Chadema kulikoni? Utitiri wa Vyeo (Mpango madhubuti wa kulindana huku mkibomoa chama)

Status
Not open for further replies.

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,355
2,000
Ukiona mtu anajadili mambo ya aina hii ujue ni dalili za fikra zilizonyauka.Taifa sasa hvi liko katika wakati mgumu,tutumie muda na raslimali zetu kulitoa Taifa hapa lilipo.Watanzania hawataki kusikia nani kalala na nani au nani mwenye vimada.Labda tupiganie kuweka mfumo wa kuhakikisha ufisadi na matumizi mabaya ya kodi za wananchi kugharamia matumizi binafsi yanakwisha.Badala ya kujadili ideas za kuhakikisha tunakuwa na taifa adilifu na kuweka mfumo wa kuzuia matanuzi kupitia kodi wewe unataka watu wajadili vitu vya hovyo ati nani kalala na nani.Watanzania wanataka kusikia hoja na fikra sahihi za kutukwamua hapa tulipo na si urijali wa kitandani.

Nuclear 1, It is absolutely wrong to use tax payers money to sponsor harlots, concubines, political thugs and politicians on yearly pilgrimages.Hapa ndipo tunapotakiwa kujadili.Vijana ambao hawajaoa/kuolewa kuwa na uchumba bila kuathiri public interests tangu lini ikawa uhaini?Acha uzushi na majungu na sasa tujadili ideas,tuachane na personal vendatta! Tuna kazi kubwa ya kubadilisha taifa hili kifikra,nitaanza hapa kukubadilisha wewe kifikra mkuu.

Sir,the demographic orientation of the nation today is youthful and the aspiration of the youth demands dynamism, vibrancy and change. Tanzanians now demand and clamor for old ideas to be discarded while new and fresh perspectives are embraced in an effort to find solutions to the socio-economic deadlock that the nation has been saddled with for so long!

It is our candid expectation that along with old ideas, the old, sacred and fat vultures of the old order will have enough wisdom to take a back seat and retire into oblivion.

Mkuu Ben umenena vyema na kama kawaida mimi huwa nazikubali post zako. Kwa sasa Tanzania ina tatizo kubwa la ufisadi; lakini mkuu Ben umewahi kupitia Kamusi ya Kiswahili Sanifu na kudurusu maana ya ufisadi. Bahati mbaya sina citation hapa lakini kama una nafasi na una Kamusi ipitie uone maana ya ufisadi. Hii itasaidia kuwa na mijadala hai na kulitumia neno fisadi katika muktadha muafaka.

Ben Tanzania pia inasumbuliwa na ukosefu wa uadilifu. Kuna Dr. (PhD) wangu aliniambia kuwa kuna utafiti ulifanywa na kuonyesha kwamba 75% ya makampuni (taasisi) yamefanikiwa kwa sababu ya kuwa na wafanyakazi waadilifu. Unaweza ukawa na wafanyakazi wote ambao vyuoni walipata distinctions lakini kama si waadilifu kampuni haiwezi kufanikiwa. Uadilifu ni neno pana kweli (kunatofauti kubwa kati ya Honesty na Integrity). Kutokuwa mwaminifu katika mahusiano pia ni ukosefu wa uadilifu. Kama si mwaminifu kwenye mahusiano huwezi kuwa mwaminifu kwenye maeneo mengine (ni mawazo yangu tu). Pia kiongozi yeyote ni public figure na yuko subject to public scrutiny in his/her public life.

Ni vyema tukasisitiza tuwe na viongozi waadilifu. Walichokisema vijana hapa ni Rushwa ya Ngono; sijui kama kuna lugha nyingine zaidi ya hiyo.

Sitaki mtu aje hapa na mfano wa Billy Jaferson.
 
TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
2,000
Sasa mkuu hujui hasira za kushindwa Bavicha wanadhani Mbowe na Slaa ndio walichangia.Hawajui ni demokrasia ilifanya kazi.Hawa wote nawafahamu vizuri kwa majina yao ndio maana najibizana nao kwa njia hiyo.Hiki ni kigenge tu cha wahuni kisicho na athari yoyote ndani ya chama.Huku wakipiga majungu JF siye wenzao tuko Arumeru i[tunapiga kampeni za nyumba kwa nyumba na ushindi uko mikonon/QUOTE].

chadema ikishinda arumeru njooni mnikate kichwa changu. napatikana sinza mori hapa karibu na hospitali ya wachina.
njooni mnitoe hata utumbo
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,592
2,000
Mkuu Ben umenena vyema na kama kawaida mimi huwa nazikubali post zako. Kwa sasa Tanzania ina tatizo kubwa la ufisadi; lakini mkuu Ben umewahi kupitia Kamusi ya Kiswahili Sanifu na kudurusu maana ya ufisadi. Bahati mbaya sina citation hapa lakini kama una nafasi na una Kamusi ipitie uone maana ya ufisadi. Hii itasaidia kuwa na mijadala hai na kulitumia neno fisadi katika muktadha muafaka.

