Chadema maji ya shingo Tarime katika uchaguzi mdogo wa udiwani, tegemeo lao la mwisho lashitukiwa

Deo Meck Mbagi

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
360
525
CHADEMA MAJI YA SHINGO TARIME KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI, TEGEMEO LAO LA MWISHO LASHITUKIWA
  • Waliweka mgombea “kanyaboya” ili kujaza viongozi wao vituoni kufanya fujo.
  • Nia ni kuwa na mawakala wawili wa Chadema dhidi ya mmoja wa CCM ili kuvuruga uchaguzi.
  • Washitukiwa na sasa wanaswakwa baada ya Katibu wa NCCR-Mageuzi Tarime kufikisha taarifa kwa Msimamizi wa Uchaguzi na katika jeshi la Polisi.
  • Mgombes huyo feki na mawakala feki kufikishwa mbele ya vyombo vya dola kujibu tuhuma za kughushi nyaraka.
  • Milioni 20 zilizotolewa makao makuu kugawanywa kwa vijana zaliwa na viongozi.
  • Mgombea wao domo zege, asiyeweza kumudu kuongea hata dakika 10 awa kikwazo kwao.
  • Esther Matiko na timu yake wapita kwa wanachi wakigawa 1000 na 2000 kutafuta kura.

Hali ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yazidi kuwa mbaya kuelekea uchaguzi wa marudio wa udiwani wa kata ya Turwa ndani ya jimbo la Traime Mjini utakaofanyika hapo kesho tarehe 12 Agosti 2018.

Kumbe walichukua mwanachama wa CHADEMA ambaye wanatarime wote wanamjua kwa uanachama wake wa chadema na kazi zake za bodaboda na kumtumia aliyewahi kuwa Mwana-NCCR-Mageuzi na baadae kuhamia CHADEMA, Julius Andrea, akajifanya kuwa yeye ndie Katibu wa NCCR-Mageuzi ili kumtambulisha kama mgombea bila kuwashirikisha viongozi wa NCCR-Mageuzi wilaya ya Tarime wenye dhamana ya kuteua wagombea wa ngazi hiyo.

Mgombea huyo hakuwahi kufanya kampeni hata siku moja hali iliyopelekea viongozi wa Wilaya waishio maeneo ya mbali na mjini kutojua kinachoendelea hadi juzi tarehe 8 Agosti ndipo waliposhtuka kuwa wana mgombea, walipochunguza wakagundua ni mwanachadema, walipotafiti zaidi wakaambiwa hata majina ya mawakala yaliyopelekwa kusimamia kura za NCCR-Mageuzi ni viongozi wa ngazi mbalimbali wa chadema wakiongozwa na Katibu wa Mkoa wa Chadema, Emmanuel Chacha Heche.

Katibu wa NCCR-Mageuzi Tarime, Mzee Joseph Wandwi baada ya kupata taarifa hizo aliwasiliana na Kiongozi wake wa Kitaifa kutoka Tarime, Bi. Suzan Agostino na akamwelekeza achukua hatua ya kuandika barua kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kumweleza huyo mgombea hawamtambui, sio mwanachama wao, hajateuliwa kwa vikao vya chama chao, na hata mawakala waliopelekwa sio wa chama chao. Alishangaa kuwa katika kata hiyo NCCR-Mageuzi inaongoza mtaa wa Kokehogoma ila hata Mwenyekiti huyo wa mtaa ambaye aligombea udiwani mwaka 2015 hakushirikishwa wala hawakumchukua hata kuwa wakala kwa sababu nia ya mgombea huyo sio kushindana bali kutumika kwa faida ya chadema.

“hawa CHADEMA ni viumbe wa ajabu, nafikiri watakuwa na undugu wa karibu na shetani, hawa watu walitutenda mambo mabaya sana katika UKAWA, Tarime nzima walishindwa kumuachia hata kata moja mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa NCCR-Mageuzi Bi. Suzan Agostino, aliyegombea kata ya Legicheli, ambaye kimsingi alikuwa na nguvu na kupelekea kata kwenda CCM kwa ubinafsi wao. Wao ushirikiano wanaoutaka ni kwa faida yao pekee sio kwa faida ya washirika wote, sisi hatuwezi kuendelea kuwa daraja lao, na kosa zaidi ni kughushi muhuri na nyaraka za chama kwa kumtumia Julius Andrea ambaye alikwishahamia Chadema siku nyingi baada ya jengo (nyumba) letu la ofisi kuuzwa na Mwenyekiti wetu James Mbatia” alisema Mzee Wandwi.

