Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 69,486
- 122,822
Tindo, umelirudia hili mara kwa mara, kiasi kwamba inanibidi niheshimu fikra na pengine hata kuanza kushawishika jambo husika lifikiriwe na kujadiriwa ndani ya chama na Mbowe mwenyewe asilionee kinyongo. Ninapata taabu sana kuitetea hoja yako, lakini haina maana kwamba sioni mantki ndani yake.
Na wazo hili linatokana na uamini kwamba CHADEMA ni chama cha watu wengi wenye msimamo wa pamoja kuhusu chama chao.
Watu hawa ndio wenye uwezo wa kuamua, kama Mbowe aendelee kuongoza chama chao, au awekwe kiongozi mwingine.
Hii haitakuwa na maana kwamba Mbowe ameshindwa kuongoza, (bali litakuwa ni hitaji la kuleta mawazo mapya ndani ya chama)? Hili ni swali.
Je, uwepo wa Mbowe unazuia mawazo mapya? Hao wenye mawazo mapya yenye manufaa makubwa lakini wakashindwa kuyawasilisha ndani ya chama kwa vile sio viongozi wakuu wa chama, ni mawazo ya namna gani hayo; na hawa viongozi wana commitment kiasi gani ndani ya chama chao?
Wanachama wa CHADEMA wanawafahamu vizuri viongozi wao kuliko sisi tulio nje ya chama.
Kwa kuunga mkono msimamo wako; je kukiitishwa uchaguzi wawachague viongozi na wakataka Mbowe aendelee kuwa kiongozi wao bado utaona wamekosea? Kwa bahati nzuri msimamo wako juu ya swali hilo pia unajulikana!
Tatizo juu ya hili kufanyika sasa pia linajulikana. Sio wakati sahihi kufanya hivyo; na watasambaratishwa wasijue ni nini kimewatokea. Wewe hili huliamini kuwa linawezekana kutokea!
Kutaka Mbowe ajitoe katika uongozi, hasa wakati huu, wazo hilo sio la kuitakia mema CHADEMA na nchi kwa ujumla.
CHADEMA kama wanata mabadiliko, wakati sahihi wa kufanya mabadiliko hayo sio sasa, itabidi wasubiri baada ya 2020.
Mkuu nashukuru sana kwa kunitendea haki. Ukijaribu kuangalia michango yangu kwa cdm haina shaka kwamba naikubali cdm na pia naitaka mema cdm kama chama. Hata msimamo wangu kuhusu Lowassa uko wazi na wala sikuyumba mpaka majuzi anaondoka cdm.
Tuje kwenye hili la Mbowe, ukweli ni kuwa Mbowe ni jabali hasa na mhimili halisi wa cdm, lakini hili suala la kwamba sio muda muafaka Mbowe kuachia madaraka silipendi sana kwani hata wakati wa JK ilisemwa hivyo hivyo. Wasiwasi wangu Mbowe anaweza kuendelea kuwa mwenyekiti kwa sababu hizi hizi za kwamba muda sio sahihi. Hivi ni kweli ndani ya cdm taasisi ni Mbowe tu ndio jasiri na wengine wote ni wadhaifu? Angalia post yangu namba 31 hasa post paragraph ya pili utapata ni kipi nasimamia.
Huenda Mbowe anaweza akachaguliwa tena na wanachama hilo sina shida nalo kwani ndio demokrasia, lakini wangalau akijadiliwa kutapatikana mabadiliko ya dhati. Kwa mfano huyo katibu mkuu kuna haja ya kuendelea kuwa na mtu wa hivyo wakati huu? Huoni kama tungekuwa na katibu mkuu imara Mbowe naye angezidi kuwa imara. Tuje kwenye mfano halisi mfano masahibu yaliyompata Lisu yangempata Mbowe na hata kufa Cdm ndio ingekufa? Tujue cdm ndio maisha yetu na ndio silaha yetu, iwapo leo tutashindwa hata kuhoji nafasi ya mwenyekiti wetu tutapata wapi nguvu ya kuhoji nguvu ya rais? Nashukuru sana Kalamu1 umejitosa kwenye hili, tusione aibu kuhoji uwajibikaji wa yoyote.