Ben,
Kuna mahala nimekusoma ukisema hivi:-
Nachotaka mimi kuelewa ni perspective gani nyie vijana mnazo ambazo hazifungamani na old ones?. Nachokiona ni unafiki mkubwa wa vijana, vijana wetu wanatumiwa zaidi kutumikia kambi za kina EL, JK, Seif, Lipumba, Mbowe, Dr.Slaa na kadhalika while hawa wote hawana jipya la kumkomboa Mtanzania tofauti na msimamo wa vyama vyao. Nyote kwa ujumla wenu mnatumikia vyama na itikadi zake.
Ikiwa vijana mnashindwa kuja na new ideas ila mnataka kutumia ujana wenu ku discredit wazee kwa kutumia kabila au dini.. Hii kweli ndio sifa mnayotaka sisi wazee tuwakubali kwamba mnaweza kuongoza nchi ilihali nyie wenyewe mna makabila na dini zenu!. Nani anapingana na mfumo wa elimu na Afya iliyopo..Nani anapingana dhidi ya jinsi wakulima, miners, na wafanyakazi wanavyo nyanyaswa na kusukumwa chini zaidi kuwa ngazi za matajiri?..
Jamani hata Ukapteni wa team ya mpira hupewa mwenye sifa na uzoefu ambao kauonyesha na experience matters. hadi sasa hivi mnashindwa kutuonyesha zaidi ya Zitto wakati ule kuonyesha msimamo wake juu ya posho na sii vijana wote wanaafiki.
Mimi nauliza nyie vijana what do you bring on the table?..Ni fikra zipi mpya mlonazo, maana nawaona mkibishana sana juu ya Ufisadi wengine mkisema Ufisadi sio tatizo bali tatizo ni uzalishaji. Ni mawazo sawa kabisa na wazee sioni tofauti yoyote baina ya vijana na wazee ikiwa upeo wenu wote unaishia palepale.. Utazalisha vipi ikiwa kila unachopanda kinakuwa sabotage.. Na hakuna kijana hata mmoja anayepiga vita Ufisadi kwanza ili tukija panda mimea ikue na tuvune kilicho bora. Wote mmejipanga nyuma ya JK, RL na wengineo kwa nini sisi wananchi tusiwaamini hao hao mnaowasujudia?
Mkuu Mkandara,
Asante sana kwa mchango wako.Wachanijisemee na nisiwasemee wengine.
1.Kwenye chama cha siasa ninapenda kuunga mkono itikadi.Kwa hali iliyopo Tanzania vyama vyetu vina mapungufu kwenye itikadi hasa kuhusu mfumo wa uchumi ambao ni kigezo kinachotoa muongozo wa aina ya Siasa nchi inafanya na uongozi kwa ujumla.Nikiwa mwanachama wa Chadema naona itikadi ya chama changu ni nzuri kulinganisha na itikadi za vyama vingine hata tuki-fanya modification hatutapata shida sana ukilinganisha na vyama vingine
2.Ukiniona naunga mkono mtu au kambi (kambi ni jambo la kawaida wakati wa uchaguzi kwenye vyama vya siasa) basi ujue naunga mkono kile anachosimamia kulingana na itikadi ninayoamini kwamba inaweza kutuondoa kutoka level moja kwenda nyingine.
3. Ninaamini tufikie hatua vijana sasa tuwashinikize wenzetu na kuwatia moyo tuachane na siasa za matukio.Suala la posho ni tukio,kiongozi wangu na rafiki yangu Zitto Kabwe alilipigania kutokana na kuona kwamba mfumo wa uongozi na itikadi inayozalisha viongozi au wawakilishi walafi kwa gharama ya walipa kodi utachukua muda kuurekebisha.Roho ilimuuama kuona watanzania wanaendelea kugharamia anasa za wawakilishi wetu huku wao wa kiteseka katika kupata huduma stahiki za kijamii.Hata hivyo,tatizo la posho kama nilivyosema ni tukio/tunda la mfumo mbovu.
Nilifurahi kuona vijana wenzangu kama akina January na Nape ingwa ni kutoka chama tofauti na changu wakiunga mkono hoja aliyoisimamia Zitto.
