake alikataa. Kinachoitwa makubaliano kati ya serikali ya Rwanda na ile ya Kongo kinaonekana wazi kuwa utekelezaji wa mpango wa awali ambao Laurent Kabila alikataa Aidha, kukamatwa kwa Jenerali Laurent Nkundabatware na kuhifadhiwa nchini Rwanda kunaelezwa kuwa sura kamili ya “kuheshimu kazi ya maandalizi aliyokuwa akifanya nchini Kongo.”

Kuna madai kuwa Nkundabatware, Mnyarwanda kutoka Rwanda, lakini Rwanda inasema ni Mkongomani, hakuwa na jeshi lolote nchini Kongo Aliongoza majeshi ya Rwanda hadi hapo ilipoonekana kuwa mazingira yamekuwa mazuri kwa Rwanda kuingilia kwa kisingizio cha “kufukuza Interhamwe na kuweka usalama mpakani.” “Hata akipelekwa Kongo leo hii, Kabila atamlinda Jenerali Nkundabatware, labda kama wakuu wa Kongo na Rwanda watakuwa wamegundua kuwa amewasaliti,” ananukuliwa Mutereba Rwakibela mpiganaji wa kundi la M23 mjini Goma.

Rwanda imeingia Kongo. Nani ataiondoa? Hali ya amani eneo la maziwa makuu imezorota, Baadhi ya nchi jirani zimekuwa watazamaji tu wakati nyingine zikiwa katika maandalizi ya kunufaika kutokana na mgogoro wa nchi hii. Moses Byaruhanga, aliyekuwa waziri katika ofisi ya rais (Siasa) nchini Uganda, alisema nchi yake inaunga mkono “shirikisho la Kivu na Kisangani” na kwamba wanasubiri kuona serikali ya Kinshasa inalionaje suala hilo.

Katika medani za kijasusi, kumekuwa na taarifa za kukamilisha kumegwa kwa mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kutoka Jamhuri ya Kongo na kuzifanya muungano wa Jamhuri ya Kivu Kauli ya msemaji wa ikulu Uganda inaongeza uwezekano wa kuimega Kongo pale inapohusisha jimbo jingine la Orientale yenye makao makuu yake ya jimbo Kisangani ambako kwa nyakati tofauti majeshi ya Uganda yanadai kuwinda waasi wa Lord’s Resistance Army (LRA). Kiongozi wa LRA, Joseph Kony amekuwa akipambana na majeshi ya serikali ya Yoweri Museveni kwa zaidi ya miaka 20.

Uganda sasa inadai kuwa Kongo inatumika kama kichaka cha waasi hao. Kauli ya Uganda haipishani na mipango inayodaiwa kufanywa na Rwanda ingawa Rwanda, kupitia balozi wake mjini Dar es Salaam iliwahi kukaririwa ikisema haina mpango wowote wa kuigawa Kongo. Jumuiya ya kimataifa imetekwa kwa propaganda za Interhamwe, Wanyamulenge, waasi wa LRA na kumbukumbu za mauaji ya kimbari.

Lakini ujasusi wa Rwanda unapita kwenye kipindi kigumu kwani Idara ya ujasusi nchini Rwanda (NISS) inatumia kila njia kudhibiti wanaoitwa wahaini, mathalani mauaji ya aliyekuwa mkuu wa ujasusi bwana Patrick Karegeya. Kutokana na kuonekana kuanza kuwasaliti kwa kutoboa siri ya "mkataba wa lemela" hadharani.

Baada ya kuitazama kwa kina kabisa kipengele cha kwanza (1) sasa ni vyema tujielekeze kwenye hoja ya pili (2) "Mvutano wa kisiasa kongo-DRC kwa Joseph kabila kutaka kusalia Madalakani".

1471618878583.jpg


2-MVUTANO WA KISIASA KONGO-DRC KWA JOSEPH KABILA KISALIA MADALAKANI.

Mvutano huu umetafsiliwa kama mgogoro wa kikatiba kwa kuwa muhura wa kabila kumalizika mwezi september mwaka huu wa 2016 kitendo hicho cha kabila kudai kuwa usalama na hali ya nchi aijakaa sawa kuruhusu uchaguzi kufanyika kitu kilicho pelekea kuwepo kwa mivutano ya kisiasa ya ndani. Wataalamu wa mambo wameeleza kuwa kukwamishwa kwa uchaguzi Kongo-DRC ni kutokana na sababu kubwa 3 ambazo ni

1- Kupunguwa kwa ushawishi wa Joseph kabila katika siasa za kongo-DRC juu ya kuwepo na vuguvugu la mabadiliko na mageuzi ya kiuchumi kutoka kwenye milengo ya kisiasa inayopinga vikali hali ya mambo yanayoendelea hivi sasa kongo-DRC kwa muda mulefu wakongo wamekuwa na hamu ya kuyatazama maendeleo kitu ambacho serikali ya Joseph kabila imeonekana kushindwa kutekeleza maendeleo kama alivyo haidi. Katka Kongo miundombinu ni mibovu na wala hakujakuwa na jitihada zozote zinazoonesha kuwepo kwa marekebisho ya nchi chini ya uongozi wak kabila kwa mda wote alipoudumu kama Rais.

