CHADEMA kupeleka malalamiko yao UN na Jumuiya ya Kimataifa shambulio la risasi Mbunge Tundu Lissu

Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe amesema watapeleka malalamiko yao kuhusu kupigwa kwa Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki na watu wengine wanaopotea kwa UN na Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya Serikali.

Haya si mambo ya kushabikia
ni hatua mbaya sana kwa taifa, wapinzani nadhani si kwamba wanaichukia nchi kama inavyopotoshwa bali hawana imani na mamlaka husika huku ndani na ndo maana wanaamua kwenda nje kwa mamlaka nyingine,
kwa wale wenye uelewa kidogo juu ya uwekeza na wawekezaji kutoka nje, wenye uhuru wa akili juu ya diplomasia lazima washutuke, lakini ukiwa na watu ambao akili zao hazina visa ya kuvuka mipaka hawawezi kuona hatari iliyoko mbeleni,
hii nchi si kisiwa, hii bado change kimaendeleo ingawa ni kubwa kiumri, hii nchi inahitaji marafiki, hii nchi inahitaji umoja na mshikamano wa humu humu ndani na nje ya nchi, anapotoka mtu akataka kutugawa kwa sababu tu ya kuwaza kinyume na anayowaza lazima tukae kutafakari upya maamuzi yetu, lakini niseme kwamba maendeleo yetu hayawezi kuletwa na wanafiki, wambea na waoga, maendeleo yetu yataletwa na watu majasiri.
 
Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe amesema watapeleka malalamiko yao kuhusu kupigwa kwa Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki na watu wengine wanaopotea kwa UN na Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya Serikali.

Yaaani Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimataifa iache kushughulikia mzozo wa Rohingya kule Myanmar, madhara ya vimbunga Irma na Maria, tishio la silaha za kinuklia za Korea Kaskazini, na majanga mengineyo, washughulishwe na uvamizi wa Lissu? Kweli Mbowe atawale chadema milele....
 
Pia kuna walio amini kuwa dunia ni kama sahani mpaka hapo Christopher Columbus alipozunguka kwa kwenda magharibu na kujikuta akitokea mashariki.
 
Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe amesema watapeleka malalamiko yao kuhusu kupigwa kwa Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki na watu wengine wanaopotea kwa UN na Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya Serikali.

Wakae chini tujenge nchi, jirani hawezi kuja kukujengea nchi! Wasijidanganye!
 
Back
Top Bottom