Mbunge wa Msalala CCM Ezekiel Maige amekitabiria ushindi mkubwa chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Maige amesema hiyo inatokana na vita ya makundi ndani ya chama hicho ambacho baadhi ya wanachama wananyooshea vidole wanachama wenzao kwamba ni mafisadi.
Ametoa mfano katika jimbo lake mwenyewe la Msalala kwamba ana uhakika jimbo hilo litachukuliwa na CDM kutokana na chuki na fitina za wanaCCM wenyewe.
SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
Sasa yeye anangoja nini CCM? Si ajivue gamba, na ku-confess mbele ya Watanzania wote uzembe alioufanya maliasili hata kupelekea twiga wetu kuibiwa wakiwa hai? Anaendeleaje kubaki kwenye chama ambacho ni dhahiri kinaelekea kufa?
​Anasema hata CCM wakilipitisha jina lake 2015 hatashinda
Kwa hiyo kajiandaa kuwa mfanyabiashara maana siasa itakuwa imeshamshinda.
Kiongozi, huyu hajafunguka isipokuwa "Koki" imefumuka kama "shampeni". Lol!
no! Hatumtaki ajipange tu kuwa mmojawapo wa watakaolala jela,.akija cdm kunamsafisha na wiz wa twiga?Well done. Nakuomba baki huko huko SSM utusaidie kutundika kamba ya kunyoga magamba halafu 2015 karibu tukupe jimbo hilo hilo tu. Usiogope kufukuzwa, hilo Gamba si wazazi wako na CDM watakupokea tu.
CHADEMA haihitaji mafisadi na wezi! Nadhani huu ni wakati muafaka kwa mafisadi kujiandaa kisaikolojia kuishi magerezani!
no! Hatumtaki ajipange tu kuwa mmojawapo wa watakaolala jela,.akija cdm kunamsafisha na wiz wa twiga?
Ni kweli silaha pekee waliyobaki nayo CCM dhidi ya CDM ni kupiga majungu, na kupenyeza fitina. Hoja zilishawaishia siku nyingi! ndo maana utasikia ukabila, udini, ukanda nk. Uzuri wananchi wameshawashtukia.Nape alishaliona hilo na ameahidi hata ccm ikiwa ni chama cha upinzani bado yeye hatahama, na ataendelea kupiga majungu hadi abaki pekeyake.
no! Hatumtaki ajipange tu kuwa mmojawapo wa watakaolala jela,.akija cdm kunamsafisha na wiz wa twiga?
Hao akina rejao ni bendera fata upepo wala usiwawaze hao!!Naona Maige ameanza Kufunguka. Bado Rejao, ritz na MAFILILI.
TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
Nape hana majibu, majibu yake yatakuja muda si mrefu kwa Maige kufunguliwa mashtaka ya kutorosha nyara za serikali, kugawa vitalu kwa kutofuata taratibu, Kupunguza tozo katika mahoteli ya kitalii (Ingawa hili la Mwangunga),Mi nataka majibu ya nape tu, juu ya hil alilosema maige!