Ben Tanzania pia inasumbuliwa na ukosefu wa uadilifu. Kuna Dr. (PhD) wangu aliniambia kuwa kuna utafiti ulifanywa na kuonyesha kwamba 75% ya makampuni (taasisi) yamefanikiwa kwa sababu ya kuwa na wafanyakazi waadilifu. Unaweza ukawa na wafanyakazi wote ambao vyuoni walipata distinctions lakini kama si waadilifu kampuni haiwezi kufanikiwa. Uadilifu ni neno pana kweli (kunatofauti kubwa kati ya Honesty na Integrity). Kutokuwa mwaminifu katika mahusiano pia ni ukosefu wa uadilifu. Kama si mwaminifu kwenye mahusiano huwezi kuwa mwaminifu kwenye maeneo mengine (ni mawazo yangu tu). Pia kiongozi yeyote ni public figure na yuko subject to public scrutiny in his/her public life.

Ni vyema tukasisitiza tuwe na viongozi waadilifu. Walichokisema vijana hapa ni Rushwa ya Ngono; sijui kama kuna lugha nyingine zaidi ya hiyo.

Sitaki mtu aje hapa na mfano wa Billy Jaferson.

Mkuu wangu,

Kama utasoma post yangu tena utaona mahali nilikosizitiza kuhusu maadili.Nimesizitiza tupigania kubadili fikra na mfumo mzima unaoruhusu Kuwa na taifa lisilo adilifu.Pia mimi ni muumini mkubwa wa falsafa ya kama huwezi kuwa mwaminifu katika mambo madogo huwezi kuwa mwaminifu kwenye mambo makubwa.Ofcourse,infidelity consitutes the breach of trust and trust actually is a central character component of a good leader. Rejea mandishi ya cal thomas / infidelity and Leadership aliyoandika juu ya mgombea Urais Garry Hart na concubine mwanamama Donna Rice

Hata hivyo,post ya nuclear1 ilikuwa imekaa kuchafua watu tu.Siwezi kuwasemea wengine.Lakini mimi nazingatia uadilifu,na sijawahi kupenda kuwa promiscous naamini katika maadili.Ila pia nimetoa angalizo,tujadili ideas zitakazoondoa fursa kwa watu wasio na uaminifu katika social life kushika public office . Rejea tena maandishi ya Cal Thomas mkuu halafu rejea pia post yangu ya awali nilipomjibu nuclear1.Pia kuhusu tafsiri ya ufisadi,asante kwa ushauri na nitalizingatia hilo zaidi kwenye mjadala.
 
Hamuyu

Senior Member
Mar 29, 2010
118
195
Mkuu hapo umeweka ***** mwingi sana, kwa bahati mbaya sina muda, ila ukiteuliwa kuwa Mkurugenzi kwa nafasi hiyo unakuwa mjumbe wa Sekretarieti hivyo sio sawa kutenganisha Ukurugenzi na ujumbe wa Sekretarieti, Mnyika pia ni mjumbe wa Kamati Kuu asiye na kura kutokana na nafasi yake ya kuwa Mkurugenzi ni ex official member, mengine mengi ni ***** tu sina muda, CDM ni chama makini soma katiba yake na kanuni utaelewa kwamba hatupeani vyeo kama sadaka.
 
nahavache

JF-Expert Member
Apr 3, 2009
869
250
Hivi kuwa mjumbe nako ni cheo? Ni vizuri CHADEMA ikawa na timu ndogo yenye tija. Ila huu ni uzushi mkubwa sana na huyu jamaa ni mharibifu. Kuwa na changamoto ni jambo jema, lakini CHADEMA iwe makini na habari zake kutoka kwa TUNTEMEKE
 
panadol

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
349
0
Mkuu Tuntemeke Kubali kataa Nyota ya Mnyika, Zitto zinang'aa sana Unachofanya hapa Tanga na Sumbawanga wanasema "Unajaribu Kusafiria Nyota za Jamaa".

Mi Nakushauri Kuliko kupigania Kuia CDM ili Tikose wote ni Vyema Muangalie nini Kilichofanya Chama Chenu cha KAFU KIFE

Hapa si suala la nyota ya mtu fulani kinachozungumzwa hapa ni suala la mtu mmoja kulimbikiziwa vyeo lukuki wakati wapo vijana wengi wenye uwezo kufanya kazi hizo mtake msitake huo si mgawanyo mzuri wa madaraka katika hali ya kawaida sisi wananchi mmetushtua mnathibitisha kuwa hiki chama cha watu fulani kwa manufaa yao kwa hali hii ni bora nichague CCM wanaonekana wanamgawanyo mzuri wa madaraka kuliko na wameimarika kidemokrasia kuliko CHADEMA ,NCCR au CUF hivi vinaonekana ni vyama vya watu fulani kwa masilahi yao binafsi na wala si kwa manufaa ya umma wa watanzania!
 
ngilenengo1

JF-Expert Member
Feb 14, 2012
1,277
2,000
TUMTEMEKE ndugu yangu mpendwa, Kihoro chako kitakutoa mavi,

Hivi kweli Katibu wa wabunge dar unataka upewe wewe? hujui kuwa katibu wa wabunge dar wanachaguana wabunge wenyewe au ulitaka atoke ccm?

Hv mzigo anaopiga Mnyika ukipewa utaufikisha kweli? Kumbuka kuwa mtu anarundikiwa majukumu lukiki kutokana na jinsi wenzake wanayomwamini katika utebaji wake, na sio kupeaqna vyeo kwa kufurahishana.

Pia fahamu kuwa nyeo vingine vinaendana na nafasi aliyonayo kama Mbunge. Huwezi kupewa wewe? Hata yeye Mnyika angependa kupumzika lakini afanye je? Ndo kasha aminiwa hivyo!

BAdala la vivu tumwombee Myika kwa Mungu ili alisaidie Taifa hili kwa nafasi ya Urais kwa siku zijazo.

Mungu ibariki Tanzania, MUNGU mbariki MNYIKA JOHN
 
ngilenengo1

JF-Expert Member
Feb 14, 2012
1,277
2,000
Mkuu nimekusikia na bila shaka malalamiko yako yamefika hakuna sababu ya kuendelea kupiga madongo ikiwa kweli nia yako ni kuufikisha ujumbe huu kwa wahusika. Majibu ulopewa hawakuridhisha na nadhani sii rahisi kwa kiongozi yeyote ktk jumuiya zetu kuweza kuwaridhisha wanachama wake kwa ahadi za uongo ama majibu ambayo hayakutegemewa..

Umesema wewe ni mwanachama wa Chadema, sawa sasa imekuwaje hili swala limekuja wakati huu au ndio kwa sababu ya uchaguzi wa Arumeru? maana hukuridhika na Uteuzi wa John Mrema sasa baada ya hapo umekuja natuhuma nyingine kubwa zaidi kwa viongozi na sio tena vijana wa BAVICHA..Mbona waonekana kama unatakja kumchagulia baba mke ili hali mapenzi na huduma za mtoto hazihusiani na zile za mama?

Anyway, kuhusiana na hao waajiriwa, Je unaweza kutupa list ya watu walioomba nafasi hizo hizo na kukataliwa akachaguliwa huyo H. M maana nijuavyo mimi kuna kazi za ajira ofisini ambazo huombwa na sii lazima mtumishi huyo awe mwanaharakati. Kama huyo mdada yupo kitengo cha Uhasibu na yeye ni darasa la saba unajuaje kama kazi anazozifanya ni kufagia na kutunza barua na files za kiofisi, kazi ambayo wewe mpiganaji msomi usingeikubali?.

Mimi nadhani ungetenganisha kabisa kazi za kukitangaza chama na kazi za kiofisi ambazo hazihusiani kabisa na wanaharakati wapambanaji halafu zaidi ya haya hoja yako imetoka ktk kuhoji nafasi hizi za kukitangaza chama zinavyotolewa na kwenda zaidi ya kwamba hawa watu wa Ofisini makao makuu wanaficha uchafu wa Mbowe na Mnyika. Mkuu wangu unajua kwamba hizi ni tuhuma nzito sana kwa mwanachama kufanya hivyo?. Hivi kweli unataka sisi tuamini kwamba internal/external auditing wameshindwa kugundua uchafu wa Mbowe, dr.Slaa au Mnyika kutokana na hawa watu ambao unasema wameajiriwa na wamemaliza darasa la saba?.

Mkuu wangu tumeyasikia mengi sana, na mengi ni uzushi japokuwa yapo ya ukweli ambayo chama kinatakiwa kuyatazama. Na nina hakika sasa hivi chama kipo ktk wakati mgumu zaidi kutokana na ukubwa wake kila mtu anataka nafasi lakini isiwe sababu ya mtu kutafuta mchawi. La muhimu kuliko yote ambalo nawaomba sana viongozi wa CDM ni kuitafuta suluhu ya mgogoro huu hasa kutoka kambi ya Zitto na Mbowe kama kambi hizi zipo na iwekwe kanuni kali inayozuia makundi...wanachama should be royal to the party na ikigundulika mtu anajaribu kuunda uadui basi kiongozi huyo atapoteza nafasi yake ama mnafikoon kuvuliwa uanachama.

Mbowe na Zitto wawekwe kikaangoni na ifahamike wapi kuna tatizo maana sasa hivi imefikia mahala sasa hivi Zitto hawezi kuandika kitu JF wala kushauri kitu kwa sababu ya utovu wa hawa vijana wetu. Kuyamaliza matatizo yote haya ni kuwepo na suluhu baina ya viongozi wenyewe.. Waliyafanya vivyo hivyo kwa Mbowe alipokuja hapa kijiweni ikawa kila mtu kumtolea matusi mazito ya nguoni. Nimeona pia kwa Nape na viongozi wengine waliojaribu kujihusisha na mjadala huu lakini badala ya kuuliza maswali na kuhoja MTAZAMO wa viongozi hawa imekuwa swala la Personal na kukebehi hata sababu zao kuwepo CDM au CCM.. haipendezi wakuu zangu haipendezi. halafu naambiwa ati nyie ndio vijana mnaotaka kugombea Urais - Hekima iko wapi?

