CHADEMA, Kulikoni Jengo la Ghorofa Lililoporomoka?

CHADEMA, Kulikoni Jengo la Ghorofa Lililoporomoka?

Watanzania tunashangaa chama ambacho kinajitangaza kuwa kina kusudio la kuingia magogoni mwaka 2015 hadi leo hawajatia mguu katika tukio la kuanguka ghorofa 17. Haijulikani kwa nini Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni hawajaonekana katika eneo la tukio ama kutoa kauli kuhusiana na tukio husika. Watz tunazidi kujiuliza hawa CHADEMA wana nia njema na wananchi ama nia yao ni kuingia IKULU tu! Tafadhali wafuasi wa CHADEMA mliopo JF chukueni hatua kwa kutoa ushauri kwa viongozi wenu waandamizi kuwa wabadilike ili wawe serious latika matukio ya kitaifa.

unahitaji maombi, pole sana, yani uue ukisubiria nani atakuja msibani. Pole sana, kaa mwenyewe na msiba wako, unatafuta sympathy kwa upuuzi wenu, to hell na mr. Dhaifu, ukienda ofisi ya waziri mkuu utasikia kuna kitengo cha maafa, juzi wanahangaika kuwatafuta strabag wako zao likizo, hela zote za maafa wamegawana na kuna watu wanalipwa mshahara, dr. Slaa sio muuza sura kama kibaraka wenu Mbatia aka viti maalum
 
ww mafilifidu,nahisi una umri wa miaka 10 hivi,kulingana na uzi uliouweka,wakati mwingine.ulichokiandika ni cha kitoto sana.jitahidi ule vizuri ukue kiakili kwa kweli.Sasa mtotoo,unatakiwa uulize kwa wakubwa zako kama CDM ni chama cha siasa au cha majanga
 
ccm kweli ni janga la taifa!!

Logic hawawezi, propaganda zimewashinda, wamebakia kama empty cans tu, wanajikaanga wenyewe na mafuta yao.

Small mind minds!
 
Hakuna kitu katika nchi hii CHADEMA hawajawahi kuzungumzia, kuonya, kukemea, kushauri na kuelekeza...proactive...wametoa uongozi wa kila namna, lakini Serikali hii ya CCM imekuwa ikipuuza kila kitu muhimu kwa ajili ya taifa hili na watu wake ambacho kimekuwa kikisimamiwa na CHADEMA!

Haya yanayotokea na kuendelea kutokea ni dalili ya yote ambayo CHADEMA wamekuwa wakisimamia kwenye kila forum wanayopata, mathalani bungeni, nje ya bunge na kwenye nafasi zote za uongozi wa kiserikali.

Nakupatia changamoto Mkuu Mafilili; tuambie hapa tatizo moja tu katika nchi hii ambalo halina uhusiano na ufisadi, sema moja tu...na utuambie hapa iwapo tatizo kama hilo la kuanguka kwa majengo na jengo hilo la juzi, havina uhusiano na ufisadi. Ni ufisadi huo CHADEMA imesimamia na CCM wameshindwa kuchukua hatua...kuanzia list of shame.

Sasa hoja yako kuwa CHADEMA hawako serious, haina mashiko hapa, wasiokuwa na makini na masuala ya taifa hili na watu wake, ni watawala hawa wa serikali ya CCM ambao wameiharibu nchi hii kiasi cha kufikia hatua ya kila mtu, mwenye uhusiano na CCM anaweza kufanya jambo lolote hata kama ni kuhatarisha maisha ya watu na mali zao, kama alivyofanya diwani wa CCM aliyekuwa mkandarasi wa ujenzi ulioua watu!

Pamoja na hayo, ni vyema tukakushukuru kwa kuona umuhimu wa kutaka viongozi wako wafike eneo la tukio ili waendelee kutoa uongozi, ingawa watawala wamekuwa wakiweka pamba masikioni, kwa sababu akili zimevizwa na ufisadi na ubadhirifu. Thinking for their own ends, by whatever means, no matter that would eventually cost our countrymen and women.

Mafilili, tuendelee? Au umeelewa tayari!

Pamoja umuhimu wa kutembelea eneo la tukio, lakini dawa nzuri zaidi ni kuwaondoa watawala hawa wa CCM ambao ufisadi, ubadhirifu na uzembe wao na kufeli kwa sera zao, dniyo kumeligikisha taifa hapa lilipo, ikiwemo kukabiliana na majanga yanayoweza kuepukika.

