Vyama vingi hasa vya upinzani kikiwemo CHADEMA vinabebwa na majina ya watu hasa wale walio na umaarufu lakini ukimuuliza hata mwananchi wa kawaida nini sera ya CHADEMA kuhusu ardhi haijui,nini sera yake kuhusu elimu,afya,usalama wa taifa,polisi,kuhusu vyuo vikuu, kuhusu uwekezaji ,nishati na madini yetu, gesi hakuna hata mtu mmja anaweza kueleza watu tukaelewa ila ukitaja unamjua dk slaa au unamjua mh mbowe ama zito watakwambia ndio na ndio maana nipo CHADEMA.
My take
NCCR ilikufa kwasababu chama kilibebwa na watu na sera za chama hazikueleweka kwa wananchi kama CHADEMA hivyo Mrema alipoondoka kwa kuwa watu walifata majina na umaarufu wa kiongozi wote wakahama chama kikapungua nguvu,vilevile TLP, CUF na UDP utaona vyama sera zao hazieleweki ispokua viongzi wao ndio wananchi wanawajua. Sasa CHADEMA wanakubalika sehemu za mijini na sababu kubwa ni vijana wengi hawana ajira na hivo kupiga kura za kuiadhibu CCM ila si kwamba wameelewa sera za chama ambacho wanakichagua ilakwakua no other choice. Hivyo ili CHADEMA wafanye vizuri wasitumie jina la mtu au umaarufu wa mtu watangaze sera zao vijijini wananchi wakielewa sera hapo ndipo chama kitakua na nguvu na si nguvu ya soda.