CHADEMA ipo hatarini

CHADEMA ipo hatarini

Aiseeee! Kumbe mkuu Logo nawe ni agent wa TISS, haaaaaaa! Hapo ndo ujue kuwa intelejensia ya CHADEMA ni zaidi ya uijuavyo.

Ahsante Rais wangu Dr.W.Slaa kwa ukakamavu wako na msimamo wako, Usiwe na shaka kwan hata kama TISS watawanunua vijana wangapi wa CHADEMA lakin Struggles zipo pale pale hadi 2015 tutakapoiondoa CCM madarakani.
 
Last edited by a moderator:
Logo

Nitatumia fursa hii kujibu sehemu ya pili ambayo bila shaka unataka kuendeleza malumbano na Katibu Mkuu bila sababu yoyote. Sitakujibu ile sehemu ya kwanza kwa sababu tayari umeshajibiwa.Mtu akikusoma vyema, hasa baada ya comment yako ya pili, anakuona kama mtu mpenda mabadiliko. Kwenye comment yako ya awali mtu angeweza kukuona kama mpenda mabadiliko na mwana CHADEMA!

Lakini baada ya kurudi kwa nia ya kulumbana na Katibu Mkuu (wako?) ni dhahiri hauko kwenye kundi la wanachama.Tuje kwenye hoja yako ya pili, baada ya ile ya kwanza kujibiwa. Hivyo nitakujibu kama mtu unayetaka kuonesha kuwa unapenda mabadiliko. Ingawa hujalionesha hilo wazi, hivyo hata hiyo 'penda' yako inaweza kuwa tooo questionable.Kweli ni bahati mbaya sana kuwa mtu kama wewe unayeonekana unapenda mabadiliko ya dhati unashindwa kutambua wajibu ambao viongozi wa CHADEMA, kwa kushirikiana na wanachama na wafuasi wa chama wamekuwa wakitimiza kwa ajili ya kuwapigania Watanzania!

So unataka kuonesha kuwa hujui kesi ambazo zinawakabili viongozi kadhaa waandamizi wa juu kule Arusha (kabla hazijazuiwa baada ya kufunguliwa kesi nyingine ya kikatiba) zilikuwa zinahusu kuipigia makofi CCM kwenye mikutano ya hadhara!?!? Hujui kabisa kuwa mbili zinatokana na wao kushiriki wakiwa mstari wa mbele kwenye maandamano ya Januari 5, kupigania haki ya watu wa Arusha kumpata Meya aliyechaguliwa kihalali, bila kujali anapatikana kutoka chama gani!

Aidha, unataka kuinesha hujui kuwa nyingine inatokana na mkesha wa Novemba 7 wakati wa sakata la Lema kuwa mahabusu! Tena ilikuwa baada ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Lissu na viongozi wengine, kuwaongoza maelfu ya wanachama na wafuasi kushiriki mkutano huku mvua kubwa ikinyesha.

Ni mkesha huu ambapo CCM waliona wazi Tahrir Square inanukia...Unataka kuonesha kuwa hujui kuwa viongozi waandamizi wa CHADEMA wameshtakiwa pamoja na wanachama na wafuasi wa chama hicho Mahakama ya Wilaya Mufindi baada ya tukio la Nyololo, eti wakishtakiwa kwa mkusanyiko usio halali, wakati walikuwa wanafanya vikao vya ndani, baada ya kufungua matawi, kabla polisi hawajamuua Daudi Mwangosi! Mmojawao ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Mussa Yusuf.

Je unataka kuonesha kuwa hujui viongozi wa CHADEMA (wa juu, wa kati, wa chini) wamekuwa wakipambana bega kwa bega na wananchi, wanachama na wafuasi wa chama hicho kupigania haki na matumaini ya wananchi wanyonge kila mahali, hivyo kujikuta wakikamatwa pamoja na kufunguliwa mashtaka yasiyokuwa na kichwa wala miguu, kwa nia tu ya kusumbua na ku-distabilize vuguvugu, iko migano mingi tu, huko Tarime, hapa Dar es Salaam, Masasi, n.k, n.k, n.k, n.k, n.k, maeneo ni mengi kwa maana ya kwamba ni nchi nzima. Nilichofanya ni kukupatia samples tu...

