CHADEMA kisisikilizwe tena!

CHADEMA kisisikilizwe tena!

Haya ndiyo Mwanakijiji anasema "tunapenda majibu mepesi katika maswali magumu................"

Wanasiasa ni MALAYA. Hilo linajulikana kwa kila mtu mwenye KUFIKIRI mbali ya PUA lake.

Katika hao MALAYA, unachotakiwa kutafuta ni yule mwenye NAFUU.

Sasa unafuu wa CCM na CHADEMA wewe unauona wapi?

Kama ukisikia Mwanasiasa anasema "yeye ni Malaika....." basi huyo HAFAI KUWA MWANASIASA.

Fumbuka macho ndugu. Tukiacha Chadema, tuende wapi? Au tupaki na CCM siyo?

Tena CCM ya Kikwete, ya Lowassa, ya Rostam Azziz, ya Chenge, ya Rashid wa Tanesco, ya Mattaka wa ATCL, ya TRCL, ya Airport za Tanzania, ya mashule yasiyo na waalimu, ya maji machafu mbele za nyumba, ya hakuna maji safi, ya foleni za kufa mtu Dar................

Kama ntachagua Malaya, basi mie nachagua Chadema. Ila ukweli ni kuwa wote ni MALAYA.

Mwenye akili kanielewa.

Mhhhh
Huyu anayechapa umalaya kabla ya kubarehe(chadema),mhh muogopeni huyo. Akibarehe mmekwishaa.
 
Ndugu wasomaji,

Tumeshuhudia jinsi nchi yetu ilivyokumbwa na vurugu za kisiasa jijini Arusha. Katika vurugu hizo damu ilimwagika. Ni wakati wa masikitiko makubwa kwa nchi yetu na vilevile ni wakati wa tafakuri na mafunzo muhimu. Je, ni nini kilichopelekea vurugu na kumwagika kwa damu?
Mkuu ze Basi la Marcopolo; naomba nipingana nawe katika kusema kuwa matatizo ya Arusha yametokea Hai huo ni Uongo na kuoanisha mambo kwa makusudi ili kudanga Umma. Hai ni Hai na Arusha ni Arusha hata taarifa za Serikali yako haikuwai kuonyesha mlingano huo batili; Ukipenda chama husipende hadi viongozi wake penda maslahi na mikakati yake katika Kujenga nchni yetu, CCM ilikufa na Mzee nyerere labda kama hujui pokea hiyo taarifa, na kwa kuonyesha kuwa unadangaya Umma angalia hata jina lako hamna mtu duniani anaitwa ZEmarcopolo hapo tu ni mwanzo wa utata wa hoja zako, yaani hata wewe mwenyewe ni Mtata.

Maneno yako takribani yote 829 ni ya uongo kasoro majina ya watu; ebu lete ushahidi kuwa CDM walikuwa wanapinga huyo Maria hasipige kura Arusha, huna kumbukumbu kwa mambo yaliyofanyika January 5, 2011 utaweza kukumbuka ya 1995 au ya 2005 au hata ya kwenye kampeni kuwa Kikwete alitoa ahadi zipi na kafanya nini hata sasa!! Kweli wewe ni basi tena la abiria; Chadema hawakuwa wanapinga kupiga kura kwa huyo mama siku ya kupiga kura, Chadema wanapinga Kura kupigwa wakati wapo katika udhuru kujali mikakati yao kama Chama wewe unageuza kuwa wanapinga huyo mama kupiga kura!!? huoni tofauti hapo!
Tujiulize;
wewe umekuja na swala lako jipya unataka kulifanya kuwa ndilo la Arusha, nadhani unautapia ubongo; Ugonjwa mbaya sana ni ugonjwa wa kukosa uwezo wa kufikiri na kutambua mtu wa namna hiyo ufikiri kulingana na njaa aliyonayo na tumbo ndio driving engine ya mwili wake, ni watu wepesi kununuliwa ata kwa bia na nyama choma ilikumsifia bwana wake, katika hali mbaya sana kiuchumi na kisiasa ambayo Tanzania inayo sasa mtu mwenye akili timamu hawezi hata kidogo kusema uongo kama wako kwa makusudi ili kupotosha Umma kwa kwa kununuliwa bia alafu hasionekane siyo taahira hata kidogo; hayo maneno yako hata mtoto wako na mkeo hawawezi kuyakubali watasema baba kaolewa na Mafisadi.

Kweli umekuwa mpumbavu hivyo au hukusoma hiyo mada kabla ya kuituma; au ni ufinyu wa Elimu na uelewa!! mbona hapo hamna hoja hata moja ya Arusha au wewe SiMWEMA au Makamba maana kama ni hoja ya Mwanasiasa nitaelewa kwa sababu wanasiasa wa CCM wamekuwa na akili nyepesi hivyo tokea zamani.

Umepoteza muda na umetumia ovyo nafasi ya Mawasiliano kwa kuweka Umimi katika tatizo la Jamii nzima umeonekana una akili kumbe ni tumbo limezidi uwezo ubongo wako.

Pole sana, umejitungia tatizo lako jipya ukalipa uhalali kuwa ndilo la Arusha alafu ukalielezea na ku-conclude utoto wako ni sawa na kuambiwa toa insha juu ya wanyamapori alafu wewe ukatoka insha ndefu yote inaelezea mapori na miti ya porini alafu ukasema umejibu swali.
 
PUMBA Bado zinakuja tu; mwanzisha mada hana point kabisa jamaa mweupe kweli wwwwwwuuuiiiii
 
Ndugu wasomaji,

Tumeshuhudia jinsi nchi yetu ilivyokumbwa na vurugu za kisiasa jijini Arusha. Katika vurugu hizo damu ilimwagika. Ni wakati wa masikitiko makubwa kwa nchi yetu na vilevile ni wakati wa tafakuri na mafunzo muhimu. Je, ni nini kilichopelekea vurugu na kumwagika kwa damu?

Kimsingi mgogoro wa kisiasa ulisafirishwa kwenda Arusha. Chanzo chake ni halmashauri ya Hai. Katika halmashauri hiyo CHADEMA kiliwaorodhesha Mh. Lucy Owenya(MB) na Mh. Grace Kihwelu (MB) kuwa wapiga kura katika uchaguzi wa mwenyekiti wa halashauri hiyo. Kuorodheshwa kwao kulikipa CHADEMA nafasi kubwa ya kuweza kushinda uchaguzi huo. Tukumbushane tu, kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe (MB) ni mjumbe katika halmashauri hiyo ya Hai. Kwa kutokuelewa sheria ipasavyo wajumbe kutoka CCM walipinga ushiriki wa wabunge hao wa CHADEMA katika uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri. Hata hivyo wabunge hao wa CHADEMA waliruhusiwa kupiga kura na kumpa ushindi mgombea toka chama hicho. Hivi sasa halmashauri ya Hai inaongozwa na CHADEMA.

Tujifunze katika hili kuwa mwenyekiti wa CHADEMA anatambua kuwa wabunge wa viti maalum wanaweza kusajiliwa katika halmashauri fulani na kukipa chama chao "advantage" katika maamuzi yatakayofanywa katika vikao vya halmashauri hiyo. Katika kufahamu hili ndipo mwenyekiti huyu akawachukua wabunge wake hao wawili ili waweze kushinda uchaguzi. Pingamizi kutoka CCM kisheria halikuwa na nguvu yoyote.

Je, CHADEMA walifanya nini baada ya kukutana na changamoto huko Hai?

Walichokifanya CHADEMA ni kupinga uamuzi wa mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha wa kumruhusu Mh. Mary Chatanda (MB) toka CCM kushiriki katika uchaguzi wa meya wa jiji la Arusha. Kigezo walichokitoa ni kwamba swala hilo si sahihi kisheria.

Tujiulize;
iwapo swala hilo si sahihi kisheria, ni kwanini Mh. Freeman Mbowe (MB) aliwasajiri Mh. Lucy Owenya(MB) na Mh. Grace Kihwelu (MB) toka CHADEMA kwenye uchaguzi wa Hai?
Je Mh. Freeman Mbowe (MB) alikuwa anajaribu kuvunja sheria?
Kwa vile waliopinga ushiriki wa wajumbe hao toka CHADEMA huko Hai ni wajumbe toka CCM, je CHADEMA inawatumia wajumbe wa CCM kuwajulisha sheria ya nchi inaruhusu vitu gani?
Iwapo CHADEMA hawajaridhishwa na maamuzi ya mkurugenzi wa Hai, je, ni sahihi kukataa maamuzi halali ya mkurugenzi wa jiji la Arusha kama majibu kwa mkurugenzi wa Hai?
Kwanini CHADEMA hawakuandamana Hai?

Kimsingi, maamuzi ya mkurugenzi wa jiji la Arusha ni maamuzi sahihi. Na wale wote waliowakatalia Mh. Lucy Owenya(MB) na Mh. Grace Kihwelu (MB) kushiriki uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri huko Hai hawakuwa sahihi - na kwa vitendo, mwenyekiti wa CHADEMA amedhihirisha kulitambua hili.

Kitendo cha wajumbe kutoka CHADEMA kukataa kuchiriki uchaguzi kwa kisingizio cha kuwepo kwa Mh. Mary Chatanda (MB) kama mjumbe kingepelekea jiji la Arusha kushiindwa kupata meya, iwapo mkurugenzi angeendelea kusubiri wajumbe wafikie theluthi mbili. Je, ni kwanini CHADEMA waliona sawa kwa jiji la Arusha kushindwa kufanya uchaguzi wa meya ilhali wakijua kuwa maamuzi ya mkurugenzi kumruhusu mjumbe huyo toka CCM ni sahihi?
Ninaamini CCM hawatajibu tukio hili kwa kuongeza mbunge mwingine wa viti maalum, kwa sababu kwa kufanya hivyo watakuwa wanaweka wananchi wa Arusha katika "political roller-coaster"

Hivi karibuni imeripotiwa kuwa CHADEMA kimeamua kumsajili Mh. Anna Komu (MB) kama mjumbe wa halmashauri ya jiji la Arusha. Maamuzi haya ni sahihi kisheria na yanathibitisha kuwa viongozi wa CHADEMA wanatambua kuwa Mh. Mary Chatanda (MB) ni mjumbe halali kwa sheria za nchi. Hata hivyo viongozi hao hawajaonyesha tabia ya kiung'wana ya angalau kuomba radhi kwa kuupotosha umma wa Arusha. Hii imedhihirisha kuwa viongozi hawa sio watu wawajibikaji.

Wito: CHADEMA kisisikilizwe tena mpaka viongozi wake wakuu waliochochea vurugu zilizosababisha vifo huko Arusha (Dr. Wilbroad Slaa, Mh. Freeman Mbowe, Mh. Ndesamburo, ) watangaze kujiuzuru/ kuomba radhi umma kwa upotoshaji walioufanya.

Kwa nini kisisikilizwe?
CHADEMA kimekuwa chama ambacho viongozi wake wamekuwa wakifanya maamuzi bila kuyafanyia utafiti na tafakuri ya kutosha na inapodhihirika kuwa maamuzi hayo si sahihi wamekuwa wakitafuta lugha za "longolongo" za "ujanjaujanja".
1.Tumeshuhudia wakianzisha mchakato wa kutokumtambua Rais. Walipgundua kuwa uamuzi huo hautekelezeki/ hawawezi kuutekeleza, wakachezacheza na maneno bila kuwaomba radhi wananchi waliowapa support.
2. Tumeshuhudia viongozi wa CHADEMA wakisema kura zao za urais zimeibiwa na mgombea wao akiahidi kuleta vidhibiti vya kuhujumiwa kwenye uchaguzi. Mpaka sasa mgombea huyo wa CHADEMA hajatoa kidhibiti chochote wala hakuomba radhi kwa kutoa ahadi hewa.
3. Tumeshuhudia viongozi na waasisi wa CHADEMA wakiwanyima wanachama wao haki yao ya kikatiba ya kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama hicho.
4. Tumeshuhudia viongozi wa CHADEMA wakiwanyima wanawake wanachama wa chama hicho kuchagua wabunge wao wa viti maalum.
5.Tumeshuhudia viongozi wa CHADEMA wakichangamkia kupeleka mchakato wa katiba bungeni. Walipokumbushwa na mwanazuoni Prof. Issa Shivji kuwa kufanya hivyo ni kuukabidhi mchakato huo kwa CCM wamekosa moyo wa kukiri upungufu kwenye mkakati wao huo/ angalau kumshukuru Prof. Shivji kwa angalizo hilo muhimu.
6. Tumeshuhudia viongozi wa CHADEMA wakitoa tamko la kutokuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi waliyoshitakiwa. Viongozi wanaotegemewa kuonyesha mfano wa kutii utawala wa sheria wanaonyesha dharau kwa mahakama!
7.Leo tunashuhudia CHADEMA ikipeleka mbunge katika halmashauri ya jiji la Arusha jambo ambalo walipinga lisifanywe na CCM.

Je ni lini tutaanza kuwawajibisha viongozi wa CHADEMA?

Kama tunataka kuwaandaa viongozi wa CHADEMA kuwa viongozi wa taifa wawajibikaji, ni LAZIMA tuwawajibishe kuanzia sasa kwa maamuzi yao yote yanayokosa busara.
kweli wewe marcopolo umechoka saaaaaaaaaaaaaana, huna hoja ful crap!
unataka watanzania wawasikie kina nani tena?
CHADEMA inapigania haki za wanyonge CCM wanapigania kuendeleza ufisadi.
CHADEMA inalenga kuwa na katiba itakayoleta maendeleo CCM inalenga kwenye kuendelea na ya sasa ili kuwakandamiza watanzania
CHADEMA inapigania elimu bora, makazi bora, maslahi bora, afya bora CCM inapigania bora elimu, hakuna kabisa issue ya makazi, hakuna kabisa issue ya maslahi, bora afya -mijengo ya zahati bila dawa na wataalam
CHADEMA inapigania kuwawajibisha MAFISADI CCM inasimamia walipwe haraka pesa zao na madai yao na hawaguswi
CHADEMA inapigania umoja wa kitaifa CCM wanaendelea na propaganda zao za udini -stupid
CHADEMA inapigania uhuru wa kweli CCM inapigania kuwakandamiza watanzania-

WAKATI CCM INAENDELEA KUUA WATANZANIA CHADEMA INATEKELEZA ILANI YAKE
 
Ze Marcopolo,

Ungeomba angalao darasa la kanuni,taratibu na sheria

Pia,hilo suala la kutaka uongozi wa CHADEMA kujiuzulu nadhani limefunikwa na hisia mfu,uelewa finyu na wingu la kudumaa kifikra ulipoichambua hoja ndiyo maana umefikia kwenye suluhisho.Nikipata muda nitarudi kukuelimisha. Mkuu,hongera kwa kujaribu kujenga hoja au hisia.We know how you feel

Ungekuwa na hoja ungetumia muda ulioutumia kuandikia mistari hii kuelezea hizo kanuni unazodhani unazifahamu peke yako kama vile ni zako binafsi.
 
Ndugu wasomaji,


Mkuu ze Basi la Marcopolo; naomba nipingana nawe katika kusema kuwa matatizo ya Arusha yametokea Hai huo ni Uongo na kuoanisha mambo kwa makusudi ili kudanga Umma. Hai ni Hai na Arusha ni Arusha hata taarifa za Serikali yako haikuwai kuonyesha mlingano huo batili; Ukipenda chama husipende hadi viongozi wake penda maslahi na mikakati yake katika Kujenga nchni yetu, CCM ilikufa na Mzee nyerere labda kama hujui pokea hiyo taarifa, na kwa kuonyesha kuwa unadangaya Umma angalia hata jina lako hamna mtu duniani anaitwa ZEmarcopolo hapo tu ni mwanzo wa utata wa hoja zako, yaani hata wewe mwenyewe ni Mtata.

Maneno yako takribani yote 829 ni ya uongo kasoro majina ya watu; ebu lete ushahidi kuwa CDM walikuwa wanapinga huyo Maria hasipige kura Arusha, huna kumbukumbu kwa mambo yaliyofanyika January 5, 2011 utaweza kukumbuka ya 1995 au ya 2005 au hata ya kwenye kampeni kuwa Kikwete alitoa ahadi zipi na kafanya nini hata sasa!! Kweli wewe ni basi tena la abiria; Chadema hawakuwa wanapinga kupiga kura kwa huyo mama siku ya kupiga kura, Chadema wanapinga Kura kupigwa wakati wapo katika udhuru kujali mikakati yao kama Chama wewe unageuza kuwa wanapinga huyo mama kupiga kura!!? huoni tofauti hapo!
Tujiulize;
wewe umekuja na swala lako jipya unataka kulifanya kuwa ndilo la Arusha, nadhani unautapia ubongo; Ugonjwa mbaya sana ni ugonjwa wa kukosa uwezo wa kufikiri na kutambua mtu wa namna hiyo ufikiri kulingana na njaa aliyonayo na tumbo ndio driving engine ya mwili wake, ni watu wepesi kununuliwa ata kwa bia na nyama choma ilikumsifia bwana wake, katika hali mbaya sana kiuchumi na kisiasa ambayo Tanzania inayo sasa mtu mwenye akili timamu hawezi hata kidogo kusema uongo kama wako kwa makusudi ili kupotosha Umma kwa kwa kununuliwa bia alafu hasionekane siyo taahira hata kidogo; hayo maneno yako hata mtoto wako na mkeo hawawezi kuyakubali watasema baba kaolewa na Mafisadi.

Kweli umekuwa mpumbavu hivyo au hukusoma hiyo mada kabla ya kuituma; au ni ufinyu wa Elimu na uelewa!! mbona hapo hamna hoja hata moja ya Arusha au wewe SiMWEMA au Makamba maana kama ni hoja ya Mwanasiasa nitaelewa kwa sababu wanasiasa wa CCM wamekuwa na akili nyepesi hivyo tokea zamani.

Umepoteza muda na umetumia ovyo nafasi ya Mawasiliano kwa kuweka Umimi katika tatizo la Jamii nzima umeonekana una akili kumbe ni tumbo limezidi uwezo ubongo wako.

Pole sana, umejitungia tatizo lako jipya ukalipa uhalali kuwa ndilo la Arusha alafu ukalielezea na ku-conclude utoto wako ni sawa na kuambiwa toa insha juu ya wanyamapori alafu wewe ukatoka insha ndefu yote inaelezea mapori na miti ya porini alafu ukasema umejibu swali.

Arafat,
Kama hujajua kuwa mgogoro uliotokea Arusha asili yake ni Hai basi unahitaji kuyapitia mabandiko ya awali kabla ya kurukia mjadala huu ambao unaonyesha kuwa mbali kuliko kiasi cha taarifa ulizo nazo.
Na kama hilo hulijui basi siwezi kuendelea kuchambua hoja zako nyingine ambazo ni hafifu mno.
 
Baada ya kufuatilia michango yote hapa, nimegundua kuwa kuna wachangiaji ambao hawajaelewa mada kuu.
Ninachoelezea hapa ni uwajibikaji wa viongozi, pale wanapokiuka maadili ya uongozi. Ninasisitiza kuwa viongozi wa CHADEMA wawajibike kwa kukosa busara na nimeshauri wafanye hivyo kwa kujiuzuru au kuomba radhi. Sijawaambia wakiue chama kama wengine walivyoninukuu.
Je, CHADEMA mna viongozi haohao wasio na busara tu? Kwa nini hao wasio na busara wasikae pembeni kuwapisha wale wenye busara ili chama kianze kujijengea heshima kwa jamii ya waelewa? Tangu kuisha kwa uchaguzi mkuu, viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakitoa maamuzi ambayo yamekishushia heshima chama hicho na mengine yamepelekea umwagaji damu... WAWAJIBIKE!
 
Kilaza mwenyewe wee Kibwengo,

Nilikuwa namjibu ZeMarcopolo na si wewe. Yeye aliku-quote vibaya na imeonekana kama ni UJUMBE wako. Ukisoma maneno ya ndani si wewe uliandika ila mwingine.

Kilaza sasa hapa ni nani? Lione miguu imekaa kama Kuku anataga........

Unapenda sana kurukia Wanaume wanapoongea siyo? Angalia usije kutua kwenye ncha kali za Wanaume wa kikweli.

Mwenyewe ndiyo usome kwa makini na uje kujibizana na mie....... Domo kaye weee............

Tunasema HUJUWI na siyo UJUI, Mzaramo weee.....

,
Mpuuzi hata ujui unachoongea,nenda chadema au Tume then omba fomu za wabunge wa viti maalum za chadema soma kwa umakini halafu uje ujibizane na mimi.KILAZA.
 
Kila anayeingia kwenye Siasa ni kuwa kashabarehe kuwa MALAYA.

Kama hujabarehe basi huwezi hata kuchukua form, labda wakubebe na kukutupa kwenye Ofisi ya ubunge, Waziri, Rais, Diwani nk ila madhara yake ya kubebwa na kupachikwa kwenye cheo si unayaona Tanzania inakokwenda?

Umalaya ninaousema mie si ule wa kujiuza MWILI. Ni uwezo wa kudanganya kwa kujifanya una machungu sana ya nchi yako. Kwa wale akina dada unamkuta analia machungu hasa kumbe hamna lolote. Na kwa wanaume Majigolo, utaliona linamsifia Kizee wa watu na mama anafikiri Kijana anafaidi kweli kumbe anaombea tu amalize kazi na achukue hela yake.

Wakati wa kampeni wanaenda kila sehemu. Hata Sikonge wanafika ila wakishapata madaraka, huwaoni tena. Muda ukifika wanakuja tena na kujifanya wana uchungu sana na nchi yao. Huu ndiyo UMALAYA ninaousema. Wengine hubadili vyama, wengine hubadili misimamo, wengine hubadili .................... Ili muradi Mkono uende kinywani au MADARAKA.

Ukiona WANAUME wanakumbana Vikumbo, ujuwe vitu vitatu POWER, SEX and MONEY.
Mhhhh
Huyu anayechapa umalaya kabla ya kubarehe(chadema),mhh muogopeni huyo. Akibarehe mmekwishaa.
 
UNalazimisha tukubali kula pumba zako. Flow ya simulizi lako ni nzuri lakini ni flow ilo beba uhuni na umamruki.
Kifupi wewe ni bingwa wa kuandika uongo ili ukubalike kama ukweli.
Hii Story iko POWERED BY PESA YA UFISADI
 
Hahahaaaaa hahaaaaa,

Chadema ni MAFISADI siyo? Hili hata mie nakubaliana nawe kabisa.

Jamani, Chadema ni MAFISADI. Hebu yaone hapa yalivyopendeza.

165348_142463672477012_142460699143976_247901_5579287_n.jpg

Duh! Naona unataka kupindisha bandiko, CCM sio Malaya kabisa tena tuombe radhi! Chadema inajulikana kwa ufisadi kiwembe!
 
Naona umechukia kwelikweli hadi umetuma ujumbe mara mbili.

Nimeuliza swali moja, kama si CHADEMA basi ni nani? Hutaki kusema.

Kama Kudanganya, mbona CCM wameshamaliza PhD zote na hadi za Kupewa na University za Kata?

Kama Kuuwa, wameuwa sana huko Zenji, Mwembe Yanga, Kolimba, Arusha, Mbeya, Albino nk nk.....

Kumbuka maneno ya Mkuu FMes kuwa "viongozi wa Tanzania ni reflection yetu wenyewe....."

Kama uko Tanzania, unaweza kukuta hata wewe mwenyewe hapo ulipo una tabia fulani CHAFU SANA.

Mie mwenyewe ninazo na ndiyo maana sijagombea Sikonge hadi leo na tumeacha Mwalimu wa darasa la Tatu awe mbunge.

Kama si CHADEMA ni NANI KWA TANZANIA? CCJ? CUF? TLP au tubaki CCM?

Kama CCM wakianza kuomba msamaha, basi watamaliza siku Yesu anarudi.
Nimesema CHADEMA kisisikilizwe tena mpaka viongozi wake wakuu waliochochea vurugu zilizosababisha vifo huko Arusha (Dr. Wilbroad Slaa, Mh. Freeman Mbowe, Mh. Ndesamburo, ) watangaze kujiuzuru/ kuomba radhi umma kwa upotoshaji walioufanya.

Sasa ugumu hapo uko wapi?
Ni swala la viongozi kuwajibika tu na chama kikaendelea na viongozi werevu wenye busara. Au hao waliosababisha vurugu Arusha ndio watu pekee wanaoweza kuiongoza CHADEMA?
 
CCM wametumia kila njia na sasa wameshindwa.

Wakimkamata na KUMFUNGA SLAA kwa kweli sijui nini kitatokea.

Kuna mambo mengine heri wayaache tu maana yatalipua nchi zaidi ya Kuwakamata Mafisadi.......


Dk. Slaa afanyiwa njama kufungwa
• Lengo ni kuwanyamazisha viongozi wengine wa upinzani

na Edward Kinabo


NJAMA nzito zinasukwa ndani ya Jeshi la Polisi, Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake ili kuhakikisha Dk. Willibrod Slaa anafunguliwa mashtaka mapya na kuhukumiwa adhabu ya kifungo jela kwa makosa yanayohusiana na vurugu zilizotokea jijini Arusha hivi karibuni, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka polisi, vigogo wa CCM na serikali wameamuru kuwatisha wapinzani na wananchi kwa jumla, kwa "kumtoa kafara kiongozi mkubwa wa upinzani, kwa mara ya kwanza" kama njia pekee iliyobaki kuinusuru serikali ya CCM madarakani.
Vyanzo hivyo, vinasema njama hizo ni kuhakikisha Dk. Slaa anatiwa gerezani ili kuwatisha na kuwanyong'onyeza viongozi wengine wa chama chake wanaodaiwa kuisumbua CCM na serikali yake kwa kufanya kile kilichoitwa "siasa mpya za kuhamasisha umma kuichukia na kuipinga CCM na serikali ili nchi isitawalike."
Hatua ya Jeshi la Polisi kushirikiana na Idara ya Habari (MAELEZO) kutengeneza na kutangaza video kupitia vyombo vya habari, yenye picha na ujumbe wa kikituhumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya uchochezi, imetajwa kama njia ya jeshi hilo kujikosha kwa mauaji, na vile vile kujenga mazingira ya kuwatia hatiani viongozi wakuu wa CHADEMA kwa kupalilia propaganda chafu dhidi yao, zisizoeleza chanzo cha kauli zao kali.
Hatua hiyo imekifanya chama hicho kutayarisha mkanda wa video utakaaoonyesha hali halisi ilivyokuwa ili kusahihisha kile ambacho chama hicho kimeita "uchakachuaji wa polisi."
Hata hivyo, baadhi ya wafuatiliaji na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini wameliambia gazeti hili kuwa serikali "ikifanya kosa la namna hiyo la kufunga Dk Slaa, inaweza kujikuta nchi ikiwaka moto na kulazimisha wananchi kuing'oa serikali madarakani kwa nguvu kama ilivyotokea Tunisia katika siku chache zilizopita.."
"Yeyote aliyewashauri serikali na polisi kufanya hivyo haitakii mema serikali na CCM. Upepo wa sasa kisiasa ni mgumu na mbaya kwa serikali, hivyo inapaswa kufanya maamuzi makini, si kukurupuka; sasa hivi mabavu na dhuluma si mbinu nzuri ya kutumiwa na serikali; vinginevyo yatatokea yasiyotarajiwa," kilisema chanzo kimoja kutoka serikalini.
Katibu mkuu huyo wa CHADEMA pamoja na viongozi wenzake na wafuasi wao 31, walifunguliwa kesi Januari 6 mwaka huu, wakikabiliwa na shtaka la kukusanyika kinyume cha sheria Januari 5 jijini Arusha, siku ambayo chama hicho kilifanya maandamano ya amani kushinikiza kurudiwa kwa uchaguzi wa meya.
Maandamano hayo hata hivyo yalivurugwa kwa nguvu ya silaha na vipigo kutoka kwa Jeshi la Polisi, hatua iliyozusha vurugu na mashambulizi zaidi ya risasi zilizoua watu watatu.
Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena keshokutwa katika Mahakama ya Mkoa wa Arusha.
Taarifa zaidi za uchunguzi zinasema vigogo wa CCM na serikali kwa kulitumia jeshi hilo la polisi na mawakili wa serikali, wataongeza mashtaka mapya dhidi ya Dk. Slaa na baadhi ya viongozi wengine wa chama hicho ili mwishowe wahukumiwe adhabu ya kifungo kwani shtaka moja lililopo sasa katika kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, halina nguvu ya kuwapeleka gerezani kama watatiwa hatiani.
Wakati Dk. Slaa akiwa ndiye mlengwa mkuu, njama hizo zinalenga kutumia taratibu za kawaida za kisheria katika kuongeza mashtaka mapya ya kumtuhumu kufanya ‘uchochezi' yeye na wanasiasa wengine watatu ambao alihutubia nao mkutano wa hadhara katika Uwanja wa NMC jijini Arusha jioni ya siku hiyo ya maandamano.
Wanasiasa hao ni mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo, mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, na kada wao maarufu, John Heche, kutoka Tarime.
"Watadai kuwa Dk. Slaa na wenzake hao watatu walitoa kauli za uchochezi katika viwanja vya NMC na wataishawishi mahakama ione kwamba kauli zao zilikuwa chanzo kikuu cha vurugu zilizotokea Arusha na kusababisha watu wauawe ….na kwa hiyo watajaribu kuwahusisha moja kwa moja na vifo hivyo ili mwishowe waje wahukumiwe kwenda jela kwa kufanya uchochezi uliosababisha madhara makubwa kwa jamii," alisema mtoa taarifa wetu mwingine aliye karibu na baadhi ya wajumbe wa kamati maalum iliyodaiwa kuundwa siku mbili tu baada ya tukio la Arusha ili kufanikisha mkakati huo.
"Hivi sasa wanajaribu kuwaandaa vizuri wananchi kwa kuonyesha picha za video na kutoa machapisho mbalimbali kwenye magazeti ili waamini kuwa Dk. Slaa na viongozi wa CHADEMA ndiyo chanzo cha yote yaliyotokea Arusha," aliongeza.
Hatua ya Jeshi la Polisi kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuwaeleza kile ilichokiita "taarifa ambazo wananchi hawajaambiwa kuhusu vurugu za Arusha zilizotokea Januari 5 mwaka huu" imeelezwa kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa njama hizo ili kuuandaa vema umma uje unyamazie kile kitakachowafika viongozi hao wa CHADEMA.
Katika mkutano huo, Kamishna Paul Chagonja anayehusika na operesheni na mafunzo katika jeshi hilo, alitumia maelezo ya mdomo, maandishi na picha za video kutoa tuhuma dhidi ya viongozi wa CHADEMA kuwa ndio chanzo cha vurugu zilizotokea Arusha na kusababisha mauaji.
Tukio hilo lilifuatiwa na kurushwa zaidi kwa picha hizo za video katika vituo vya televisheni na redio na kuchapwa kwenye magazeti taarifa nzima ya polisi yenye maelezo hayo ya tuhuma dhidi ya viongozi wa CHADEMA.
Hata hivyo, picha za video zilizoonyeshwa kwa wanahabari wiki iliyopita na hata kurushwa kwenye vituo vya televisheni zilionekana dhahiri kupingana kwa kiasi kikubwa na maelezo na sababu zilizotolewa kama kigezo cha kuyasambaratisha maandamano hayo kwa silaha.
Picha hizo zilionyesha kundi moja tu la viongozi na wafuasi wa CHADEMA lililoanza maandamano kwa amani kutoka eneo ilipo Hoteli ya Mount Meru likitumia njia moja kuelekea Sanawari Mataa na hakukuonekana makundi mengine yaliyokuwa yakitumia njia nyingine kuandamana ambayo yangeleta bughudha na kuwapa polisi shida ya kulinda kama alivyodai kamishna huyo.
Aidha, picha hizo za video pia hazikuonyesha waandamanaji walioanza kufanya fujo au kuashiria kufanya fujo mpaka walipofika eneo la Sanawari Mataa ndipo Jeshi la Polisi lilipovuruga hali ya amani kwa kuanza kufyatua mabomu ya machozi.
Kwa upande mwingine, sinema hiyo iliyorekodiwa na Jeshi la Polisi kuhusu matukio yaliyotokea Arusha ilionekana kuchakachuliwa au kuhaririwa sana kwa kukatwa baadhi ya vitendo vya kikatili vilivyofanywa na askari polisi kama vile vya kumpiga sana na kumdhalilisha kijinsia Josephine Mushumbusi, ambaye ni mchumba wa Dk. Slaa.
Matukio mengine ambayo yalirushwa kwenye picha za vituo vya televisheni hapo kabla lakini hayakuonekana katika kanda hiyo ya polisi ni pamoja na tukio la polisi kuvunjavunja vioo na kuliharibu gari lililokuwa limewabeba Josephine na Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Owenya.
Wakati picha hizo, ambazo polisi hawakuzitumia, zilionyesha kuwa vurugu zilianza baada ya polisi kuanza kuyatawanya maandamano hayo kwa mabomu na kuwakamata baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wapatao 31, Jeshi la Polisi limekuwa likitumia zaidi picha za video za mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya NMC jioni ili kuhalalisha hoja kwamba chanzo kikuu cha vurugu na mauaji yaliyotokea Arusha ni kauli za Dk. Slaa, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, na wanasiasa wengine waliohutubia mkutano huo.
Picha hizo zilimwonyesha Dk. Slaa na Ndesamburo wakilalamikia kusambaratishwa kwa maandamano yao kwa mabomu, risasi na vipigo vya polisi pamoja na kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho, akiwemo mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, hivyo kuwasisitizia wananchi kuendelea kudai haki ikiwa ni pamoja na kuwatoa viongozi hao polisi walikokuwa wakishikiliwa.
"Kipande hicho cha mkanda wa Arusha ndicho watakachokitumia zaidi katika kuijengea nguvu kesi yao dhidi ya Dk. Slaa na wenzake kwamba walitoa kauli za uchochezi," alisisitiza mtoa habari wetu.
Mwanasiasa mwingine aliyewahi kushtakiwa na kuhukumiwa adhabu ya kifungo kwa kukutwa na hatia ya kutoa kauli za uchochezi ni mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila.
Mtikila alifungwa jela katika gereza la Ukonga, Dar es Salaam Desemba 14, 1999 kwa hatia ya uchochezi na kutumikia kifungo cha mwaka
mmoja.
Mwaka huo alipatikana na hatia ya kutoa kauli chafu na za uchochezi dhidi ya viongozi wa CCM na serikali yake juu ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Horace Kolimba.
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni, Gabriel Mirumbe, alimtia hatiani kwa maelezo kwamba mwanasiasa huyo alitoa maneno ya chuki dhidi ya viongozi wa CCM na serikali kwamba walimuua Kolimba na ni mashetani.


Dk. Slaa afanyiwa njama kufungwa
 
Arafat,
Kama hujajua kuwa mgogoro uliotokea Arusha asili yake ni Hai basi unahitaji kuyapitia mabandiko ya awali kabla ya kurukia mjadala huu ambao unaonyesha kuwa mbali kuliko kiasi cha taarifa ulizo nazo.
Na kama hilo hulijui basi siwezi kuendelea kuchambua hoja zako nyingine ambazo ni hafifu mno.

ZeMarcopolo haiingi akilini hata kidogo mimi nimekwambia hoja siyo kupiga kura kwa Bibie Maria Hoja ni kwanini kura zipigwe wakati wengine wapo faragha kujadili jinsi ya kujipanga ki-Chama kabla ya kupiga kura?? hiyo ndio hoja ya msingi hapa.
 
ZeMarcopolo haiingi akilini hata kidogo mimi nimekwambia hoja siyo kupiga kura kwa Bibie Maria Hoja ni kwanini kura zipigwe wakati wengine wapo faragha kujadili jinsi ya kujipanga ki-Chama kabla ya kupiga kura?? hiyo ndio hoja ya msingi hapa.

wewe unajua alichokisema Lema kuwaambia viongozi wake? Hujui kilichopelekea kipigo chake? au unataka ligi tu
 
Ndugu ZeMarcoPolo nimesoma kila post katika thread hii, hakuna hata mmoja aliye thubutu kujibu hoja zako! Fact ni kwamba ur article is too strong for these week minds! Thanks bro, Keep it up!
 
wewe unajua alichokisema Lema kuwaambia viongozi wake? Hujui kilichopelekea kipigo chake? au unataka ligi tu

Mjepu,
Huyu Arafat hata hajui uhusiano kati ya mvutano wa Arusha na ule wa Hai, yaani hana taarifa zozote juu ya kiini cha mvutano. Halafu kitendo cha wajumbe wa CHADEMA kususia uchaguzi anakiita ni kitendo cha kutoka nje kujadiliana. Yaani ameamua kulijadili hili swala kihuni. Ndio maana nimempotezea tu.
 
Back
Top Bottom