Kuna matatizo CDM tuyazungumze kwa kutafuta suluhu na sio kujenga majungu. Binafsi yangu sikubaliani na maswala mengi ya kimsimamo na mengine ya kisera na Chadema lakini nayaweka wazi bila kutaja jina la mtu japokuwa sikubaliani na msimamo au mtazamo wa kiongozi au viongozi. Ila wanaponisoma hapa JF wanajua fika kwamba Mkandara hakubaliani na mimi/sisi ktk swala kadhaa wa kadhaa.. inatosha kuwakilisha ujumbe.

La Mwisho, nataka ujue kwamba watu wote walioko ktk kampeni za Romney au hata Obama hawana ajira ofisi za Republican wala Demokratic, hii ni team ya kampeni ambayo haihusiani kabisa na ajira za ofisi za chama. Ila kulingana na mzingira yetu tunawatumia vijana hao pia ktk kazi ambazo ni za chama inapobidi lakini hakuna ulazima..
Ndg. Makandara nakupa BIG UP saana. Maelezo yako nayakubali 99% THANX
 
Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
0
Yawezekana hili nalo lipo,ni comment iliyonitia nguvu kuwa kunawengi wanaojua maovu ndani ya chadema.Ngoja tupeleleze then tuje na data kamali juu ya huuu ufisadi.

Hayo maneno mkuu. Maumivu ya kichwa huanza polepole! Nilikuwa najiuliza siku zote. Hawa mashujaa ambao hukabiriana na risasi za moto wakiwa front line wako wapi? Nahisi hapa kuna tatizo kubwa kuliko hata CCM.
 
makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,642
2,000
a. Mnyika ana uroho wa madaraka na hii ni hatari huwezi kusema no please..unajua vyao hadi 10 lol..

b. Mnyika ameziba nafasi 7 muhimu za vijana wengine kuonyesha uwezo wao...na ajira pia..

c. Mnyika either ana uwezo sana au ni kwamba ni yes man..vyeo zaidi ya 10?

conclusion: Nimesahau kumbe tunaongelea chagga development manifesto..lol

Topical pambaf!!!

Mbona hao wa Chama Cha Magamba wana vyeo lukuki kwa kila mmoja na hamuwasemi???Yaani kwa viongozi wa CDM kuwa na vyeo zaidi ya kimoja imekuwa nongwa???Hii ni kuonyesha kuwa mtu anapewa kushika madaraka au nafasi kutokana na uwezo wake kiutendaji. Hizi kelele zenu ni za wivu tu!

Hebu acheni hizo enyi wanafiki na wambeya!
 
MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,373
2,000

Tusiwalaumu CHADEMA, ni halali kwao vyeo kupeana wachache hiyo yote kwa kuwa wana watu wachache wenye uwezo na sifa za madaraka. Walio wengi ni wafuasi wa kuandamana tu!!
!:shock::shock: Mtu kama Albedo alichozoea ni kushika bango wakati wa maandamano!!
 
OPTIMUS TZ

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
391
0
clip_image002.gif
By TUNTEMEKE
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na umakini wa viongozi wake katika kuhakikisha kwamba vijana ni nguvu mabadiliko na wanauwezo wakuongoza na kulinda rasilimali za chama na mgawanyo wa madaraka.Sasa the top wa chama hicho wameamua kimyakimya kugawa madaraka/vyeo kwa watu wanaoona watatumika kulinda siri na mambo mbalimbali ya viongozi wa juu(zidumu fikra za Mwenyekiti)

Naweza kusema CHADEMA sasa imekomaa na kukua kuliko vile jamaa walivyokuwa wanategemea,kiasi kwamba imewawea vigumu kuukumbatia mbuyu huu wenye matawi yake karibia tanzania nzima.Hii imewapa wakati mgumu wamiliki wa chama namna gani wanaweza kulinda rasilimali zao na vyeo vyao....

Hao watu makini (tunaowaita sisi watanzania)wamekuja na mpango kabambe wa kuwagawia madaraka wale watu wanaoona watahakisha wanadumisha fikra za mwenyekiti

Naomba kutumia baadhi ya watu kama mifano tu...ilikuleta maana ya kile ninachokisema.

A.JOHN MNYIKA(Mbunge wa Ubungo)
Huyu ni mbunge wa jimbo la ubungo,amepewa majukumu ya fuatayo kuhakikisha nguvu ya vijana inaonekana.
1.Huyu ni mwenyekiti wa taasisi ya kiraia iitwayo ubungo foundation development.
2.Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa kinondoni
3.Mkurugenzi wa vijana makao makuu ya CHADEMA
4.Katibu wa wabunge wa CHADEMA
5.Waziri kivuli wa nishati na madini
6.Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA
7.Mjumbe wa sekretarait wa CHADEMA makao makuu
8.Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA TAIFA
9.Mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA TAIFA
10.Katibu wa wabunge mkoa wa Dar es salaam
Hivi huyu mtu anajigawaje katika majukumu yote haya,bila shaka ni kpenzi cha the top kwa sababu anadumisha fikra za mwenyekiti.

B.HEZEKIEL WENJE
1.Mbunge wa Nyamagana Mwanza
2.Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema
3.Mjumbe wa sekretarait wa Chadema
4.Na sasa Katibu mkuu wa chadema amemteua kuwa mkurugenzi wa mambo ya nje wa chadema ambapo automatic anahudhuria vikao vya utendaji wa chama makao makuu...ambavyo karibia kila baada ya siku 2 mbili vinafanyika nainatakiwa ahudhurie,,,Jimbo lipo wazi pale mwanza kwa sababu muda wake mwingi yupo pale makao makuu kwenye vikao vya chama.

C.MWIGAMBA
1.Ni mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima(freeman mbowe)
2.Ni mwenyekiti wa mkoa wa arusha
3.NI muhasibu wa chadema makao makuu
Huyu ameacha mkoa ukiwa hauna mwenyekiti(Dr.slaa analiona hilo) nakuitwa kuja kusimamia fedha za chama(uhasibu wa chadema makao makuu)Hadi dakika hii Arusha hapana mwenyekiti wa mkoa wa chama.

D.BENSON MLAMBA
1.Katibu wa CHADEMA mkoa wa tanga
2.Afisa wa habari wa chadema makao makuu
Huyu ameondolewa tanga kuja pale makao makuu kwa sababu za kusaidia kukumbatia mbuyu usiguswe na watu wengine.Ameacha mkoa wa tanga bila kuwa na katibu...huku Dr. akijua kwamba mkoa wa tanga hatuna diwani wala mbunge na chama kina suasua,Kwa mantiki hiyo huyu mtu alikuwa nakazi ya kujenga chama pale tanga.

MY TAKE:
Kumbuka hakuna chama chenye vijana wasomi na wenye utashi/uthubutu mkubwa wa kufanya mambo katika tanzania hii kama CHADEMA.....Lakini hili si rahisi kuliona Dr.slaa kwa sababu vijana waliowengi wameshatumika kwenye mbio za uchaguzi mkuu na sasa hawana thamani tena ndani ya chama hiki.
Kuna vijana wengi sana wamejitolea kujenga chama na wengine wameshapoteza degree zao kwa sababu wanakipenda chama.Wengine wamethubutu kuingia katika vinyang'anyiro mbalimbali vya udiwani,ubunge na wengine wamekuwa wakijitolea kuratibu kampeni mbalimbali za CHADEMA lakini kwa sasa nikama makarai mabovu ya kujengea nyumba.

Je?Kama chadema bado hawachukua dola wamesahau vijana wao,itakuwaje wakishika dola?
Au huu ndio ule mkakati madhubuti wa kulinda na kula keki ya chama watu wa chache huku mkiweka MORANI(tajwa) pembezoni msiguswe?.

Najua kunawatakao tukana na kukejeli kwa sabubu wamepofoka na mapenzi yao juu ya chama,huku wakijisahau kuwa chadema kinamapungufu yake hasa katika matumizi ya rasilimali watu(vijana) na kuwa dampu kama taka.

a. Mnyika ana uroho wa madaraka na hii ni hatari huwezi kusema no please..unajua vyao hadi 10 lol..

b. Mnyika ameziba nafasi 7 muhimu za vijana wengine kuonyesha uwezo wao...na ajira pia..

c. Mnyika either ana uwezo sana au ni kwamba ni yes man..vyeo zaidi ya 10?

conclusion: Nimesahau kumbe tunaongelea chagga development manifesto..lol

Mzazi Shetani aliyendani yako anakusumbua sana hii ya mwisho inahuska vipi unataka kueneza chuki tu Myika ni mchagga?
 
Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
6,824
2,000
Tuntemeke kaka angu! acha wivu wa kike....kama umesoma na kuelimika ningekuomba utafute kazi ya kufanya, hasa kazi
uliyoisomea kuliko upuuzi huu unaoufanya hapa! yaani ulitegemea au bado unategemea siasa ikutoe kimaisha? Achana na
fikra hizo ndugu yangu....si unaona sasa unavyojionesha kuwa wewe ni bonge la mswahili na una wivu wa kike? Mkuu acha kutegemea siasa,tafuta kazi,uipende kazi na hiyo kazi itakutoa kimaisha....siasa fanya kama part time tu na si vinginevyo.
Binafsi mie mwenzio ni kijana,umri wangu siko chini ya miaka 30 na sijafikisha miaka 35....huwezi amini nina ofisi yangu na
nina mastaff kama 9 hivi tena wengine ni watu wazima kabisa na wananitegemea mimi! Japo sometime silali usingizi kwa
presure za mikopo ya bank,lakini siku zinakwenda na ofisi yangu inazidi kuwa kubwa ndani ya bongo. Naipenda ofisi yangu,naipenda kazi yangu na ninawapenda mastaff wangu....ila pia imetokea tu kuwa mimi ni mshabiki wa Chadema,lakini oneday nitakwenda pale K/ndoni kuchukua kadi ya uwanachama. So fanyakazi mkuu na uache majungu.

