CHADEMA inaweza kupoteza wabunge wengi 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA inaweza kupoteza wabunge wengi 2015

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by WATANABE, Jun 10, 2011.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Baada ya chadema kuwa chama kikuu cha upinzani, nilitegemea kuwa ingeanzsiha mara moja utoaji mkubwa wa elimu ya uraia kwa wananchi ikiwa na lengo la kuwafanya wananchi kutambua na kuelewa kwa kina wajibu wa mbunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 63.-(2) Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

  Kutokana na hilo chadema inawaacha wabunge wake wakishiriki kalamu mbili ambazo zilimshinda fisi; Wakati wabunge wake wakitamani sana kuonekana wakiisimamia Seikali ipasavyo, jambo ambalo linahitaji mbunge atumie muda wake mwingi akifanya utafiti na ufuatiliaji wa utendaji wa serikali katika kukusanya na kutumia fedha na raslimali mbali mbali; wakati huo huo wanatumbukia katika mtego wa CCM wa mbunge ambaye ni tarishi wa kupikea maendeleo kutoka serikalini kuu, mawaziri n.k na kuyafikisha jimboni kwa lengo la kuwafurahisha wananchi ili wamchague tena.

  Kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa wabunge wa CDM hawataweza kufanikisha kalamu yoyote vizuri na kutimiza matarajio ya wananchi, japokuwa wengi wao wanaonyesha uwezo mkubwa sana wa kuisimamia Serikali,jambo ambalo si wananchi wengi wakiappreciate kama utarishi wa kupokea maendeleo kutoka serikali kuu na kuyafikisha jimboni. Baada ya kudanganya wananchi kuwa imewatema mafisadi CCM, licha ya wabunge wa CCM kushindwa kutimiza wajibu wa mbunge ipasavyo na badala yake kutimiza utarishga wa maendeleo ya jimbo moja moja; wananchi wataona kuwa wabunge wa CDM walishindwa kuleta maendeleo waliyoahidi na hivyo kuwatosa.

  CHADEMA inapaswa kuiga mfano wa Mhe Benjamin William Mkapa ambaye baada ya kuingia madarakanai kwa kuuza ilani ya CCM ya mwaka 1995, mapema kabisa alitangaza hadharani kuwa ilani hiyo haitekelezeki na akapanga mipango yake mipya kama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo chini yake Serikali ya Tanzania ikaanza kulipa madeni ya nje jambo ambalohalikuwemo katika ilani hiyo. Serikali yake iliheshimika kwa wafadhili na kufanikiwa kukopeshwa na kupatiwa misaada iliyowezesha kukuza uchumi na kudhibiti mfumuko wa bei katika kipindi chote cha utawala wake, japokuwa yalikuwepo mapungufu kadhaa.

  Hivyo CHADEMA inatakiwa kuwaelimisha watanzania mapema iwezekanavyo kuwa mfumo wa mbunge kutoa kipaumbele katika maendeleo ya jimbo na kushindwa kutimiza wajibu wake wa kuisimamia Serikali kwa kuunga mkono na kupigia makofi kila hoja ya Serikali ndio maaan Tanznaia ni inakuwa katika kundi la nchi maskini zaid hapa duniania licha ya raslimali tulizonazo. Aidha ubinafsi wa kupendelea jimbo atkalo ni sawa na rushwa kwa wananchi ili wamchague kwa kuwa majukumu yake ni kuisimamia Serikali yenye wajibu wa kuwatumikia watanzania wote ili hatimaye Serikali iweze kupata mapato mengi zaid ya kuwahudumia watanzania wote kinyume na hali ilivyo sasa ambapo fedha zinafujwa ovyo, madini yanasombwa ovyo, raslimali zetu zinzhmishwa kiholela n.k.

  CHADEMA inapaswa kuwaelimisha watanzania kuwa mfumo ulioasisiwa na CCM wa kuwapima wabunge kwa kutegemea maendeleo waliyopelekea katika majimbo wanayotoka ulikuwa na lengo la kudhoofisha dhana ya "KUISIMAMIA SERIKALI".Mana halisi ya "mbunge" ni kuwa wananchi katika jimbo fulani wanapatiwa kiti kimoja katika bunge ambalo lina wajibu wa kuisimamia Serikali ambayo kwa mujibu wa Katiba ndio yenye mamlaka ya kukusanya, kupanga na kutumia fedha, madini na raslimali zote za Tanzania kwa manufaa ya wananchi wote na sio wa jimbo moja moja.

