kwa mawazo hayo kweli kabisa itakuchua mda sana kukua kiakili ndugu ya embu jaribu kufikiri zaidi ya hapo kwa kweli.Akijibu moja kati ya post humu JF jana DR W. Slaa alisema yafuatayo, namnukuu:4) 'Logo anakejeli kauli kuwa " tuna Mungu".... Hata siku mmoja siwezi kuwa na huruma na mtu anayemkufuru Mwenyezi Mungu.'Nijuavyo ni kwamba rais wa nchi hatakiwi kuegemea imani yoyote ya dini kwa vile kuna raia wanaoamini kuna mungu na wengine hawaamini.Kwa wale wana dini, kukufuru mungu maana yake ni kufanya kinyume na mungu alivyoagiza au kupinga kuwepo kwake.Swali, serikali chini ya CHADEMA itasimamia mungu yupi? Maana hata mungu ambaye wenye dini wanamuamini wako tofauti. Kuna wanaoabudu Yesu kama mungu wengine Allah, wengine majah n.k.Hii pia si huenda ikawa kinyume na uhuru wa kuabudu?Jee hapa sio kupalilia ile dhana ambayo imekuwa ikienezwa na wapinzani wa CHADEMA kuhusu dini? Au DR amekosea?Ufafanuzi please, CHADEMA mkisema mna mungu nadhani mnamaanisha kitu fulani ambacho wengine hatukijui. Fafanua please.NB: Moderators naamini mnafanya kazi zenu kwa uadilifu. Tutendeeni haki na sisi wengine ambao tuna challenge hawa wanasiasa.
Dah....
Wewe mtu si vizuri kujifanya Dr Slaa...
Najua Dr Slaa hajakomaa Kisiasa..lakini si kiasi hichi ulichoandika wewe..
Too low....
Kwanza Kiswahili kibovu...
Pili mipasho kama ya kizaramu...
Tatu umeandika kama umelewa...
Usiingize psychological warfare kwenye mada.
Lipi hapo linalokufanya ushindwe kuelewa kile kilichoandikwa na ujumbe wa mwandishi.
Kuna zaidi anayeshinda hapa JF zaidi yako?. Nyani haoni la kwake.
Haina tatizo, kuna hoja zingine zinahitaji fikra pana na kama maji ni marefu una uhuru wa kubonyeza SKIP kwenye keyboard/keypad yako
Mbali na maelezo toka kwa Dr Salaa na Kamanda Makene, ndugu yangu Logo ninakuomba uzingatie nukuu ifuatayo " MWANADAMU ANAPO ACHA KUTAFAKARI MAMBO MUHIMU ANAKUWA ANAJIWEKA KWENYE KUNDI LA WANYAMA WENGINE. ANAWEZA KUISHI NA KUTENDA KAMA WANYAMA WENGINE .MUNGU ALITUPATIA AKILI NA UTASHI ILI TUISHI NA KUTENDA KWA KUTAFAKARI . NDIYO MAANA TUNAFIKIA HATUA YA KUWA NA MAADILI ,MIIKO ,UTAMADUNI ,MIONGOZO ,MIFUMO NA FALSAFA YA KUTUONGOZA KATIKA MAISHA ." By Padre Privatus Karugendo ,January 2, 2013 kwenye makala yake Gazeti Raia Mwema
Ni kweli unachosema, kila mtu kajaaliwa kipawa chake, wewe unauwezo tu wa kupigania familia yako, mwache Slaa mwenye kipawa cha kuwapigania watanzania wote awapiganie.Du ! Kama kweli hilo ni jibu la Dr Slaa , kamwe sitamwamini mwanasiasa yoyote :scared:
Ngoja nipiganie tu familia yangu
Dr Slaa kamaliza, i too much dought Logo, upeo wangu unanituma kuamini sio mtu mzuri hata kidogo, he can be a TISS agent, for sure, ameingiza propaganda kwa umakini sana.
Amechomekea kuwa CHADEMA kinapendwa na wavuta bangi na wasio na kazi.
Amechomeka propaganda ya udini, yeye kajiita ni mchungaji na kampa uchungaji na Tumaini Makene.
Logo wherever you are, umeshtukiwa, be cursed.
Haya mabandiko mawili ya DR Slaa yananipa wasi wasi sana juu ya huu uwezo uliotumika kufikiri na kujiu posts za Logo.
Kiongozi hapaswi kuhamaki kwa vile tunaamini kwamba hekima na busara ni miongoni mwa vigezo vikuu vya kuwa kiongozi.
Upeo wako wa kujenga hoja sio mdogo, hadi Dr amestuka, kama una nia njema na CDM, carry on, kama uko against also carry on.Hayo ni mawazo yako, sijasema CHADEMA kinapendwa na wavuta bangi au na watu wasio na kazi, nimesema maandamano yaliyokuwa yafanyike yangekuwa na watu wengi kama hao. Kiswahili kigumu? Hivi siku hizi hata kusema mchungaji ni udini? Mmepoteza hata maana ya udini. Hata kama wewe ni mwanaCHADEMA tuweni na pointi tunapochangia siyo kubishana tu kipuuzi.