CHADEMA Kumfungulia Mashtaka Salma Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Kumfungulia Mashtaka Salma Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mlalahoi, Sep 13, 2010.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kutoka wall ya Facebook page ya Chadema

  Mpaka kieleweke mwaka huu
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Safi sana wajue Watanzania tunahasira na kodi zetu mwaka huu!!!!
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Huyu mama kusema kweli sipendi style yake ya maisha , sipendi hekima zake, sipendi mwenendo wake , sijui yukoje. sorry Kikwete najua nakukwaza nifanyaje sasa wakati simpendi japo si mkwe wangu , anatia hasara taifa nawe wacheka nae.
   
 4. k

  kiparah JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Sorry, hata mi simpendi (samahani Kikwete).
   
 5. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  :shocked:
   
 6. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ana kiherehere sana yule mama.
   
 7. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni matatizo ya ma FL yanayozidi powers za waume zao na hivyo kuwafanya waonekane kituko. Ilikuwa Sitti Mwinyi hivihivi... Kenya kuna Lucy Kibaki hapa sasa Salma Kikwete... na nina hakika Tanzania ijayo Josephina Slaa itakuwa hivihivi na anavyoonyesha kuwa Gold Digger kufuata waume wenye mshiko... Tutakoma!
   
 8. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  She is very unfair kwa taifa hili, hajui kabisa majukumu yake kama FL, ni muhimu sasa afunguliwe mashitaka ili iwe fundisho..
   
 9. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kuna mfanyakazi mmoja wa ikulu aliwahi kuniambia kuwa ingekuwa matumizi ya ikulu yanawekwa wazi kisha yakalinganishwa na mahitaji ya nchii hii, watu wangeandamana hadi ikulu kuitoa familia ya Kikwete na kuipeleka kunakostahili - gereza la ukonga
   
 10. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  FL wetu utafikiri waziri..duh
   
 11. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hapana, mimi huyo mama nampenda kwa style nyingine ila siyo kwa uozo huu, naaanza kumchukia jamani.
   
 12. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndio tatizo la watu wa level ya standard 7
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hii ilishawekwa tena humu:

  Kutoka Mama Maria hadi Mama Salma


  Msomaji Raia​
  Septemba 8, 2010 [​IMG] Tumepotea au hatukujua?

  SUALA la nafasi ya wake wa marais wetu limekuwa linajadiliwa siku za karibuni kwa mshindo unaohitaji kuzingatiwa ili kama Chama cha Mapinduzi (CCM) kikizinduka na kuona umuhimu wa kurekebisha Katiba, basi wazingatie maoni haya.

  Ni mjinga tu anayeweza kupuuza uzito wa hoja zinazotolewa kuhusiana na nafasi ya mke wa rais katika mwenendo wa kisiasa katika Taifa letu. Hii ni kwa sababu, miaka 50 ya uhuru tumekuwa na wake wanne wa marais na wote wameonyesha picha tofauti.
  Tusipofanya mapema, tunaweza kushangaa siku moja tunapata mke au mume wa rais anayeweza kuwa kituko kwa Taifa.

  Tusidanganyane kwa sababu tumeishayaona nchi za jirani. Kule Uganda, tulishuhudia mume wa Specioza Kazibwe aliyekuwa Makamu wa Rais akimtandika vibao mbele ya walinzi wake huku walinzi wakishindwa wafanye nini maana mume kamrudi mkewe ambaye ni bosi wao!
  Sasa tuna Rais wa Uganda ambaye mkewe ni mbunge na waziri katika baraza la mawaziri. Vikao vya cabinet vinaanzia kitandani mpaka ofisini. Kama kuna suala la kuamuliwa kwa kura, mke aweza kupingana na mumewe? Wengi watasema ndiyo, kwani kuna ubaya gani? Watu wa namna hii wanachezea matashi ya mwili, tuwapuuze.

  Kule Kenya, tulitaharuki mke wa Rais alipofukuza wafanyakazi Ikulu na kwenda mitaani kugombana na kufungia vyombo vya habari. Hata ndani ya mataifa makubwa, vituko haviishi lakini kwa kuwa wana taratibu zinazoeleweka, mke wa rais anaweza tu kufanya vituko vyake ndani ya shuka au kabatini.
  Watanzania wamekuwa na Mama Maria Nyerere kwa miaka 24 Ikulu, kisha wakafuata wengine wawili waliokaa miaka kumi kumi kila mmoja. Na sasa tunaye anayemaliza mwaka wa tano.
  Ukiwaangalia hawa kwa haraka, hutaacha kuona tofauti kubwa iliyopo baina yao katika kutunza na kuheshimu nafasi yao kama wake wa marais.