  Chini ya mfumo huo mbovu ili mbunge aweze kupata maji, barabara, shule n.k katika jimbo lake hulazimika kuwapigia magoti mawaziri, makatibu wakuu n.k huko wizarani na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ambao kwa pamoja alipaswa kuwasimamia kama mwakilishi wa wananchi. Sasa kama mbunge atapokea upendeleo kutoka kwa watu anaopaswa kuwasimamia, atawezaje kutimiza majukumu yake ya kuwasimamia?.

  Ni kutokana na mapungufu haya, hivi sasa hapa nchini fedha za umma, mali za umma, madini na raslimali zote za Tanzania hazina watu wa kuhakikisha vinatumika kwa kadri ya matarajio ya wananchi kutokana na wabunge kugeuzwa matarishi wa maendeleo ya jimbo moja moja, hali hii inawaacha viongoizi, watumishgi wa Serikali pasipo kuwa na usimamizi wa moja kwa moja kutoka kwa wananchi na hiki ndicho chanzo cha umaskini wa wwatanzania na Tanzania.

  Katika utoaji huo wa elimu ya uraia CHADEMA pia inapaswa kuhakikisha wananchi wanapata ufahamu wa namana ya kutimiza shauku na lengo lao la kuchagua mtu/watu wa kuwaletea maendeleo yaani kuchagua watu ambao watakuwa na kauli ya mwisho katika fedha/mafungu ambazo yatatumika kuleta maendeleo katika majimbo yao k.m kupitia katiba mpya wananchi waelimishwe umuhimu wa kupendekeza mfumo wa Serikali za miitaa ambazo wananchi wanamchagua meya ambaye ni mtendaji badala ya utaratibu wa sasa ambao halmashauri zinakuwa chini ya wakurugenzi wenye kauli ya mwisho juu ya matumizi ya fedha.

  Mfano halisi wa hali hii ni bajeti ya 2011/12 ambapo zaidi ya Shs Trilioni 6 zitapelekwa katika halmashauri za wilaya zilizo chini ya wakurugenzi na wawakilishi wa wanancdhi yaani wabunge na madiwani wakiwa na sauti ndogo sana kuhusu matumizi ya fedha hizo. Sasa katika mazingira haya maendelo wananchi wanayoyatarajia yatakujaje pasipokuwepo msimamazi wa wananchi?

  Wananchi wanataraji maendelo kutoka huko na mbunge na diwani ilihali fdha na mafungu yapo chini ya mtu mwingine aliye chini ya Serikali Kuu. Matokeo yake ni wizi a ufisadi wa kutisha. Kwa maneno mengine watanzania wengi hawatambui kuwa licha ya shauku yao ya kuchagua watu wa kuwaletea maendeleo kama vile wabunge na madiwani, viongozi hawa ni wa kisiasa zaidi. Mfumo unapaswa kubadilishwa ili watanzania wachague watendaji kama vile meya mtendaji ambaye atakuwa ndiye kiongozi na muwajibikaji mkuu katika halmashauri.

  Endapo Chadema itashindwa kufanya haya si ajabu wabunge wake wengi wakashindwa kurejea bungeni na ikashindwa kuongeza idadi ya wabunbge wake katika uchaguzi wa 2015 kutokana wapiga kura kukosa elimu ya uraia ya kutosha kujua wanatakiwa kufanya nini ili hatimaye taifa liweze kupata maendeleo kwa pamoja na sio jimbo moja moja. Ikumbukwe kuwa CCM inashamiri kutokana na ujinga wa wananchi ndio maana kutoka 1992 imekata kuwapatia wananchi elimu ya uraia.
   
 2. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Yaleyale ya sheikh Haya Sisemi (Yahya Hussein).
   
 3. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tena nafikiri huyu ndiye mrithi wa sheikh haswaa.
   
 4. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Widom Seeds,mwanaharakati na BoaraKufa mnataka kusema Waziri Mkullo alitaja makadiri ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011/12 naye ni Sheik Yahya?
   
 5. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Inawezekana, kwa kuwa anataja mambo ambayo yeye mwenyewe anajua kabisa hawezi kuyatekeleza
  bila msaada wa wahisani
   
 6. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Sasa kuna ubaya gani na sisi kama tutainisha mapungufu tunayoyaona ndani yenye kuweza kutukossha ushindi siku za usoni
   
 7. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tafadhali tuelewe tufanyie marekebisho neno hilo niliweka rangi nyekundu. Je, ulitaka kumaanisha karamu? maana neno kalamu (kitu kinachotumika kaandikia) sidhani kama linaendana na ulichokuwa unaandika.
   