Hakuna wakati CHADEMA imewahi kupoa. It has been always active, kila wakati kwa namna tofauti, kwa agenda tofauti au zile zile, alimuradi kwa ajili ya kuwatumikia au kutoa utumishi bora kwa watu. Hivyo hoja yako kuwa kuna CHADEMA ya zamani na mpya, haina mashiko hata kidogo, unless imejengwa katika msingi mbovu wa hoja, bila ushahidi yakinifu. Ukisema hivyo utaulizwa, zamani inaanzia lini hadi lini na 'sasa' (mpya yako) inaanzia lini hadi lini.

Ungemsoma Katibu Mkuu Dr. Slaa vyema kwa utulivu ungeweza kuona ujumbe mzito aliokupatia kuwa si lazima kutumia mbinu ile ile kila wakati kumkabili adui yule yule. This is war. You need Tsa Nzu kaka. Mkuu Logo, hao wachache ambao wewe unawabeza na hao unaowaita wavuta bangi na wasiokuwa na kazi (shukuru wewe unayo na bangi huvuti) ndiyo jeshi la ukweli. Ndiyo wapiganaji wa ukweli. Wanajua wanachokipigania. Wanajua wajibu wao. Wanajua nidhamu ya jeshi ni kumlinda kamanda, si kuombea ukamatwe pamoja na kamanda.

Sasa kamanda naye akikamatwa nani apiganishe vita au unataka morale ishuke na adui ashinde!?!? Kaka hizi ni principles za kawaida kabisa katika medani za vita.Hao unaowabeza na kuwaita wachache, ndiyo kila siku wakija kwenye mikutano, wakija kwenye maandamano, wakiandika hapa, wakitoa maoni yao kwenye sanduku la kura, wakihoji mambo kila mahali, serikali ya CCM na chama hicho wanazidi kupata hofu! Wanatetemeka.

Hakuna wakati katika maisha ya siasa za upinzani na kudai mabadiliko na uhuru wa kweli, CCM imewahi kupata hofu kama inayoonesha sasa. Imefikia mahali wanaogopa hata kuitisha uchaguzi wa vijiji na vitongoji! Kwa sababu wanajua CHADEMA imetapakaa kila mahali, wananchi wameijua na wameikubali, wamekataa propaganda zote, zote kabisa za watawala, ikiwemo hii ya sasa ya ugaidi.Hao ambao wewe unawabeza, ndiyo waliokwenda kupiga kura za mabadiliko kwenye uchaguzi mkuu uliopita. Ndiyo waliolinda kulinda bila kujali mabomu, silaha na kila hila za watawala wakilitumia Jeshi la Polisi. Ni bora jeshi la watu wachache wanaotanguliza moyo mbele kabla ya silaha.Wanotanguliza dhamira ya dhati kabla ya maslahi.

Ni wale wanaoona wanachopigania si kwa ajili ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu, au kiongozi yeyote. Wanaona bigger picture, wanaiona Tanzania na Watanzania wanahitaji ukombozi, wanahitaji uhuru, wanahitaji haki, wanahitaji matumaini. Wanahitaji mabadiliko ya kimfumo na kiutawala.

Wakati wewe unadiriki hata kusahau kuwa viongozi wa CHADEMA wa ngazi zote wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki, sambamba na wanachama na wafuasi wa chama, wenzako hao wanataka mabadiliko ili wasivute hizo bangi na wapate hizo kazi ambazo sasa hawana kutokana na sera mbovu za CCM zilizoshindwa na ufisadi uliokithiri hadi kuachia mianya ya viongozi kushirikiana na wauza mihandarati ambayo ndiyo vijana unadai wanavuta!

Yote uliyoyasema huwezi kuyatenganisha na ubovu na kushindwa kwa utawala unaoporomoka wa CCM.Watu hawako mahabusu, magerezani au mahakamani kwa sababu ya maandamano. Tangu lini maandamano yakakamata watu! Watu wako huko kwa sababu serikali hii ya CCM imeamua iwe hivyo.

Kwa sababu sasa ukionekana kuhoji, kuuliza maswali magumu, kudai haki, kutetea matumaini ya wanyonge, kupinga unyanyasaji na dhuluma za watawala dhidi ya wananchi, kwanza unakuwa lebeled, kisha unabambikiwa kesi. U give a dog bad name before u kill it. Lakini Watanzania wanaangalia na wanajua kuwa CCM haiwezi kufanya tena siasa. Haiwezi kujibu hoja kwa hoja, bali matusi na kutengeneza propaganda.

