Chadema Kortini tena Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Kortini tena Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, Feb 22, 2011.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  MAMIA ya wakazi wa Jiji la Arusha leo wanatarajia kujitokeza kwenda Mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili vigogo wa Chadema, wakiongozwa na Mweyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe na Katibu mkuu, Dk Wilbrod Slaa.
  Viongozi hao wa chadema , wakiwepo pia wabunge watatu, Philemon Ndesamburo (Moshi mjini), Joseph Selasini (Rombo) na Godbless Lema (Arusha mjini) na wafuasi wengine 24 wanakabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali Januari 5 mwaka huu.

  Kesi hiyo, inayosikilizwa na hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Arusha, Charles Magesa imekuwa ikihudhuriwa na mamia ya watu hatua ambayo husababisha ulinzi kuimarishwa mahakamani.

  Katika kesi hiyo, washitakiwa hao, wanatetewa na Mawakili, Method Kimomogoro na Abert Msando wakati upande wa mashitaka unaongozwa na mwanasheria wa serikali Zakaria Elisaria na wenzake.

  Kwa mara ya kwanza leo, Mchumba wa Dk Slaa, Josephine Mushumbusi anatarajiwa kuungana na washitakiwa wengine mahakamani baada ya kukosekara mara mbili kutokana na ugonjwa.

  Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba pia anatarajiwa leo kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi hiyo baada ya kukamatwa hivi karibuni na polisi na kushitakiwa kwa kosa hilo moja la kufanya mkusanyiko usio halali.

  Washitakiwa wote wapo nje kwa dhamana, kesi hiyo ilitokana na maandamano waliofanya wafuasi wa Chadema, kupinga uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo (CCM) ambapo Chadema wamekuwa wakidai alichaguliwa kinyume cha taratibu.

  Katika maandamano hayo, watu watatu waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa kwa risasi baridi na moto.


  Source: Mwananchi
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Sasa ngoja tuanze kujiandaa kuelekea huko....
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu, ngoja ni'lobby kwa mkoloni nichomokee huko...Hii ni never miss bana!
   
 4. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  the freedom is coming
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hapo kwenye red nimepafurahia sana...mwenye macho na aone!...na mapambano na yaendelee!
  Kila la heri Albert Msando, na kuna maelfu kwa maelfu ya watu wanaokusaidia kimoyomoyo!, amini usiamini.
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  God is on our side. Amen
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Police arusha wamejiandaa kuwakabili wafuasi wa chadema wanaotaka kwenda kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wao leo

  Nawasihi wafuasi wa CDM wasienda maana virungu vya police vitawaumiza
   
 8. m

  maselef JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Polisi hawana sababu za msingi kuwazuia watu kwenda kusikiliza kesi
   
 9. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,092
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 280
  Hata wakiwazuia watu watakwenda tu...
   
 10. n

  niweze JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Polisi wanajiandaa kwenda kuwalaki CDM, mbona hamkujiandaa kuwalinda wananchi Gongo la Mboto?
   
 11. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #11
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Polisi wawaachie na kuimarisha ulinzi na sio kusababisha chokochoko...........
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kwenda kusikiliza kesi ni haki ya kila raia na ni darasa zuri tu. Mimi nilianza kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi tangu miaka ya 1980 kila nilipokuwa likizo. na ilipa uwezo mkubwa na ufahamu mzuri wa kujieleza na kujitetea. hao polisi waache upuuzi.
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sure!...Nasikia Polisi wanakusanyika kujiandaa kuzuia peoples power...wamekosa kazi ya kufanya bana!
   
 14. L

  LAT JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  ukitujuza yanayojiri tutashukuru
   
 15. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwani CDM wameonyesha nia ya kufanya maandamano? kwenda tu mahakamani na kusikiliza kesi kwangu mimi si shida, unless kama chadema wameonyesha nia mbaya yoyote.
  Kazi ya polisi ni kuangalia usalama wa maeneo hayo. sio kupiga au kuzuia watu kwenda kusikiliza kesi, wana haki ya kujua kinachoendelea mahakamani juu ya viongozi wao.

  Ombi: Wanachadema Arusha endeleeni kuonyesha mshikamano, ila tunawasihi msionyeshe nia yoyote au ishara yoyote ya vurugu au kubishana na hao jamaa. ninachohisi, hawa polisi wanafuata amri walizopewa, na sasa chadema inachukiwa na kuwekewa mikakati. so onyesheni uzalendo na Mungu atawatangulia.
   
 16. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa mkuu!!
   
 17. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Lazima waende wakapigane vita ya ukombozi!
   
 18. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Acha virungu Gadaffi alitumia mpaka ndege za kivita na helicopter na mwisho kakimbia, nguvu ya umma haizuiwi na kirungu hata siku moja.
   
 19. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Hata mimi ni mmoja wao nitakwenda kusikiliza kesi hii inayowahusu wakombozi wa taifa hili!
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Tutakuta huko...
   
Loading...