PreGE2025 CHADEMA Kumshtaki Msajili wa Vyama vya Siasa Kupinga Kutengua Viongozi Walioteuliwa

PreGE2025 CHADEMA Kumshtaki Msajili wa Vyama vya Siasa Kupinga Kutengua Viongozi Walioteuliwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
897f03d4-9643-4802-93a2-0f979864edc6.jpg


Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), John Heche amesema chama hicho kimewaelekeza wanasheria wa chama hicho kumshitaki Msajili wa Vyama vya Siasa wakipinga kutenguliwa kwa viongozi walioteuliwa na Baraza Kuu Januari 22, 2025.

Soma pia: Heche amvaa Msajili

Mei 13, 2025, Msajili wa Vyama vya Siasa alikiandikia chama hicho akitengua uteuzi wa viongozi walioteuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu na kuridhiwa na Baraza Kuu, akiwamo Katibu Mkuu, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) Ally Ibrahim.

Wamo pia wajumbe wa kamati kuu walioteuliwa na kuidhinishwa na Baraza Kuu, Godbless Lema, Rose Mayemba, Salma Kasanzu, Hafidh Ally Saleh na Dk Rugemeleza Nshala ambaye pia aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.

Hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia malalamiko ya Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro, Lembrus Mchome ambaye katika barua yake ya Februari 18, 2025 kwenda kwa Msajili alidai kuwa kikao cha Baraza Kuu kilichowaridhia kilikuwa hakijatimiza akidi.

Hata hivyo, chama hicho kimewateua viongozi hao walioenguliwa kukaimu nafasi zao kwa kipindi cha mwaka mmoja, wakati wakiendelea na kesi watakayofungua.
 
Back
Top Bottom