Mzee Wandwi anaendelea kusema “mgombea huyo tumebaini hajawahi kufanya hata mkutano mmoja, yuko bize kufanya shughuli zake za bodaboda, anataka kukidharirisha chama chetu kwani tukipata kura kiduchu katika kata ambayo tunaongoza hadi mtaa ni aibu kwetu kama chama. Siku pekee walipoigiza kufanya uchaguzi ni juzi, baada ya chadema kuzuiwa kufanya mikutano kwa kukiuka maadili ya uchaguzi ndipo wakakitumia chama chetu kuitisha mkutano na kuutumia kuomba kura za chadema huku wazungumzaji wakiwa viongozi wa Chadema” Nimeandika barua kwa mkurugenzi, pia nimetoa taarifa jeshi la Polisi kwa niaba ya uongozi wa NCCR-Mageuzi Tarime, nikiwa mtendaji mkuu wa chama ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watu hao wanaokitumia chama chetu kwa maslahi yao, hivyo mgombea huyo Steven Solomon Chacha, Julius Andrea na viongozi wa Chadema waliojigeuza kuwa mawakala wetu wachukuliwe hatua stahiki, naamini jeshi la Polisi litawatia nguvuni muda wowote”.

Imebainika kuwa baada ya ushawishi wa Chadema kupungua Tarime kwa wabunge wao na viongozi wa halmashauri kushindwa kutekeleza ahadi zao, na kwa kuwa Tanzania nzima inafahamu Tarime imekuwa ngome yao muda mrefu basi waliamua kumuweka mwanachama wao agombee kupitia NCCR-Mageuzi ili wakiona mwelekeo wao wa kampeni sio mzuri basi viongozi wao hao wafanye fujo katika vituo ili kuharibu uchaguzi huo usifanyike ili wapate nafasi ya kujipanga upya.

Taarifa toka ndani ya Chadema Tarime zinasema kuwa waliamua kuweka viongozi wao wakiongozwa na katibu wa mkoa kwani wanachama wengine waliogopa kwenda kufanya watakayo viongozi wao kwani pindi wakamatwapo na polisi kwa kufanya fujo wengine hutelekezwa hivyo viongozi hao wakaamua kubeba jukumu hilo wenyewe.

Hivyo walipanga kuwa, kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi kitakuwa na wakala mmoja na wao watakuwa wawili wawili basi watatumia wingi wao dhidi ya wakala huyo wa CCM ili kuleta taharuki, fujo na vurugu ndani ya vituo pindi watakapoona wanazidiwa kura katika vituo husika.

Mgombea wa Chadema Charles Mnanka amewakatisha tama wanaomuuza kwani hana uwezo wa kujieleza katika majukwaa ya kuomba kura, hali ambayo wanachama na mashabiki wa chama hicho hawajazoea “sisi tulizoea kuwa na wagombea wenye uwezo mkubwa wa kuongea maana tunajua wakienda halmashauri watatutetea ila viongozi wetu walichagua kiongozi bubu kwa sababu alitoa hongo kwa wajumbe na viongozi kwa kuwa ni mfanyabisahara na ana visenti na wakamuacha kijana mwenye uwezo mkubwa, Kamanda Machage Sasita, ambaye ni Mwenyekiti wa mtaa wa Gimenya kupitia Chadema, kwanza ana uwezo mkubwa ndio maana alichaguliwa na anafanya kazi vizuri, pili ana ukoo mkubwa ambao pamoja na kuwa wengi ni wana-CCM lakini pindi agombeapo huwa wanatupa kura” alieleza Mwita Chacha ambaye ni kada kindakindaki wa Chadema.

