Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amewahakikishia wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwamba chama hicho kitashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki utakaofanyika hivi karibuni.Dr Slaa amesema chama chake kina nguvu kubwa jimboni humo na katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 chama chake kilifungua matawi 69 yaliyo hai mpaka leo katika kila kona ya jimbo hilo.
Dr Slaa amesema CHADEMA ilijifunza mengi katika jimbo la Igunga na kutahadharisha vitendo vya ugawaji rushwa kurubuni wapiga kura kamwe havitavumiliwa Arumeru.Pia alisema chama chake kimejipanga kutoa elimu kubwa ya uraia kwa wananchi wa Arumeru mashariki kupitia kampeni mara zitakapozinduliwa.Dr Slaa ameahidi kampeni safi na za kistaarabu.
SOURCE:MTANZANIA
Nimeipenda hii inayosema ''Dr Slaa ameahidi kampeni safi na za kistaarabu''
Inabidi vyama vyote vitoe ahadi hii,ule ****** wa Igunga usijirudie tena!!
Tuna mwamini sana Dr Slaa!
Wameru ni wajanja sana kwa mambo mengine, sidhani kama wanaweza kuendelea kuiamini ccm, ambayo kadiri siku zinavyosonga mbele inazidi kuhitaji oxygen zaidi ya kuipa uhai!
Sisi yetu macho lakini Slaa, asijiaminishe sana na ushindi Arumeru.