Makene

0752691569/0688595831
 
tehe tehe JF is never boring.
mtoa mada nakushauri ufute hii post yako usapata BP na kisukari bure kwa kujitakia
 
Kabla ya kuchangia naomba kukumbushwa kama lile jengo lilikuwa na mkono wa diwani wa CCM?
 
Sema unataka wafanye nn?, maana kufka hapo sio mpaka waonekane kwenye vyombo vya habari, au uwaone ww,.
 
Dr. Magumashi alienda kuangalia mradi wake ulivyoporomoka.
 
Mbona huu ni mwanzo tu,maghorofa Meng sana hayana viwango vnavyostahili na Yatapolomoka tu!Mpaka leo cjui km kuna anayewaza kuingia gharama za kuchek ni kwa kias gan neighbouring buildngs zmekuwa affected!
 
vipi hamjapata mkanda wa video viongozi wa chadema wakipanga mpango wa kuangusha hilo ghorofa.?

waku wa usalama wanamalizia kuandika story màana ya awali zimeshindwa vibaya kwa sasa wana mtafuta mtunzi bora kabisa ndunia ili awasaidie...
 
Hao walioenda wangekuwa makini na werevu wangezuia hiyo ajali isitokee
 
Viongoz wa cdm walihudhuria mazishi ya Mbunge wa Chambani marehem Salim Hemed, walikuwa visiwani, hata hivyo CHADEMA TV na timu ya viongoz HQ walifika. Ila chadema kupitia Mbowe walishaonya juu ya kandaras za majengo marefu ambayo mengi yanajengwa kwa wizi wa fedha za Watz, hayo ni matokeo tu
 
Nchi hii na uchakachuaji utamaliza watu wasio na hatia. Innocent people have right to live plz! Malumbano yasiyo jenga hayana maana. Watz tuwe serious na tuwajibike ipasavyo.
 
Mafilili akili ndogo inajadili watu, akili ya wastani inajadili matukio. Na akili kubwa inajadili kuhusu ISSUES. So pima mwenyewe.
 
CCM,inashangaza kweli kweli,wanatumia rushwa kupata tenda,kumbuka mkandarasi wa lile jengo ni diwani wa CCM,tenda amepata bado anachakachua jengo linajengwa chini ya kiwango,linaporomoka linaua watu wasio na hatia,halafu CDM waende wakatoe tamko!hii inaweza kutokea tz peke yake. Bila kuficha ukweli CCM na Serikali yake watabeba malipo ya wahanga hawa wasio na hatia.
 
CDM=Chaga Development Mission

CCM=Chukuwa Chako Mape.kama walivyo chukuwa chao mapema wakajenga ghorofa lisilo na kiwango kinacho kubalika sasa limeporomoka na kusababisha maafa ya watu wasiyo na hatia.Eti ndiyo viongozi wake wanajifanya kwenda mbiombio ili waonekana kuwa wamesikitishwa sana na tukio hilo wakati waliyosababisha ni wao wenyewe kwa kupitia diwani wao.Ccm hawana lolote wanakwenda kufanya tathimini ya watu waliyo waua ili waweke kumbukumbu zao sawa.
 
Hakuna dili ndo mana hawakufika Chama cha wapiga dili
 
Wewe ni kichaa kamili, CDM ni janga la taifa ambacho wanashindwa kutumia fursa muafaka wajitangaze badala yake mnashabikia maandamano tu!
kwa hiyo unataka watu wajitangaze wapate umaarufu kupitia maisha ya watu, are you of sound mind?
 
Watanzania tunashangaa chama ambacho kinajitangaza kuwa kina kusudio la kuingia magogoni mwaka 2015 hadi leo hawajatia mguu katika tukio la kuanguka ghorofa 17. Haijulikani kwa nini Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni hawajaonekana katika eneo la tukio ama kutoa kauli kuhusiana na tukio husika. Watz tunazidi kujiuliza hawa CHADEMA wana nia njema na wananchi ama nia yao ni kuingia IKULU tu! Tafadhali wafuasi wa CHADEMA mliopo JF chukueni hatua kwa kutoa ushauri kwa viongozi wenu waandamizi kuwa wabadilike ili wawe serious latika matukio ya kitaifa.

nawashangaa ccm....kila siku mpo busy kuimaliza CDM..... I thought u cld be happy if CDM will remain mute.....tulipiga kelele sana wakati waziri kmuu akiwa Lowasa kwa jengo lilianguka keko mpaka tume ikaundwa kuchunguza majengo holela but until today matokeo na mapendekezo ya tume yalikaliwa na ccm then wataka nini tena?what we are doing right nw is to list all wrong deed which ur commiting nw and on 2015 u will know what we were doing.....
 
Back
Top Bottom