2-Kusalia madalakani kwa Joseph kabila ili kumalizia utekelezaji wa mkataba wa Lemela ili kuhakikisha anafanya kile ambacho wakubwa walio muweka madalakani kinatekelezwa kwa hiki ndio kitu ambacho kabila amekuwa akionekana kuwa mratibu mzuri wa kuhakikisha anaiuza kongo-DRC mikononi mwa wanyaranda na waganda pamoja na mabeberu wa magharibi. Imekuwa ikitajwa mara kwa mara na kuaminika kuwa Joseph kabila si mkongomani. "Kabila hayuko mkongo hivyo hata uchungu na kongo hana na kuigawa nchi kwake ni kitu cha kawaida na unaona kajikusanyia mali ya nchi nzima na ndio tajili wa kwanza kongo-DRC" alisema Makebo Matata mkazi wa mji wa Goma. aliongeza kusema "Hiv hii hali unaiona ikiendekea huku mashariki mwa kongo-DRC ni kile kinachoitwa kumalizika kwa 'mkakati Mugharabu' wa kuiuza Kongo kwa mkataba wa msituni" alimaliza Matata kwa kusema hivyo.

3-Ushawishi wa siasa za Moise Katumbi Kongo. Katumbi ambaye huko nyuma alikuwa gavana wa jimbo la Katanga ameonekana kung'ara katika medani za siasa mala baada ya kutangaza nia yake ya kuwa atagombea urais ameanza kuwa tishio kwa serikali ya kabila kutokana na kuonekana kuwa na mvuto na ushawishi mkubwa kwa wakongomani kutokana kuonekana kuwa mtu wa maendeleo kitu kinachojionesha katika utawala wake kule katanga hali iliyopelekea kabila kuanza kumdhibiti kisiasa.

Hivi karibuni mahakama moja mjini kinshasa imemuhukumu miaka mitatu kwenda gerezani katumbi kwa kosa la ubadhilifu wa kuuza Nyumba kinyume na sheria. Hata hivyo amekuwa akikabiliwa na tuhuma ya uhaini ya kuingiza wageni nchini kongo-DRC kwa kutaka kuihujumu serekali ya kabila. "Sisi tutamchagua Katumbi hatuto kubali hujuma zozote anazofanyiwa na kabila" alisema mama moja kwa shahuku.

Mwisho japo sio kwa umuhimu wake kuna umuhimu mkubwa sana Tanzania kuingilia hali ya mambo DRC ili kuinusuru na kile kinacho itwa "kuuzwa kwa nchi" je sisi Tanzania tuko na haja ya kuwa taifa msuluhishi juu ya hili?.
Katika kutamatisha makala hii Hadi leo hii, ardhi ya Congo bado imebarikiwa lakini Raia wake wamelaaniwa. Magonjwa, vita, umasikini na uhalifu ndio mkate wa kila siku wa wananchi wa CONGO, hali utajiri wao unajenga Ulaya na Marekani.

PAMOJA NA KUITAZAMA DRC SWALI LA KUJIULIZA KATIKA TAMATI YA MAKALA HII JE NI NANI WA KUIOKOA CONGO DRC?

"Kufatia mauaji ya mjini Beni wikii hii nitumie fursa hii kutoa salam za lambilabi kwa taifa la kongo-DRC "Mécoñdeleancè por le Congolé"."

"Mungu ibriki Afrika, Mungu ibariki kongo-DRC, Mungu wabaliki wakongomani."
 
good,DRC nashindwa kujua ni kwa nni hawana stability-hawa ADC haswa ni nani ana wa.finance?naskia militia wao(ADC) wapo wa tanzania pia,Kwa nini nchi jiran wasifanye joint operation ili wawe cornered,nashindwa kujua DRC sijui wanashida gan
 
Kazi nzuri, uandishi mzuri unamvuta msomaji aendelee kusoma zaidi. Actually a good you've done but work on the difference between R&L and use each where deserves to be used.
"Afrika sisi Tulishindwa kufikia malengo yetu tuliyokuwa tunaota wakati wa zama za ukombozi miaka ya 1960 sababu tuliona haya kujikosoa" haya ni maneno ya Baba wa taifa la Namibia Sam Nidjoma

Naamini kujikosoa na kukosolewa ni sehemu ya kujiimalisha zaidi kweli naitaji mapinduzi juu ya R&L coz kutokana na kabila langu hilo limeniathili sana lakin thanx kaka
 
"Afrika sisi Tulishindwa kufikia malengo yetu tuliyokuwa tunaota wakati wa zama za ukombozi miaka ya 1960 sababu tuliona haya kujikosoa" haya ni maneno ya Baba wa taifa la Namibia Sam Nidjoma

Naamini kujikosoa na kukosolewa ni sehemu ya kujiimalisha zaidi kweli naitaji mapinduzi juu ya R&L coz kutokana na kabila langu hilo limeniathili sana lakin thanx kaka
Unatokea huku kwetu kwa kina "ong'wise" au "nkoyii"?
 