Zikiwemo za kupalilia udini, ukanda na ukabila bila kujali kama taifa laweza kuparanganyika. Kwa sababu kile si chama cha siasa tena. Kilichobaki pekee ni vitisho, manyanyaso na hata kuua, ili kuwatisha wapigania mabadiliko. Hivyo watu wanahoji kwenye maandamano, mikutano au kwenye vyombo vya habari, wanafuatiliwa, wanakamatwa, wanafungwa na kunyanyaswa. Badala ya kuwatisha, hiyo imekuwa ikiongeza mori na hasira na ukubwa wa jeshi la wapambanaji.

Maandamano ya CHADEMA ni moja ya forums ambayo Watanzania wameiamini na kutumaini kuwa ndiyo mahali pa kutoa hisia zao za kutofurahishwa na status quo. Sehemu ya kuendeshea haraki za kuuondoa mfumo huu unaoatamiwa na CCM, ukilea ufisadi na ubadhirifu, matokeo yake kukwamisha maendeleo.

Na kwa sababu hiyo forum haijawahi kuwaangusha wala kuwatupa, imekuwa nao kwenye kila hali, wataendelea kuiamini na kuitumikia ili nayo iwatumikie vyema, hadi kieleweke. Na kitaeleweka.Hivyo kamanda Logo, usikate tamaa. Usipungukiwe kama wewe ni miongoni mwa wapiganaji kweli. Pigania Tanzania na Watanzania. Hila za kuulinda mfumo huu mbovu, kukilinda chama kilichokwisha kuacha misingi yake na kinaporomoka kwa kasi ndiyo maana tuna serikali legelege, ziko nyingi sana.

Hivyo CHADEMA lazima wawe na mikakati anuai pia ya kupambana (pro-active na reactive) huo ndiyo ujumbe mkubwa na mzito aliokupatia Katibu Mkuu, Dr. Slaa. bahati mbaya hukuelewa. Kuiondoa CCM madarakani si harusi mkuu. Tushikamane na twende pamoja.

Makene

0752 691569 / 0688 595831
 
Kila siku mnaambiwa muwe makini na makanjanja wa siasa mnakuwa wabishi.
We unashangaa nini? huo ndio uwezo wa Slaa over.
Hata ukiangalia majibu yake ya pili kuna makosa mengi ya kiuandishi na hoja za ajabu na woga, sijui alikuwa anaandika anatetemeka? Sielewi.
Huwezi kumlinganisha huyu mbumbumbu wa kuzugwa na wavaa suti nyeusi(wanaojifanya TISS) na mtu kama Prof.Lipumba

chuki ndo kusema na we uwezo wako ndio umeishia hapo au sio? Acha kuongea pumba kwan huna adabu kabisa kutoa maneno ya kijinga kama haya kwa Rais wako.
 
Last edited by a moderator:
Wanataka kutuaminisha kwamba kuna Tatizo kumbe mulishawaamusha wananchi muda mwingi wamejitambua wanaedneleza libeneke

Mkuu wangu Lwesye upo sahihi kabisa, Wanachojaribu CCM kufanya ni kutia watu hofu kuwa CHADEMA ipo hatarini kufa ili wananchi wakate tamaa kukiunga mkono na wanaamua kutumia social medias like JF sababu wanajua ndiyo njiaa pekee ya kupeleka habar kwa urahisi.
 
Last edited by a moderator:
Dawa ni kubadili mfumo wa siasa zenu sio kulalamika.Haraka ya kwenda ikulu na kutofuata utawala wa sheria itawagharimu.

mkakati wa chadema ulishaanza kitambo ikiwa ni pamoja na kumuua chacha wangwe,kumtesa kibanda,na sasa mpango mzima ulikuwa kwa msacki bahati mbaya umevuja.
 
mkakati wa chadema
ulishaanza kitambo ikiwa ni pamoja na kumuua chacha wangwe,kumtesa
kibanda,na sasa mpango mzima ulikuwa kwa msacki bahati mbaya
umevuja.
hivi inakaaje? mi nadhani humtendei haki Amani Simba, la kama unalipenda sana jina lake basi jiepushe na kuweka hoja mfu ambazo zinaweza kumfanya mwenzako asomeke vijana kwenye jamii
 
Du watu wabaya, huitaji akili nyingi kujua kuwa huyo aliyejibu hapo sio Dr, kwanza siajawahi kuona anajibu post humu hata siku 1
 
chuki ndo kusema na we uwezo wako ndio umeishia hapo au sio? Acha kuongea pumba kwan huna adabu kabisa kutoa maneno ya kijinga kama haya kwa Rais wako.

Rais gani hata hotuba yake mwenyewe imejaa matusi na makosa ya kiuandishi, Rais gani anakurupuka kwa kila jambo.
CDM iko halijojo..
 
Aisee huu ni utata mkubwa kweli kama ndo dr slaa aliejibu basi ni aibu kubwa sana kwake na kwa wanachama wake.
Rais gani asieweza kupangilia hoja,maakosa mengi ya kiuwandishi n.k nadhani ni wakati kwa wale wachache mliobakia kusherehekea cdm muondoke na kuungana na wazalendo walioko ccm.
 
CDM for 2015 ijapo haya yamekuja ila utamu ni kwamba CCM wamemaliza siraha zote wamebaki kamata,kutisha,tesa na kuua
 
Aisee huu ni utata mkubwa kweli kama ndo dr slaa aliejibu basi ni aibu kubwa sana kwake na kwa wanachama wake.
Rais gani asieweza kupangilia hoja,maakosa mengi ya kiuwandishi n.k nadhani ni wakati kwa wale wachache mliobakia kusherehekea cdm muondoke na kuungana na wazalendo walioko ccm.

Amefafanua vizuri post yake ya pili.
 
Hii mada imekuwa ngumu kweli kweli!!

Unajua kwanini? Inahamsisha utendaji zaidi. Daima sisi kama wanachama tunapenda kuona chama chetu kinakuja na mziki mnene zaidi wa chama tunachokipinga ili tuweze kucheza vizuri.
 
Ni kweli kabisa,
Mandamano yasiyo na mpango ni kero kwa wananchi
Pia mikutano ya hadhara kila siku tena saa za kazi ni kupoteza muda muhimu ambao ungetumika kujenga nchi

ni kweli kabisa hata utapeli nao hauna mpango kabisa aisee na wizi wa kijanja-janja
 
hivi kweli dr.slaa ndio anaepost kwenye hii stredi? Siamini macho yangu,,,kazi ipo

Ndo yeye mwenyewe, mimi nimeongea na Makene nikajiridhisha.
 
Mh Katibu mkuu, kwa hiyo unaridhika na kasi ya ukuaji wa chama? I thought you would aim to grow at a much higher pace than that!

Sikupenda sana ulivyo down play mawazo ya Logo kwamba anafikiri ki 47!.

Hii inawatisha vijana wako kutoa ushauri kwa kuhisi kudhalilishwa kama msemo ulioutumia hapa.

Aliyejibiwa kaelewa na wengine wengi wameelewa, hapo unaona vijana wametishwa nini? Chadema hatuumi maneno ili kuvutia watu, tunachana live tu, uchukie, usichukie shauri yako..tunakwenda mbele mpaka kitaeleweka tu
 
Aliyejibiwa kaelewa na wengine wengi wameelewa, hapo unaona vijana wametishwa nini? Chadema hatuumi maneno ili kuvutia watu, tunachana live tu, uchukie, usichukie shauri yako..tunakwenda mbele mpaka kitaeleweka tu

CHADEMA tunatisha
 
WanaJf greatbthinkers, I think it is time, to take the challenge of being great thinkers and we should not be taken for a ride!

Hapa ndipo ninapoona tofauti ya mahamba na CDM? I shall never be taken for a ride by some mamluki's.
 
Akijibu moja kati ya post humu JF jana DR W. Slaa alisema yafuatayo, namnukuu:

4) 'Logo anakejeli kauli kuwa " tuna Mungu".... Hata siku mmoja siwezi kuwa na huruma na mtu anayemkufuru Mwenyezi Mungu.'

Nijuavyo ni kwamba rais wa nchi hatakiwi kuegemea imani yoyote ya dini kwa vile kuna raia wanaoamini kuna mungu na wengine hawaamini.

Kwa wale wana dini, kukufuru mungu maana yake ni kufanya kinyume na mungu alivyoagiza au kupinga kuwepo kwake.

Swali, serikali chini ya CHADEMA itasimamia mungu yupi? Maana hata mungu ambaye wenye dini wanamuamini wako tofauti. Kuna wanaoabudu Yesu kama mungu wengine Allah, wengine majah n.k.

Hii pia si huenda ikawa kinyume na uhuru wa kuabudu?

Jee hapa sio kupalilia ile dhana ambayo imekuwa ikienezwa na wapinzani wa CHADEMA kuhusu dini? Au DR amekosea?

Ufafanuzi please, CHADEMA mkisema mna mungu nadhani mnamaanisha kitu fulani ambacho wengine hatukijui. Fafanua please.

NB: Moderators naamini mnafanya kazi zenu kwa uadilifu. Tutendeeni haki na sisi wengine ambao tuna challenge hawa wanasiasa.
 
Back
Top Bottom