Ujasiri wa kutetea mabeberu au?? Hatuhitaji wasaliti hapa TZ kamwe!!Haya si mambo ya kushabikia
ni hatua mbaya sana kwa taifa, wapinzani nadhani si kwamba wanaichukia nchi kama inavyopotoshwa bali hawana imani na mamlaka husika huku ndani na ndo maana wanaamua kwenda nje kwa mamlaka nyingine,
kwa wale wenye uelewa kidogo juu ya uwekeza na wawekezaji kutoka nje, wenye uhuru wa akili juu ya diplomasia lazima washutuke, lakini ukiwa na watu ambao akili zao hazina visa ya kuvuka mipaka hawawezi kuona hatari iliyoko mbeleni,
hii nchi si kisiwa, hii bado change kimaendeleo ingawa ni kubwa kiumri, hii nchi inahitaji marafiki, hii nchi inahitaji umoja na mshikamano wa humu humu ndani na nje ya nchi, anapotoka mtu akataka kutugawa kwa sababu tu ya kuwaza kinyume na anayowaza lazima tukae kutafakari upya maamuzi yetu, lakini niseme kwamba maendeleo yetu hayawezi kuletwa na wanafiki, wambea na waoga, maendeleo yetu yataletwa na watu majasiri.