Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
nimefuatilia kwa umakini mitazamo yote iliyotolewa na wanajamvi kuhusu mada hii ,Binafsi ninaona tunahitaji kwenda mbali zaidi kuhusu mada hii ,kwa kawaida siyo kila sera ni lazima ziendani na katiba bali hazipaswi kuvunja baadhi ya vipengele vya katiba husika, kwa analysis aliyoifanya ng'wamapalala haitoi picha ni wapi imekiuka katiba ya chama .lakini pia huenda hajaelewa jambo moja ndani ya sera hii lengo kwa sasa si kuvunja mfumo wa sasa unaotambuliwa kikatiba ya nchi bali ni kuiunganisha mikoa hii kisera ili kuharakisha maendeleo katika kanda husika kulingana na geographia ya maeneo husika . pia ni kuupanua zaidi mfumo wa utawala kuwakaribia zaidi wananchi tofauti na mfumo wa sasa ambao hautoi fursa ya moja kwa moja kwa wananchi kusimamia na kupanga matumizi ya rasilimali walizonazo badala yake kila kitu kinatoka dar es salaam .kichama ni kuimarisha kanda za ushindi na kuendelea kuifinya ccm katika maeneo ambayo inayatawla kwa sababu tu wakazi wake hawana elimu ya kutosha ya uraia. sasa kwa mfumo huu wana nafasi kubwa ya kuipata . Binafsi naamini vinginevyo ccm watumie mbinu chafu katika uchaguzi ujao kubaki kwake kuko mashakani.:lying:
Umeleta ufafanuzi mzuri pia. Mkoloni aliweka mipaka ya majimbo kama ambayo chadema wanafanya sasa. Wenzetu Wakenya wangali na majimbo yale, sisi tumeyavuruka kabisa na kila awamu wanazidi kuigawanya mikoa.
Nyerere kwa wakati ule aliona hatari ya majimbo kutokana na hali ya baadhi ya makabila yalikuwa bado na nguvu za kichifu au kitemi. Leo hali hii imekufa, sioni khofu ya mfumo wa majimbo ya kikanda. Leo kila kona sote tu watanzania.