4. Mabadiliko tunayopigania yamekuwa yakitafsiriwa vibaya kwamba ni kuiondoa CCM.Kumbe kuiondoa CCM ni kama kuondoa tu kikwazo kilichoko mbele ya safari yetu kuelekea kwenye mabadiliko.Kuiondoa CCM ni kuruhusu uwanja mpana wa kuleta mageuzi makubwa ya kifikra ambayo in turn yatatusaidia katika kujenga taifa adilifu,linalowajibika.Ni kweli vijana wengi sasa hivi hasa wasomi na wanasiasa vijana hawajadili tatizo katika wizara ya Elimu au Afya kwa kujenga hoja na kuzishindanisha dhidi ya Itikadi fulani baina ya chama kimoja na chama kingine au baina ya kiongozi mmoja dhidi ya Mwingine
5. Wakati sisi tunafikiria miaka 2 au mitatu ijayo na kujenga mawazo/fikra tegemezi kama viongozi hatujui kwamba tunajenga taifa lenye fikra tegemezi.Ni kama kwenye corporate world,director anatoa dira ya kampuni na subbordinates wake.The smartness of directors determines the growth and success of the company.
Hatujui kwamba wenzetu mataifa ya Ulaya na Asia wote wanaweka mikakati na fursa za miaka 100 ijayo kwa ajili ya wajukuu kujinufaisha na raslimali za Afrika ikiwemo Tanzania.Waliopo sasa ulaya wanatunyanyasa kiuchumi kutokana na furasa walizowekewa na babu zao mwaka 1900's. Sisi tunajadili matukio.
Mkuu Mkandara,Tunafanya maandalizi ya kutoa darasa la itikadi kupitia taasisi ya wanafunzi wanachama wa chadema wa sekondari na vyuo vikuu (CHASO). Vijana wengi ni wanafiki kutokana na njaa,hawaamini kama wanaweza kuwa succesfully bila kujipendekeza na kupata visenti vichache.Haya yote ni matokeo ya mfumo mbovu ambao tunatakiwa kupambanan nao.Mfumo wa kuunga watu mkono bila principles ndiyo huu unaotujengea fikra tegemezi,ufisadi,kukosa maadili majungu nk.
Unategemea kijana anayegeuzwa kibaraka wa kiongozi fulani kwa ajili ya vijisenti,siku akikutana na majaribu ya Marekani au taifa lolote la magharibi (ofcourse hawajawahi kuwa na nia njema na Afrika,ingawa diplomacy inanikataza kutamka haya ila siyo Rhetorics) kumfanya awe shushu/kibaraka kwa malipo ya madola na magari ya kifahari aache?Je,kwa mazingira haya uzalendo na uhuru wa taifa hauko mashakani?
Tunachofanya sasa ni maandalizi ya kupambana kubadilisha mfumo,we need a very radical reform based on Ideologies.We need radical reform socially,politically and Economically. We nee catalyse change, to change the attitude hasa unapokuwa ndani ya chama cha siasa.Tuandae mazingira ya kuunda responsible government,responsible policy and responsible Nation
No responsible government can afford to produce and abandon graduates to roam the streets, for we know that such attitude will force them into crime as a way of earning a living. We need device methods of taking statistics on the number of graduates turns out every year. This will enable us to provide employment opportunities and meaningfully engage them in other positive areas of livelihood. Our commitment to gainful employment will have the vulnerable groups particularly the youth and women as the main targets.
We were suppose to therefore bring to reality the small and medium scale industries that will engage our youths and women so as to enable them achieve economic empowerment and self reliance. Every single person willing to work should be able to get job training that leads to a job and earn a decent living
Tanzania's problems goes beyond probing past leaders. I think we need a generational shift that will bring about a re-orientation of our national psyche which should place value on service rather than looting. The political office is so attractive now because its an avenue to share the Natural resources money and even loot the treasury without any opposition. Imagine servicing a single Mp as a stting allowance 300,000 + more than 7m per month salary. This is crazy. Yet the country is laden with poverty stricken masses. We need the change.
We will appeal to our youth to see this as a call to change. Its high time we sideline the money bags and old corrupt politicians and take our destiny in our own hands. Lets put hands together and support a worthy cause....Hayo na mengine mengi....!