Naibu Katibu Mkuu wa Chadema ndugu Salum Mwalimu amemwomba Rais John Magufuli kuwatumbua wahusika wote wa sakata la Lugumi bila ya kupoteza muda.
Mwalimu amesema iwapo Rais Magufuli atashindwa kuwatumbua wahusika hao ambao baadhi yao ni vigogo serikalini wao kama Upinzani watapiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa bungeni kwani atakuwa ameshindwa kumshauri vizuri Rais.
Naibu Katibu Mkuu huyo amemtaka Rais Magufuli kumtumbua Waziri wa Mambo ya ndani, Charles Kitwanga kwani ameonekana kama mhusika mmojawapo wa Lugumi.
Pia katika hatua nyingine Salum Mwalimu amewataka Bavicha kusambaza mitandaoni hotuba ya Waziri Kivuli wa mambo ya ndani, Ndugu Godbless Lema ambayo ilizuiliwa bungeni. Lengo la kusambaza hotuba hiyo ni kutaka Watanzania wengi waweze kusoma hotuba hiyo na kujua nini kinaendelea.
Source: Taarifa ya habari ya Efm jioni hii.