Chadema kulikoni? Utitiri wa Vyeo (Mpango madhubuti wa kulindana huku mkibomoa chama) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kulikoni? Utitiri wa Vyeo (Mpango madhubuti wa kulindana huku mkibomoa chama)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUNTEMEKE, Mar 4, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na umakini wa viongozi wake katika kuhakikisha kwamba vijana ni nguvu mabadiliko na wanauwezo wakuongoza na kulinda rasilimali za chama na mgawanyo wa madaraka.Sasa the top wa chama hicho wameamua kimyakimya kugawa madaraka/vyeo kwa watu wanaoona watatumika kulinda siri na mambo mbalimbali ya viongozi wa juu(zidumu fikra za Mwenyekiti)

  Naweza kusema CHADEMA sasa imekomaa na kukua kuliko vile jamaa walivyokuwa wanategemea,kiasi kwamba imewawea vigumu kuukumbatia mbuyu huu wenye matawi yake karibia tanzania nzima.Hii imewapa wakati mgumu wamiliki wa chama namna gani wanaweza kulinda rasilimali zao na vyeo vyao....

  Hao watu makini (tunaowaita sisi watanzania)wamekuja na mpango kabambe wa kuwagawia madaraka wale watu wanaoona watahakisha wanadumisha fikra za mwenyekiti

  Naomba kutumia baadhi ya watu kama mifano tu...ilikuleta maana ya kile ninachokisema.

  A.JOHN MNYIKA(Mbunge wa Ubungo)
  Huyu ni mbunge wa jimbo la ubungo,amepewa majukumu ya fuatayo kuhakikisha nguvu ya vijana inaonekana.
  1.Huyu ni mwenyekiti wa taasisi ya kiraia iitwayo ubungo foundation development.
  2.Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa kinondoni
  3.Mkurugenzi wa vijana makao makuu ya CHADEMA
  4.Katibu wa wabunge wa CHADEMA
  5.Waziri kivuli wa nishati na madini
  6.Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA
  7.Mjumbe wa sekretarait wa CHADEMA makao makuu
  8.Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA TAIFA
  9.Mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA TAIFA
  10.Katibu wa wabunge mkoa wa Dar es salaam
  Hivi huyu mtu anajigawaje katika majukumu yote haya,bila shaka ni kpenzi cha the top kwa sababu anadumisha fikra za mwenyekiti.

  B.HEZEKIEL WENJE
  1.Mbunge wa Nyamagana Mwanza
  2.Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema
  3.Mjumbe wa sekretarait wa Chadema
  4.Na sasa Katibu mkuu wa chadema amemteua kuwa mkurugenzi wa mambo ya nje wa chadema ambapo automatic anahudhuria vikao vya utendaji wa chama makao makuu...ambavyo karibia kila baada ya siku 2 mbili vinafanyika nainatakiwa ahudhurie,,,Jimbo lipo wazi pale mwanza kwa sababu muda wake mwingi yupo pale makao makuu kwenye vikao vya chama.

  C.MWIGAMBA
  1.Ni mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima(freeman mbowe)
  2.Ni mwenyekiti wa mkoa wa arusha
  3.NI muhasibu wa chadema makao makuu
  Huyu ameacha mkoa ukiwa hauna mwenyekiti(Dr.slaa analiona hilo) nakuitwa kuja kusimamia fedha za chama(uhasibu wa chadema makao makuu)Hadi dakika hii Arusha hapana mwenyekiti wa mkoa wa chama.

  D.BENSON MLAMBA
  1.Katibu wa CHADEMA mkoa wa tanga
  2.Afisa wa habari wa chadema makao makuu
  Huyu ameondolewa tanga kuja pale makao makuu kwa sababu za kusaidia kukumbatia mbuyu usiguswe na watu wengine.Ameacha mkoa wa tanga bila kuwa na katibu...huku Dr. akijua kwamba mkoa wa tanga hatuna diwani wala mbunge na chama kina suasua,Kwa mantiki hiyo huyu mtu alikuwa nakazi ya kujenga chama pale tanga.

  MY TAKE:
  Kumbuka hakuna chama chenye vijana wasomi na wenye utashi/uthubutu mkubwa wa kufanya mambo katika tanzania hii kama CHADEMA.....Lakini hili si rahisi kuliona Dr.slaa kwa sababu vijana waliowengi wameshatumika kwenye mbio za uchaguzi mkuu na sasa hawana thamani tena ndani ya chama hiki.
  Kuna vijana wengi sana wamejitolea kujenga chama na wengine wameshapoteza degree zao kwa sababu wanakipenda chama.Wengine wamethubutu kuingia katika vinyang'anyiro mbalimbali vya udiwani,ubunge na wengine wamekuwa wakijitolea kuratibu kampeni mbalimbali za CHADEMA lakini kwa sasa nikama makarai mabovu ya kujengea nyumba.

  Je?Kama chadema bado hawachukua dola wamesahau vijana wao,itakuwaje wakishika dola?
  Au huu ndio ule mkakati madhubuti wa kulinda na kula keki ya chama watu wa chache huku mkiweka MORANI(tajwa) pembezoni msiguswe?.

  Najua kunawatakao tukana na kukejeli kwa sabubu wamepofoka na mapenzi yao juu ya chama,huku wakijisahau kuwa chadema kinamapungufu yake hasa katika matumizi ya rasilimali watu(vijana) na kuwa dampu kama taka.
   
 2. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180

  Wewe ni Mzushi na Mzandiki mwenye kutaka kupandikiza migogoro CDM.Huna nia njema na chama zaidi ya Uchafuzi tu.Okay kwa mnyika;

  JOHN MNYIKA(Mbunge wa Ubungo)
  Huyu ni mbunge wa jimbo la ubungo,amepewa majukumu ya fuatayo kuhakikisha nguvu ya vijana inaonekana.
  1.Huyu ni mwenyekiti wa taasisi ya kiraia iitwayo ubungo foundation development.-INA UHUSIANO GANI NA CHADEMA?
  4.Katibu wa wabunge wa CHADEMA-KATIBU NI SILINDE LABDA UKO LESS INFORMED
  6.Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA-KWA UWEZO WAKE ANASTAHILI
  8.Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA TAIFA-zitto ni nani?
  10.Katibu wa wabunge mkoa wa Dar es salaam-Hii si nafasi ya CDM

  Mkuu,hata kama unavitaka vyeo hivi wewe huwezi pewa kwa sababu huna sifa yoyote zaidi ya uzandiki
   
 3. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Majungu Express on the move...vijana hivi vyeo vitawaumiza sana matumbo fanyeni kazi mjiletee maendeleo kwani lazima wote muingie Bavicha? Heche sasa yuko kwenye full time employment hadi 2016.
   
 4. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hivi anakaimu ukatibu mkuu wakati dr slaa yupo?
  Na naibu si zitto kabwe?
  Kuna thread moja jana wadau walisema unahasira za kukosa uenyekiti bavicha. Mkuu sasa tunaunganisha moja na moja.
   
 5. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Mkuu EasyFit,
  Umetoa point ya maana sana,watu wafanye kazi.Huyu jamaa anaitwa TUNTEMEKE amekalia majungu tu always.Ananikera sasa
   
 6. aloveragel

  aloveragel Member

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chama kinajengwa na wanachama wenyewe na uongozi imara ni hule wenye uzoefu wa kutosha hli kwenda na mkikiki sa unataka wakuweke wewe NONSENSE ambaye hata exprience ya kuongoza watu kumi shida utaweza vjana zaidi ya mili 20 waliotapakaa nchi nzima 2mia akili umetumwa na MAGAMBA au NAWE NI MWANAASHA KWA KUSHINDWA KUFIKIRI JAMBO DOGO
  my take.
  chama kinaitajika kiwe na watu MAKINI na wenye uzoefu wa kutosha kwani kinapanuka kwa kasi mno

  USHAURI WAKO MZURI LAKINI HATUTAUFANYIA KAZI
   
 7. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  TUNTEMEKE tena wewe sio tu unastahili kuwa dumped tu,wewe unastahili kuwa shreaded
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  a. Mnyika ana uroho wa madaraka na hii ni hatari huwezi kusema no please..unajua vyao hadi 10 lol..

  b. Mnyika ameziba nafasi 7 muhimu za vijana wengine kuonyesha uwezo wao...na ajira pia..

  c. Mnyika either ana uwezo sana au ni kwamba ni yes man..vyeo zaidi ya 10?

  conclusion: Nimesahau kumbe tunaongelea chagga development manifesto..lol
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu, Tuntemeke, ukileta ukosoaji wowote wa Chadema humu jukwaani, najua kitakachokupata.

  Japo mimi sio Chadema na huwa huru to speak my mind, nimekusoma na kugundua mwenzangu una matatizo!. Kwa wewe ni Chadema, si busara kuleta sebuleni kuanika nguo zenu za ndani mbele ya wageni!. Acha kwanza huyu mgeni kwa jina la 'Arumeru' apite ndipo uendelee kutuanikia mauchafu yenu ya ndani mbele ya kadamnasi ya watu kwa kudhani yatasaidia!.

  Kisaikolojia unaonekana kuna vitu umeumizwa, na inawezekana wewe nyota yako ni nnge, hivyo umedhamiria ku hit back with a sting, ili kujeruhi Chadema, ili kikiangukia pua huko Arumeru, wewe ndio upate gratification!.

  Just do the right thing at the right time!, this is not the right time kwa hayo. Sasa Chadema needs to come together mote than anyother time, ili kikishindwa, kisitafute mchawi bali kikae chini na kujitathmini upya, sio kuangalia wapi kilipoangukia, bali pale walipo jikwaa!.

  Pasco
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Hiyo ndio chadema bana..lol
   
 11. T

  Topical JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Unamshauri mwenzako kuficha maovu..

  Sio tabia nzuri kuendekeza vyama vinavyopata ruzuku ya serikali..

  Heri yeye amesema kuliko anayetaka kuficha ukweli.
   
 12. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Mkuu Pasco,

  Ni kweli kuan hulka hiyo hasa katika challenges zizazo iface CDM.Ila mleta mada anaonekana kama yuko kwenye vita na CDM,Sio mkosoaji kama anavyojiita yeye.Ni mtu ambaye anahuzunika kutokana na kukosa nafasi fulani.So anaamua kukichafua chama kwa nguvu zote.Nina wasiwasi atakuwa sio MwanaCDM kwa maana ya kuwa na Mapenzi na CDM.Amekuwa Pandikizi na CDM wamemgundua na kumweka pembeni,so is fighting the war
   
 13. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Majibu ya mwanamke si kuzote niyakukukurupuka..wewe mtu gani atapewa vyo zaidi ya 10?akina mabere marando hawapo?akina mwesiga baregu wapo wapi?
   
 14. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Bavicha,bavicha yaani kila kelel wewe unaelekza bavicha sehemu ambyo kituo kilisha hamishwa mapema.Utasema majungu,utasema kila aina ya neno lakini ukweli utabakia palepale CHADEMA inawasomi wengi na wenye uzoefu wa kazi lakini nafasi yao inafutika kutokana na mtindo huu wa mora
   
 15. aloveragel

  aloveragel Member

  #15
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwel PAA MBUMBUMBU we marando unajua yupo wapi nenda darasan bwana mdogo jamii forum inatakiwa iheshimke m2 anayechangia anakiwa awe na elimu kuanzia bachelor huyu pu..bavu kama mwanaasha nimekudharau sana kwa kukurupuka pasipo kujua mambo kavae nguo ndo uje uchangie
   
 16. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mawazo ya TUNTEMEKE hayapishani na haya

   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Topical, sijamshauri kuficha maovu kwa sababu mimi mwenyewe ni mkosoaji!. Kwa vile yeye ni Chadema tena anaonekana ni inside man, kwanza sio busara siri za ndani kuzitoa nje!. Pili saa hizi mmekusanyika sebuleni wageni kibao kujadili mahari ya mwali mpya kwa jina la Arumeru, sio vizuri kuanza kuanika kulalamika mbele ya wageni kisa tuu wewe ulikosa nyama!. Acha wageni wa mahari waondoke kalipieni hiyo mahari mumpose mchumba na mkishampata mchumba "Arumeru" ndipo unapeleka malalamiko yako. Hii sio timing nzuri kulalamika!. Mwenzenu ambae haio, mwishoe ataoa huku mnashuhudia!, shutuma zote za kumkosa mchumba zitakushukia wewe!.

  Ila pia huyu jamaa ana tabia za kike zinaitwa 'naging' yaani analeta gubu kwa Chadema kama mke aliyeichoka ndoa sasa anafanya visa ili apewe talaka ndipo aende kwa bwana mwingine!. Namshauri ajiendee zake kwa huyo bwana bila kuleta kashfa kibao!. Tuntemeke just go!.
   
 18. W

  WikiLeaks Member

  #18
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Please can someone help me to differentiate these two photos who is who

  [​IMG] and [​IMG]

  thanks, see you soon.
   
 19. b

  bensonlifua92 Member

  #19
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
   
 20. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Just imagine jamaa anasema tukae kimya eti kwa sababu mgeni amewasiri?yaani hakuna kuisema CHADEMA kwa sababu ya uchaguzi wa arumeru?upo adicted na mapenzi ya chadema kiasi hiki?...pole.
  Kunautofauti gani na CCM waosema no kuandamana au kudai haki yako yoyote hadi BUSH aoondoke?akisha ondoka ndipo tufungue midomo yetu.Pole sana pasco
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...