CHADEMA kutimuana si mwanzo mzuri

CHADEMA kutimuana si mwanzo mzuri

SINA

Senior Member
Joined
Nov 28, 2011
Posts
167
Reaction score
64
Ndugu zangu,

Napenda kutoa ushauri kwa CHADEMA wasifanye makosa yaliyofanywa na TANU kuona kwamba kila atakayekuwa na mawazo tofauti na uongozi basi huyo aliitwa kibaraka na kufukuzwa chamani. Hii ilipelekea waliobaki kwenye chama kuwa na mtazamo mmoja hivyo kudumaza maendeleo ya nchi. Tukumbuke wale walioambiwa vibaraka siku za nyuma tuliwaimba nyimbo za kuwabeza na kuonyesha walivyokuwa wabaya kwenye jamii yetu ya Tanzania na tukaunga mkuno viongozi wetu matokeo yake leo tunawakumbuka kama walikuwa na mtazamo wa mbali katika kuendeleza nchi yetu.

CHADEMA ichukuwe tahadhari kubwa katika hili vinginevyo tutakikumbuka kama tunavyovikumbuka vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF. Watu wanaweza kusema hivyo vyama ni tofauti na CHADEMA la hasha Mabere Marando, Prof. Safari. Prof. Beregu n.k walikuwa vyama hivyo vilivyo kufa.

Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki demokrasia ya Tanzania
 
Fanya utafiti ya kinachoendelea ndio uandike.
 
baada ya tanu kufukuzana, malengo yao yalitimia (kuleta uhuru)?? au yalishindikana??
 
Hekima na busarA umetoa....HEKO
hiki sio chama cha magamba ambapo fisadi mmoja kama lowasa ni mkubwa kuliko chama chenyewe,chama kitajengwa na wenye moyo hata kama tutabaki wawili. Anayeleta mambo ya kimagamba anatimuliwa aende akaungane na wenye magamba wenzake
 
Lakini ushauri ulio tolewa unamantiki ucha ushabiki wa KIJINGA
 
Kilicho waua magamba ni kulindana, mtu anafanya kinyume na taratibu wanapoza mambo na kumlinda kwamba ni mwenzao. Nadhani kingine kinacho wafanya magamba washindwe kuwajibishana ni kwamba kila mmoja ni mkosaji hivyo wanaona bora kuvumiliana sababu watakao fukuzwa wanaweza kusema hadharani maovu ya wengine wanao komalia wafukuzwe.

Big up CDM..fukuza wahalifu, hakuna kujali umaarufu wa mtu.
 
Fukuza tu umaskini wetu utaisha lini wasipofukuzwa?
 
Huwezi kuwa vitani halafu mmojawapo wa wapiganaji wenzenu akaamua kutumia mafunzo mliyompa kuwageuzia silaha na kuwashambulia ninyi halafu bado mkashindwa kumtofautisha yeye na adui yenu.tena huyo ni hatari zaidi kuliko Adui yenu....
 
samaki anakunjwa akiwa m'bichi.. Hatulei maradhii
 
Ndugu zangu,

Napenda kutoa ushauri kwa CHADEMA wasifanye makosa yaliyofanywa na TANU kuona kwamba kila atakayekuwa na mawazo tofauti na uongozi basi huyo aliitwa kibaraka na kufukuzwa chamani. Hii ilipelekea waliobaki kwenye chama kuwa na mtazamo mmoja hivyo kudumaza maendeleo ya nchi. Tukumbuke wale walioambiwa vibaraka siku za nyuma tuliwaimba nyimbo za kuwabeza na kuonyesha walivyokuwa wabaya kwenye jamii yetu ya Tanzania na tukaunga mkuno viongozi wetu matokeo yake leo tunawakumbuka kama walikuwa na mtazamo wa mbali katika kuendeleza nchi yetu.

CHADEMA ichukuwe tahadhari kubwa katika hili vinginevyo tutakikumbuka kama tunavyovikumbuka vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF. Watu wanaweza kusema hivyo vyama ni tofauti na CHADEMA la hasha Mabere Marando, Prof. Safari. Prof. Beregu n.k walikuwa vyama hivyo vilivyo kufa.

Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki demokrasia ya Tanzania

Acha woga mkuu,
Hakuna haja ya kulea mamluki ambao hawana nia njema kwa chama
NI KUFUKUZA TU.
Na nyie mnaojifanya kuihadharisha CHADEMA, kwa madai kuwa kufanya hivyo kutaivuruga mmekosea sana! Na inaelekea nyie ndo mnawatuma hao was.henzi ili kuidhoofisha chadema ili muendelee kuitafuna TANZANIA YETU!CHADEMA haiko tayari kulea mamluki wanaorudisha nyuma harakati za kusaka uhuru wa pili wa taifa letu.

Kutokuwafukuza wanachama wa namna hiyo, wanaotumiwa na CCM ni kuhatarisha uhai wa chama
 
Ni bora wabaki wanachama hai 10,kuliko mia na kenda wanaoangusha chama.Naweza kushauri wale waliofanya makosa ya bahati mbaya,lakini hawa wanaofanya ya makusudi,tema ilhali wakijua wanatumiwa kuua chama.Acha waadabishwe.
 
Hila kama wakilea wasaliti ndio mwanzo mzuri? Nani kafukuzwa?

Wakiwaacha utakuja na mada inasema chadema ni sawa na Maccm!
 
fukuza fukuza, safi sana BAVICHA, uwezi kuacha vichaa wanakuonyesha nyembe wakikwambia tunaomba kuona damu yako nawe ukatulia waione. Toa kabisa MBU hao.
 
Huwezi kuwa vitani halafu mmojawapo wa wapiganaji wenzenu akaamua kutumia mafunzo mliyompa kuwageuzia silaha na kuwashambulia ninyi halafu bado mkashindwa kumtofautisha yeye na adui yenu.tena huyo ni hatari zaidi kuliko Adui yenu....
Wewe si ulikua nao au!?
 
Ukiwa na mbwa kichaa utamtwanga risasi au ukimhurumia sana utamning'iniza afe.

Hawa ni vichaa, hawafai.
 
Back
Top Bottom