CHADEMA kuiunga mkono Jubilee ni kujisaliti

CHADEMA kuiunga mkono Jubilee ni kujisaliti

chadema ni matapish nisiyotaka kuyaina wala kusikia
 
Hiyo ni pi
22df30600bdd8a57c1a1c59d0174a846.jpg


Hill ndilo jibu lako. Muulize kwanza Mwenyekiti wenu kwanini alikuwa anaunga mkono mpinzani wakati yeye ni chama tawala

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni picha tu,,na haijulikani imepigwa lini,na inaweza kuwa imekuwa edited.But let say inamaanisha kuwa JPM na ODM ni marafiki sio mbaya.Rais wetu hajawahi toa kauli ya kuunga mkono chama chochote kwenye uchaguzi wa kenya na waziri wa mambo ya nje alishakana uhusika wa Tanzania kwa namna yoyote katika uchaguzi wa kenya.Hayo mapicha mnayoleta yanaonesha nia ovu ya kulazimisha yasiyo kuwapo yawepo.Mtasubiri sana Watanzania sio nyumbu kama mnavyodhani
 
Sweetness i always respect ur opinion but neno "kamwe" nimelitafsiri " never" just remember never to say never there is always a 1st time.....
Thats why I said wajirekebishe.
 
22df30600bdd8a57c1a1c59d0174a846.jpg


Hill ndilo jibu lako. Muulize kwanza Mwenyekiti wenu kwanini alikuwa anaunga mkono mpinzani wakati yeye ni chama tawala

Sent using Jamii Forums mobile app[/
Hiyo ni picha tu,lete clip ya kauli na mkutano wa CCM ulokaa na kutoa azimio la kuunga mkono NASA kama nyie mlivyo fanya.ukikosa nenda kale malimao unywe na supu ya upupu
 
Mpaka sasa hakuna ushahidi wowote unaonyesha kuwa kuna aliyeibiwa kura,ushahidi unaoweza ukamfanya Lissu asitoe pongezi wala kumuunga mkono mtu aliyetangazwa na tume kuwa kashinda.

Hata hivyo Lissu ni mtu huru mwenye utashi wake ambaye anaweza kufanya kitu chochote anachoamini kuwa ndicho sahihi pasipo kuingiliwa na mtu yeyote na hajamlazimisha mtu yeyote kuamini kile anacho kiamini kwa kuwa kila mtu anahaki ya kufuata na kuunga mkono kile anacho amini kuwa ndicho kitu sahihi.
 
Wana haki ya kufanya hivyo kama chama
Hawana haki Wewe kwa sababu kulinganisha na taarifa waliyotoa walidai wanamuunga Kenyatta kwa kuwa Odinga aliwasaliti mwaka 2015 licha ya wao kumuunga mkono 2013.
Hivi kwa urafiki uliokuwepo kati ya Odinga na Magufuli, hivi Odinga angeacha kumuunga mkono JPM? Cha ajabu wao wameingia mazima.
 
Wale they are moved by people and not ideas, wanamuunga mkono Kenyata kisa tu eti Raila ni rafiki ya Magufuli, nyie CHADEMA, hamjui kuwa Uhuru na Raila watapita tu? Yaani nyie kamwe hamtakaa mtawale Tanzania maana hamjui hata mnasimamia nini? Jirekebisheni.
Hiki ni cha cha kimaslahi hawajui waendapo ndio maana wanashindwa kusimama pamoja siku zote bahati mbaya wakawaambukiza huo ugonjwa na wenzao upinzani kwisha Tz.
 
Alitusaidia kipindi cha tetemeko na mi naunga mkono kutoa pongezi nyingi
 
Nimemsikia mwanasheria mkuu wa CDM akisema kuwa wao kama chama walimuunga mkono mgombea wa urais kupitia chama tawala nchini kenya na kwamba kimsingi wamefurahishwa na ushindi wake wa urais nchini humo.

Ifahamike kuwa uchaguzi huu umekuwa na dosari kadhaa kabla na wakati wa uchaguzi. Dosari ambazo huku kwetu hazijawahi tokea. Siku chache kabla ya uchaguzi, mkuu wa IT wa tume ya uchaguzi nchini humo aliuawa kinyama.

Inasemekana mtu huyu ndie alokuwa na password ya data base za IT na kifo chake kimehusishwa na uchaguzi huu.Ilipofika siku ya uchaguzi upinzani uligundua kutokea kwa udukuzi katika data base ya IEBC na kutoa taarifa lakini hakuna hatua iliyo chukuliwa badala yake waliambiwa kuwa kama hawaridhishwi na matokeo waende mahakamani na tume ikaendelea kutangaza matokeo.

Swali fikirishi,kwa nini Musando afe siku chache kabla ya uchaguzi? na kwa nini muuaji achukue vidole vyake? Unaweza pata connection kuwa inawezekana kweli kuna mchezo mchafu ulifanyika kwenye data base ya IEBC though hatuna uhakika.

Wapinzani waliomba issue ndogo tu, waruhusiwe kuangalia taarifa za matokeo direct kwenye data base lakini walikataliwa.Kwa nini wakataliwe ? mimi na wewe hatujui

Maswali ninayo jiuliza;
unawezaje kumsupport mtu ambae wapinzani wanadai kaiba kura? Wewe ni mpinzani 2020 unatazamia kuingia kwenye vita kama alokua nayo mpinzani mwenzako leo,vipi huo wembe ulomyoa mwenzio leo ukikunyoa 2020, utalalamika?

Uchaguzi hauwi huru na haki kwa kuwaruhusu wafungwa na diaspora kupiga kura tu, bali unakuwa huru na haki katika hatua zote za uandikishaji, kampeni, upigaji wa kura, kuhesabu na kutoa matokeo.

Kwa hawa wenzetu kutokana na madai ya upinzani kulikwa na tatizo katika kuhesabu kura za urais ndio maana waliomba access katika data base za IEBC wakanyimwa. Jiulize kwa nini walinyimwa.

Mwisho niwashauri ndugu zangu hawa kabla hawaja toa matamko wawe wanafanya uchunguzi wa kutosha,si vema kutoa tamko leo afu kesho likakugharimu.

Wajifunze kutokana na makosa yao wenyewe:
-2008 lowasa fisadi;2015 wanamsafisha.
-2005-2015 Rais wa awamu ya nne dhaifu 2017 wanamsifia kuwa alikuwa rais bora sana

-Kabla ya 2015 walisema wanataka rais mkali atakae simamia nchi;leo Kaja JPM wanaanza kulia
Hapa tulipofanyiwa hayo Odinga alisema tukubali matokeo. Hayo tumefanyiwa 2015 natunayategemea 2020. Hatuna cha kupoteza CCM ndio wanamsafisha maana hata mahakama ya mafisadi hawajampeleka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale they are moved by people and not ideas, wanamuunga mkono Kenyata kisa tu eti Raila ni rafiki ya Magufuli, nyie CHADEMA, hamjui kuwa Uhuru na Raila watapita tu? Yaani nyie kamwe hamtakaa mtawale Tanzania maana hamjui hata mnasimamia nini? Jirekebisheni.
Victoire tumemshauli kama alivyo tushauri akubali matokeo wajenge Kenya yao marumbano hayana nafasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi mnazani chadema kumpigia kampeini Uhuru kunawaongezea ushawishi ndani ya Tanzania? kwenye sura ya kenya kwa vyama vya upinzani na taifa kwa ujumla unaonyesha taswira gani kama mwana diplomasia mkuu, nchi gani ametoka mwanachama wa chama chochote kwenda kumpigia kampeini uhuru? jiulize hayo maswali kwanza arafu utapata jibu.
 
Mpaka sasa hakuna ushahidi wowote unaonyesha kuwa kuna aliyeibiwa kura,ushahidi unaoweza ukamfanya Lissu asitoe pongezi wala kumuunga mkono mtu aliyetangazwa na tume kuwa kashinda.

Hata hivyo Lissu ni mtu huru mwenye utashi wake ambaye anaweza kufanya kitu chochote anachoamini kuwa ndicho sahihi pasipo kuingiliwa na mtu yeyote na hajamlazimisha mtu yeyote kuamini kile anacho kiamini kwa kuwa kila mtu anahaki ya kufuata na kuunga mkono kile anacho amini kuwa ndicho kitu sahihi.
Hahaha hakuongea kama yeye,alisema kwa niaba ya chama yeye sio chama chama ni CHADEMA,,note that Bros
 
Back
Top Bottom