Vyama vingi hasa vya upinzani kikiwemo chadema vinabebwa na majina ya watu hasa wale walio na umaarufu lakini ukimuuliza hata mwananchi wa kawaida nini sera ya chadema kuhusu ardhi haijui,nini sera yake kuhusu elimu,afya,usalama wa taifa,polisi,kuhusu vyuo vikuu, kuhusu uwekezaji ,nishati na madini yetu, gesi hakuna hata mtu mmja anaweza kueleza watu tukaelewa ila ukitaja unamjua dk slaa au unamjua mh mbowe ama zito watakwambia ndio na ndio maana nipo chadema. Mytake nccr ilikufa kwasababu chama kilibebwa na watu na sera za chama hazikueleweka kwa wananchi kama chadema hivyo mrema alipoondoka kwa kuwa watu walifata majina na umaarufu wa kiongozi wote wakahama chama kikapungua nguvu,vilevile tlp,cuf na udp utaona vyama sera zao hazieleweki ispokua viongzi wao ndio wananchi wanawajua. Sasa chadema wanakubalika sehemu za mijini na sababu kubwa ni vijana wengi hawana ajira na hivo kupiga kura za kuiadhibu ccm ila si kwamba wameelewa sera za chama ambacho wanakichagua ilakwakua no other choice. Hivyo ilichadema wafanye vizuri wasitumie jina la mtu au umaarufu wa mtu watangaze sera zao vijijini wananchi wakielewa sera hapo ndipo chama kitakua na nguvu na si nguvu ya soda.
Kila mtu anapenda chama chake na hujitahidi kubuni mbinu za kukichafua chama pinzani kama unavyojaribu kufanya. Hivi CCM inaeleweka sera yake kweli?. Tufuatane taratibu kwa hoja hapa:-
Sera ya elimu CDM wanasema elimu itolewe bure kwakila mwananchi hii ilinadiwa sana na Dr Slaa wakati wa uchaguzi na mpaka sasa inanadiwa na wananchi wanaikubali.
CCM wao wanasema bola liende hivyohivyo una hela peleka mtoto wako kwenye shule nzuri huna shauri yako.
CDM kwenye ardhi wana sema ni mali ya wananchi na wote watapimiwa ili wamilki kihalali
CCM wao wana sema hati ya kumiliki ardhi ni kwa viongozi na matajiri tu (chunguza utaona ukweli)
CDM kwenye afya wanasema lazima kuboresha hospitali zetu na vituo vya afya ili wananchi na viongozi wao tutibiwe haphapa nyumbani sio India na Ulaya.
CCM wao wanasema viongozi watatibiwa nje ya nchi kwenye hospitali nzuri lakini wananchi watibiwe hapahapa Muhibili na sehemu zingine ambako hakuna dawa, madakitari wasilipwe vizuri lakini wabunge walipwe vizuri hatakama wana sinzia tu bungeni.
CDM kwenye usalama wa taifa wanasema kazi ya wanausalama ni usalama wa nchi sio usalama wa CCM, sio kuiba kura wakati wa uchaguzi na mambo kama hayo.
CCM wao wanasema wananchi wapigwe tu, wapinzani waibiwe kura zao, mafisadi walindwe kwa gharama yoyote ile, ndio maana unaona twiga anaingia kwenye ndege, Banki kuu inaibiwa, Mikataba mibovu kila sehemu na mambo kama hayo.
CDM kuhusu vyuo vikuu wanasema ni viwanda vya kutoa wataalamu mbalimbali kwaajili ya maendeleo ya taifa, na watafiti wa kutoa ushauri ilikutatua matatizo ya nchi kwa ufanisi, kwahiyo vyuo vikuu vinatakiwa vihudumiwe vizuri mikopo ya wanafunzi itolewe bila ubaguzi na walimu walipwe vizuri.
CCM wao wanasema hakuna hela za kuendeshea vyuo, ndio maana unaona maprofesa wanaacha kufundisha wanakuwa wabunge wanako lipwa vizuri
CDM kuhusu madini wanasema huo ndiyo utajiri wa nchi mikataba yake iwe ya manufaa kwa wananchi na ichangie kwenye pato la taifa na kila mtu aone manufaa kutoka kwenye madini.
CCM wao wanasema mikataba kwanza siri halafu wageni wapate asilimia 97 sisi asilimia 3 ni hivyohivyo kwenye maliasili zote.
Sasa we mleta maada kama CCM inapendwa kwa sera zake ikowapi sera nzuri hata moja tu ya CCM?. Kama wewe ni mtanzania mwenzetu hujui kuwa twiga wetu sikuhizi wanapanda ndege kwenda Uarabuni? Hujui wizi wa Benki kuu?, Richmond, Kagoda, Mikataba mibovu ya madini, Elimu watoto wakifeli tunatengeneza utaratibu wa kuwafaulisha bila kusoma, Kuwa mkulima kwa sera za CCM ni sawa na laana badala ya utajiri. Tuache ushabiki wa kitoto kwenye mambo muhimu kama ustawi wa taifa. sasahivi hakuna mbinu yoyote kutoka CCM ya kulikwamua taifa kutoka hapa tulipo ni mabadiliko tu yanayoweza kutukwamua. Walio kosea zamani tutawaombea msamaha wasishitakiwe kama alivyofanya mzee Mandela.