CHADEMA ipo hatarini

CHADEMA ipo hatarini

Mpaka sasa sijajua kinachojadiliwa ila nadhani nakiona kinachobishaniwa! Pole pole ndiyo mwendo TUTAFIKA TU!!

Hakuna mabishano, ila kulikuwa na sindano moja tu ndani ambayo wengi waliimeza wakidhani ni nofu ilipofika kwenye koo ikagoma kwenda, sasa wakawa wanatema mate au na kufanya wawezalo ili waiteme, si mabishano ila kutiana munkari.
 
Hakuna mabishano, ila kulikuwa na sindano moja tu ndani ambayo wengi waliimeza wakidhani ni nofu ilipofika kwenye koo ikagoma kwenda, sasa wakawa wanatema mate au na kufanya wawezalo ili waiteme, si mabishano ila kutiana munkari.
Utu uzima dawa na kabla hawajaliita jando ni tamaduni duni wengine tulikuwepo huko!! NAANGALIA!!

 
Heshima kwako Dr.W. SLAA,nimesikitika sana kwa majibu ya kitoto na kipuuzi haya uliyoyajibu,kama kweli wewe ndo umejibu basi I THINK IS HIGH TIME kwa wewe kuwaachia hiki kijiti cha ukatibu mkuu waendeshe wengine mheshimiwa wangu,umepoteza uwezo wako wa kufanya utafiti kabla ya kujibu,umejibu kwa dharau ya hali ya juu tena kwa ubabe.

Sikutegemea kama unaweza mwambia mwanachama unayemuongoza kuwa anafikiria ki 47" hata sijui unamaanisha nini,je hujui kilichotokea karibuni kwenye mkutano alioufanya Tundu Lissu hapa DSM? walikuja watu wangapi? hukumbuki kauli alizozitoa kwa viongozi wa Chadema DSM? yote hayo ni dalili kuwa wanach wanapoteza imani na Chadema,iwe kwa matukio ya kweli au kwa kutengenezewa na Wapinzani wa CDM lakini matukio hayo yanashiria negative impresion for CDM,unazungumzia kushinda kwa uchaguzi wa vitongoji? Hoja ya kitoto sana hii mzee wangu,maana hakuna asiyejua overall ya uchaguzi huo ni CCM inaongoza kwa mbali na kama ndio ungekuwa ni uchaguzi mkuu basi CCM WANGEKUWA WANARUDI TENA MADARAKANI,

Pia naanza kupata hisia za kuwa si mtu wa kushikilia msimamo wa CHAMA CHAKO, NAONA UNAMJIBU KUWA ANA MAWAZO YA KIZAMANI TU KWA SABABU ANASHAURI MTUMIA MAANDAMANO NA MIKUTANO YA WAZI..JE NI NANI ASIYEJUA KUWA CDM TUNAAMINI KATIKA MAANDAMANO? MARA NGAPI MMEKUWA MNATUSISITIZA TUHUDHURIE MAANDAMANO?(NGUVU YA UMMA)..

HILI LA KUTUAMBIA KUNA VITONGOJI CDM IMESHINDA HATA MAKAO MAKUU HAMJAFIKA -mzee umenishangaza sana kwa kweli siamini kama ni wewe umejibu kitoto hivyo,nataka nikuhakikishie kuwa WANANCH HAWACHAGUI VIONGOZI KWA SABABU NYIE MNAOJIITA WA MAKAO MAKUU MMEFIKA ILA NI KWA SABABU WANAIMANI NA WAGOMBEA WANAOKUWA WAMEGOMBEA MAENEO HAYO PAMOJA NA IMANI YAO KWA CHAMA(CHAMA SIO MAKAO MAKUU TU). NINA SEHEMU NYINGI SANA AMBAZO NYINYI MNAOJIITA MAKAO MAKUU MMEFIKA NA BADO CHAMA KIKAMWAGWA VIBAYA SANA,..USIWE NA JAZIBA KWENYE UKWELI,SAIZI HATA UKIPITA VIJIWENI WALE WATETEZI WA CDM WAMEPUNGUA AU WAMEKUWA NEUTRAL...
Mpululu, wewe ni kama yule aliyeanzisha uzi, huna tafiti lakini unataka kulazimisha kile unachokifahamu wewe ndio uwe utafiti, Dar Es Salaam watu wamejawa na woga kutokana na maisha na shughuli zao kila siku, lakini wanakipenda chama na wanakichangia chama mfano jimbo la Kinondoni na Segerea huko ambapo Tundu Lissu alikwenda Chadema ni kama haipo lakini ukifika wakati wa Uchaguzi chadema inajidhihirisha kutokana na matokeo ya kura

Jambo la msingi na ambalo linaigharimu chadema ni ulinzi wa kura, na najua viongozi wa chama wanalijua hili na wameshalifikiria na tayari lipo kwenye utekelezaji na ndio maana kuna mafunzo yanataraji kutolewa kwa vijana na wamama (BAVICHA & BAWACHA) naimani itakuwa agenda

Sitaki kukubali ushauri kwa chadema itafute mbinu za shortcut ili ishinde, kila jambo jema linafuata taratibu na ndio maana hata ngano haipandwi leo ikavunwa kesho itaanza jani, mche, suke, suke-pevu kisha mavuno sasa huyu anayelazimisha CHADEMA iache process hiki sio chama cha uhaini

Kuhusu matokeo ya chaguzi, imeonekana wazi na kama nilivyotangulia kusema hapo juu, chadema inachokikosa ni ulinzi wa kura, Chadema itakapotoa mafunzo na kukabiliana na kila uzandiki wa CCM, watu wa Daresalaam wakaacha woga, na wakajitokeza kulinda kura Chadema tunashinda 90%

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema

Joash R. Mussa
 
Hayo ni mawazo yako, sijasema CHADEMA kinapendwa na wavuta bangi au na watu wasio na kazi, nimesema maandamano yaliyokuwa yafanyike yangekuwa na watu wengi kama hao. Kiswahili kigumu? Hivi siku hizi hata kusema mchungaji ni udini? Mmepoteza hata maana ya udini. Hata kama wewe ni mwanaCHADEMA tuweni na pointi tunapochangia siyo kubishana tu kipuuzi.

Mkuu ni vyema ukatuomba wana JF msamaha yakaisha; Thanx Lord, Dr. Slaa amekushtukia kwani mpango wako ulikuwa ni kututoa kwenye mstari;

UHASAMA wa taifa (TISS) ni vyema mkazingatia maadili ya kazi yenu kuliko kutumiwa na chama TWAWALA.
Hivi nyie hamfikirii baada ya uchaguzi mkuu unao tarajiwa kufanyika nchini kote mwaka 2015 mtaficha wapi nyuso zenu?
 
Back
Top Bottom