CHADEMA, Lowassa apewe onyo mara moja

mtu kupewa onyo kwa mapungufu yake haimaanishi kuwa haitajiki, tunaopenda kujenga chama tunasema mapema ili tusijelaumiana huko mbele
kulaumiana nanani? tangu lini mwanajeshi akavujisha siri za kambi kwa maadui? nyie si ndo wale fisi mnavaa ngozi za kondoo?
 
nikweli kabisa. bila lowassa mm nisingewapigia kura UKAWA
 
Una cheo gani huko CDM hadi unaagiza Lowassa apewe onyo? Halafu unaye muagiza atoe hilo onyo hujamtaja.
 
Ndio kwanza wanna mpango wa kumteua Lowassa uenyekiti.
 

Mkuu watakaokushambulia ni wafuasi wa Lowasa na si wa Chadema
 
Kwani ukinunua ng'ombe mwenye mimba si unanunua na ndama wake akizaliwa? Ndivyo ilivyotokea kwa CHADEMA na Lowasa. Kanunua chama na kila kitu kizuri kinachotokea kimetokana na ushawishi wake
Asante mkuu, huo ukweli kwamba chama kimenunuliwa ndio mgumu kukubalika ndani ya vichwa vya wanachadema, kwani Lowassa anapetumia hizo "nime" bwana mkubwa Mbowe wala hajitokezi kupinga, maana yake ni kweli kabisa anayelipa hela ndio anayechagua wimbo.
 
Mh rais Ngoyai yupo sahihi, wewe waongozwa chuki tu, aliyoyasema ni kweli tupu, lini upanzani ulishawahi kuongoza halmashauri? Na lini upinzani wamekuwa Na idadi kubwa ya wAbunge mjengoni, hebu pungezi kumuwaza lowassa mtapata kansa vichwani mwenu
 
Kipindi hiki ambacho Lowassa amejipa uongozi na utukufu pale Chadema, watu wanajiuliza Mbowe mwenye chama chake yuko wapi? Je, ataendelea kumvumilia Lowassa kwa uongozi na utukufu aliojivika?

Tunaamini tabia anayojijengea Lowassa ndani ya Chadema sio nzuri kama ingalikuwa ni mwanachama mwingine ana tabia kama aliyonayo Lowassa nadhani mwenye chama chake Mbowe angalikuwa ameshamuwekea figisu figisu za kumtimua!

Huyu Lowassa ni nani pale Chadema?

Tehe tehe tehe at Kibirizi Kigoma.
 
aise sisi na lowasa wetu hata mje na baya gani hatuwasikilizi mtuachie lowasa wetu
 
Story za namna hii sio kipaumbele chetu kwasasa.... Najua wazi mweleka wa umeya Dar hautaenda hivihivi kuna Post nyingi sana zitafuatia za namna hii
 
Tuko makini kuliko unavyofikiri
 
Lowassa ndiye mwarobaini wa CCM.

Ni hazina kutoka kwa Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…