CHADEMA iseme inataka nini kwa Wabunge 19 Viti Maalum

Nje ya mada, ni kuwa mimi sijui hesabu au, maana Nyalandu anasema alipata kura 30 sawa na 100% ya kura zote. Hizo kura 24 za Tundu Lissu zilitoka wapi?
 
Mwenyekiti ana majina yake, m'beleji ana majina yake, robart amsterdam ana majina yake na pia katibu mkuu ana majina yake. Sasa tatizo ni kwamba hao wote majina yao hayakupita na badala yake yamepita ya Mdee ambae amewazidi mbinu vigogo wa chama chake.

Ndio maana sasa kila siku unasikia kelele za hao wabunge waliochaguliwa na Mdee na hasa lawama nyingi amepewa Mdee kutokana na sababu hizo nilizokuambia hapo juu.
Kama vile kuna ka-ukweli hivi!
 
Nje ya mada, ni kuwa mimi sijui hesabu au, maana Nyalandu anasema alipata kura 30 sawa na 100% ya kura zote. Hizo kura 24 za Tundu Lissu zilitoka wapi?
Tundu Lissu hawezi jibu hili swali kwani akijaribu yatakayo mkuta yanafurahisha
 
Unataka kutuaminisha kuwa hizo nafasi huwa wanazipata kwa kuwekwa nyumba ndogo na vigogo? Kuna madai ya wale wabunge wa kike wa CHADEMA waliounga mkono juhudi kipindi cha mwendazake kuwa viongozi wa CHADEMA huwa watoa hizi nafasi za viti maalumu kwa rushwa za ngono na 10% kwenye malipo yao ya ubunge.
hivi hii kitu ina ukweli ndani yake? Kuwa vigogo wa chama walikuwa wakitoa km hisani hizi nafasi.
 
Miezi zaidi ya mitano sasa inaelekea huku kukiwa na mvutano baina ya CHADEMA na Wanachama wake 19, walio Bungeni kwa sasa.

Chama hicho kila kinapojitokeza hadharani kinaeleza kuwa Wanachama hao wamefukuzwa hivyo hawana sifa ya kuwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano.

Wanasema sababu ya kufukuzwa kwao, ni kwenda tofauti na msimamo wa chama wa kutotambua matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Kwamba maazimio na matamanio ya chama hicho ni kubaki wakati wote bila kutambua matokeo ya jumla yaliyowapatia nafasi yoyote ya kiuongozi, kimapato na uwakilishi baada ya oktoba mwaka jana.

Lakini katikati ya hoja yao hiyo, msimamo wao huo haugusi ruzuku zilizotokana na uchaguzi huo. Msimamo wao huo hauwahusi madiwani na Mbunge mmoja waliopata kutokana na Uchaguzi huo.

Na kila wakiulizwa sababu ya kuruhusu madiwani na Mbunge mmoja kuwa halali, na kuwaharamisha wabunge 19, nafasi zilizotokana na uchaguzi huo, huwezi pata jibu sahihi.

Sana sana watakueleza kuwa wamekiuka maagizo ya chama, na ukiuliza ni maagizo gani watakwambia msimamo wa chama ni kutotambua matokeo yoyote ya uchaguzi wa 2020 na kila kilichookana nacho.

Ukiwauliza madiwani na mbunge mmoja nafasi yao ikoje kwenye msimamo huo, watakuambia wao wamechaguliwa na wananchi kwa kura halali ambazo chama kimesusia kwa msisitizo wa kutopeleka viti maalum, yaani ni vurugu tupu maelezo yao.

Kwa msingi huo sasa hata wafuasi na wanachama wa chama hicho hawajui usaliti wa wabunge 19 ni upi na uhalali wa mbunge mmoja na madiwani walioruhusiwa kuapa ni upi. Katikati ya sintifahamu hiyo, watanzania tukaona wameomba fursa ya kukutana na Rais Samia kwa ajili ya kutafuata muafaka.

Watu makini mfano Absalom Kibanda alipowashauri kama wapo radhi kutafuta muafaka waanze na sakata la wanachama wao 19,matusi yakawa mengi, huku hoja ikiwa utaongeaje na wasaliti waliokubali matokeo ya 2020 kinyume na msimamo wa chama.

Jana Mnyika kahojiwa na chombo cha habari anasema ruzuku ya chama hicho haitokani na nafasi ya ubunge wa viti maalum walivyopata chama chake. Hili ni sawa kabisa nami naunga mkono, sasa swali langu kwao je wameanza kutambua uhalali wa matokeo ya 2020?

Je, wamechukua na wanatumia ruzuku iliyotokana na matokeo wasiyokubaliana nayo?

Au wanataka tuamini/niamini yale yanayosemwa katika korido za ofisi mbali mbali za chama hicho, kwamba shida si uhalali wa matokeo, bali shida ni kwanini majina yaliyotakiwa kwenda kutoka kwa baadhi ya viongozi nje ya vikao vya bawacha hayajawekwa katika umafia mzima wa kupeleka majina bungeni.

Au niamini kuwa msimamo wa walioingia bungeni kukataa kuchangia 100m kwa kila mmoja baada ya kuapishwa ndiyo sababu?

Nitarejea
Chadema ni wakora wabobezi ,wakuogopwa kama ugonjwa wa ukoma,kifupi ni janga la taifa
 
Sio CHADEMA waseme, sisi wananchi hatutaki hela zetu zitumike kinyume na katiba ya nchi yetu.

Kama CHADEMA wanafigisu zao na COVID-19 waende wakazimalize kisha warudi kutupa mrejesho ila sio kwa uamuzi wa spika kutumia kodi zetu kinyume na katiba.
 
BAWACHA wamemzidi maarifa baba mwenye nyumba na waandamizi wake
Mwenye kigoda aka "mwenye nyumba" kapandikiza wanywa gongo humu ili wamchafue Halima Mdee lkn kwa bahati nzur au mbaya mwenye kigoda na wanywa gongo wake wanaonekana kushindwa mbinu za kivita na shujaa Mdee
 
Mbona naona kama hujui chochote kile?
huyu mtoa mada hajielewi alafu anauliza majibu anajijibu kisha aelewi anachojibu, hivi wewe unaona wametokana na chama gani na wamepitishwa na nani mpaka kuwa wabunge wa kuteuliwa?mbona macho na masikio unayo?kwanini unasumbua watu watafakari andishi lako?sisi kama chadema hatuwatambui elewa hivyo
 
Mwenye kigoda aka "mwenye nyumba" kapandikiza wanywa gongo humu ili wamchafue Halima Mdee lkn kwa bahati nzur au mbaya mwenye kigoda na wanywa gongo wake wanaonekana kushindwa mbinu za kivita na shujaa Mdee
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 umenifanya nicheke sana mkuu..... Umenikumbusha story za kutekwa yowe nchi nzima kujathibitika kumbe faru John kafanya yake.

Kwa hali hii hawa jamaa wakiingia Bongo movie wataikuza sana hii industry hata kuwapiku hollywood!
 
Sio CHADEMA waseme, sisi wananchi hatutaki hela zetu zitumike kinyume na katiba ya nchi yetu.

Kama CHADEMA wanafigisu zao na COVID-19 waende wakazimalize kisha warudi kutupa mrejesho ila sio kwa uamuzi wa spika kutumia kodi zetu kinyume na katiba.
Hivi kweli mkuu unaionea uchungu kodi yako au unaona uchungu sababu hawa BAWACHA wanavuta mpunga wakati mwenyekiti ana sintofahamu akilini mwake!
 
Back
Top Bottom