Mkuu mimi nina maoni mawili tu hapa:
Mosi, kitu kimoja kikubwa CHADEMA haina, ambacho nadhani ni muhimu kwa siasa za Afrika ni kuwa na wanachama watiifu ambao ni watu kutoka vyombo vya dola kama TISS, JWTZ, POLISI na Mahakama.
Hili ndilo linawabeba CCM na kuwapa kiburi cha kufanya watakavyo hapa nchini bila hata kuzingatia miiko ya kisheria.
CHADEMA kimejitahidi sana kufika vijijini kuliko vyama vingine vya upinzani. Lakini bahati mbaya sana ni kwamba chaguzi za Afrika hazifanikishwi kwa boski la kura peke yake, lazima mkono wa dola utumike tu.
Pili, kitu kingine kikubwa zaidi na muhimu ambacho CUF inacho ambacho vyama vingine vya upinzani havina ni kwamba CUF imewahi kufanikiwa kushika dola kule Zanzibar kwa nguvu zao wenyewe kabla hata ya UKAWA kuzaliwa.
Walifanikiwa kuunda Serikali ya Umoja ya Zanzibar na kutoa Makamu wa Raisi: Hivyo nadhani kwenye suala zima la uzoefu wa kiuongozi CUF watakuwa wako mbele kidogo ya CHADEMA. Pia mtandao wao kule visiwani ni mkubwa sana kuliko chama chochote cha upinzani hapa Tanzania.
Umetoa hoja nzuri na ya msingi sana. Mimi naomba kuchangia kwenye hili moja tu;
Kwamba, CHADEMA na vyama vilivyo nje ya dola kwa ujumla wanapaswa kuwa na watu (wanachama) watiifu ktk taasisi nyeti za umma (serikali) hususani TISS, JWTZ, POLISI na Mahakama...
Yes, nakubaliana na wewe 100% na ndiyo njia ya pekee kuwaondoa CCM madarakani....
SWALI NI; How?
Moja ya zana (tools & weapons) muhimu kuzitumia kufanikisha hili ni;
FEDHA
- Hii ndiyo silaha wanayotumia watawala wengi na vyama vyao ktk nchi za ki-Africa na dunia ya tatu kuhakikisha wanabaki madarakani....
- Wanahakikisha kuwa vyama vya upinzani vinakuwa dhaifu (weak) kiuchumi (kifedha) ili washindwe kujiimarisha na kuwa na ushawishi ktk jamii/watu...
- Na ndiyo maana ya hizi harakati zinazoendelea sasa za kununua wabunge, madiwani na wanachama wengine maarufu wa vyama hivi...
- Tukumbuke vyanzo vikuu vya fedha ndani ya vyama hivi ni RUZUKU toka serikalini na MICHANGO ya wanachama waaminifu....
- Binafsi niwapongeze CHADEMA kwani mpaka sasa kina umri wa takribani miaka 28 na graph yake ya ukuaji, inapanda tu pamoja na kupitia misukosuko mikubwa mara zote ktk chaguzi zote chini ya mfumo wa vyama vingi....
- Hata mwaka huu, wanaodhani vinginevyo, wanajidanganya. Kuna kila dalili na sababu kuwa, CHADEMA na UPINZANI kwa ujumla watazoa viti vingi sana kuanzia Udiwani hadi Ubunge....
- Na kwenye Urais, CCM wakae chonjo kwani pamoja na kuwa mazingira ya uchaguzi kwa akili na macho ya kibinadamu yanawapendelea (favour) wao, lakini lipo kosa watalifanya na ndiyo utakuwa mwisho wao...!!
SASA, KWANINI FEDHA? WATATOA WAPI FEDHA AMBAYO NDIYO POWER KATIKA SIASA?
- Ni rahisi tu kujua kuwa, FEDHA ndiyo inayowafanya TISS, JWTZ, POLISI na MAHAKAMA (majaji & mahakimu) kuwa royal kwa CCM...
- You want them to be raoyal to you, overtake what is being provided to them by your opponent...!!
- Kwa taarifa ya wote wasiojua, ni kuwa, moja ya kada za umma zenye upendeleo maalumu "kimaslahi na marupurupu" ya wazi kisheria na ya kificho ni hizi tajwa...
- Hii siyo kwa bahati mbaya. Ni kwa sababu moja tu, that is, "to maintain their royalty", kwa mtawala aliyepo madarakani - CCM..!!
NOW, WHAT SHOULD THEY DO?
1. Defenetely, hawana fedha. They are weak economically kama taasisi. Wanachoweza kufanya ni aidha kupata economic assistance toka nje wakati huohuo wawe na uwezo wa kuepa sheria za kifedha za nchi kwa sbb kwa utaratibu wa kawaida, hawawezi kukubaliwa kupokea fedha toka nje...!!
2. Kuitumia kikweli kweli slogan ya " PEOPLE'S POWER" ama kwa kiswahili "NGUVU YA UMMA" ili ku - organize "civil disobedience" dhidi ya utawala wa serikali wasiyoitaka. Sababu za kuwaambia watu, wakubaliane nazo na kisha wawaunge mkono lazima ziwe very CLEAR and GENUINE na kamwe zisiwe za kufikirika tu.....!
Lakini, ili hii ifanye kazi kwa ufasaha pasipo kuleta madhara (casualities), tunarudi palepale, kwamba, kuna ulazima ingalau wawe na ushawishi wa kiwango fulani kwenye vyombo hivi kama ikivyotokea Tunisia, Libya na Egypt...!
Huko ktk nchi hizi, ilifika mahali POLISI na jeshi wakawa upande wa umma. Wakakataa kuua watu....!
MUHIMU:
- Lazima tukubaliane kwa dhati kabisa kuwa, mpaka sasa utawala huu chini ya CCM ulishafeli kukidhi marajio ya wananchi kiuchumi na kijamii na kwa mantiki hii umeshajitegenezea mazingira yote ya kuondolewa madarakani...
- TISS, JWTZ, POLISI na MAHAKAMA wote wanalijua hili kwa ukamilifu wake. Lakini, kwa kuwa wanapata kila wanchohitaji kwa ajili ya maisha yao na familia zao, watakuwa watiifu tu kwa sbb hiyo na siyo kitu kingine..!!
- Vyama vilivyo nje ya mfumo wa serikali (upinzani) wakitumia fursa hii kwa usahihi na kwa umakini, wanaweza kuangusha mbuyu kwa kuusukuma kwa mikono tu bila kutumia greda....!!