Mkuu achana na huyo jamaa mimi nafikiri kunakitu alitegemea kukipata pale chadema amekikosa labda kwa sababu ya majungu yake , uwezo mdogo au hana mvuto sasa ameamua kupandikiza chuki na majungu mimi natamani sna wamtaje huyu mtu kwani hafai na anatakiwa kutegwa kama anaukoma.
Ni kweki chama kinatakiwa kukosolelewa lakini siyo kwa staili hii ya kuattack mambo ya pesornal kwanini asiwambie privite anakuja kuanika hapa.
 
Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,195
Hapa si suala la nyota ya mtu fulani kinachozungumzwa hapa ni suala la mtu mmoja kulimbikiziwa vyeo lukuki wakati wapo vijana wengi wenye uwezo kufanya kazi hizo mtake msitake huo si mgawanyo mzuri wa madaraka katika hali ya kawaida sisi wananchi mmetushtua mnathibitisha kuwa hiki chama cha watu fulani kwa manufaa yao kwa hali hii ni bora nichague CCM wanaonekana wanamgawanyo mzuri wa madaraka kuliko na wameimarika kidemokrasia kuliko CHADEMA ,NCCR au CUF hivi vinaonekana ni vyama vya watu fulani kwa masilahi yao binafsi na wala si kwa manufaa ya umma wa watanzania!

Vyeo gani hivyo Mkuu?
 
Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,195

tusiwalaumu chadema, ni halali kwao vyeo kupeana wachache hiyo yote kwa kuwa wana watu wachache wenye uwezo na sifa za madaraka. Walio wengi ni wafuasi wa kuandamana tu!!
!:shock::shock: mtu kama albedo alichozoea ni kushika bango wakati wa maandamano!!

lipu kafu
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Ben,
Kuna mahala nimekusoma ukisema hivi:-
Sir,the demographic orientation of the nation today is youthful and the aspiration of the youth demands dynamism, vibrancy and change. Tanzanians now demand and clamor for old ideas to be discarded while new and fresh perspectives are embraced in an effort to find solutions to the socio-economic deadlock that the nation has been saddled with for so long!
Nachotaka mimi kuelewa ni perspective gani nyie vijana mnazo ambazo hazifungamani na old ones?. Nachokiona ni unafiki mkubwa wa vijana, vijana wetu wanatumiwa zaidi kutumikia kambi za kina EL, JK, Seif, Lipumba, Mbowe, Dr.Slaa na kadhalika while hawa wote hawana jipya la kumkomboa Mtanzania tofauti na msimamo wa vyama vyao. Nyote kwa ujumla wenu mnatumikia vyama na itikadi zake.

Ikiwa vijana mnashindwa kuja na new ideas ila mnataka kutumia ujana wenu ku discredit wazee kwa kutumia kabila au dini.. Hii kweli ndio sifa mnayotaka sisi wazee tuwakubali kwamba mnaweza kuongoza nchi ilihali nyie wenyewe mna makabila na dini zenu!. Nani anapingana na mfumo wa elimu na Afya iliyopo..Nani anapingana dhidi ya jinsi wakulima, miners, na wafanyakazi wanavyo nyanyaswa na kusukumwa chini zaidi kuwa ngazi za matajiri?..

Jamani hata Ukapteni wa team ya mpira hupewa mwenye sifa na uzoefu ambao kauonyesha na experience matters. hadi sasa hivi mnashindwa kutuonyesha zaidi ya Zitto wakati ule kuonyesha msimamo wake juu ya posho na sii vijana wote wanaafiki.

Mimi nauliza nyie vijana what do you bring on the table?..Ni fikra zipi mpya mlonazo, maana nawaona mkibishana sana juu ya Ufisadi wengine mkisema Ufisadi sio tatizo bali tatizo ni uzalishaji. Ni mawazo sawa kabisa na wazee sioni tofauti yoyote baina ya vijana na wazee ikiwa upeo wenu wote unaishia palepale.. Utazalisha vipi ikiwa kila unachopanda kinakuwa sabotage.. Na hakuna kijana hata mmoja anayepiga vita Ufisadi kwanza ili tukija panda mimea ikue na tuvune kilicho bora. Wote mmejipanga nyuma ya JK, RL na wengineo kwa nini sisi wananchi tusiwaamini hao hao mnaowasujudia?
 
