CHADEMA lazima itashinda uchaguzi 2015 - Maige

cdm waweza kushinda urahisi kama wafuatao watajiunga cdm; Dr Magufuli, Ama Lowassa kwa vile sidhani kama cdm kwa sasa wana kiongozi mwenye sifa ya kuwa Rais wa nchi

Huyo magufuli ambae hata kwake chato hawamtaki????? Lowasa fisadi hana sifa tena. Washauri waanzishe chama chao ili waweze kugombea au wagombea binafsi
 
Uchaguzi wowote ambao unajulikana fulani atashinda umepungukiwa sana katika demokrasia.

Nasikitika kuona watu wanashabikia hili.
 
Maige toka atoswe uwaziri.. roho inamuuma sana... sasa anatapatapa... mwisho wa siku mtamskia kahamia chadema...
 
Wezi wa jinsi hii nawapenda sana. Wakikamatwa pabaya huanza kutaja wenzao wote! Tamu sana hii ya Maige
 
haya bwana maige lakini rudisha kwanza twiga wetu na pesa ulizochota halafu ndo useme hayo.
 
Ndugu Maige anapaswa kupongezwa,angalau kwa kutoa kauli ya kuwakatisha tamaa CCM wenzake.Tunashukuru kuwa hatimaye ameuona ukweli na kuusema.
Bila shaka waandamizi wa CCM wamesikia huo usemi na huko walipo wanaendelea kuvimba kwa hasira!
Ili kuyapa uzito maneno yake,ningependa Maige aende hatua moja mbele:aondoke CCM na atume maombi ya kujiunga na CHADEMA na bila shaka maombi yake yatafanyiwa kazi.
Kama Mungu anasamehe hata CHADEMA ipo fursa ya kupata msamaha.
 
Makundi yataishaje kama hawagawani 'mshiko'. Maige anaweza kusema mgao wa yale mauzo ya wanyama hao ulikuwaje? Au zile hela alizokutwa nazo hotelini Arusha alikula na nani? Na vipi kuhusu biashara yake ya malori, kapata wapi hela ya kununulia malori, au ni mkopo tena toka CRDB?

Na bado kuna watu wanataka tuamini matatizo yetu yatatuliwa na watu wa umri fulani? Leo tumeona picha ya kijana mwingine akitundika miguu juu ya meza kama Obama huku akifurahia kiyoyozi na hapo tunaambiwa anatatua matatizo ya wanavijijia 300+km, tena wanavijiji wasio na umeme, internet! Nchi imejaa wasanii.
 
ndo tujue kwamba katika siasa lolote linawezekana!kiongozi yoyote akivuliwa madaraka atasema hovyo kwa waliomvua madaraka,sio kwa ccm tu bali kwa chama chochote!
Lakini Maige kwanini ayaseme haya sasa na si wakati akiwa serikalini?
 
Angerudishiwa uwaziri ili asiongee hayo jamani anaua chama chetu


CHAMA chenu kipi kife? Maana kama ni CCM tayari ni marehemu!
Sasa unataka ife mara ngapi? CCM jiandeeni kuwa chama pinzani mwaka 2015.

Kudadadek.

Pepooooooooooooooooz...................
 
Mbunge wa Msalala CCM Ezekiel Maige amekitabiria ushindi mkubwa chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Maige amesema hiyo inatokana na vita ya makundi ndani ya chama hicho ambacho baadhi ya wanachama wananyooshea vidole wanachama wenzao kwamba ni mafisadi.

Ametoa mfano katika jimbo lake mwenyewe la Msalala kwamba ana uhakika jimbo hilo litachukuliwa na CDM kutokana na chuki na fitina za wanaCCM wenyewe.


SOURCE: NIPASHE JUMAPILI

Hii ya Maige ni sawa na yule mnyang'anyi aliyetundikwa msalabani na Yesu. Alimwambia "Baba usinisahau katika ufalme wako". Yesu alimjibu, "Amini nakwambia, leo utakuwa nami peponi". Anayetubu husamehewa. Wakati mwingine, mfumo mbaya (sawa na malezi) huwafanya hata watu wema kuwa wabaya. Waingereza wanasema "Opportunity makes a thief".
 
Katika hali isiyo ya kawaida waziri huyu aliyetemwa ambae anaonekana kama kondoo wa kuchinjwa kinyuma na walipigwa chini wengine ameonekana akiwa anasononeka sana na kuvuliwa kwake kwa uuzaji wa TWIGA na Wanyamapori ambao yeye anakiri akipata muda atasema wale wanyama walikuwa wa nani liwalo na liwe, Akiendelea kukinyamba chama chake kwa kutanabaisha kuwa safari imefika kikomo na sikio la kufa halisikii dawa.....akiwa kama abiria ndani ya basi ajualo linaenda kupinduka sasa Maige kufanya uamuzi wa busara kuamua kushuka kwenye basi hilo......ntawajuza lini na wapi ngojea niendelee kupelemba habari hizi kwakina baadae ni dadavue humuhumu jamvini.....JF reporter Geita
 
Hatupokei wezi, anajua kwa vile 2015 tunahamia magogoni ndiyo ahamie? kama yeye si fisadi alishindwa nini kuwazuia au kufichua anayehujumu rasilimali za nchi kwa manufaa binafsi? Kuitaka CDM ni tamaa zake za madaraka? He is just a dreamer hatakiwi huku.
 
Back
Top Bottom