CHADEMA ipo kwenye wakati mgumu

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Kama kuna wakati CHADEMA inapitia wakati mgumu basi ni hiki kipindi ambapo ipo njia panda labda iwafukuze wabunge 19 wanawake ambao wao wanaona ni waasi au iwasamahe na kisha kuruhusu waendelee kutinga mjengoni.

Mpaka sasa mimi binafsi sijaona hatima ya hawa kinamama ambao walifanya janja na kisha kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu.

Kamati kuu ya CHADEMA mpaka sasa haijatupa feedback, imeamua nini

CHADEMA wana wakati mgumu kuchagua option mbili kufukuza hawa akina mama 19 ili wajenge status kwa wanachama na wafuasi wao kuwa sio chama cha lelemama ambacho hulea wasaliti au wawaruhus hawa waasi 19 ili waendelee kuwa wa viti maalumu ili angalau wawe wanapata ruzuku.

Maaana kwa Spika kuapisha majina mengine ambayo yatakuwa tofauti na hawa waasi19 ni ngumu. Hivyo ni dhahiri kuwa Cdm walegeee ili wawasamehe hawa akina mama ili waingie bungeni na Chama chao kipate angalau ruzuku ya kulipia pango pale Kinondoni mabondeni kwenye mashamba ya mpunga.

Lakini hii mpaka Chama hiki kinafilisika kifedha na kisiasa ni sababu ya kuwa na siasa chafu za kupinga umoja na maendeleo ndio maana wananchi walikiadhibu.

Maoni yangu ni kuwa huu ni wakati wa kujifunza, hivyo wakomae kisiasa na kama wakirudi na kusimama kama ilivyokuwa kipindi Dk Slaa ni Katibu mkuu, basi wasirudie makosa tena.
 
Lengo la Post yako ni kuhusu hao akinamama au siasa zao chafu kama unavyodai.

Samahani mleta Uzi, umesha kula ukashiba?
 
Mambo ya Chadema yaache kama yalivyo, kulingana na uelewa wako.

Cha msingi katafute mkate wa familia yako.
Chadema ni taasisi ya kijamii kila mtu ana haki ya kuitolea maoni. Hiyo hoja yako muflisi ipeleke chumbani kwako, maana ya chumbani ubaki huko huko.
 
Back
Top Bottom