Tuwe na mawazo ya kujenga siyo ya kutiana ujinga kama haya. Yaani kwa ushauri wako watu wavuruge chama kwa kutumiwa, kwa lengo la kudhoofisha juhudi na harakati za kuleta mageuzi ya kweli ktk nchi hii, ili kila mtanzania ajione kuwa anayo haki ktk nchi pekee aliyopewa na mwenyezi Mungu, halafu watu wamuangalie tu kwa kisingizio cha kuharibu chama?. Hapana CDM lazima ijenge imani kwa wananchi kwa kuonyesha kuwa hata ikipewa madaraka ya kuongoza nchi itafanya tofauti na CCM. Kwa kutokulea ujinga ambao mwisho wake ni rushwa, uporaji na ufisadi. Doa ambalo leo hii limeifanya CCM ishindwe kujinasua kwa kuwa kila mtu ni mchafu kuanzia ngazi ya juu hadi chini. Ni nani wa kumfunga paka kengele shingoni?. CDM isiteteleke ktk hili na wananchi tuko nyuma yake. mamluki, wababaishaji na chumia tumboni wote lazima washughulikiwe ili hatimaye tubakie na wale tu wenye dhamira ya kweli ktk harakati za kuleta mageuzi ya kweli. Wenye majungu, rushwa, ubabaishaji, kujikweza, wizi, ufisadi na ubovu wowote ule ktk jamii waende huko CCM ambako ni sawa na dodoki linazoa kila aina ya uchafu.