CHADEMA itabaki kuwa CHADEMA tu

Ni mawazo yangu niombe radhi kutoa maoni yangu,

Lowassa na Duni waligombea wenyekiti?

Leo brother utalala na viatu, hutaki mimi nijadili nje ya Mbowe, lakini yoyote akijadili unahusisha na nafasi ya uenyekiti!!
 
Leo brother utalala na viatu, hutaki mimi nijadili nje ya Mbowe, lakini yoyote akijadili unahusisha na nafasi ya uenyekiti!!
Point yako ni moja tu unataka Mbowe aachie madaraka kwa vile kakaa muda mrefu, umeeleweka.

Mimi nimekujibu kuwa Mbowe hawezi kutolewa kwa propaganda za CCM atatolewa na wana Chadema wenyewe.
 
Mkuu usiwe loyal kwa chama chochote, kuwa loyal kwa UPINZANI
Tunahitaji Chadema na vyama vingine vya upinzani viunganishe nguvu ili kuing'oa CCM fullstop!.

Kinachotokea leo ACT, ni mkondo wa umeme tu kutoka CUF ya zamani kutafuta waya mwingine wa kupita na hivyo kupitia ACT lakini upinzani ni ule ule.

leo hii hata kama ACT itafanyiwa figisu, mkondo uleule utakwenda kupitia kwa CHAUMA ya Hashim Rungwe!.
Nimekuelewa, nilikuwa nawakumbusha historia ya Chadema watu walioanza kusema kwa ujio wa ACT Chadema inakwenda kufa.
 
Mali ngapi za Mbowe zimevurugwa na hana lolote alilofanya? Ukiniambia viongozi wa cdm hakuna anayetaka kugombea uwenyekiti nitakuelewa lakini sio kwamba Mbowe ndio mwenye uwezo kulingana na wakati wa sasa
Tindo, naona hutaki kuelewa ninachokieleza.
Kwa hali kama hiyo, najikuta sina njia nzuri ya kujieleza kwako ili 'ukubali' kuelewa ninachoandika, hata kama hukiafiki.

Tumekwishakubaliana umhimu wa kuwa na uchaguzi ndani ya CHADEMA, ili hata kama Mbowe akitakiwa aendelee kuongoza pasiwepo na lawama kama hizi unazoleta humu.

Sasa naona hata hiyo subira tu, ya kuruhusu hizi chaguzi zipite salama bado unaona huridhiki! Kuna agenda yoyote inayokupa msukumo huo? Hii haiwezi kutokana tu na kuwa shabiki mkereketwa wa chama!

Napenda pia ujue maslahi yangu ninayoyasimamia katika mijadala kama hii. Kukikosekana upinzani wenye nguvu Tanzania, tutaingia katika hali ngumu zaidi kuliko tuliyo nayo sasa hivi. Maslahi yangu ni kuona kukiwa na vyama imara zaidi ya chama kimoja. CHADEMA wakifanikiwa kushinda na kuunda serikali, bado nitatamani kuiona CCM na/au vyama vingine vikiendelea kutoa michango yao katika siasa za nchi hii. Sitapenda CHADEMA waivuruge/waifute CCM. Nitawapinga kwa nguvu zote.

Sasa nashindwa kuelewa hasa matakwa yako ni yapi.
 
Kama cdm ni taasisi basi utetezi wa kwamba Mbowe ndio anayefaa tu kwenye uenyekiti ni utani wa mchana kweupe.
Maneno haya yametoka wapi? "Mbowe ndio anayefaa tu kwenye uenyekiti".
Unapojadili mada na kuja na njia za namna hii kukazia hoja inakuondolea uhalali wa hoja zako.
 
Siku tutakayokubaliana kwamba Mbowe anapaswa kuwajibika kama kiongozi mkuu wa chama kwa upuuzi alioufanya 2015, chama kitapiga hatua kubwa sana.

Tuendelee tu kumtetea na kumkingia kifua kwa kusababisha chama kimpoteze Katibu mkuu mwenye ushawishi DR Slaa mwenyewe.
Tutofautishe kumtetea Mbowe na kukitetea chama.

Hakuna anayemtetea Mbowe bali maslahi ya chama, hata Mbowe akiondoka bado wapenda demokrasia wataendelea kukitetea chama.
 
True kwa hakika Chadema uchaguzi wa 2015 kilijipaka shombo chenyewe kiasi cha kuanza kupoteza mwelekeo.

Kwa hili top leadership ya chama inapaswa kubeba lawama na kuanza kushughulikia makosa yake la sivyo kutaendelea kuonekana ombwe ambalo ACT wanaanza kulitumia kujijenga

Sent using Jamii Forums mobile app
Nguo ikichafuka dawa yake siyo kuitupa ni kuisafisha hatuwezi kujua hata kuondoka kwa Lowassa inawezekana ni njia mojawapo ya kukisafisha chama.

Wakati wa magamba matatu CCM ilifanya kosa la kutaka kuwafukuza kina Lowassa, Rostam na Change lkn walikuja kugundua baadae wamekosea, leo hayo magamba ndiyo yamekuwa lulu kwa CCM.
 
ACT Wazalendo wanahitaji muda ili kujiimalisha hasa vijijini Chadema haijafika hapa over a single night.
 
Mleta uzi uko sahihi sana kuhusu cdm. Ila cdm 2015 ilituangusha sana kwa tamaa ya viongozi wachache kukubali kuchukua asali ya Lowassa na kumpa nafasi adhimu mzee toka ccm aliyetaka urais tu bila kujali chama. Lile ni kosa la wazi na kubwa sana kufanywa na taasisi. Sikutegemea taasisi kubwa kama cdm ingeweza kufanya maamuzi mazito kwa kuchukua mgombea ambaye hata Mimi nisiyejua siasa nilijua kabisa ni kosa la dhahiri. Kwa kosa lile ni dhahiri Mbowe anapaswa kuachana na uenyekiti na kumuachia mtu mwingine ili tuanze upya.

Halafu cheo muhimu cha katibu mkuu ndani ya cdm kimepwaya mno kiasi kwamba kuendelea kuwa na katibu mkuu kama huyo ni kosa kubwa. Kwa sasa tunapaswa kuwa na katibu mkuu mtu kama Heche au Marcos Albanie. Huyo katibu mkuu wa sasa kachangia kuifubaza sana cdm.
Lowassa hakuletwa Chadema na Mbowe, tunavyojua tangu mwanzo Mbowe alikataa lkn kwa kuheshimu maamuzi ya kamati ilibidi akubali
 
Hapa ndipo hasa ninapomuambia Quinine, sio mara moja au 2 kwenye nyuzi mbali mbali nimekuwa nikisema ni muda sahihi wa Mbowe kuachia kijiti kwa mwingine. Lakini amekuwa akigoma kwenye eneo hili japo tunakubaliana kwenye mengi. Nahisi huyu Quinine ndio Mbowe mwenyewe.
Ulimsikia MBOWE akisema hatoki kwenye ueNYEKITI?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom