CHADEMA, Kulikoni Jengo la Ghorofa Lililoporomoka?

CHADEMA, Kulikoni Jengo la Ghorofa Lililoporomoka?

Watanzania tunashangaa chama ambacho kinajitangaza kuwa kina kusudio la kuingia magogoni mwaka 2015 hadi leo hawajatia mguu katika tukio la kuanguka ghorofa 17. Haijulikani kwa nini Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni hawajaonekana katika eneo la tukio ama kutoa kauli kuhusiana na tukio husika. Watz tunazidi kujiuliza hawa CHADEMA wana nia njema na wananchi ama nia yao ni kuingia IKULU tu! Tafadhali wafuasi wa CHADEMA mliopo JF chukueni hatua kwa kutoa ushauri kwa viongozi wenu waandamizi kuwa wabadilike ili wawe serious latika matukio ya kitaifa.
Typical CCM? hamjali wananchi bali mnang'ang'ania umoja wa kuiba kura ni ushindi... Mgekuwa mnajali hili Jengo lisingeporomoshwa na DIWANI wenu! Huoni haya kuitupia lawama CDM? kwamba mlichakachua uchaguzi wa 2010 mkitegemea CDM ndo wawasaidie kutawala? Too low kwa chama yenye miaka 51 plus! ... au ndo menopause imeshawaingia?...
 
Huyu mtoa mada amejitahd pia kuipost na facebook. Hongera umejitahidi kukusoa.
toa na sifa pia kama umeona panapofaa.
 
Amini nawaambia,sio kila achekae ana furaha,sio kila aliae ana uchungu,sio kila ahudhulia misiba ana uchungu wa kufiwa,yawezekana ameua yeye,sio kila aliyefika katika eneo la janga la ghorofa ana uchungu na wafiwa na majeruhi,yawezekana wapo kwenye maonesho ya mavazi ama wao ndio wametoa kafara,wenye uchungu wa kweli wanatafakari nini chanzo cha janga hili ambalo linajirudia kila mwaka!!
 
Dr Jakaya yupo pamoja kwenye raha na dhiki: tangia eneo la tukio, MOI na sewahaji kaonekana

Kwanini hakwenda Iringa wala kutoa salamu za rambirambi wakati Daudi Mwangosi alipouawa na polisi Iringa? Sioni sababu ya kuhadaa umma!
 
Waliofika wamesaidia nini? Waliotoa kauli zimeongeza nini? Bado wapo ndugu zetu wengi maiti zao hazijaonekana , Chadema wapo kwenye majonzi, walioenda na kutabasamu wametoa suluhisho lolote?
walikuwa wanasubiri waende waseme wanatafuta umaarufu wa kisiasa.akiwa kwenye msafara askari wanakufa akikaa nchini siku chache matukio ya ajabu yanatokea ama kweli mshikaji kalaaniwa na nduo taabu ya kuwa na viongozi wanaoenda kuhiji vibuyu kila jumamosi.
 
Dr Jakaya yupo pamoja kwenye raha na dhiki: tangia eneo la tukio, MOI na sewahaji kaonekana
angezikwa pamoja marehemu tujue kama kweli yupo na kwenye dhiki mnaleta siasa kwenye misiba.
 
Watanzania tunashangaa chama ambacho kinajitangaza kuwa kina kusudio la kuingia magogoni mwaka 2015 hadi leo hawajatia mguu katika tukio la kuanguka ghorofa 17. Haijulikani kwa nini Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni hawajaonekana katika eneo la tukio ama kutoa kauli kuhusiana na tukio husika. Watz tunazidi kujiuliza hawa CHADEMA wana nia njema na wananchi ama nia yao ni kuingia IKULU tu! Tafadhali wafuasi wa CHADEMA mliopo JF chukueni hatua kwa kutoa ushauri kwa viongozi wenu waandamizi kuwa wabadilike ili wawe serious latika matukio ya kitaifa.

Sema wewe na siyo Watanzania, maana wengine tuna akili timamu.
 
Mbona kifo cha mwangosi walisema na maziko wakihudhuria na ahadi ya kumsaidia mjane ilitoka.
Kifo cha waandamanaji arusha walisema? Kifo cha mabomu walisema.
 
Kwa hasira kidogo nimtukane mleta uzi maana naona amethiriwa na mfumo ccm wa kuahidiwa wakiwapa kura watawaletea barabara za juu wakati ni ahadi hewa (hizo za chini tu zimewashinda)!
Hatuhitaji viongozi wauza sura kwenye majanga yanayowakumba watanzania, tena katika majanga ambayo si natural disasters but man-made disasters! mara ngapi kunatokea ajali za kuzama meli na viongozi wanauza sura na kuunda tume but mwisho wa siku tunabaki vilevile? hakuna hatua zozote zinachukuliwa, maafa ya aina ileile yanaendelea kutokea na kuua watanzania? bull shit...
 
penye bold wewe akili yako ni finyu kama KATIBU WAKO MKUU mwenye tamaa ya kuwa RAIS kupitia Kanisa


Kelele nyingi kumbe tabu yako ni hii? Halafu hilo engo la ghorofa 17 lililoporomoka mbona hatulifahamu?
 