 8. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hawa ndio vijana waliotumwa na Nape kujibu mapigo kwenye mitandao ya jamii...kaazi kweli kweli!
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,605
  Likes Received: 4,708
  Trophy Points: 280
  Nape kazi yako tunaiona, misukule yako inajitahidi kweli tatizo ni kuwa wote wana mtindio wa ubongo, unaenda kuchukua watu wa mihadhara ndiyo waje wafanye mashambulizi hapa, pole sana.
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Bunge la sasa Tanzania ni sehemu ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi kimfumo waliojiweke wao.
  chadema kwa kulijua hilo imebidi waingie vitani kwa staili ambayo mtu mvivu wa kufikiri hawezi kutambua.

  Ushahidi ni semina elekezi,pale kikwete alitaka kuielekeza serikali yake nini cha kufanya ila tuliona jaji mkuu,spika.
  hapo ndipo utakapogundua tz hakuna bunge ila kuna chadema tu.
   
 11. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu mimi mtazamo wangu upo tofauti na wewe,

  Kwenye halmashauri kuna baraza la madiwani likiongozwa na meya na wabunge huwa ni wajumbe wa baraza hili. hivyo kwa kuwa baraza hili ndilo hupanga mipango/na kupitisha matumizi ya halmashauri ya wilaya.

  Mbunge anayo nafasi yake ya kutoa mawazo yake na kushauri nini kifanyike kwa manufaa ya wananchi, na baadae asimamie utekelezaji wa kile walichopanga na awaelimishe wanachi nini walipanga na nini ushauri wake kwa baraza la madiwani.

  Na kwa kuwa yeye sio mtendaji mkuu wa wilaya awe tayari kuwashitaki watendaji kwa wananchi ili wanachi waone nani anabana maendeleo yao na ndipo watampa madiwani wa kutosha na kumrudisha kuwa mbunge katika uchaguzi unaofuata.

  Mimi naamini wananchi wameanza kuelimika na wanafunguka kwa haraka sana, na wataona nini wanatakiwa kukifanya ili nchi hii iweze kwenda mbele.
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mpenzi njoo huku chumbani tujifungie tufanyie marekebisho pamoja !
   
 13. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Njoo nikuvike hiyo nepi !
   
 14. M

  Marytina JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  craaaaaaaaaaaaaaap
   
 15. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nape (Naam !) kazi yako (wewe huna kazi wafanya nn sasa ?) tunaiona (sawa si macho unayo) , misukule yako (akili finyu ya kuwaza misukule) inajitahidi (tunashukuru) kweli tatizo ni kuwa wote wana mtindio wa ubongo (na wewe una udumavu wa fikra na juzi umetoka hospitali ya vichaa) , unaenda kuchukua watu wa mihadhara (mbona wewe ni kibaraka wa Pengo na umetumwa na CDM kwa niaba ya kanisa ) ndiyo waje wafanye (njoo na wewe ufanye pia) mashambulizi hapa , pole sana (na wewe pole kwa kuwa na fikra mgando na kutumiwa vibaya )
   
 16. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hawa (wewe haumo kwa hiyo, mbona tunakujua sana kuwa umo )ndio vijana (wewe mzee kumbe ) waliotumwa (wewe pia umetumwa na kanisa) na Nape kujibu mapigo (wewe wajibu nini sasa ?) kwenye mitandao ya jamii (ipi hiyo hebu, itaje kama waijua )...kaazi kweli kweli (kazi ipo kwa ww kutumiwa vibaya na kuwa na fikra mgando)
   
 17. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mtabiri wa hali ya hewa,pole na kazi mkuu!!
   
 18. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #18
  Jun 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ikumbukwe kuwa CCM inashamiri kutokana na ujinga wa wananchi ndio maana kutoka 1992 imekata kuwapatia wananchi elimu ya uraia.........................................Nimeipenda hiyo................ kumbe mnajua eeh
   
 19. M

  MPG JF-Expert Member

  #19
  Jun 10, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ni limbukeni kweli unawaza kwa kutumia makamasi naona umetumwa na NAPE haya nenda ofisi za CCM ukachukue posho kwa upuuzi uliotumwa uje uandike,LIMBUKENI MKUBWA WEWE.
   
 20. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 10, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  think twice? Eh yaani wewe unafikiria mara mbili tuu! akili zako ni haba huwezi kufikiria zaidi ya mara mbili? majibu yako mwenyewe hapo juu ni ushahidi tosha kuwa una shida ya kufikiria
   
Loading...