Mkuu Comred Mbwana,upo sahihi sana kwa utafiti huu ulioufanya. Ikumbukwe kwamba Laurent Kabila aliuawa kwa mipango ya Paulo Kagame na mjomba wake Yoweri Kaguta. Na hiyo ni kwa sababu Laurent Kabila alikataa katakata kuigawa Congo kwa Watusi wa Rwanda na Uganda. Wao ndio waliomuweka madarakani Joseph Kabila (ambalo sio jina lake halisi). Yeye anaitwa Hyporite Kanambe na ni mtusi wa Rwanda kwa baba na mama pia ni mpwa kabisa wa waziri wa ulinzi wa Rwanda James Kabarebe. Wakongomani wana haki zote za kumtimua madarakani Kanambe maana wanaongozwa na mnyarwanda. Vurugu zote zinazoendelea Beni wahusika wakuu ni Kagame,Museveni na Kanambe mwenyewe. RAIA yeyote wa Congo anaeonekana kuwa kikwazo kwa kutekelezwa kwa mkataba wa lemela lazima auawe. Kumbuka jinsi Joseph Kabila ( Kanambe) alivyomuua kanali Mmadou Ndala alipoongoza kikosi chake kuwadhibiti m23. Kimsingi utafiti wako ni mzuri na umekuja na ukweli mwingi.
 
Ahsante mkuu umeitendea haki wikeend yangu
Kwa solo zuri.

Lakini mi naamini kongo itagawanyika tu
Dalili zote zipo wazi,

Labda kabila aangushwe
 
Safi sana,lakini vipi kuhusu vikundi kama raia mutomboki,maimai nyatura?.nk.lakini pia nafikiri mataifa ya nje yanaitumia rwanda kuidhoofisha kongo.
Yeah makundi mengi ya waasi kongo-DRC ni vikosi mikakati ama ya mataifa ya magharibi au Rwanda na Uganda.
Makundi kama FNL ni ua Uganda na USA.
 
Mkuu Comred Mbwana,upo sahihi sana kwa utafiti huu ulioufanya. Ikumbukwe kwamba Laurent Kabila aliuawa kwa mipango ya Paulo Kagame na mjomba wake Yoweri Kaguta. Na hiyo ni kwa sababu Laurent Kabila alikataa katakata kuigawa Congo kwa Watusi wa Rwanda na Uganda. Wao ndio waliomuweka madarakani Joseph Kabila (ambalo sio jina lake halisi). Yeye anaitwa Hyporite Kanambe na ni mtusi wa Rwanda kwa baba na mama pia ni mpwa kabisa wa waziri wa ulinzi wa Rwanda James Kabarebe. Wakongomani wana haki zote za kumtimua madarakani Kanambe maana wanaongozwa na mnyarwanda. Vurugu zote zinazoendelea Beni wahusika wakuu ni Kagame,Museveni na Kanambe mwenyewe. RAIA yeyote wa Congo anaeonekana kuwa kikwazo kwa kutekelezwa kwa mkataba wa lemela lazima auawe. Kumbuka jinsi Joseph Kabila ( Kanambe) alivyomuua kanali Mmadou Ndala alipoongoza kikosi chake kuwadhibiti m23. Kimsingi utafiti wako ni mzuri na umekuja na ukweli mwingi.
Good kaka kwa kuongeza uyakinifu wa kile kinacoendelea kongo-DRC juu ya kabila
 
Nikweli Laurent Kabila aliuliwa njama zilifanywa na Museven na Kagame na ikumbukwe kwamba muda mwingi kagame amekua akitumiwa na wazungu, hasa Marekani na inafahamika sababu ya kuuliwa Raulent Kabila ni kukiuka mkataba wa Remela

Mbali na hivyo pale Congo wazungu hawataki mzawa halisi kwa baba na mama kutawala Congo

Na hata ikitokea akatawala mzawa wala hadumu muda mrefu

Patrice Lumumba alikua asili ya Congo kwa baba na mama wazungu hawakumpenda na hakukawia

Mobutu mama alikua Mkongo baba yake anasadikika alikua na asili ya Afrika ya kati kule kwa kina Jean bedel bokasa,Mobutu alikaa kwa muda mrefu madarakani

Raulent Kabila alikua ni mcongo kwa baba na mama hakukawia madarakani aliuliwa

Joseph Kabila sio mcongo kwa baba na mama ni rais Congo tangu kipindi kile cha mpito na ukaja uchaguzi mpaka sasa anamihula miwili msishangai na watatu akawa rais

Kisekedi na Jean piere bemba hawa ni wacongo kwa baba na mama hawataweza kua ma rais Congo
 
Back
Top Bottom