Mikutano mingi ya chadema imekuwa haihudhuriwi na wakazi wa kata ya Turwa, wengi hutoka kata za Sabasaba, Nyamisangura, Bomani, Nkende na huwa wanasomba watu hadi kutoka Sirari ili kujaribu kutengeneza hamasa, ndio maana baada ya mikutano yao kata ya Turwa wahudhuriaji karibia wote wanarudi mjini na wengine hupanda magari pale jembe na nyumbo na pale kwa Mzee Murumbwa ili warudi Sirari. Hali ya kukata tama ndio iliwapelekea viongozi wao kushindwa kuuza sera bali wakaanza kutukana hadi wakazuiwa kuendelea na kampeni za majukwaani baada ya kamati ya maadili kukaa na kupitia malalamiko yaliyotolewa dhidi yao. Kutokana na hofu ya kushindwa hivi sasa Esther Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini anapita kwenye nyumba za wakazi wa Turwa akihonga shilingi 1000, na 2000 na kuomba watu wawahurumie na kumchagua mgombea wao “BUBU”.

CHADEMA wamehaha sana kuirejesha kata hii, nguvu inayotumia ni kubwa sana ndio maana alikuja Mwenyekiti wao wa Taifa Mh. Freeman Mbowe ili kuzindua kampeni na kuwaachia zaidi ya milioni tatu za kampeni, hata hivyo baada ya hali kuwa mbaya zaidi chadema makao makuu wametuma kiasi cha milioni 20 ili vijana wa chadema wapewe mgawo wapate nguvu zaidi ya kufanya kazi ila inaonekana baadhi ya viongozi wameamua kugawana pesa hizo kwani matumaini ya kushinda ni madogo sana. Lakini pia walimleta Zitto Kabwe katika hali ya kutafuta kujinasua na anguko katika ngome yao ambapo wanajua kushindwa kwao Tarime kutapeleka ujumbe nchi nzima kama ambavyo waliposhinda uchaguzi mdogo wa Tarime mwaka 2008 ndipo walipata hamasa nchi nzima na kuzindua Operesheni Sangara iliyowajenga huku salaam yao ikiwa “MAMBO KAMA TARIME”. Hivyo kwa Chadema huu ni zaidi ya uchaguzi wa kata, ni uchaguzi wenye sura ya kitaifa kwao, wako radhi wapoteze jimbo la Buyungu na kata zote Tanzania ili wapate hii ya Tarime. Ila Chama Cha Mapinduzi kimekaa imara sana kuhakikisha hilo halitokei.

page 1.jpg
page 2.jpg
page 3.jpg

NB: Nimeambatanisha barua ya Katibu wa NCCR-Mageuzi kwenda kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ambayo pia ina majina ya viongozi wa CHADEMA waliojigeuza kuwa mawakala wa NCCR-Mageuzi.

Imeandikwa na;-

Deo Meck, mubashara kutoka Tarime.
 
DEO meck mbona tulioko hapa Turwa Tarime hatuyasikii haya unayoyaandika? Inasikitisha sana baada ya wewe naenda CCM umeanza kuwa mnafiki.sijui kama na wewe ni mpiga kura kesho pia sijui kama umejiridhisha mitaa yote 7 ndani ya kata CCM wanakubalika vipi zaidi ya CHADEMA.Mwisho kama unaamini kiongozi mzuri ni yule anaechaguliwa na wananchi hebu kesho mruhusu uchaguzi huru ndo utaona CHADEMA ina nguvu Tarime.
Lakini pia usiwasingizie watu toka sirari kuwa ndo wanajaza mikutano ya CHADEMA,kuwa mkweli kwa hili Turwa ni kubwa tangu kibumaye-rebu-songambele..JITAHIDI KUWA MKWELI KWA MAENDELEO YA TURWA.
 
Huu ufundi wa kuhalalisha wizi wa kura tu. Poleni sana mnaonunua watu ila upinzani upo moyoni mwa watu. Leteni maendeleo hata kuwasaidia vijana watano tu kwenye kata na mkiwaonesha hadharani mbona uchaguzi mtashinda?? Acheni kuwaponda kwa marungu wapinzani, leteni maendeleo sisi tuwaponde kwa kura
 
Back
Top Bottom