  Tatizo hapa si kuomba wafanane, bali wawe na utaratibu wa kuishi na kufanya kazi zao ndani ya Ikulu ya nchi. Inapofika mahali mke wa Rais anakwenda kuwanadi wagombea urais, ubunge na udiwani wa chama tawala kwa gharama za walipa kodi wote, suala hili linakuwa limevuka mipaka.

  Fedha ya Ofisi ya Mke wa Rais (First Lady) ni fedha ya Serikali na haina budi kutumika kwa shughuli za Serikali tu. Wakati naandika makala hii, niliwasiliana na mtu wangu aliye Makao Makuu ya CCM Lumumba kujihakikishia ikiwa Mama Salma amepewa mgawo wa mafuta ya kampeini. Nimeambiwa hakupata na hatapata, ila likiandikwa, wakubwa watatoka na risiti kuwa amepata.

  Siamini kuwa amepata fedha kutoka mfuko wa shirika lake la WAMA, kwa sababu kwanza ni kinyume cha taratibu za wanaompa fedha hizo, lakini Mama mwenyewe anaona hizo ni fedha zake binafsi na kazi ya kumnadi mumewe ni ya Serikali. Tukiacha kuweka utaratibu, kuna siku fedha ya Serikali itatumika kutunza hata nyumba ndogo za wake wa marais kama zinavyotunza nyumba ndogo za marais wenyewe.

  Mama Maria Nyerere, Mungu amjalie maisha marefu zaidi. Aliingia Ikulu wakati hakuna wakaguzi wa serikali, hakuna TAKUKURU, hakuna vyombo vya habari, hakuna simu za mkononi na wala hakuna wa kumhoji kwa sababu kofia ilikuwa moja. Akakaa na kuzeekea Ikulu. Akatoka akiwa mtanzania YULE YULE tuliyemweka, akijua kupika na kulima, kuzaa na kulea, kuhani na kufiwa, naam, kutunza mume na Taifa zima. Akamtunza mmewe na kwa kufanya hivyo akaridhika kuwa analitunza Taifa. Hakuwahi kuitwa “shemeji” na waziri yeyote hata angekuwa na umri mkubwa kuliko Kambarage!

  Hata mzee Kenneth Kaunda hakudiriki kumwita shemeji. Leo hii, tuna mawaziri, tena vijana, wanamwita mke wa rais shemeji! Kisa wanamchotea mafungu kutoka wizara kuchangia WAMA.

  Kizazi kimoja kamili kikatimia, Mama Maria akahamia kijijini Butiama. Waliokaa naye wakimlinda Mwalimu, wakimtibu Mwalimu, wakimsaidia kuandika hotuba, hatukuwasikia wakigombea kuwa wabunge – mpaka walipomaliza kazi hiyo.

  Walikaa Butiama, wakalima na Maria, wakala ugali wa Maria, wakashiriki shida za Maria na furaha zake pia.
  Ukizungumza nao, hata siku hizi, watakuambia Mama alikuwa mkali kwetu na kutufanya tulijali sana Taifa letu masikini. Mpaka leo ukimwuliza Mama Maria atakuambia Tanzania ni masikini, tuihurumie. Anawashangaa sana wanaokaa madarakani wakatoka matajiri.

  Ukimwuliza tufanye nini, atakuambia tuombe sana, Mungu anasikia. Hii ndiyo tunu, yenye thamani kubwa kutoka hekima ya Mama aliyekaa Ikulu kizazi kimoja. Wanaomdharau kuwa alizubaa, kama alivyonukuliwa mmoja wa wake wa marais waliomfuata, anajidharau mwenyewe.

  Akaja Mama Sitti na wake wenza wake. Nani alikuwa wa kwanza kwa mzee, namwachia mwenyewe aseme, lakini, mama wa Taifa alikuwa Sitti. Yaliyotokea kipindi cha miaka 10, inadai kiandikiwe kitabu.
  Mama akawa sehemu ya utawala, akawa mtafutaji wa mikataba ya Serikali (Mungu ndiye anajua ujira wake), akaajiri na kufukuza, akaagiza na kusimamia lakini akajihadhari sana asiongee na wana habari.