Watanzania tunashangaa chama ambacho kinajitangaza kuwa kina kusudio la kuingia magogoni mwaka 2015 hadi leo hawajatia mguu katika tukio la kuanguka ghorofa 17. Haijulikani kwa nini Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni hawajaonekana katika eneo la tukio ama kutoa kauli kuhusiana na tukio husika. Watz tunazidi kujiuliza hawa CHADEMA wana nia njema na wananchi ama nia yao ni kuingia IKULU tu! Tafadhali wafuasi wa CHADEMA mliopo JF chukueni hatua kwa kutoa ushauri kwa viongozi wenu waandamizi kuwa wabadilike ili wawe serious latika matukio ya kitaifa.

Kwa kawaida mchawi ndiye anakuwa wa kimbelembele anaposabaisha mauti, hii yote ni kujifafishaa machoni kwa wafiwa.! Kama una akili utakuwa umeelewa!
 
Watanzania tunashangaa
chama ambacho kinajitangaza kuwa kina kusudio la kuingia magogoni mwaka
2015 hadi leo hawajatia mguu katika tukio la kuanguka ghorofa 17.
Haijulikani kwa nini Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe ambaye ni Kiongozi wa
Upinzani Bungeni hawajaonekana katika eneo la tukio ama kutoa kauli
kuhusiana na tukio husika. Watz tunazidi kujiuliza hawa CHADEMA wana nia
njema na wananchi ama nia yao ni kuingia IKULU tu! Tafadhali wafuasi wa
CHADEMA mliopo JF chukueni hatua kwa kutoa ushauri kwa viongozi wenu
waandamizi kuwa wabadilike ili wawe serious latika matukio ya
kitaifa.

kuna watu wanamamatope vichwani mwao.we ni mfano kati yao.yan uzembe ufanywe na wengine alaf lawan uwape wengine!!
 
Kuua waue sisiem chadema wakahani. Shame on you.
 
Mbowe kasema kutoa rambirambi kwa wafiwa wa ajali hiyo SIO MUHIMU!!!
ZeMarcopolo
Dunia ya leo ni ya sayansi na technologia ndugu wangu. Kamwe kwa mawazo na propaganda zako za namna hii nchi yetu tz haiwezi kwenda kokote.
 
Last edited by a moderator:
matumizi mabaya ya ubongo.
Kwani JK kaenda kama rais au mkiti wa ccm? Na kinana ameenda? Nape?
Au ndio kafara ya kujitangaza kichama?
 
Watanzania tunashangaa chama ambacho kinajitangaza kuwa kina kusudio la kuingia magogoni mwaka 2015 hadi leo hawajatia mguu katika tukio la kuanguka ghorofa 17. Haijulikani kwa nini Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni hawajaonekana katika eneo la tukio ama kutoa kauli kuhusiana na tukio husika. Watz tunazidi kujiuliza hawa CHADEMA wana nia njema na wananchi ama nia yao ni kuingia IKULU tu! Tafadhali wafuasi wa CHADEMA mliopo JF chukueni hatua kwa kutoa ushauri kwa viongozi wenu waandamizi kuwa wabadilike ili wawe serious latika matukio ya kitaifa.

Kitengo cha MAAFA kipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu; kama kweli watu wako serious na haya majanga ya kila siku ni vyema angeulizwa Waziri Mkuu mwenyewe kuwa hicho kitengo anachokiongoza kina manufaa gani ama kina saidia nini pale maafa yanapotokea badala ya kuanza kuangalia nani amefika kwenye eneo la tukio na nani hakufika.

Ni vyema tukatambua pia kwamba Kitengo cha Maafa kina bajeti yake inayotokana na kodi za wananchi; lakini hali iliyozoeleka kwa sasa ni kuwa kila linapotokea janga lolote Serikali inakuwa ya kwanza kusema hawana fedha na kwa hali hiyo wajanja fulani ndani ya Serikali wanaanza kutembeza bakuli kuomba msaada kwa ajili ya kukabiliana na janga husika. Nafikiri wakati umefika sasa wananchi tufahamishwe kuwa hizo fedha zinazotengwa kwa ajili ya shughuli za Kitengo cha Maafa zinatumiwa na nani na kwa wakati gani. Sambamba na hilo inabidi wananchi wafahamishwe pia kuhusu michango inayotolewa kila janga linapotokea inatumika vipi ama inaishia kwenye mifuko ya wajanja wachache. Mfano mzuri ni michango iliyotolewa wakati wa janga la mafuriko yaliyotokea hapa Dar Es Salaam yaliyopelekea vifo vya watu kadhaa.

Mbali na hayo, ifike mahali sasa viongozi pamoja na wanasiasa wengine wenye dhamana ya kuongoza nchi yetu waache kutumia maafa na majanga pale yanapotokea kama sehemu yao ya kwenda kujijenga kisiasa na kujidai kuwa karibu na wananchi. Kinachotakiwa sio kuwahi kwenye eneo la tukio ili uonekane kuwa unajali kwa kuwa wa kwanza kufika lakini huna msaada wowote wa namna ya kukabiliana na tatizo husika. Kinachotakiwa kufanywa na viongozi walioko madarakani ni kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo/maafa yanayotokea kila mara badala kukaa ofisini kusubiri janga litokee ili wawahi kwenye eneo la tukio na kuita vyombo vya habari kwa ajili ya kuripoti na kuuza sura kwenye television na magazeti.

MWENYEZI MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Back
Top Bottom