CHADEMA itasababisha Mauaji mwaka 2015

Toa maoni yako, sio kejeli kwa hii thread, mnakuwa kama mmekunya viroba wakati wa jua kali. Mnaudhi kweli yani.
 
Ludovick nakushauri uende kwa wanasaikolojia haraka usipuuzie maana una tatizo moja kubwa sana lililopo kichwani mwako. Tatizo lako ni kujua kuwa unafanya kosa kubwa na ukiwa peke yako linakusumbua hilo jambo ulilowahi kufanya. Kitu unachokifanya husitahili kabisa plesase muombe Mungu sana akusaidie ili uweze kujirudi na uwe na akili yako kama zamani.
 
Inawezekana kwa kiasi fulani umesema kweli, lakini unanishangaza, je wewe ni mwanachadema kweli? Je kuwa mwanachama si nipamoja na kutii viongozi waliochaguliwa kihalali?
 
Hivi we kijana umeludi tena,ulipoteleaga wapi?au magaidi wenzio maccm yalikupeleka masomoni ulaya ukajifunze mbinu za kutengeneza mabomu na keteka watu? Ni machafuko gani chadema wataleta? Kwani wao ndo wanamiliki majeshi na vyombo vya usalama? Njaa mbaya sana,kama umeshwa kufikili kwa kutumia ubongo tumia hata ----,kwa dunia ya leo mmebaki wajinga wachache sana mnaofikilia kizama za mawe.
 

Wewe nafikiri bado umeathirika sana na lile tukio la kutekwa na kuteswa kwa kibanda pamoja na kuandaa ile clip feki ya Lwakatare ndio maana unaandika vitu visivyokuwa na kichwa wala miguu, kama kweli upo timamu hasa kiakili naomba unipe ufafanuzi katika mambo haya ninayoyaweka hapa chini.

1. Hapo nilipoweka RED na BLUE vipi kuhusu mambo yaliyotokea kule Mwanza na Shinyanga ambapo vijana walikusanyika kudai matokeo yatangazwe na yalicheleweshwa na kutangazwa kwa mashinikizo? pale Mwanza walikubali kushindwa ili kuepusha vifo kwani vijana hawakuwa tayari kumuona macha anakuwa Mbunge wao, Kule Shinyanga matokeo yaligeuzwa na eti Masele akashinda kwa kura 1, na inatakiwa ujue maeneo yote ambayo matokeo yalicheleweshwa kutangazwa bila sababu za msingi CCM walikuwa wameshindwa kwani hata kule Igunga baadhi ya wasimamizi wametoa ushuhuda kuwa kilichotangwaza sio kile walichokiwasilisha makao makuu.

2. Naomba uniambie katika haya matukio hapa chini je yamesababishwa na CHADEMA?
Hapa ninatoa mifano hai ya matukio yaliyotokea ndani ya nchi hii ambayo Polisi hawajatupa majibu hadi sasa juu ya nani waliohusika na matukio haya na mengine kuna viongozi wa jeshi la Polisi walitumia posho na kukaa Arusha zaidi ya mwezi pasipo kutoa majibu wa taarifa hadi leo hii.

1. Aliyemmwagia Tindikali Said Kubenea

2. Aliyemteka na kumtesa Dr. Ulimboka
3. Aliyemuua Mwangosi
4. Waliomuua kwa kumchinja Mwenyekiti wa CHADEMAkule Usariver
5. Wale vijana wa UVCCM waliowashambulia wabungewa CHADEMA kule Mwanza
6. Waliomteka na kumtesa Kibanda
7. Waliomuwekea sumu Mwakyembe
8. Waliomgonga kwa makusudi Mwakyembe kwa lengola Kumuua
9. Waliomuua yule Kada wa CHADEMA kule Igunga
10. Waliommwagia tindikali kijana Musa kule Igunga
11. Waliomuua yule kada wa CCM kule Ndago Singida
12. waliolipua Bomu katika Mkutano wa CHADEMApale Soweto
13. Waliolipua Kanisani Olasit, Yule kijanawaliyemrundikia zile tuhuma sidhani kama ni mtuhumiwa halali.
14. Waliomuua Padri kule Zanzibar
15. Waliowamwagia Tindikali wale Mabinti wa UK
16. Waliowatuma akina Masogange kupeleka ileSembe(Madawa ya kulevya) Kule South Africa
17. Waliommwagia tindikali yule boss wa Home shoping center

3. Na wewe ulipohusika katika lile tukio la kumteka na kumtesa Kibanda ulitumwa na CHADEMA? kama ni CHADEMA ni nani aliyekutuma? na kama sio CHADEMA ulitumwa na nani? na ni wa chama gani?
 

Kijana hivi kweli wewe unaweza kujiita CHADEMA kweli mtu kila siku unakesha kwenye mitandao kuitukana.

Wewe ni kijana uliyeamua kununuliwa kama nyanya sokoni. Huwezi kabisa kuishauri CHADEMA ni chama imara wewe shauri ccm ambayo inapukututika kwa speed kubwa mpaka sasa inatumia mbeleko ya polisi.

Zile pesa alizokununua nazo ili uisingizie CHADEMA Ugaidi zimekwisha kukugharimu sasa zitaendelea kukugharimu zaidi. Wewe huwezi kuaminiwa tena na jamii kijana hata ukitubu.
 
mawazo ya kiwiziwizi haya!

Hivi unafikiria kwakutumia nini?halafu na wewe unajiita kamanda?wewe ni mtoto wa shetani,unachoongea kinakushuta wewe mwenyewe.huna kabisa ubongo kichwani,nadhani unaakili za zombie,bora unyamaze kuliko kututia hasira tunaoonewa na kuteswa na ccm.with tunapigania ukombozi wewe unaupinga.
 
Kweli naona kama kuna dalili ya vurugu 2015 ambacho sikubaliani ni pale unaposema CDM ndiyo itakuwa chanzo nasema HAPANA. Kitakacholeta vurugu ni pale kama tume ya uchaguzi haitafanyiwa marekebisho. Kwani kwa muundo ulivyo ni vigumu kuamini mpinzani anaweza kushindwa kihalali. Bw Iskariote unawapaka tu matope CDM
 
Chadema wanajua fika kuwa wanachofanya ni utoto na wehu wa hali ya juu lakini ni vema vyomba vya dola wakajipanga vema kuwazibiti mapema hawa wahuni ili tusifike huko.
 
Ipo siku chadema watayakumbuka maneno ya ludovick tena mda siyo mrefu tutakuja ambizana hapahapa jf na ukweli utakuwa bayana.
 
Siku hizi Ludovick unaandika mambo ya msingi sana
 
Yote haya kafanya kilewo na kundi lake la mauaji.
 
Simiyu Yetu Na CCM Yenu Ni Wajingawajinga Fulani, Mnadhani Kuwatumia Mapolisi Kutawafanya Msalimike 2015?, Mkae Mkijua Hata Hao Mapolisi Mnawalazimisha Tu Nao Wameshayachoka Maagizo Ya Kipumbavu Kutoka Lumumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…