Balozi Chriss

Senior Member
Jan 21, 2011
154
0
Kaka umekurupuka kuleta hii hoja yako hapa.Bila kuwa na sirikali kwenye Uongozi wowote ule daima kutakuwa na misuguano.Naomba tu nikushauri ufuatilie japo kwa kuadithiwa tu ni kwa jinsi gani Umoja wa Sovieti ulisambaratika na kwa nini Siasa za Urusi kwa sasa zimetawaliwa na Putin tu......T 2015 CDM.......
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Kaka umekurupuka kuleta hii hoja yako hapa.Bila kuwa na sirikali kwenye Uongozi wowote ule daima kutakuwa na misuguano.Naomba tu nikushauri ufuatilie japo kwa kuadithiwa tu ni kwa jinsi gani Umoja wa Sovieti ulisambaratika na kwa nini Siasa za Urusi kwa sasa zimetawaliwa na Putin tu......T 2015 CDM.......
Unanambia mimi?
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,592
2,000
Ben,
Kuna mahala nimekusoma ukisema hivi:-
Nachotaka mimi kuelewa ni perspective gani nyie vijana mnazo ambazo hazifungamani na old ones?. Nachokiona ni unafiki mkubwa wa vijana, vijana wetu wanatumiwa zaidi kutumikia kambi za kina EL, JK, Seif, Lipumba, Mbowe, Dr.Slaa na kadhalika while hawa wote hawana jipya la kumkomboa Mtanzania tofauti na msimamo wa vyama vyao. Nyote kwa ujumla wenu mnatumikia vyama na itikadi zake.

Ikiwa vijana mnashindwa kuja na new ideas ila mnataka kutumia ujana wenu ku discredit wazee kwa kutumia kabila au dini.. Hii kweli ndio sifa mnayotaka sisi wazee tuwakubali kwamba mnaweza kuongoza nchi ilihali nyie wenyewe mna makabila na dini zenu!. Nani anapingana na mfumo wa elimu na Afya iliyopo..Nani anapingana dhidi ya jinsi wakulima, miners, na wafanyakazi wanavyo nyanyaswa na kusukumwa chini zaidi kuwa ngazi za matajiri?..

Jamani hata Ukapteni wa team ya mpira hupewa mwenye sifa na uzoefu ambao kauonyesha na experience matters. hadi sasa hivi mnashindwa kutuonyesha zaidi ya Zitto wakati ule kuonyesha msimamo wake juu ya posho na sii vijana wote wanaafiki.

Mimi nauliza nyie vijana what do you bring on the table?..Ni fikra zipi mpya mlonazo, maana nawaona mkibishana sana juu ya Ufisadi wengine mkisema Ufisadi sio tatizo bali tatizo ni uzalishaji. Ni mawazo sawa kabisa na wazee sioni tofauti yoyote baina ya vijana na wazee ikiwa upeo wenu wote unaishia palepale.. Utazalisha vipi ikiwa kila unachopanda kinakuwa sabotage.. Na hakuna kijana hata mmoja anayepiga vita Ufisadi kwanza ili tukija panda mimea ikue na tuvune kilicho bora. Wote mmejipanga nyuma ya JK, RL na wengineo kwa nini sisi wananchi tusiwaamini hao hao mnaowasujudia?

Mkuu Mkandara,

Asante sana kwa mchango wako.Wachanijisemee na nisiwasemee wengine.

1.Kwenye chama cha siasa ninapenda kuunga mkono itikadi.Kwa hali iliyopo Tanzania vyama vyetu vina mapungufu kwenye itikadi hasa kuhusu mfumo wa uchumi ambao ni kigezo kinachotoa muongozo wa aina ya Siasa nchi inafanya na uongozi kwa ujumla.Nikiwa mwanachama wa Chadema naona itikadi ya chama changu ni nzuri kulinganisha na itikadi za vyama vingine hata tuki-fanya modification hatutapata shida sana ukilinganisha na vyama vingine

2.Ukiniona naunga mkono mtu au kambi (kambi ni jambo la kawaida wakati wa uchaguzi kwenye vyama vya siasa) basi ujue naunga mkono kile anachosimamia kulingana na itikadi ninayoamini kwamba inaweza kutuondoa kutoka level moja kwenda nyingine.

3. Ninaamini tufikie hatua vijana sasa tuwashinikize wenzetu na kuwatia moyo tuachane na siasa za matukio.Suala la posho ni tukio,kiongozi wangu na rafiki yangu Zitto Kabwe alilipigania kutokana na kuona kwamba mfumo wa uongozi na itikadi inayozalisha viongozi au wawakilishi walafi kwa gharama ya walipa kodi utachukua muda kuurekebisha.Roho ilimuuama kuona watanzania wanaendelea kugharamia anasa za wawakilishi wetu huku wao wa kiteseka katika kupata huduma stahiki za kijamii.Hata hivyo,tatizo la posho kama nilivyosema ni tukio/tunda la mfumo mbovu.

Nilifurahi kuona vijana wenzangu kama akina January na Nape ingwa ni kutoka chama tofauti na changu wakiunga mkono hoja aliyoisimamia Zitto.

4. Mabadiliko tunayopigania yamekuwa yakitafsiriwa vibaya kwamba ni kuiondoa CCM.Kumbe kuiondoa CCM ni kama kuondoa tu kikwazo kilichoko mbele ya safari yetu kuelekea kwenye mabadiliko.Kuiondoa CCM ni kuruhusu uwanja mpana wa kuleta mageuzi makubwa ya kifikra ambayo in turn yatatusaidia katika kujenga taifa adilifu,linalowajibika.Ni kweli vijana wengi sasa hivi hasa wasomi na wanasiasa vijana hawajadili tatizo katika wizara ya Elimu au Afya kwa kujenga hoja na kuzishindanisha dhidi ya Itikadi fulani baina ya chama kimoja na chama kingine au baina ya kiongozi mmoja dhidi ya Mwingine

5. Wakati sisi tunafikiria miaka 2 au mitatu ijayo na kujenga mawazo/fikra tegemezi kama viongozi hatujui kwamba tunajenga taifa lenye fikra tegemezi.Ni kama kwenye corporate world,director anatoa dira ya kampuni na subbordinates wake.The smartness of directors determines the growth and success of the company.

Hatujui kwamba wenzetu mataifa ya Ulaya na Asia wote wanaweka mikakati na fursa za miaka 100 ijayo kwa ajili ya wajukuu kujinufaisha na raslimali za Afrika ikiwemo Tanzania.Waliopo sasa ulaya wanatunyanyasa kiuchumi kutokana na furasa walizowekewa na babu zao mwaka 1900's. Sisi tunajadili matukio.

Mkuu Mkandara,Tunafanya maandalizi ya kutoa darasa la itikadi kupitia taasisi ya wanafunzi wanachama wa chadema wa sekondari na vyuo vikuu (CHASO). Vijana wengi ni wanafiki kutokana na njaa,hawaamini kama wanaweza kuwa succesfully bila kujipendekeza na kupata visenti vichache.Haya yote ni matokeo ya mfumo mbovu ambao tunatakiwa kupambanan nao.Mfumo wa kuunga watu mkono bila principles ndiyo huu unaotujengea fikra tegemezi,ufisadi,kukosa maadili majungu nk.

Unategemea kijana anayegeuzwa kibaraka wa kiongozi fulani kwa ajili ya vijisenti,siku akikutana na majaribu ya Marekani au taifa lolote la magharibi (ofcourse hawajawahi kuwa na nia njema na Afrika,ingawa diplomacy inanikataza kutamka haya ila siyo Rhetorics) kumfanya awe shushu/kibaraka kwa malipo ya madola na magari ya kifahari aache?Je,kwa mazingira haya uzalendo na uhuru wa taifa hauko mashakani?

Tunachofanya sasa ni maandalizi ya kupambana kubadilisha mfumo,we need a very radical reform based on Ideologies.We need radical reform socially,politically and Economically. We nee catalyse change, to change the attitude hasa unapokuwa ndani ya chama cha siasa.Tuandae mazingira ya kuunda responsible government,responsible policy and responsible Nation

No responsible government can afford to produce and abandon graduates to roam the streets, for we know that such attitude will force them into crime as a way of earning a living. We need device methods of taking statistics on the number of graduates turns out every year. This will enable us to provide employment opportunities and meaningfully engage them in other positive areas of livelihood. Our commitment to gainful employment will have the vulnerable groups particularly the youth and women as the main targets.

We were suppose to therefore bring to reality the small and medium scale industries that will engage our youths and women so as to enable them achieve economic empowerment and self reliance. Every single person willing to work should be able to get job training that leads to a job and earn a decent living

Tanzania's problems goes beyond probing past leaders. I think we need a generational shift that will bring about a re-orientation of our national psyche which should place value on service rather than looting. The political office is so attractive now because its an avenue to share the Natural resources money and even loot the treasury without any opposition. Imagine servicing a single Mp as a stting allowance 300,000 + more than 7m per month salary. This is crazy. Yet the country is laden with poverty stricken masses. We need the change.

We will appeal to our youth to see this as a call to change. Its high time we sideline the money bags and old corrupt politicians and take our destiny in our own hands. Lets put hands together and support a worthy cause....Hayo na mengine mengi....!
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,355
2,000
Mkuu wangu,

Kama utasoma post yangu tena utaona mahali nilikosizitiza kuhusu maadili.Nimesizitiza tupigania kubadili fikra na mfumo mzima unaoruhusu Kuwa na taifa lisilo adilifu.Pia mimi ni muumini mkubwa wa falsafa ya kama huwezi kuwa mwaminifu katika mambo madogo huwezi kuwa mwaminifu kwenye mambo makubwa.Ofcourse,infidelity consitutes the breach of trust and trust actually is a central character component of a good leader. Rejea mandishi ya cal thomas / infidelity and Leadership aliyoandika juu ya mgombea Urais Garry Hart na concubine mwanamama Donna Rice

Hata hivyo,post ya nuclear1 ilikuwa imekaa kuchafua watu tu.Siwezi kuwasemea wengine.Lakini mimi nazingatia uadilifu,na sijawahi kupenda kuwa promiscous naamini katika maadili.Ila pia nimetoa angalizo,tujadili ideas zitakazoondoa fursa kwa watu wasio na uaminifu katika social life kushika public office . Rejea tena maandishi ya Cal Thomas mkuu halafu rejea pia post yangu ya awali nilipomjibu nuclear1.Pia kuhusu tafsiri ya ufisadi,asante kwa ushauri na nitalizingatia hilo zaidi kwenye mjadala.
Tuko pamoja. Ila pia mkuu sikugusia suala la Nuclear1 kwa makusudi kabisa; nilijikita zaidi kwa Ryntemeke, PAA na TII ambao wametoa sindano za moto.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom