CHADEMA kuandamana Mwanza Feb 24; kupinga ufisadi, JK ajiuzulu

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamepanga kuandamana tarehe 24 Februari, 2011.

Maandamano hayo yanayotarajiwa kua ufuasi mkubwa sikuhiyo kutokana na chama hicho kuwa na wafuasi na wapenzi wengi jijini hapa. Viongozi wa juu wa CHADEMA wanatarajiwa kuongoza maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia stendi ya Buzuruga na kuishia kwenye uwanja wa wazi wa Furahisha uliopo Kirumba jijini hapa. Lengo kuu la maandamano hayo ni pamoja na kushinikiza Rais Kikwete ajiuzulu, kupinga mambo mbalimbali kama kupanda kwa gharama za umeme, kupinga ufisadi, kupinga DOWANS kulipwa na kuongezeka kwa gharama za maisha.

Kutokana na ughali wa maisha nchini maandamano hayo huenda yakasimamisha shughuli nyingi mjini na watu kwenda kuunga mkono maandamano hayo yanayotarajiwa kuanza mishale ya saa nne asubuhi. Wimbi hili la maandamano huenda likaenea mikoa yote ambayo ina wafuasi wengi hasa wa upinzani.
 
Jamani siyo siri me nshawaogopa hawa watawala wetu na visingizio, hope wamepata kibali. hawa mawakala wa mafisadi wasije wakawapiga risasi!
 
Mbona CDM yenyewe iko kimya na siku karibu zinakwisha! Kuna watu wengi kutoka mikoa jirani wangelitaka washiriki maandamano hayo.
 
bora waanaie huko mikoani kwani hapa DSM mijitu inajifanya mijanja lakini ndio mijinga nambari one inayohadaika na kijani na njano na uoga uliowajaa ile hali ni mimaskini ya kipatoa fikra wengi wao.
"kuchamba kwingi,huondoka na mavi"
Nguvu ya umma haiwezi kushindwa jambo na kuhusu maandamano yalishatangazwa kitambo ratiba yake hivyo kama ni mfuatiliaji mzuri basi utakuwa unajua hilo na kujipanga kogea road muda na saa zikiwadia
 
Safi wana mwanza...Naomba Mungu maandamano yenu yawe chanzo cha kuung'oa utawala dhalimu wa ccm.Wana jf tulikuwa tunasubiri wakuanzisha,Mwanza hao sasa tuwaunge mkono ili yale tunayoyabandika humu kwa hasira na uchtngu tuyatende,WAKATI NI HUU!
 
Nilijua tu Mikoani ndiko kwenye nguvu, hiyo ndio gear nzuri ya kuanzia kuliwasha gari la uhuru. Mwanza, Mbeya, Mara, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Dodoma, Iringa, Songea na Tabora Sijui kama Mkwere kama atatoka mzima hapo naona ameenda kwa Bgabo Kumba hifadhi ya muda kabla hajakwenda Saudia. Bring it On nguvu ya Umma. Cameroun wanalianzisha Alhamisi 24 Feb 2011
 
Kwa hali tuliyo nayo sasa maandamano ndio suluhu pekee. Haya wa Mwanza wameanza, wale wote wenye nia njema na Taifa hili wasibaki nyuma. Hata Misri hawakuanzia Cairo, na Libya pia hawajaanzia Tripoli kwa hiyo Mwanza n sehemu mwafaka hasa ukizingatia wna wa Dar es salaam wapo usingizini
 
Naomba yawe maandamano ya amani. CHADEMA wayasimamie vizuri kama walivyosimamia maandamano ya mazishi ya mashujaa Arusha.

Ila Mwema hajaleta bado habari za kiintelijensia?
 
Tunawaunga mkono wananchi Mwanza na tulio nje ya Mkoa wa Mwanza tujiandae kwa maandamano yetu kupinga popote wizi na ufisadi.

Kundaandamana na Kupinga Ujambazi na Kupigania "Haki" Yako Tunalindwa na UN Nation Decoration
Kama Mubarak na Ben Ali Wangeombwa Vibali, Watunisi na Wamisri Wangekuwa Bado Wanatawaliwa
 
chonde chonde media,,, tusaidieni live coverage jamani ...... mungu atawaongezea saba mara sabini
 
Naomba yawe maandamano ya amani. CHADEMA wayasimamie vizuri kama walivyosimamia maandamano ya mazishi ya mashujaa Arusha.

Ila Mwema hajaleta bado habari za kiintelijensia?


Hivi unafikiri mkuu wananchi wakitaka yawe ya amani, watawala watataka yawe ya amani?
 
Mwanza hakuja haja ya kibali, hapo ni full kujipanga tu. Milimani najua kuna wakurya, washashi ndo hawaambiliki ukiongea na akina Omera na jamaa zangu wasukuma wakisema nduhu gete hapo hata uje na SMG. CDM twende kazi.
 
always maanadmano ya cdm ni ya amani lakini wavurugaji ni hao vibaraka wa mafisadi. hawawezi kuzuia sauti ya umma,.....pipoz..........
 
Maandamano ni haki ya wananchi kikatiba lakini bado itapendeza kama CHADEMA watafuatilia kibali cha kuandamana ili kuepusha maneno mengi kama ya Arusha ambapo Jeshi la Polisi limeitupia lawama CHADEMA na CHADEMA imeitupia lawama Polisi.
 
Kibali wanacho? maana wenye nchi hawakawii last minutes wakadai taarifa za kitelejensia zinaonyesha maandamano yatakuwa na uvunjifu wa aman
 
Back
Top Bottom