  Taratibu nguvu ya maamuzi ikahama kwa Mzee na kuelekea kwa “rais kivuli” wetu Sitti.
  Hata mawaziri wakamsalimu Mama kabla ya kumwona Baba kwa jambo lolote nyeti. Aliyetaka mkataba akamwona Mama kama alitaka mambo yamnyokee. Mzee akakemewa na Mwalimu, haikutosha, akaamua kuhamishia ofisi yake Lumumba kusikiliza matatizo ya wananchi. Kumbe tukichekea nanyi, tutavuna mabua – wahenga walisema! Madaraka matamu, hata kwa mama wa Taifa. Mama Sitti atakumbukwa kwa mengi, lakini moja halitasahaulika – alimfanya Mwalimu akakosa uvumilivu.

  Ndipo akaja Anna Mkapa: Huyu alikwaa bingo au aliramba dume, haswa kwa sababu alilala masikini akaamka tajiri. Kilichokuwa kinaendelea kati yake na Ben wanakijua wao na Mwalimu Nyerere. Kitu kimoja ni wazi, kuingia Ikulu kwa Ben kuliokoa mahusiano yao na kumfanya Mama Anna agundue lulu iliyofichika ndani yake kwa muda mrefu.

  Yeye badala ya kumuingilia mumewe katika maamuzi ya kuongoza nchi, aliamua kuunda ka-serikali kake pembeni na kukaongoza kwa ufanisi mkubwa. Tunamjua Ben, haingiliki, hata ukimwuliza Manji anajua! Kwa hiyo ilikuwa ni busara kwa Anna kuamua kutomwingilia katika masuala ya kuongoza Serikali.
  Sikumbuki hata kumwona Anna akihutubia mkutano wa kampeini zilizomwingiza madarakani Ben, au hata zile za kipindi cha pili. Kama alifanya, basi zilikuwa sehemu chache na hakuwa na kauli mbiu kama ya “shuka kwa shuka”.

  Lakini Mama Anna akaasisi kitu kimoja kizuri lakini cha hatari pia. Akaanzisha asasi (EOTF) akidai kusaidia wanawake. Wengi tukadhani huu ni mwanzo mzuri wa kutatua tatizo la wake wa marais wajao. Alipoondoka, akaenda na EOTF yake na huo ukawa mwanzo na sababu ya kusajili nyingine.

  Kama kujibu mapigo, Salma akaingia na WAMA. Tofauti za WAMA na EOTF ziko nyingi, lakini iliyo kubwa ni kuwa WAMA ina harufu kubwa ya siasa na madhambi yanayozaliwa na siasa (ueneo, udini, itikadi, u-mtandao, ufisadi, n.k), wakati EOTF ilijaa ujasiriamali na ukabila kidogo.

  Wote wawili Mama Anna na Mama Salma wana vyombo vizuri lakini wanaelemewa na kukosa maono. Ikiwa hali hii itaachwa kuendelea, kuna uwezekano tukaja kuwa na mke wa rais anayeweza kutumiwa vibaya na maadui wa Taifa, kwa sababu tu, tumeruhusu wake wa marais kuendesha vyombo visivyodhibitiwa na Bunge ambalo ni sauti ya wananchi.

  Hivi sasa tuna Mama Salma ambaye amejisahau kuwa yeye ni mama wa Watanzania wote na kujiona ni mama wa CCM-Mtandao kwa sababu baadhi ya wabunge wamedai sehemu nyingine haendi kwa sababu hakuna wana mtandao.

  Ukiwaangalia hawa mama wanne, kutoka Maria hadi Salma, ni ama tumepotea njia, au hatukujua njia nzuri ya kuwatumia akina mama hawa, hasa wakati wa Mama Maria. Miaka yote 24 ilipotea bure, na hii 25 ya Mama Sitti hadi Salma ndiyo miaka ya faida kwa Taifa kwa sababu ya vituko tulivyoshuhudia – ufisadi, ujasiriamali, na upiga debe.
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kikwete mzee wangu Samahani kwa haya ninayoyaweka hapo chini

  1. Umekuwa rais wa aina yake ambaye mara ya kwanza siku nne baada ya kuapa umetoa kauli kuwa URAIS ni wako huna share na mtu. umesahau kuwa URAIS ni wetu sisi wananchi ambao tumekupigia kura kukupa dhamana.
  2. wakati unachukua fomu za kuteuliwa tena kipindi cha pili ukasema kuwa URAIS ni suala la kifamilia. ukiwa na maana ya kulinda madudu ya kumkabidhi mwanao fomu za kuomba wadhamini ndani ya chama. hii ina maana hujui kuwa URAIS ni TAASISI ambayo ni tukuka na familia haina nafasi kuumiliki. kama wanafamilia wanakutaka uwe rais lakini wananchi hawakutaki utakuja na kauli gani tena?
  3. Mama Salma ni mjumbe kamati kuu ya CCM, ilhali Ridhwani ni mjumbe kupitia UVCCM, mwanao (nimesahau jinale) ambaye yupo chini ya miaka kumi na nne naye ni mjumbe kamati kuu UVCCM kupitia chipukizi. Najua unajua kuwa hiyo ni IMLA na ukiukwaji mkubwa wa madaraka yako kwa kushawishi nduguzo kuingia ktk nafasi nyeti za kitaasisi.
  4. Kuna malalamiko yenye maudhui ndani yake kwamba mwanao RIDHWANI ni mharibuji katikam kila mimbari anayokanyaga, mfano suala la MSASAUNI lilikuzwa baada ya kuhitilafiana na mwanao, Francis Kifukwe alionja machungu ya sekeseke la dogo, Alihusika kuvuruga uchaguzi wa serikali ya wanafunzi Chuo cha biashara (business college) ambapo alimpigia chapuo Ally Mayay kuwa rais ambaye amekuja kumkingia kifua kuingia ktk kamati ya utendaji wa Yanga. Suala la BASHE linadushulishwa ni kuhitilafiana kati ya Bashe na ridhwani
  5. Umesita mno kuchukua hatua dhidi ya kilio cha wananchi kuhusu ufisadi, majambazi, wauza unga na watendaji wabovu wa serikali yako ambapo hakuna hatua uliyochukua hata kutolea kauli mtambuka
  6. Ukiwa rais ambaye unatawala (siyo kuongoza) watu wa jinsia zote umesita kumkanya mkeo kutoa kauli tata hasa ile ya kuwaasa wanawake wasijitokeze kugombea nafasi ya urais ili wakuachie wewe umalizie mhula.
  7. Unaitumia IKULU kukukampeinia kurudi madarakani. ninaposema ikulu rejea wito wa msajili wa vyama kuamuru myang'oe mabango ya promo yenu kwa kuwa picha zilipigwa na ikulu. Pia matumizi ya USALAMA wa TAIFA kuhakikisha na kutumia taarifa wanazokupa kwa mtaji wa kisiasa. Najua kama siyo wewe rais basi msaidizi wako aliwaagiza UwT wafuatilie suala lililotolewa maamuzi na mahakama kuu dhidi ya Slaa ambapo MNATAKA kuitumia taarifa hiyo kummaliza wiki chache kabla ya uchaguzi. Hii ni dhihaka kwa wananchi na dola
  Maoni yangu kwako ni kwamba IKEMEE familia yako na jamaa zako wanaotumia cheo chao kujiimarisha ktk mfumo.
  Uwache kutumia public office, funds and power to reinstate your presidency.
  Iache UwT ifanye kazi zake kikatiba na si kuiendesha kama jeshi binafsi la ulinzi na kuwafanyizia wabaya wako.
  ukiona huwezi haya yote JITOE kwenye kinyang'anyiro cha uraisi ili upate utukufu na heshima kwetu.

  Wewe ni rais wangu leo lakin siyo guarantee ya kuwa rais wangu awamu ijayo.
  Nina kura yangu kama wananchi wengine, usitumie nguvu kubwa (ya dola) kuitaka
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Du kumbe ni standard 7 yule maza!
   
 16. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Yeye anaangalia matumizi au anatekeleza matakwa ya watumiaji?
   
 17. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Imelda Marcos mpya wa Africa kwa kuiingiza nchi yetu kwenye matumizi makubwa yasiyo na ulazima wala faida yeyote ile!
   
 18. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Siku za imelda marcos na wewe marcos zinahesabika, utangoka kwa kura au risasi ewe mchawi mkuu kikwete
   
 19. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu mama anasahau kuwa Watanzania sio mabwege tena labda yeye na mwenzi wake ndo wamebaki kwenye ubwege. Uzuri hiki cheo cha FL si cha kikatiba, siku moja sheria inamhukumu. Anasahau hana kinga. Ama kweli kitanda cha ikulu kimegeuka kitanzi cha Watanzania
   
 20. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  vyote viwili
   
Loading...