CHADEMA kimekuwa Chama kikubwa mpaka kimepitiliza

CHADEMA kimekuwa Chama kikubwa mpaka kimepitiliza

Joined
Sep 28, 2014
Posts
78
Reaction score
113
Chadema kimekuwa chama kikubwa mpaka kimepitiliza sana,yaani mbali na wanachama wake,kimekokota waliokata tamaa kupiga kura, kimekokota wanachama wa ccm kwa wingi sana na wengine bado wanaongezeka mfano kule kyela (mbeya )

Kwa sasa Chadema kinawanachama wenyekadi milion 6.0,wanachama wengine namaanisha wapenzi na washabiki ni wanakadiriwa kufikia milion 9. na bado wanachama wanaendelea kuongezeka kila kukicha.hivyo basi kwa tathmin hiyo chadema huwezi linganisha na ccm yenye wanachama milion 5.3

Hivyo basi kwa sasa ikitokea Chadema igawanywe vipande na kutengeneza vyama vingine vya siasa inauwezo wa kutengeneza vyama zaidi ya vinne vya siasa na bila Chadema kuyumba wala kutetereka na kubakia chama imara na chenye nguvu zaidi.

Hasa kivutio kikubwa ndani ya Chadema ni sera na itikadi yake kwani sera ya chadema. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (#ThePeople’sPower) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.

Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.

Historia inaonyesha kuwa “UMMA” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.

CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi.

Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.

Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.

Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
 
People's.... CHADEMA ni Mpango wa Mungu
 
Ama kweli naamini cdm imekuwa maana imefika hadi huku kwetu ifwagi wilayani mufindi wananchi wameanza kufunguka kifikra
 
ngoja waje magamba lazima wajambe ushuzi wa kijani humu
 
Chadema kimekua japo hakijapata viongozi waaomi karibu wote ni mbumbumbu wachochezi na wanaiombea nchi iaitawalike hawafai kwa Tanzania labda somalia
 
Tumebakiza moja tu,kuupigania Uhuru wa vyombo vya habari ili Uwazi na Uwajibikaji uongezeke!
 
Hata sisi tunaendelea kuwavua magamba huku tuliko mpaka basi,
yaani mpaka october 2015 CCM itakuwa inatafutwa kwa darubini
 
Siyaamini maneno yako Yaani ni Wewe au mtu mwingine duh kumbee hakika CDM ni mpango wa Mungu

Sasa Kamanda "tukishakomboa" nchi mawaziri na viongozi wengine wa serikali yetu tutawatoa wapi? Maana sisi makamanda wengi wetu hatuna sifa za kuwa viongozi hasa kutokana na level za elimu zetu.

...hebu tujadiliane kamanda...
 
Ccm inapoteza nguvu kwenye mizizi imebakiza majani,mwezi wa 11 tutakatq matawi ili majani yakauke
 
Sasa Kamanda "tukishakomboa" nchi mawaziri na viongozi wengine wa serikali yetu tutawatoa wapi? Maana sisi makamanda wengi wetu hatuna sifa za kuwa viongozi hasa kutokana na level za elimu zetu.

...hebu tujadiliane kamanda...
Level gani ya elimu unayoihitaji? kama ni chuo kikuu wako wengi tu, Kwenye chama kuanzia ngazi ya msingi mpaka kitaifa kuna viongozi wametulia na degree zao. lakini kikubwa tuanchokiitaji ni uwajibikaji kwa wananchi na kuchukua ufisadi kwa vitendo. Mfano: Andrew Chenge ni msomi wa Havard University lakini ni bonge la fisadi.....nadhani tuanze na viongozi wanaochukia rushwa then tuingize mambo mengine ya education level ambayo kimsingi viongozi wengi wa chadema wana sifa hizo zote

 
Back
Top Bottom